Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.2.2 Siasa

Kufahamu wazi, na kuwa na imani thabiti katika Ufalme wa Mungu ujao maana yake ni kwamba tutatambua ya kwamba serikali ya mwanadamu haiwezi kuleta ukamilifu. Kujihusisha kokote katika siasa za wanadamu basi hakuelekeani na tumaini la Ufalme. Yesu alitabiri ya kwamba mambo yataharibika toka kwenye ubaya hadi ubaya zaidi katika "siku za mwisho" kabla ya kuja kwake (Luka 21:9-11,25-27). Haiwezekani kuamini maneno yake na wakati uo huo kujaribu kustawisha nafasi ya ulimwengu kupitia tawala za wanadamu au kusaidia matokeo. Maono ya Msamaria mwema unaonyesha jinsi gani Mkristo atasaidia mazingira ya ulimwengu - kutenda mema kwa watu wote kadri tupatavyo nafasi (Gal. 6:10).

Taarifa ya waamini wa kwanza inawaonyesha walijitoa kuishi maisha ya kiroho katika kutazamia kurudi kwa Kristo, zaidi wakidhihirisha kuhusika kwao na mazingira ya ulimwengu kwa kuhubiri kwao. Hakuna taarifa ya kuhutubia kwao jamii, uchumi na matatizo ya utawala wa ulimwengu uliowazunguka.

"Kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu" (Yer 10:23); kufahamu ubaya mkubwa na uovu wa mwili wa mwanadamu maana yake ni kwamba tutatambua ya kuwa uongozi wa mwanadamu haufai kwa watu wa Mungu. Kwa hiyo kupiga kura hakupatani na huu ufahamu. Aliye juu ndiye anayemiliki katika Ufalme wa mwanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote" (Dan 4:32). Hawa watawala wamepewa uwezo wa mwisho na Mungu (Rum 13:1); basi kupiga kura katika mfumo wa kidemokrasia kunafuatana na upigaji kura juu ya mtu ambaye Mungu amemchagua kuwa katika mamlaka. Hivyo imetolewa taarifa ya kwamba Mungu alimpa mataifa fulani yawe katika mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babel (Yeremia 27:5,6).

Kwa sababu ya kutambua kwetu ya kuwa Mungu ametia mataifa mikononi mwa viongozi wao, tuwe waangalifu sana na kuwa raia walio kama mfano, tukikaa na kuheshimu sheria za nchi tunamoishi, ila zikihitilafiana na sheria za Kristo. "Kila mtu na atii mamlaka iliyo kuu… na ile iliyopo imeamriwa na Mungu….. kwa sababu hiyo lipeni kodi…. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi…. Astailiye heshima, heshima" (Rum 13:1-7)

Kujihusisha kwa jumuiya zinazoitwa za Kikristo katika mifano ya makatazo ya kisiasa na kususia kulipa kodi basi ni ishara inayoonyesha kusoma kwao kwa kutoangalia mambo haya yenye msingi wa Biblia. Lakini, mfano wa Petro kuendela kumhubiri Kristo alipokatazwa na mamlaka kufanya hivyo, ni kuonyesha ni jinsi gani tunaweza tu kutii amri za mwanadamu zisipoleta utata na amri za Kristo: "Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe" (Matendo 4:17-20; 5:28,29).

Msimamo wa Kristadelfiani kwa lazima ya kutotumikia jeshi katika miaka ya karibu huu ni mfano mwingine.


  Back
Home
Next