Misingi Ya BIBLIA Somo La 4: Mungu Na Mauti Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali |
4.2 Nafsi Au RohoKwa mwangaza unaosonga mbele inabidi kutofikiri kuwa mtu anayo'Nafsi au Roho isiyokufa’ au kitu chochote kisichokufa ndani yake cha kawaida. Tutajaribu kutengeneza vizuri chafuko linalozunguka neno'Nafsi’: Maneno ya Kiebrania na Kiyunani ambayo yametafsiriwa'nafsi’ katika Biblia ('Nephesh’ na'Psuche’ moja moja) pia yametafsiriwa kwa namna zifuatazo: -
Kwa sababu hii'Nafsi’ inaitwa mtu, mwili au mwenyewe. Neno mashuhuri'Okoa Roho zetu’ maana yake'Tuokoe katika mauti’. Kwa hiyo nafsi au Roho ni'wewe’ au mambo yote yanayomfanya kuitwa mtu. Inaeleweka, basi, ya tafsiri tulizo nazo Afrika ya Mashariki (U.V) inatumia neno'nafsi’ mara nyingi badala ya neno'Wewe’ au'Mtu’. Katika Biblia ya kiswahili cha kisasa neno linalotumika ni kiumbe hai. Wanyama aliowaumba Mungu wameitwa ni viumbe wenye uhai viendavyo ….. kila kiumbe chenye uhai (Mwa. 1:20, 21). Neno la Kiebrania lililotafsiriwa "Kiumbe" hapa ni'Nephesh’, pia limetafsiriwa'nafsi’; kwa mfano katika Mwa. 2: 7; "…….. naye mtu akawa nafsi hai". Hivyo mtu ni'nafsi’ kama nao wanyama ni'nafsi’. tofauti pekee iliyopo kati ya Wanadamu na Wanyama ni huo ubora wa akili waliyonayo; ameumbwa kwa mfano wa mwili wa Mungu (Mwa. 1:26). ona somo la 1:2, na watu wengine wameitwa kumjua Mungu kwa Injili ambamo ndani yake tumaini la kutokufa limefunuliwa kwao (2 Tim. 1: 10). Kwa habari ya asili ya desturi yetu na kawaida ya kufa kwetu, haipo tofauti kati ya Mwanadamu na Wanyama: - "Linalowatokea wanadamu huwatokea na wanyama; jambo moja lawatokea (elewa limekaziwa mara dufu): anavyokufa huyu ndivyoanavyokufa huyu ….. wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama ….. wote (yaani wanadamu na wanyama) huenda mahali pamoja (Kaburini); wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena" (Mhu. 3: 19,20). Mwandishi wa kitabu cha mhubiri aliyevuviwa aliomba ya kwamba Mungu awasaidie waufahamu huu ukweli mgumu, " ya kuwa (wanadamu) wao wenyewe wanafanana na wanyama" (Mhu. 3:18). Kwa hiyo inategemewa ya kuwa watu wengi itawawia vigumu kuukubali ukweli huu; Kwa kweli utakuwa ni wa kuweza kufedhehesha kutambua kuwa sisi na wanyama ni sawa sawa, tukiishi kutokana na akili hizo hizo za kujilinda wenyewe, kuishi na kupona mbali na kifo kuwepo, na kuendelea kuzaana. Biblia zote za aina mbili yaani U.V na Biblia - Habari njema - B H.N. hii tafsiri ya mhubiri 3:8 inasema kwamba Mungu anamjaribu mwanadamu kwa kumfanya aone kuwa yeye ni mnyama tu. Yaani wale wanaojinyenyekeza mno ili kuwa watu wake wa kweli wanatueleza ukweli huu, bali wale ambao sio watashindwa'jaribu’ hili. Elimu ya mwanadamu - wazo la kwamba watu wapo katika ukuu na thamani - kwa utulivu imeeneza ulimwenguni pote kwa karne hii ya ishirini. Ni kazi ya kufaa kusafisha fikira zetu kwa mvuto wa Elimu ya mwanadamu. maneno yaliyo dhahiri ya zaburi 39:5 yanasaidia: "Kila mwanadamu, ingawa amestawi ni ubatili" Njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu" (Yer. 10:23). Moja zaidi ya mambo ya msingi tunayoyajua ni kwamba miili ya wanadamu wote - kwa kweli, vyote "Viumbe hai" hatimae hufa. Basi,'Nafsi’ au Roho, inakufa; ni kinyume kabisa na kitu kingine kisichokufa. Haishangazi kuwa karibu theluthi ya matumizi yote ya maneno yaliyotafsiriwa'nafsi’ katika Biblia yameunganika na kifo na kuunganika kwa nafsi. ukweli kabisa wa neno Roho, nafsi umetumika kwa namna hii ukionyesha kwamba hakiwezi kuwa kitu fulani kisichoharibika na kisichokufa: -
Ikiwa'nafsi au Roho’ anatajwa mtu au mwili kuliko cheche fulani isiyokufa ndani yetu imeonyeshwa kwa mistari mingi ambamo neno hili linatokea. Mifano mingine iliyowazi wazi ni: -
Huu ni ushahidi wa kutosha wa nafsi hakitajwi kitu chochote cha kiroho ndani ya mtu; hapa,'nafsi’ (Kiyunani'psuche’) ina maana uhai wa mwili wa mtu tu, ndivyo lilivyotafsiriwa hapa
|