Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

4.3 Roho ya Mtu

Kuna chafuko lisilo la heri katika fikira za watu wengi kati ya nafsi na roho. Hili limesumbua kwa ukweli kwamba katika lugha zingine na tafsiri za Biblia, maneno ya Kiingereza'nafsi’ na'roho’ yanafanana.'Nafsi’ kwa ukubwa yanatajwa yote yanayofanywa na mtu wakati mwingine yaweza kutaja roho vile vile. Ingawa hivyo, kwa kawaida kuna tofauti katika maana kati ya'nafsi’ na'Roho’ kama yalivyotumika katika Biblia; nafsi na Roho zaweza'kugawanyika’ (Ebra. 4: 12).

Kiebrania na Kiyunani maneno'Roho’ ('Ruach na'Pneuma’ mbali mbali) vile vile yametafsiriwa kwa namna ifuatavyo: -

Uhai       Roho

Akili       Upepo

Pumzi

Tumejifunza jambo la'Roho’ katika somo la 2.1. Mungu anatumia roho yake kutunza viumbe vya asili, na mwanadamu amejumuika. Roho ya Mungu iliyo ndani ya mwanadamu kwa sababu hii ni nguvu ya uhai iliyo ndani yake "mwili bila roho umekufa" (Yakobo 2:26). Mungu akampulizia katika (Pua ya Adamu) Pumzi (Roho) ya uhai; mtu akawa nafsi hai (Kiumbe) (Mwa. 2:7)" Ayubu anaisema'roho ya Mungu’ kuwa' Roho ya Mungu i katika pua yangu’ (Ayubu. 27:3;Isaya 2:22). Roho ya uhai iliyo ndani yetu tunapewa tukizaliwa, nayo tunakuwa nayo mwili unapokuwa hai. Roho ya Mungu ikiondolewa toka kitu chochote, mara moja inapotea - roho ya nguvu ya uhai. Mungu "akijikusanyia roho yake na pumzi zake; wenye mwili wote wataangamia pamoja, nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi. Ikiwa una ufahamu, sikia neno hili" (Ayubu. 34:14 -16). Sentensi ya Mwisho inadokeza tena ya kuwa mwanadamu anakuta hii inaweka wazi umbile lake halisi kuwa vigumu kupatana.

Mungu anapotwaa roho yake toka kwetu tunapokufa. Sio mwili pekee unaokufa, bali fahamu zetu zote zinakoma. Daudi alipofahamu jambo hili lilimfanya amwamini Mungu kuliko viumbe kama Binadamu. Zaburi.146:3 -5 ni kukabiri ugumu kwa madai ya wanadamu: "Msiwatumainie wakuu, wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake, Pumzi yake (roho) hutoka, hurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea (Maana amefanywa kwa udongo) Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake".

Wakati wa kufa, "Mavumbi hurudia nchi kama yalivyokuwa; nayo roho humrudia Mungu aliyeitoa" (Mhubiri 12: 7). Tumeonyesha awali kuwa Mungu yupo kila mahali kwa njia ya roho yake. kwa maana hii " Mungu ni Roho" (Yoh. 4:24). Tunapokufa'tunavuta pumzi ya mwisho’ katika maana kwamba roho ya Mungu iliyondani mwetu imeondoka. kama roho inavuta katika roho ya Mungu inayotuzunguka pande zote; basi wakati wa kufa "roho itamrudia Mungu" Kwa sababu roho ya Mungu hutegemeza viumbe vyote, mfuatano huu wa kufa huwatokea wanyama wote. Watu na wanyama wana roho ile ile, au nguvu ya kuwa hai, ndani yao.'Kwa maana linalowatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja (Yaani, ile ile) roho ya Pumzi; wala mwandamu hana kitu cha kumpita mnyama" (mhubiri 3: 19).

Mwandishi anaendelea kusema kwamba hakuna tofauti ya kuona kati ya roho za watu na wanyama zinakwenda wapi (Mhubiri 3: 21). Maelezo haya ya watu na wanyama kuwa na roho moja na kufa kifo kimoja, yanaelekea kurudi kutaja maelezo jinsi wote wanadamu na wanyama, waliokuwa na roho ya uhai toka kwa Mungu (Mwa. 2:7;7:15), waliharibiwa na kifo kile kile wakati wa gharika: "wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwandamu; kila kitu chenye pumzi ya uhai puani mwake kikafa ……kila kilicho hai kikafutiliwa mbali" (Mwa. 7:21 -23).Ona kwa kupita jinsi Zaburi ya 90:5 inavyolinganishwa mauti na gharika. Taarifa iliyo katika Mwanzo 7 kwa udhahiri inaonyesha hivyo kwa maneno ya msingi, watu wapo katika aina hiyo hiyo ni "wote wenye mwili ……..kila kilicho hai". Hii ni kwa sababu ya kuwa na roho moja ya uhai ndani yake kama wengine.


  Back
Home
Next