Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.2 Utakatifu

"Mtakatifu, mtakatifu,mtakatifu, ni BWANA" (Isaya 6:3). Mkazo wa tatu pamoja kwa aya hii ni moja ya mafungu mengi ya maneno yanayokaza utakatifu wa Mungu. Kimsingi ‘utakatifu’maana yake ‘kutenga’ pande mbili kujitenga ili kufuata mambo ya Kiroho. Tumetakiwa "kumfuata Mungu," kama watoto wanaopendwa (Efe 5:1). Kwa hiyo "aliyewaita alivyo mtakatifu ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote (yaani mwenendo wa maisha); kwa maana imeandikwa, Iweni watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu" (1 Petro 1:15-16; Law 11:44).

Israeli wa asili waliitwa toka Misri kwa kubatizwa kwao Bahari ya Shamu na kuwa "taifa takatifu" (Kut 19:6). Baada ya ubatizo wetu, vivyo hivyo washiriki Israeli kiroho wanapokea "mwito mtakatifu" (2 Tim 1:9). Baada ya kubatizwa "tunafanywa watumwa wa ……. Utakatifu" (Rum 6:19,22 na hudhihirisha maana yake).

Utakatifu ni hii sehemu muhimu ya Ukuu wa Mungu, hivyo linabidi liwe jambo kubwa kwa wote wanaojaribu kuwa "wanamfuata Mungu". Kama tukifanya hivi, tutakuwa "washiriki wa utakatifu wake" tutakapopewa mwili wake (Ebra 12:10; 2 Petro 1:4). Kwa sababu hii pasipo utakatifu katika maisha haya, aaminiye hawezi "kumwona Bwana" (Ebra 12:14)- yaani, hataweza hasa kweli kumwona Mungu na kuungana naye kwa uwiano wake mwenyewe katika Ufalme kama hajaonyesha utakatifu kwa maisha haya.

Huku kupewa tumaini hili kuu maana yake ni kwamba tujitenge toka ulimwengu unaotuzunguka usio na tumaini hili, tukiisha tengwa kwa uzima wa milele wa kushiriki mwili wa Uungu. Basi ‘ kujitenga’ kwetu kusiwe ni jambo fulani tunaloona tumelazimishwa kufanya; kwa ajili ya kujitenga kwetu kwa huu mwito wa juu sana na tumaini, itakuwa ni kawaida tu tunapoona tumetengeka toka mambo ya ulimwengu, unaotawaliwa na mambo ya kimwili.

Sasa tutapima baadhi ya mambo ambayo tuone tumetengeka kwayo, na ndipo katika somo la 11.3 tutajifunza yapi tumetengeka kwa maneno na matendo.


  Back
Home
Next