Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.2.3 Anasa Za Ulimwengu

Kwa ajili ya kukosa uhusiano wa kweli na Mungu na tumaini la kweli la kipindi kijacho, ulimwengu umevumbua mifano isiyohesabika ya kutafuta kujifurahisha. Wale watafutao kuupendeza mwili waepukwe na wale wanaojaribu kuendeleza nia ya roho. "Mwili hutamani ukishindni na roho, na Roho hushindana na mwili" (Gal 5:17). Kwa sababu ya upinzani huu mkubwa, haiwezekani kufikiri kwamba tunaweza kwa halali kuruhusu mwili na vile vile kudai kuifuta Roho.

Ulimwengu umeundwa kuzunguka pande zote kwa "tamaa za mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima" (1 Yoh 2:16). "Basi yeyote ajifanyae kuwa rafiki wa ulimwengu huwa adui wa Mungu" (Yak 4:4). Kuwa na marafiki wa ulimwengu, kutazama picha za filamu za ulimwengu n.k. ni kuwa "rafiki wa ulimwengu". Matakwa ya ulimwengu yatapita mapema, na wale ambao wamejiweka upande wa ulimwengu katika maisha haya watapita na dunia (1 Yoh 2:15-17). "Dunia au ulimwengu (yaani, jamii) ya waovu" itaangamia kwa kuja mara ya pili (2 Petro 2:5), kwa kuwa "dunia yote hukaa katika uovu" (1 Yoh 5:19). Ikiwa tunataka kuepuka uharibifu huo, yatupasa "tusiwe wa ulimwengu" (Yn. 17:16 linganisha Uf 18:4).

Njia nyingi za ulimwengu za kuufurahisha mwili zafuatana na kufanya hivyo kwenye gharama za afya ya mwili; uvutaji tumbaku, madawa ya kulevya na kunywa pombe kiasi kikubwa hii ni mifano. Afya yetu ya mwili, pesa zetu, hakika yote tuliyonayo kwa kweli ni mali ya Mungu. Kwa sababu hii hatuna uhuru wa kutumia mambo haya kama tutakavyo, bali yatupasa kutenda kazi ya uwakili wa kile alichotupatia Mungu. Tutatakiwa kutoa hesabu ya jinsi tulivyotumia hivyo vitu kwenye kiti cha hukumu (Luka. 19:12-26). Haya mazoea kama uvutaji sigara na unywaji pombe ni matumizi mabaya kwa pande mbili, fedha zetu na afya . "Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?. Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo….. maana mlinunuliwa kwa thamani: sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu" (1 Kor 3:16,17; 6:19,20). Matumizi mabaya ya mwili kwa mazoea kama uvutaji kwa sababu hii ni jambo si la mchezo.

Walakini, inaeleweka ya kuwa ikiwa mazoea haya yalifanywa kabla ya kuongoka, itakuwa vigumu kuyaacha mara moja. Kinachotegemewa ni kutambua ubaya wa tabia hii, na juhudi ya kweli kuiacha. Mkazo wa maisha kuongezeka unatakiwa ukabiliwe kwa kukimbilia Neno la Mungu na sala, kuliko kulegezwa na namna yoyote ya mwanadamu.


  Back
Home
Next