Misingi Ya BIBLIA Somo La 11: Maisha Katika Kristo Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali |
11.1 DibajiUbatizo unatupa tumaini la uhakika kuwa na uzima wa milele katika Ufalme wa Mungu. Tunapoamini zaidi na kufahamu uhakika wa tumaini hili, kadri linapokuwa wazi zaidi yanakuwepo majukumu juu yetu. Haya yanazunguka kuishi maisha pande zote ambayo yanafaa mtu aliye na tumaini la kupewa mwili na Uungu (2 Petro 1:4), hasa wa kushiriki Jina lake (Uf 3:12) akiisha kamilishwa kwa kila njia. Tumekwisha eleza katika Somo la 10:3 ya kuwa baada ya kubatizwa tumejipa sharti la maisha ya kusulubisha daima mawazo mabaya ya mwili wetu (Rum 6:6). Tusipopenda kujaribu kufanya hivi, basi ubatizo hauwi na maana. Yatafanyika tu mara mtu akiwa yu tayari kupokea majukumu ya maisha mapya yatakiwayo kufuata. Katika Ubatizo tunakufa kwa haya ya kale, njia ya maisha ya asili, na katika mfano tumefufuka na Kristo. "Basi ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo (kwa ubatizo), yatafuteni yaliyojuu, Kristo aliko ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini mambo ya juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa….. Basi, vifisheni(ueni) ……. uasherati, uchafu, tamaa" (Kolos 3:1-5). Baada ya kubatizwa tunajiweka wenyewe kwenye maisha ya kuangalia mambo yatokanayo na uhusiano wa mbinguni, tukifikiria ya mbinguni (yaani ya kiroho) hayo mambo, tukibadili tamaa yetu ya ulimwengu kwa tamaa ya kutaka kushinda maelekeo ya mwili wetu wa nyama na damu na kwa hiyo kuuingia Ufalme wa Mungu. Maelekeo ya tabia ya mwanadamu ni kuonyesha shauku ya kumtii Mungu kwa kushika na kuacha. Mara nyingi Mungu anaonya juu ya tabia hii. Kwa habari ya amri na hukumu Mungu anasema "ambazo mwanadamu ataishi kwazo kama akizitenda" (Ezek 20:21). Kama tukijua amri za Mungu, na kuanza kuzitii katika Ubatizo, tutajiweka maisha yote kuishi kwa utii wa hizo. |