Tumeacha Kitambo sehemu ya  11:  Purgatory
	
	TOHARANI  -  MAHALI  AMBAPO  ROHO  ZA  WALIOHAKI  HUISHI 
Purgatory:  Mahala pa  ahera pa kusafisha dhambi ndogo. 
Kanisa  la katoliki la Roma  linafundisha ya kuwa roho za watu wa Mungu zaweza kwenda mahala paitwapo'Purgatory (toharani) baada ya kufa,  ambapo ni nyumba iliyopo katikati ya'Mbinguni’ na'kuzimu’.  wanafundisha kuwa ni mahali pa kutakasia  ambapo roho itaona maumivu kwa muda kidogo kabla ya kufaa kupata wokovu mbinguni. Maombi, kuwasha mshumaa na kutoa fedha kwenye kanisa  mtu na rafiki zake imedhaniwa huweza kupunguza muda ambao roho inaweza kupata machungu katika'Purgatory’ (Toharani) kosa kubwa la mawazo haya  linawekwa  kutokana  na  ifuatavyo:- 
	Biblia ipo kimya  kuhusiana na uwepo wa sehemu hii.  
	Tumeonyesha kuwa  roho /nafsi unatajwa mwili wetu, sio kitu fulani kisichokufa ndani yetu, na ya kuwa'Kuzimu’ ni kaburi sio mahala pa  kuadhibiwa.  
	Wenye haki kamwe hawajaahidiwa wokovu mbinguni. kupewa  wokovu itakuwa kwenye kiti cha hukumu cha Kristo akirudi, sio wakati mwingine  baada ya kufa hapo idhaniwapo kuondoka katika'Purgatory’ (Toharani)  (Math. 25:31 -34; Ufu.22:12).  
	Wote wenye haki  wapokea  tuzo kwa wakati mmoja, sio  kila mtu hupata wokovu kwenye nyakati tofauti (Ebra. 11:39,40;2 Tim. 4:8).  
	Kinachofuatiwa na kifo ni ukimya kabisa wa kutokuwa na  fahamu, sio shughuli zilizodokezwa kwa mafundisho ya  Purgatory. (Toharani).  
	Tunatakaswa dhambi zetu kwa njia ya  Ubatizo katika Kristo na kuendelea katika imani  thabiti kwa kufanya matendo yake wakati wa maisha  yetu ya sasa, sio kupitia kipindi kingine kuteswa baada ya kufa. tunaambiwa'Jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale’  ya dhambi katika maisha yetu (1 Kor. 5:7);  tujitakase toka katika matendo yetu ya dhambi (2 Tim. 2:21; Ebra. 9:14).   
 
Basi muda wetu wa kujisafisha ni sasa, katika maisha  haya,  sio mahala pa kutakasa  (‘Purgatory’)  (Toharani) ambayo tunaingia baada ya kufa.  Wakati uliokubalika ndio sasa  ……  Siku ya wokovu ndio sasa" (2 Kor. 6:2). Tunapo mtii Mungu kwa ubatizo na kuendeleza tabia ya kiroho katika Maisha  haya tutaongozwa kupata wokovu wetu (Gal. 6:8)  - sio kutumia muda katika'Purgatory’  (Toharani). 
 
	Juhudi ya wengine kutuokoa  kwa kuwasha mishumaa na michango  mingine ya pesa kwa kanisa la katoliki, haita geuza wokovu wetu kabisa. " Hao wanaozitumainia mali zao …… hakuna mtu waezaye kumkomboa ndugu yake, wala kumpa Mungu fidia  kwa ajili yake …..  ili aishi siku zote asilione kaburi" (Zab. 49: 6-9).  
 
	 |