Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.4 Kumega Mkate

Tutaanza sehemu hii kwa kupima hali yao ambao hawajaoa wakati wa kubatizwa. Tumezungumzia katika somo la 5.3 juu ya haja ya kuoa au kuolewa na waumini waliobatizwa tu. Yapo mafungu ya maneno machache, yaliotiwa pamoja na mifano ya Yesu, Paulo na wengineo yanawatia nguvu wao wasio na wake kukumbuka hiari iwayo yote ya kubaki bila kuoa hivyo kama kujitoa wenyewe kabisa kufanya kazi ya Bwana (1 Kor. 7:7-9, 32-38 linganisha na 2 Tim 2:4; Math. 19:11,12,29; Mhubiri 9:9). "Lakini kama ukioa huna hatia" (1 Kor 7:28). Mitume wengi walioa (1 Kor 9:5), ndoa kama Mungu alivyoikusudia imepangwa ili kuleta faida nyingi za mwili na kiroho. "Ndoa iheshimiwe na watu wote, na (matumizi ya) malazi/kitanda yawe safi" (Ebra 13:4).

"Si vema huyu mtu awe peke yake" ila akiweza kuongoza hali ya juu katika mambo ya kujitoa kwenye mambo ya kiroho, na kwa sababu hiyo Mungu aliweka ndoa (Mwanzo 2:18-24). Kwa hiyo, "Apataye mke apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa Bwana……. Mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana" (Mithali 18:22; 19:14).

Tumepewa maelezo mafupi yaliyosawazishwa ya hali ilivyo katika 1 Kor 7:1,2: "Ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya zinaa (yaani, ili kuepuka uzinzi), kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe" (linganisha mst 9).

Kidokezo cha aya hii ni kwamba kujifurahisha kwa tamaa za ngono nje ya ndoa ni uasherati. Maonyo juu ya kufanya uasherati (ngono baina ya watu wasiooana), uzinzi (ngono ambayo mmoja au watu wawili wameoana tayari na wenza wengine) na namna yeyote ya vitendo viovu ni mengi katika Agano Jipya lote; karibu kila waraka yapo ndani. Maonyo yafuatayo ni baadhi: Matendo 15:20; Rum 1:29; 1Kor 6:9-18; 10:8; 2Kor 12:21; Gal 5:19; Efe 5:3; Kol 3:5; 1The 4:3; Yuda 7; 1 Petro 4:3; Uf 2:21.

Katika mwangaza wa mkazo huu uliorudiwa, kutotii mapenzi ya Mungu yaliyoelezwa wazi ni kosa kubwa sana. Wakati dhambi za udhaifu wa mara moja kama zikitubiwa, Mungu anapenda kusamehe(k.m. uzinzi wa Daudi na Bathsheba), kuishi namna ya maisha ambayo kwa kawaida ni ya kufanya matendo haya yanaweza kusababisha hukumu tu. Huu, Paulo aliunena: "Uzinzi, uasherati…. Na mambo kama hayo: katika hayo nawaambia mapema (kiti cha hukumu), kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao (daima) mambo ya jinsi hiyo hawataurithi Ufalme wa Mungu" (Gal 5:19,21), kwa hiyo "Ikimbieni zinaa (linganisha na 2 Tim 2:22). Kila dhambi atendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyae zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe" (1 Kor 6:18).

Imekuja kukubalika karibu ulimwenguni pote ya kwamba mume na mke vijana waweza kuishi pamoja kabla ya ndoa halali, wakifurahia maisha kamili ya uhusiano wa ngono. Kutumia neno ‘ndoa ya sheria ya kawaida’ kueleza hivi ni maelezo yaliyo sahihi kabisa ya neno. Ndoa kwa waumini inabidi iwe ndoa inayolingana na Mungu alivyofafanua; hatuwezi kuruhusu elezo la ndoa iliyofanywa na ulimwengu unaotuzunguka wenye kuupendeza mwili kuwa juu zaidi ya taarifa za Mungu wala si mwanadamu. Kwa Biblia ndoa inafanywa karibu na mambo matatu :-

  1. Lakini namna nyingine ya sherehe ya ndoa ni rahisi. Taarifa ya Boazi akimuoa Ruthu katika Ruthu 3:9-4:13 yaonyesha ya kwamba ndoa si uhusiano unaoingizwa tu; inabidi uwepo muda dhahiri wakati mtu anaolewa/oa kabisa. Kristo amelinganishwa na bwana arusi na waumini bi arusi, ambaye atamwoa ajapo mara ya pili. Itakuwepo "karamu ya arusi ya Mwana kondoo" itakayo sherekewa (Uf 19:7-9). Uhusiano kati ya mme na mke ni mfano uliopo kati ya Kristo na waumini (Efe 5:25-30); kama inavyokuwapo maana halisi ya ndoa kati yetu, basi itakuwepo arusi kati ya waaminio inayoanza ndoa yao, ikionyesha mfano wa kuungana Kristo na sisi wenyewe kwenye kiti cha hukumu.

  2. Ndoa ya Mungu kwa Israeli ilihusisha kuingia katika mapenzi ya agano la uaminifu

  3. kiroho kwa wao na mwingine (Ezek 16:8), na hili liwe ni jambo la kuangaliwa katika ndoa ya waaminio.

4. Ushirika wa mume na mke ni wa lazima ili kukamilisha ndoa (Kum 21:13; Mwa 24:67; 1Falm 11:2). Kwa sababu hii 1 Kor 6:15,16 inaeleza kwa nini ushirika ukifanywa nje ya walioona ni vibaya mno. Ushirika unamaanisha kwa maneno ya kimwili ni jinsi gani Mungu alivyowaunga pamoja wanandoa (Mwa 2:24). Kuungwa na kuwa "mwili mmoja" ni uhusiano wa kitambo basi ni vibaya kutumia miili aliyotupa Mungu isiyotakiwa. Ameipanga kwa utaratibu ili kuweza kukamilisha katika mapatano ya kimwili alivyoiunga pamoja katika ndoa.

Kutokana na hili, kwa sababu hiyo watu wawili ‘wanaoishi pamoja’ kabla ya harusi kwa kweli wanaishi katika dhambi. Isipokuwa wakitengeneza uhusiano wao kwa kuoana vyema - au kutengana - hakuna maana kwao wakiwa wamebatizwa. Tatizo linazuka kwenye tamaduni zingine katika nchi zinazoendelea ambapo hakuna wazo la sherehe au mkataba kwa watu wa kawaida. Watu wawili wanaweza kuishi kwa miaka mingi pamoja bila mambo haya, wakijiona wenyewe kama wameoana. Ni ushauri wa mwandishi wa wakati huu wa kwamba katika masuala haya hao wabatizao waeleze hali ya huyo atakaye Ubatizo, wawakutanishe na wenza wao ili watie saini kwenye fomu ya mapatano ya ndoa. Kisha uhusiano uorodheshwe na mamlaka muhimu ya Serikali haraka iwezekanavyo.

Hao waliobatizwa, muda wenza wao wakiwa bado, kwa namna iwayo yote wasiachane nao (1 Kor 7:13-15), bali wafanye kila juhudi kuwapenda, na hivyo kuonyesha mwenendo wa maisha wa kwamba wana imani halisi kwa Mungu wa kweli, kuliko kuwa ni dini ambayo imebadilishwa. Waraka 1 Petro 3:1-6 unawatia moyo walio kwenye hali hii kwamba kufanya hivi kunaweza, ndani yake, kuwa njia ya kumuongoa mwenzi asiyeamini.

Mambo yanayotawala ndoa yamewekwa kwa ufupi katika taarifa ya Mungu kwa habari zake: "Mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe: "nao watakuwa mwili mmoja" (Mwz 2:24). Jitihada hii ya umoja kati ya mume na mke kwa namna nyingine kama iwezekanavyo ni ya kulinganika na juhudi yetu ambayo inaendelea kwenye umoja na Kristo, kwa kushinda msingi wa dhambi na uchoyo wa mwili wetu. Kujitahidi huku ni juu yetu wenyewe kuliko juu ya Kristo au mwenza wetu. Zaidi tunapofaulu kwa hili, uhusiano wetu utakuwa wenye furaha na kutimilika zaidi.

Lakini tunaishi katika ulimwengu wenye dhambi kweli na kushindwa, usioweza kusimama kabisa kwenye viwango vya hali ya juu vya utakaso tuliowekewa katika Biblia na katika mfano wa upendo wa Mungu na Kristo. Desturi isiyo na upungufu iliyowekwa katika Mwanzo 2:24 ya mwanamume na mwanamke mmoja, waishi pamoja kwa umoja wa maisha kabisa.

Waumini yawapasa wawe tayari kukubali kwamba mara nyingine desturi hii haitafikiwa pande mbili katika maisha yao wenyewe na kwa hayo ya waamini wengine. Waume kwa wake waweza kushindana kwa maneno na kupoteza umoja huo wa roho ambao watakuwa nao; haitawezekana kwa mwili kukamilisha ndoa; mwanamume aweza kuwa na wake kadhaa, aliowachukua kabla ya ubatizo, kama amekuwa akiishi katika jamii mahali ndoa ya mitara imeruhusiwa. Katika suala hilo atabaki na hao wake, lakini asiongeze tena. Mtume Paulo mwenye mchanganyiko wa kupenda kuongoza wengine huruma ya mwanadamu na mwaminifu na kufuata mambo ya Mungu, kwa hiyo alishauri kwamba kutengana kuliwezekana katika kipeo cha masuala yasiyopatakana: "Mke asiachane na mmewe; lakini ikiwa ameachana naye, na akaye asiolewe" (1 Kor 7:10:11).

Huku kueleza kwa maneno ya desturi isiyo na upungufu,bali nia ya kukubali desturi ya chini maadamu haidhihaki msingi wa jambo la Mungu (k.m huo uzinzi ni mbaya), ni sura ya Andiko inayotokea kabisa. Ushauri wa Paulo kwa 1 Kor 7:10-11 ni sawa na 1 Kor 7:27,28: "…. Umefunguliwa?usitafute mke (yaani, ubaki pekee yako) "Lakini kama ukioa huna hatia". Ingawa hivyo, kuachana kwa makusudi ni kudharau mpango uliowekwa na Mungu wa kwamba mwanaume na mwanamke watambueya kuwa amewaunga kuwa mwili mmoja, hata kama juu ya matokeo ya kufaa haya wanakuta ni shida kujizoeza. Maneno ya Kristo ni ya kujitahidi kuwa sawa.

"Tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu Mungu aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja: (Yesu anatia mkazo) hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmojas. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe (kwa kuachana kutoa hati ya talaka")….. "Kila mtu atakaye mwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake. Na mke atakeye mwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini" (Marko 10:6-12)

Kwa hili eneo zima la mahusiano ya ngono, mwili ni mkono unaogusa mapendekezo na kuachilia kujihesabia haki katika tamaa za asili za kuupendeza mwili. Hao wanaojikuta wenyewe wamo katika mazingira hasa ya kujaribiwa watapata nguvu za uwezo wanaouhitaji kutoka tafakari inayorudiwa juu ya aya zinazonukuliwa katika sehemu hii. Wengine wametafuta kuhesabia haki vitendo vya kulawiti na vitendo vya mwanamke na mwanamke kuwa ni halali, kwa matakwa ya mwili. Walakini, hapana shaka ya kwamba mazoea haya yote ni machukizo mbele za Mungu.

Jambo la msingi lililo katika Mwanzo 2:24 linafafanua dhambi ya kulawiti; nia ya Mungu ni kwamba mwanamume na mwanamke waoane na kuambatana. Mungu aliumba mwanamke kumsaidia Adamu, wala si mwanamume. Mahusiani ya ngono baina ya wanaume Biblia imerudia kutoa lawama. Hii ilikuwa ni moja ya dhambi zilizofanya Sodoma iliangamizwa (Mwanzo mlango wa 18,19): Mtume Paulo anaweka wazi sana jambo hili kuendelea kufanya mazoea haya watapata hasira ya Mungu, na kutokuingia katika Ufalme wake (Rum 1:18-32; 1Kor 6:9,10).

Ukweli wa kuwahi kujiingiza katika matendo haya hautatufanya hatuwezi kupata msaada wa Mungu. Kuna msamaha wa Mungu, kama wakipenda kwa unyenyekevu na wale wanaopata msamaha wake (Zab 130:4). Iklezia ya Korintho lilikuwa na ushirika wa haki yake kwa waliotubu: "Baadhi yenu mlikuwa wotu wa namna hii: lakini8 mlioshwa (kwa kubatizwa), lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki (kwa kubatizwa) katika jina la Bwana Yesu Kristo" (1 Kor 6:9-11).

Malalamiko ya kwamba mtu hana mvuto wa mwili kuelekea jinsia tofauti ni ya maana ya kumlaumu Mungu kwamba hana haki kutukataza kufira, au kulawiti, bali anatuwekea majaribu ya kutuzidi nguvu. Mungu hatatuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea (1 Kor 10:13). Kwa kuufurahisha kupita kiasi mwelekeo wowote wa mwili, mtu anaweza kufikia kilele ambavyo hivi ndivyo kwa kawaida apendavyo mtu. Hivyo, mtumiaji kileo au madawa ya kulevya hawezi kuishi bila desturi ya kujidunga madawa fulani; lakini anatakiwa kubadili mwelekeo wa akili yake, na pamoja na tiba ya kurudisha namna ya kuishi sawa sawa.

Ufiraji/kulawiti inabidi uende kwa njia hii. Mungu ataimarisha juhudi ya mwanamme kwa haya; kama wao wenyewe huendekeza tamaa za mwili, Mungu atawatendea kama Israeli zamani:

"Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu: hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili: wanaume nao vivyo hivyo waliacha matumizi ya mke ya asili, wakawakiana tamaa; wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo (yaani, katika miili yao) ya upotevu wao yaliyo haki haki yao" (Warumi 1:26,27)

Kwa upofu wa makusudi mtu anaweza kushindwa kuona dhahiri jambo hili la unabii wa UKIMWI, na zao lingine kubwa linalotokana na magojwa ya zinaa ambayo ulimwengu wetu ulioharibika unavuna sasa.


  Back
Home
Next