Misingi Ya BIBLIA Somo La 4: Mungu Na Mauti Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali |
4.5 UfufuoBiblia imekaza kuwa thawabu ya wenye haki itakuwa kwenye ufufuo, Kristo atakapo kuja (1 Thes. 4:16).Ufufuo wa wafu wanaopasiwa (ona somo la 4.8) Litakuwa jambo la kwanza atakalofanya Kristo; hili litafuatiwa na hukumu. ikiwa'Roho’ ilikwenda mbinguni wakati wa kufa kusingekuwa na haja ya ufufuo. Paulo alisema ya kwamba ikiwa ufufuo haupo, basi juhudi yote ya kumtii Mungu haina maana (1Kor. 15:32). kweli asingefikiria kama hivi ikiwa aliamini kuwa atapewa thawabu pia na'roho’ yake ikienda mbinguni wakati wa kufa ? Kidokezo ni kwamba aliamini ufufuo wa mwili kuwa ni namna pekee ya thawabu. Kristo ametutia moyo tuwe na mategemeo ya kwamba kupewa thawabu waaminifu walio hai sasa itakuwa wakati wa "Ufufuo" (Luk. 14:14). Maana inabidi tena ituingie sana akilini ya kwamba Biblia haifundishi namna yoyote ya kuwepo mbali na kuwa na umbo la mwili - hili linatumika kwa Mungu, Kristo, Malaika na watu. Kristo atakaporudi "ataubadili mwili wetu mbaya, upate kufanana na mwili wake wa utukufu" (Flp. 3:20,21). Ikiwa sasa ana umbo lenye mwili halisi, mwili umetiwa nguvu na roho kuliko damu, hivyo tutashiriki thawabu hii. Kwenye hukumu tutapewa thawabu kwa jinsi tulivyoishi maisha haya katika umbo la mwili (2 Kor. 5:10). Wale walioishi maisha ya mwilini - yaani kufuata mwili unavyotaka watabaki na mwili wa sasa unaokufa, ambao wakati huo utaoza ukirudi mavumbini; wakati wale ambao katika maisha yao wamejaribu kuishinda nia ya mwili kwa hiyo ya Roho " Katika Roho atavuna uzima wa milele" (Gal. 6:8) kwa umbo la mwili uliojazwa Roho. Upo ushahidi mkubwa wa kuwa thawabu ya wenye haki itakuwa katika umbo la mwili. Mara huu ukifahamika, maana kuu ya ufufuo itakuwa wazi. Ni dhahiri mwili wetu wa sasa unakoma kuishi tukifa; ikiwa tunaweza kupata tu uzima wa milele na kutokufa katika umbo la mwili, kinachofuata ni kwamba mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu. mpaka kipindi hiki cha mwili ukiumbwa tena na kisha kupewa mwili wa Mungu. 1 Wakorintho 15 yote inazungumzia kwa kutoa maelezo ya ufufuo; siku zote italipa usomaji wa makini. 1Kor. 15;35 -44 yaeleza jinsi mbegu inavyopandwa na kisha inatoka ardhini ili kupewa mwili wa Mungu, Basi wafu vile vile watafufuka na kupewa thawabu ya mwili. Kama Kristo alivyotoka kaburini na mwili wake wa kufa ukabadilishwa hata kuwa usiokufa, hivyo mwamini wa kweli atashiriki thawabu yake (Flp. 3:21). kwa kubatizwa tunajiunga sisi wenyewe na kifo cha Kristo na ufufuo, tukionyesha imani yetu kwamba nasi, pia, tutashiriki thawabu aliyoipokea kwa kufufuka kwake (Rum.6: 3 -5). Kwa kuyashiriki mateso yake sasa, pia tutashiriki thawabu yake "Tutachukuwa katika mwili (Sasa) kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu" (2Kor. 4:10). "Yeye aliyemfufua Kristo katika wafu ataihuisha na miili yenu ya kufa kwa roho wake" (Rum. 8:11). Basi kwa tumaini hili "tunasubiri ukombozi wa mwili wetu" (Rum.8:23), kwa mwili huo ukiisha fanywa usife. Tumaini hili la mwili halisi la kupewa thawabu lilieleweka na watu wa mungu tangu nyakati za kwanza. Abrahamu aliahidiwa kwamba, yeye binafsi atarithi nchi ya Kanaani milele, hakika kama alivyotembea juu ya nchi ndani yake (Mwa. 13:17; tazama somo la 3.4.). Imani yake kwa hizo ahadi ilimwezesha aamini kuwa mwili wake kwa namna nyingine, tarehe zijazo, atafufuliwa na kufanywa asife, hivyo hii itawezekana. Ni dhahiri Ayubu alieleza fahamu zake jinsi, mbali ya mwili wake kuliwa na funza kaburini kwa umbo la mwili atapokea thawabu yake: "mteteaji (Mkombozi) wangu yu hai ….. hatimae atasimama juu ya nchi na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi lakini pasipo kuwa na mwili wangu nitamwona Mungu (nitamwona Mungu kwa macho yangu mwenyewe au katika mwili huu -B.H.N) nami nitamwona mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine, Ingawa mtima wangu unazimia ndani yangu" (Ayu.19:25 -27). Tumaini la Isaya lilikuwa hili hili. "Maiti yangu itafufuka ….." (Isa. 26: 19). Maneno haya kabisa yapatikana katika kifo cha Lazaro, rafiki yake Yesu. Badala ya kumfariji dada mtu kwa kusema kwamba roho yake imekwenda mbinguni, Bwana Yesu alisema siku ya ufufuo: "Ndugu yako atafufuka". Jibu la haraka toka kwa dada yake Lazaro, Martha laonyesha ni kiasi gani hili lilieleweka na Wakristo wa kwanza: "Martha akamwabia, Najua ya kwamba atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho"(Yoh. 11:23,24). Kama Ayubu, hakufahamu kuwa mauti ndio njia peke ya kwenda kwenye furaha mbinguni, bali, badala yake alitazama mbele kwenye ufufuo "Siku ya mwisho ("Hatimaye" ya Ayubu). Bwana ameahidi: "Kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba …. Nami nitamfufua siku ya Mwisho" (Yoh. 6:44,45). |