Misingi Ya BIBLIA Somo La 4: Mungu Na Mauti Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali |
4.4 Mauti ni Kutokuwa na Fahamu KabisaKutoka kile tulichojifunza mpaka hapo kuhusu nafsi na roho, kinachofuata ni kwamba muda mtu anapokuwa amekufa hawi na fahamu kabisa. Wakati matendo ya wale wanaopashwa kwa Mungu yatakumbukwa naye (Malaki 3:16; Uf. 20:12; Ebra. 6:10), Katika Biblia hakuna kinachodokezwa kuwa tunazo fahamu zozote mautini. Ni vigumu kubishana na shuhuda wazi zifuatazo kuhusu hili:-
Mautini hakika ni kutokuwa na fahamu, hata kwa wenye haki, yameonyeshwa maombi yaliyorudiwa ya watumishi wa Mungu waruhusiwe maisha yao yaweze kurefushwa, kwa sababu walijua kwamba baada ya kufa hawataweza kumsifu na kumtukuza Mungu, kwa kuwa mautini ni kutokuwa na fahamu. Hezekia (Isaya 38:17 -19) na Daudi (Zaburi 6:4,5; 30:9; 39:13; 115:17) wao ni mfano huu mzuri. mauti yamerudiwa kwa kutaja kuwa ni kulala au kupumzika, wote wawili kwa wenye haki na waovu (Ayu. 3:11, 13:17; Dan 1.12:13). Ushahidi wa kutosha umetolewa kwa ajili yetu unaosema wazi ya kwamba wazo la watu wengi kuwa wenye haki wanakwenda kwenye hali ya furaha na kupewa thawabu mbinguni moja kwa moja mara baada ya kufa, peke yake haupatikanai katika Biblia. Funzo la mauti na umbo la binadamu kweli linatoa amani kubwa ya maana. Baada ya hali yote ya magonjwa na maumivu ya maisha ya binadamu, Kaburini ni mahala pa usahaulifu kabisa. kwa wale ambao hawajui matakwa ya Mungu, usahaulifu huu utadumu milele. Sababu kuu ya huzuni hii na uhai wa kwanza hautarudi tena; matumaini yasiyofaa na hofu ya asili ya nia ya mwanadamu havitatambulika au kuogofya. Kwa kusoma Biblia, kuna utaratibu kweli wa kuivumbua; lakini, kwa bahati mbaya, pia upo utaratibu wenye kosa katika dini aliyojitungia mtu, kutokana na kutoiangalia Biblia. Jitihada za binadamu kurahisisha kilele cha mauti imepelekea aamini ya kwamba ana'nafsi /roho isiyokufa’ Mara ikikubalika kuwa kitu hiki kisichokufa kimo ndani ya binadamu, inakuwa ni lazima kudhani kwamba inabidi kiende mahali fulani baada ya kufa. hii imepelekea ya kwamba mautini inabidi ziwepo ajali fulani tofauti kati ya wenye haki na wabaya. kutengeneza wazo hili, imesemwa kuwa inabidi kuwepo sehemu ya'roho nzuri zisizokufa’ huenda toharani - mbinguni na sehemu nyingine kwa ajili ya'roho mbaya zisizokufa’ kwenda sehemu hiyo imeitwa kuzimu. Awali tumeonyesha kuwa'nafsi au roho’ isiyokufa kwa Biblia haiwezekani. Mawazo mengine potovu yaliyo ndani ya watu wengi jinsi wanavyofikiri sasa yatachambuliwa: -
Shabaha ya uchambuzi wetu sio tu tunakanusha; kwa kupima alama hizi kwa maelezo ya moja baada ya nyingine, tunaamini ya kwamba tutaeleza mambo mengi ya Biblia katika ukweli ambao ni sehemu ya picha ya kweli kuhusiana na desturi ya binadamu. |