Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.5 Ndoa

Maneno ya Kiyunani yaliyofasiriwa ‘ushirika’, kimsingi yanaelezea hali ya kuwa na kitu fulani kwa ushirikiano. ‘Ushirika’ ni neno linalohusisha ‘kushiriki kanuni na imani ile ile - hivyo kuwasiliana. Kwa sababu ya kujua na kujizoeza njia ya Mungu, tunaushirika naye na wote wengine wafanyayo yale yale kwa kuwa "katika Kristo". Ni vyepesi kuacha majukumu ambayo tunayo ya kuwa na ushirika na wengine: "kutenda mema na kushirikiana, msisahau (Ebr 13:16). Flp 1:5 umezungumzia ushirika wetu katika kuieneza Injili; basi msingi wa ushirika wetu ni mafundisho yaliyo na Injili ya kweli. Kwa sababu hii ushirika unaofurahiwa na waumini wa kweli ni mkubwa mno kuliko jumuia yoyote nyingine au kanisa. Kwa ajili ya Ushirikiano huu wanasafiri umbali mrefu ili kuwa na mwingine na kuwatembelea waumini walio pekee, na atatumia vema posta na simu kwa kuwasiliana mahali panapowezekana. Paulo anausema "ushirika wa Roho" (Flp 2:1), yaani, ushirika ambao kama ilivyofunuliwa katika Roho yake/neno.

Moja ya maelezo makubwa ya ushirika wetu ni kufanya ibada ya kumega mkate pamoja. Waumini wa kwanza "walidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kumega mkate, na katika kusali….. wakimega mkate ……. Kwa furaha na kwa "moyo mweupe" (Mdo 2:42,46). Mifano inayokuwa mbele yetu mezani yaonyesha kiini kikuu cha tumaini letu, tunavyovigawana pamoja vitatuunga pamoja katika "moyo mweupe". "Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, Je! si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ulio tu umegao, Si ushirika wa mwili wa Kristo?. Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tuliotulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja"; yaani Kristo (1 Kor 10:16,17) kwa hiyo tunawajibu wa kugawana mifano ya dhabihu ya Kristo na wote wale wanaofaidika kutokana na kazi yake, ambao "wanashiriki kugawana sehemu ya huo mkate mmoja". Wale tu waliobatizwa vema katika Kristo, baada ya kujua ukweli, wamo hali hii, ni kufanyia mzaha mifano kwa kugawana na aweye yote mbali ya hawa.

Paulo anakumbuka ni jinsi gani alishiriki Injili ya uzima wa milele na wengine "ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo" (1 Yoh 1:2,3). Hivi yaonyesha ya kwamba ushirika umelala kuzunguka desturi ya kufahamu Injili ya kweli, na kwamba hii inatuleta katika ushirika wa pande mbili na waumini wa kweli wengine, vile vile Mungu na Yesu juu ya usawa wenyeywe. Tunapotumia zaidi Injili katika maisha yetu, tukiyashinda maelekeo yetu ya dhambi, na kwa kina tunapoendelea katika kufahamu kwetu Neno la Mungu, ndipo kwa kina zaidi ushirika wetu utakuwa na Mungu pamoja Kristo.

Ushirika wetu na Mungu na Kristo na waamini wengine hautegemei tu juu ya desturi yetu ya kukubaliana na kweli zenye mafunzo ambayo yana "imani moja". Mwenendo wetu wa maisha inabidi ulingane na mambo yalioelezwa humu ndani. "Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake. Tukisema ya kwamba twashirikiane naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli: bali tukienenda nuruni twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote" (1 Yoh 1:5-7)

‘Kuenenda gizani’ inabidi kuwa unatajwa mwenendo wa maisha ambao siku zote ni wa kutumikia na watu wote walio mbali mbali na Neno la Mungu (Zab 119:105; Mithali 4:18); haitajwi udhaifu wetu wa dhambi za mara kwa mara, maana aya inayofuata inaendelea. "Tukisema kwamba hatuna dhambi twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu (yaani Neno la Mungu (Yn. 17:17; 3:21 Waefeso (5:13) linakuwa halimo mioyoni mwetu".

Kutokana na hivi itakuwa dhahiri kwamba ushirika unakoma hapo muumini akianza kufuata mafunzo au mwenendo wa maisha, ambao upo wazi ukipingana na fundisho lilowazi la Biblia: "Msishirikiane na matendo yasiyo zaa ya giza, bali myakemee" (Efe 5:11). Kila juhudi ifanywe kuwarudisha kwa kufuata mfano mzuri wa mchungaji mwema amtafutae kondoo aliyepotea (Lk 15:1-7). Ikiwa ndugu au dada anaendelea katika elimu ya uongo au tabia mbaya kabisa, ni lazima kupanga ukomo wa ushirika uliotokea (Mathayo 18:15-17). Kwa desturi hivi hufanywa kwa usaili wa washirika wanaohusika na Iklezia, na kutangaza ukweli katika gazeti la Kristadelfiani. Lakini habari isitiliwe mkazo sana ya kuwa njia hii itatumika kwa kuchukua njia ya mkato ya kushika masuala ya elimu potofu au kuendelea katika mwenendo wa maisha yasiyo ya Kiroho. Inabidi mtu awe na hakika ya kwamba kuna desturi kidogo mno baina yetu, kwa ajili ya kupotoka toka msingi wa mafundisho ya Biblia, hata kuvunja utaratibu wa ushirika ni lazima.

Moja ya maneno yaliyo wazi sana kuhusu ushirika yanapatikana katika 2Kor 6:14-18: "Msifungwe nira pamoja na wasioamini": kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza….. Kwa hiyo tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana,….. nami nitawakaribisha, nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana mwenyezi".

Tumeonyesha ni kiasi gani kwamba Neno la Mungu ni nuru. Aya hizi zaeleza ni kwa sababu gani tusifanye ushirika na makanisa yafundishayo elimu iliyopotoka; kwa sababu gani tusioane na hao wasiojua kweli, na kuepuka mienendo ya ulimwengu. Kwa sababu ya kujitenga kwetu toka ulimwengu tuna heshima kubwa sana ya kuwa wana kabisa wa Mungu na binti, sehemu ya jamaa iliyoenea duniani pote ya wengine walio na uhusiano u huu - ndugu zetu na dada. Upo "mwili mmoja" tu, yaani, kanisa la kweli (Efe 1:23), ambalo msingi wake upo juu ya hao washikao tumaini moja Mungu mmoja, ubatizo mmoja na "imani moja", yaani orodha moja ya kweli yenye mafundisho yaliyo na imani moja (Efe 4:4-6). Haiwezekani kuwa sehemu ya huu "mwili mmoja" na vile vile kushirikiana na jumuia za dini nyingine zisizo shika imani ya kweli. Kwa kuwa nuru haishirikiani na giza, twajitangaza sisi wenyewe kuwa tumo gizani kama tukichagua kushirikiana na giza.

Ikiwa kweli tunaufahamu muundo mzima wa elimu ya kweli iliyofunuliwa katika Andiko, tutaona ya kwamba hao waaminio elimu iliyopotoka katika jina la Ukristo hawana ushirika tena na Mungu zaidi ya wao kuwa hamwamini Mungu kuwa yupo.

Kama umefuatilia masomo haya kwa makini, itakuwa dhahiri ya kuwa sasa hapatakuwapo hali ya mwenendo nusu katika ushirika wetu na Mungu. Aidha tunakuwamo katika Kristo kwa ubatizo ndani yake. Aidha katika nuru kwa sababu ya kushika kwetu elimu ya kweli ya kupenda kuitii au katika giza. Mtu hawezi kuwa na unyayo katika kambi mbili.

Elimu juu ya mambo haya inatupatia kiwango fulani cha kuwajibika mbele za Mungu. Sasa hatutembei mitaani au kwenda kuzungusha maisha yetu kama wastani wa mwanadamu wa ulimwengu. Kwa nguvu anatazama kuitika kwetu. Pande zote mbili Mungu, Bwana Yesu na waumini wa kweli karibu ‘watapenda’ wewe ufanye uamuzi sahihi. Bali mengi kama Mungu, Kristo sisi wenyewe tutafanya yote tuwezayo kukusaidia - hata kwa suala la Mungu kwenye upana wa kuwa amemtoa mwana wake wa pekee kufa kwa ajili yetu - wokovu hutegemea juu ya hiari yako mwenyewe kuamua kushika tumaini kuu ambalo sasa limetolewa kwako.


  Back
Home
Next