Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.3.4 Kuhubiri

Mpaka hapa katika Somo hili tumenena majukumu yetu wenyewe kiroho. Lakini, tunao wajibu wa kukutana pamoja na wengine wanaoshiriki tumaini letu. Tena, hili liwe ni jambo lingine ambalo yatupasa kufanya. Tumeeleza ya kwamba baada ya kubatizwa tumeingia kuanza safari ya Jangwani kuelekea kwenye Ufalme. Basi ni jambo la kawaida ya kwamba tutataka kukutana na wasafiri wenzetu. Tunaishi siku za mwisho kabla ya kuja Kristo; ili kuyashinda majaribu yenye sehemu nyingi na kutatiza yanayotusumbua nyakati hizi, tunahitajika kushirikiana na hao walio katika maono yayo hayo: "Tusiache kukusanyika pamoja …… bali tuonyane: kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia (ya kuja mara ya pili)" (Ebra 10:25 linganisha na Mal. 3:16). Kwa hiyo waamini watafanya kila juhudi ili kukutana na kila mwingine kwa nyaraka na kusafiri ili kukutana na mwingine kushiriki kujifunza Biblia, ibada ya ushirika, na shughuli za kuhubiri.

Sisi sote kila mtu ‘tumeitwa kutoka’ ulimwenguni tuingie katika tumaini kuu la Ufalme. Neno ‘mtakatifu’ maana yake ‘mtu aliyeitwa atoke’, wanaweza kutajwa wote waamini wa kweli kuliko waamini wachache tu walio mashuhuri wa zamani. Neno la Kiyunani ambalo limetafsiriwa ‘kanisa’ katika Biblia ya kiswahili ni ‘Iklezia’, maana yake ‘kusanyiko la walioitwa au alikwa’, yaani, waaminio. Kwa hiyo ‘Kanisa’ linatajwa kundi la waaminio, wala si jengo ambalo wanakutana humo. Kuepuka kutolewa tumizi la neno hili, Kristadelfiani wamelekea kutaja ‘makanisa’ yao kuwa ni ‘ma- Ikelezia’. Popote palipo na idadi ya waaminio katika eneo la mji fulani, ni jambo la maana kama wakipata eneo la kukutania mara kwa mara. Sehemu hii inaweza kuwa ndani ya nyumba ya aaminiye au katika ukumbi wa kukodi. Maklezia ya Kristadelfiani wanakutana ulimwenguni pote katika maeneo kama ya vituo vya jamii, vyumba vya mikutano katika hotel, kumbi za kujenga wenyewe au katika nyumba binafsi. Shabaha ya Ikelezia ni kujenga washiriki wake kwa watu kukusanyika pamoja kujifunza Biblia, vile vile kwa watu wote pamoja kuushuhudia ulimwengu kwa kuifanya nuru yao iangaze kwa kuhubiri. Taarifa ya mfano wa Iklezia la Kristdelfiani yaweza kuwa na jambo fulani kama hivi :-

JUMAPILI saa 5 Asubuhi Ibada ya kumega mkate
  saa 11 Jioni Kazi ya watu wote kuhubiri.
JUMATANO saa 10 Jioni Kujifunza Biblia.

Iklezia ni sehemu ya jamaa ya Mungu. Kwa jumuiya yoyote iliyoungana karibu, kila mshirika anahitajika kuwa msikivu na mtiifu kwa wengine; Kristo mwenyewe alikuwa mfano mkubwa kwa jambo hili. Mbali ya ukuu wake dhahiri kiroho alitenda kazi kama "mtumishi wa wote", akawatawadha wafuasi wake miguu wakati waliposhindana miongoni mwao kama ni nani alikuwa mkubwa kati yao. Katika jambo hili Yesu ametuagiza kufuata mfano wake (Yn. 13:14,15; Math 20:25-28).

Sasa kama vipawa vya miujiza ya Roho Mtakatifu viliondolewa, hakuna mahali pa ‘wazee’ kama ilivyokuwa katika kanisa la kwanza; "maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu" (Math 23:8). Basi, Kristadelfiani wanaitana kila mtu na mwenzake "ndugu (kaka)au dada" bila kujali kuwa katika kuitana kwa kwanza kunako tofautisha nafasi zao kwa maisha haya kusema hivi, ni dhahiri kwamba kutakuwa na heshima kwa wamino waliomjua Mungu wa kweli kwa miaka mingi, au ambao wamepevuka kwa upesi katika mambo ya kiroho kwa kujiweka kwao katika Neno la Mungu. Ushauri wa waamini kama hivi utathaminiwa mno na wale watafutao kufuata Neno la Mungu. Ingawa hivyo, watachukua ushauri tu wa waumini wengine kwa upana huo kama ilivyo tafakari ya Neno la Mungu.

Fundisho linalotolewa katika Iklezia ni bayana msingi wake uwe juu ya neno la Mungu. Wale ambao wananena wazi ndani ya Iklezia kwa hiyo wanarudisha nuru ya Mungu, wakisema kwa niaba yake. Kwa kuwa Mungu ni wa kiume, kwa sababu hiyo ni ndugu pekee watafanya kazi ya kufundisha wazi toka neno la Mungu. Waraka wa 1 Kor 14:34 uko wazi; "Wanawake na wanyamaze katika Kanisa; maana hawana ruhusa kunena". Waraka wa 1 Tim 2:11-15 unafuatilia sababu hii kurudi nyuma hadi katika bustani ya Edeni; kwa kuwa Hawa - Eva alimfunza Adamu kutenda dhambi, sasa mwanamke asimfundishe mwanamume. Ni kweli Mungu alimuumba Adamu kabla ya Hawa ikiwa ni ishara ya kuwa "kichwa cha mwanamke ni mwanamume" (1 Kor 11:3), kwa hiyo mwanamume amwongoze mwanamke kiroho vile vile.

Kwa sababu ya mambo yote haya, "Mwanamke na ajifunze katika utulivu akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa,ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. Ijapokuwa ataokolewa katika (Kiyunani ‘kwa’) uzazi wake kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi" (1 Tim 2:11-15)

Kutokana na hii ni dhahiri kwamba Biblia inaweka wazi kazi fulani zilizotengeka kwa wanaume na wanawake waaminio. Wanawake wakiwa wameamuriwa katika masuala fulani "kuolewa, kuzaa watoto, wawe na madaraka nyumbani" (1 Tim 5:14), yaonyesha kwamba shughuli zao za kujitahidi kiroho ni hizo za nyumbani. Kwa hiyo kazi ya wazi katika Iklezia ameachiwa mwanamume. Hii inapingana vikali kwa mawazo ya kibinadamu ya usawa kwa mwanamke na mwanamume, kwa maisha anayoishi mwanamke anaweza kudai usawa na mumewe kwa kila namna, kutokana na kusimamia habari za gharama kwa jamaa hadi nguo za kuvaa wote. Kuzaa watoto kumeonekana kutumika isivyofaa, ambapo imeonekana kama lazima kwa kulinda mawazo mengine ya akili timamu katika anasa kabisa na uchoyo wa ulimwengu. Waumini wa kweli watajiepusha na roho ya kipindi hiki, ingawa, kama siku zote, kupambanisha baina ya vitu viwili ni kwa lazima.

Mume haimpasi kuwa mtawala mkuu juu ya mkewe, bali kumpenda kama Kristo alivyotupenda (Efe. 5:25).

"Waume, kaeni na wake zenu kwa akili (yaani, mtendee mke kwa busara kulingana na jinsi ulivyoelimika katika Neno la Mungu); na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima" (1 Petro 3:7)

Kwa maneno ya kiroho, kubatizwa katika Kristo kunamfanya mwanaume na mwanamke kuwa sawa (Gal 3:27,28 linganisha 1 Kor.11:11). Lakini hii haidhuru, jambo kuu bayana ni kwamba ‘Mume ni kichwa cha mwanamke’ (1 Kor 11:3) katika maana na mambo ya kiroho, pande zote mbili ndani ya jamaa na Iklezia.

Ili kuonyesha kutambua jambo hili, muumini aliye mwanamke atavaa kitu cha kufunika kichwa popote ndugu akifundisha Neno la Mungu. Hii ina maana kwa desturi ya kwamba kofia au kitambaa cha kichwani kivaliwe wakati wote wa mikutano ya Ikelezia. Tofauti ipasayo kati ya mwanaume na mwanamke utatiwa mkazo kwa namna wanaume na wanawake walivyo na nywele (1Kor. 11:14,15). "Kila mwanamke asalipo, au….. bila kufunika kichwa, yuaibisha kichwa chake (yaani, mumewe mst 3) kwa maana ni sawa sawa na yule aliyenyolewa. Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele; au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe…. Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani" (1 Kor 11:5,6,10).

Akiwa na kichwa "kisichofunikwa" ni "kana kwamba amenyolewa", yaonyesha ya kwamba kichwa kisicho funikwa ni kichwa kisicho na nywele. Kwa hiyo kichwa "kilichofunikwa" si kilicho na nywele bali ni kile ambacho kwa kufahamu kina mfuniko juu yake. Pasipo kufunikwa kichwa mwanamke hawezi kutegemea kufunikwa na nywele zake za asili; kufanya hivi ni kana kwamba hana nywele mbele za Mungu. Ni kosa kwa mwanaume kufunika kichwa (1 Kor 11:7); hii haitaji kuwa na nywele, bali kufunikwa kichwa kwa namna yake maalum.

Katika malezi ya mazingira ya nyakati za Agano Jipya, nyakati pekee mwanamke aliponyolewa nywele zake zilikuwa kama alidhihirika kuwa mzinzi au muasherati, au kama alikuwa amefiwa na mumewe. Maana mwanamke akinyolewa ataonyesha amempoteza au amemkana mumewe -yaani, Kristo, kimfano.

Mwanamke anawakilisha Ikelezia, wakati mwanamume anamwakilisha Kristo. Kama itupasavyo kufanya uamuzi wa akili ili dhambi zetu zifunikwe na Kristo, basi mwanamke yampasa kufanya uamuzi wa kufunika kichwa chake. Kutumaini kufunikwa na nywele zake za asili ni sawa sawa na kutumaini haki yetu wenyewe kujiokoa kama inavyopingana na hiyo ya Kristo.

Kwa kuwa nywele ndefu za mwanamke "ni utukufu wake (aliopewa na Mungu); kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi (1 Kor 11:15), mwanamke atafuga nywele zake kwa jinsi mkazo uliotiwa ili kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke. Tofauti kati ya mtindo wa nywele za kiume na kike utumike na mwanamke kama nafasi inayojitokeza kuonyesha wajibu wake.

Kwa mambo haya ya mwanamke kuwa na nywele ndefu na kufunika kichwa, yatupasa kuwa makini kwa kutofanya mambo haya kama watu wa ishara tupu. Ikiwa dada kweli yu kiroho na ana mwenedo wa utii (linganisha 1 Petro 3:5), atajitiisha chini ya kaka kama waamini walivyo kwa Kristo, atafurahi kuonyesha ya kwamba ni mtiifu kwa kila hali, ikijumuisha kufunika kichwa. Ikiwa hoja ya amri hizi imeeleweka, kama maagizo yote ya Mungu, ndipo hatutakuwa na kutotaka kuzikubali.

Siku zote ipo kazi kwa ajili ya dada ndani ya Ikelezia - kufundisha shule ya Jumapili (Sunday school), na mwenye wajibu wakukaribisha wageni usiohusisha kufundisha watu au kunena, k.m. kutunza mahesabu. Wanawake waliopevuka kiroho wanaweza kutiwa moyo na kuendesha baraza la wanawake, vijana (Tito 2:3,4 linganisha Miriamu akiongoza wanawake wa Israeli Kut. 15:20).


  Back
Home
Next