Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.3 Practical Christian Life
11.3.1 Maisha ya kikristo yenye Matendo

Baada ya kubatizwa, tuishi maisha ya kuzaa "tunda la utakatifu", tukiishi maisha yanayoongozwa na Roho kuliko mwili (Rum 6:22; 8:1; Gal 5:16,17). Ni kwa kukaa neno la Mungu ndani yetu ndipo tunazaa tunda la Roho (Yon. 15:7,8). Tumeona kwamba tumeongozwa na Roho katika maana ya kwamba Roho ya Mungu imo katika Neno lake. Katika maisha yetu yote yatupasa kuwa karibu na Neno hilo kwa kujifunza na kusoma Biblia kila mara.

Kujifunza kwa kuwaza Neno la Mungu matokeo ni mtu kutambua haja ya kubatizwa na kwa sababu hiyo akionyesha tendo hilo. Hii njia ya kuruhusu Neno livute matendo yetu na kuongoza maisha yetu iendelee; lakini ubatizo ni hatua ya kwanza katika maisha yetu ya kutii Neno la Mungu. Kweli kuna hatari sana kuwa na mazoea na Biblia pamoja na mafunzo ya msingi wa Injili, ya kutupeleka kwenye hali ambayo, ndani yake Neno haliwi na ushawishi kwetu tena: tunaweza kusoma nayo yakawa hayana matokeo ya maana juu yetu (tazama yaliyotiwa mwishoni mwa kitabu sehemu ya 2).Kwa sababu hii ni busara kuomba sala fupi kabla ya kila somo la kila Maandiko: "Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako" (Zab 119:18).

Neno la Mungu liwe chakula chetu cha kila siku kwa kweli, utegemezi wetu juu yake, na kulitamani, nia yetu iwe kubwa kuliko silika yetu ya hamu ya chakula cha mwili: "Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu" ilikuwa hisia ya Ayubu (Ayubu 23:12). Vivyo hivyo Yeremia: Maneno yako yalionekana nami nikayala: na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu" (Yer 15:16). Kutenga muda wakati wa kila siku kwa ajili ya utaratibu wa kusoma Biblia ni jambo la muhimu, basi kutengeza katika maisha yetu ya kila siku ni mfano mzuri wa kuigwa. Dakika 30 za bila kukatiza kujifunza biblia likiwa ni jambo la kwanza asubuhi linaelekea kutuanzisha kila siku katika mwendo sahihi wa kiroho. Imani hii inayofanya mazoea itakuwa yenye thamani kwa uzito wao wa dhahabu katika siku ya hukumu.

Kwa kuepuka maelekeo ya mwili kwa kusoma sehemu hizo za Maandiko ambazo kwa kawaida zinatuvuta macho, Kristadelfiani wamevumbua mpangilio wa kusoma uitwao "Mwenza wa Biblia" (hupatikana kwa wachapishaji wa kitabu hiki). Huu mpangilio unatupata idadi ya sura za kusoma kwa kila siku, ukisababisha kusoma katika Agano Jipya mara mbili na Agano la kale mara moja katika mwendo wa mwaka. Tunaposoma sura siku kwa siku, tunaweza kujipa moyo toka wazo ambalo maelfu ya waamini wengine wanasoma sura zizo hizo. Popote tunapokutana, basi tuna kiungo cha karibu sana; sura ambazo tumekuwa tukisoma kwa karibu ndizo zinafanya msingi wa mazungumzo yetu.


  Back
Home
Next