Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

4.6 Hukumu

Biblia hufunza kuhusu hukumu ni moja ya mambo makuu ya msingi wa imani moja, ambayo inabidi yaeleweke wazi kabla ya kubatizwa (Mdo. 24:25; Ebra. 6:2). Mara nyingi Maandiko yanataja'Siku ya hukumu’ (kwa mfano, 2 Pet. 2:9; 3: 7; 1Yoh. 4: 17; Yuda.6) kipindi ambacho wale waliopewa maarifa na Mungu watapokea thawabu zao. Wote hao itawapasa "kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo" (Rum. 14:10); sisi sote "kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo" (2 Kor. 5:10) ili kupokea thawabu ya maisha yetu katika umbo la mwili.Maono ya Danieli kuhusu kuja kwa mara ya pili Kristo, yamejumuisha moja ya kiti cha hukumu kwa mfano wa kiti cha enzi (Dan. 7: 9 -14). Mahubiri ya mifano yanasaidia kidogo kuongeza maelezo zaidi. Hayo ya talanta yamefananishwa na kurudi kwa Bwana, awaitaye watumishi wake na kuhesabu kadri ya jinsi walivyotumia vema pesa alizowapa (Math. 25: 14 -29).Mfano wa wavuvi umelinganishwa na mwito wa Injili kwa nyavu za kuvulia, zikikusanya kila aina ya watu; ndipo watu wakaketi (Kuweka hukumu) nao wakagawa samaki wazuri na wabaya (Math. 13: 47 -49). Tafsiri ipo wazi: "Mwisho wa ulimwengu malaika watatokea, nao watawatenga kati ya wabaya na wenye haki".

Mpaka hapo kutokana na tulichoona, ni vizuri kusadiki kwamba baada ya Bwana, akiisha rudi na kufufua kutakuwepo kukusanyika wote walioitwa na Injili kwenda mahali fulani kwa muda wa namna maalum, watakapokutana na Kristo. Hesabu itabidi wapewe, naye ataonyesha ikiwa wanakubalika au la kupokea thawabu ya kuingia katika ufalme. Ni katika maana hii tu wenye haki wanapokea thawabu yao. Yote haya yanaungwa pamoja na mahubiri ya mifano wa kondoo na mbuzi: "Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu, na Malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo ataketi kwenye kiti cha utukufu wake (Kiti cha enzi cha Daudi -Yerusalemu,Luka. 1: 32,33): na mbele yake watakusanyika mataifa yote (yaani - watu wa kutoka mataifa yote, Math. 28:19): naye atawagawa kama mchungaji anavyowagawa kondoo na mbuzi. Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari (Math. 25:31 -34).

Kurithi Ufalme wa Mungu, kupokea ahadi za Abrahamu kuhusu ufalme, ni thawabu ya wenye haki. Lakini hii itakuwa tu baada ya hukumu, itakuwa Kristo ajapo, Kwa hiyo haiwezekani kupokea thawabu iliyoahidiwa ya mwili usiopatikana na mauti kabla Kristo hajarudi; kwa sababu hii inatubidi kusema kuwa tangu wakati wa kifo hadi ufufuo, mwamini hana ufahamu unaoishi kabisa, kwa kuwa hauwezi kuishi kwa namna yoyote bila kuwa na mwili.

Ni neno la awali la Biblia kwamba Kristo akirudi, ndipo thawabu itatolewa - na sio kabla: -

  • "Mchungaji mkuu (Yesu) atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu" (1Pet. 5: 4; 1:13).

  • "Kristo Yesu atakayewahukumu walio hai na waliokufa, kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake ….. taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile" (2Tim. 4:1;8).

  • Masihi atakapokuja siku ya mwisho, "wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi (Mwa. 3:19) wataamka, wengine wapate uzima wa milele, na wengine aibu na kudharauliwa" (Dan 12:2).

  • Kristo atakapokuja katika hukumu, waliomo makaburini …. Watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu" (Yoh. 5:25 -29).

  • "Tazama, (mimi Yesu) naja upesi; na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo" (Uf. 22:12). Hatuendi mbinguni kupokea ujira - Kristo anatuletea toka Mbinguni.

Ujira upo pamoja naye Yesu kutuletea unadokezwa kwamba tumetayarishiwa mbinguni, lakini tutaletewa duniani ajapo mara ya pili;'Urithi" wetu wa nchi aliyoahidiwa Abrahamu kwa maana hii "Umetunzwa mbinguni kwa ajili yenu, Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya Imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho" Kristo ajapo.(1Pet. 1:4,5) Kufahamu hili kunatuwezesha kufasiri kwa usahihi lisiloeleweka mno fungu la maneno yaliyo katika Yohana 14:2,3: "Maana (mimi Yesu) naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali (tuzo " imetunzwa mbinguni"), nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo mimi nanyi mwepo" Yesu anasema kila mahali kuwa atakuja tena kutupa tuzo zetu (Ufu. 22:12), tumeona kwamba hizi zitatolewa kwenye kiti chake cha hukumu. Atatawala juu ya kiti cha enzi cha Daudi Yerusalemu'milele’ (Luk. 1:32,33). Maisha ya milele atayatumia hapa duniani, ni mahala atakapokuwa katika ufalme wa Mungu duniani - hapo tutakuwepo nasi pia. Ahadi ya "Kuwakaribisha kwangu" inaweza basi kusomwa kuwa ni maelezo ya sisi kukubaliwa naye kwenye hukumu. Fungu la maneno machache ya Kiyunani katika sentensi "niwakaribishe kwangu", vile vile linatokea katika Math. 1:20 kuhusu Yusufu "kumchukua kwake" Mariamu kuwa mkewe. Basi halihitaji kwa ulazima kuondoka kwa mwili kuelekea kwa Yesu.

Kama tuzo itatolewa tu kwenye hukumu Kristo atakaporudi, kinachofuatia ni kwamba wenye haki na waovu wanakwenda kwenye sehemu moja wanapokufa yaani Kaburini hakuna tofauti inayofanywa kati yao katika mauti yao.

Kwa jambo hili yafuuatayo ni ushahidi wa hakika: -

  • Yonathani alikuwa mwenye haki,Sauli mwovu,Lakini "Mautini hawakutengwa"

(2 Sam. 1:23).

  • Sauli, Yonathani na Samweli wote walikwenda sehemu moja walipokufa (1 Sam. 28:19).

  • Abrahamu mwenye haki " akakusanyika kwa watu wake" au wazee, alipofariki; walikuwa ni waabudu sanamu (Mwa. 25:8; Yoshua.24:2)

  • Aliye na busara kiroho na mpumbavu wanapata kifo kimoja (Mhub. 2: 15. 16).

Hii yote ni tofauti dhahiri kwa madai ya'Ukristo’ wa watu wengi. Mafundisho yao kuwa wenye haki mara akifa anakwenda mbinguni yanaharibu haja ya ufufuo na hukumu. Lakini tumeona ya kuwa haya ni matukio ya muhimu katika mpango wa wokovu wa Mungu,hivyo katika ujumbe wa Injili wazo la wengi kuwa mwenye haki mmoja anakufa na kupewa tuzo ya kwenda mbinguni, akifuatiwa siku nyingine, mwezi unaofuata, mwaka unaofuata, na wengine.

Wazo hili linapingana vikali na mafunzo ya Biblia ya kuwa wenye haki wote watapewa thawabu pamoja: -

  • Kondoo wanatengwa kwenye hukumu, mmoja mmoja.mara hukumu ikiisha, Kristo atawaambia kondoo wote waliokusanyika mkono wake wa kuume,

  • "Njoni, mliobarikiwa na baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari" (Math.25:34). Hivyo kondoo wote wanarithi ufalme wakati mmoja (1 Kor. 15:52).

  • Kwenye'mavuno’ ya Kristo akirudi na kufanya hukumu, wote waliofanya kazi ya injili'Watafurahi pamoja’ (Yoh. 4:35,36; Math. 13:39).

  • Ufunuo 11:8 hufafanua "Wakati wafu watakapohukumiwa" hapa Mungu'atakapowapa thawabu watumwa wake ….Watakatifu …. Nao wanaolicha jina lako’ - yaani waamini wote pamoja.

  • Waebrania 11 ni sura inayoorodhesha watu wengi wenye haki walio katika Agano la Kale mstari wa 13 unasema: "Wote hawa walikufa katika imani, bila kupokea ahadi, alizoahidiwa Abrahamu kuhusu wokovu wa kuingia ufalme wa Mungu (Ebra. 11:8 -12). kinachofuata ni kwamba kwenye kifo chao, watu hawa,mmoja mmoja hawakwenda mbinguni kupokea thawabu. Sababu hizi zimetolewa katika mstari 39,40: Wote'hawakupokea ahadi: Kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi". Kuchelewesha kuwapa thawabu yao waliyoahidiwa sababu ilikuwa ni mpango wa Mungu wa kwamba waaminifu wote "Wakamilishwe" pamoja, kwa wakati mmoja. Tendo hili litafanyika kwenye hukumu, Kristo akirudi.


  Back
Home
Next