Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

4.1 Binadamu

Watu wengi wanaonekana kutumia muda mdogo kufikiria kuhusu mauti; au kuhusu desturi zao wenyewe, ambazo ni sababu kubwa za mauti. Kukosa hivi kujihoji nafsi kunaongoza kukosa maarifa ya mwenyewe, na kwa sababu hii watu huchukuliwa kufuata maisha, Wakifanya maamuzi yao kulingana na wanavyoamriwa na haja ya mwili wao.Kupo kukataa ingawa kwa ukubwa kumefichwa - kuchukuliwa ukweli wa kwamba uhai ni mfupi mno hata watu wote pia hali ya mwisho ya mauti itakuwa juu yetu.'Uzima wenu ni nini ? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka’ "Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyoweza kuzoleka tena" "Asubuhi huwa kama majani yameayo: asubuhi yachipuka (Ujana wetu) na kumea, jioni yakatika na kukauka" (Yakobo 4:14; 2 Sam.14:4; Zab. 90: 5,6). Musa kweli mtu wa kuhubiri, alitambua hili, alimwomba Mungu: "Basi, tufundishe - tujulishe kuzihesabu siku zetu, ili tujipatie moyo wa hekima" (Zab. 90:12). Basi, kwa mtazamo wa ufupi wa maisha, tendo la kupata hekima ya kweli tutalipa kipaumbele.

Kuvutika kwa mtu na Mauti kwa hali ya mwisho ni kwa namna nyingi. Mila nyingine zimejaribu kufanya mauti na maziko ni sehemu ya maisha, hupunguza maana ya msiba na kuwa hali ya mwisho. Hao wengi wachukuao jina la "Kristo" Wamedhani, kuwa mtu anayo'Roho - nafsi isiyokufa’ au kitu fulani kinachoishi milele ndani yake kinachopona mauti; kinaendelea kuishi sehemu nyingine zaidi na jambo liletalo huzuni kwa mwanadamu, itegemewe ya kwamba moyo wa mtu umezoezwa sana kupunguza mgongano wa akili yake; kwa hiyo shabaha yote ya nadharia potovu imetokea kuhusu mauti na desturi hasa za mtu. Kama siku zote, hizi inabidi zipimwe dhidi ya Biblia ili kupata ukweli kuhusu hili jambo muhimu la kuzungumuziwa. Ikumbukwe kuwa uongo kabisa wa kwanza ulioandikwa ndani ya Biblia ni ule wa nyoka katika bustani ya Edeni. Tofauti na taarifa kamili ya Mungu kuwa mtu "hakika atakufa" kama akitenda dhambi (Mwa. 2:17). nyoka alidai, "Hakika ninyi hamtakufa" (Mwa. 3:4). Uongo huu unajaribu kukana hali ya kufikia mwisho kwa kufa kabisa hivi imekuwa ni desturi ya dini zote potovu, ni dhahiri hasa kwa eneo hili, fundisho moja la uongo laongoza lingine, lingine na lingine. kwa kinyume, neno moja la kweli laongoza lingine, kama lilivyoonyeshwa na 1 Kor. 15:13 -17. Hapa Paulo anaruka toka ukweli mmoja hadi mwingine (angalia "Kama ….Kama …. Kama….").

Kuelewa desturi zetu kweli, tunatakiwa kuona Biblia yasemaje kuhusu Uumbaji wa mtu. Taarifa imo katika lugha ya wazi, ambayo, ikichukuliwa kama ilivyo, hatuwi na mashaka hasa kuhusiana na mwili ulivyo (tazama kitambo kinachozungumziwa sehemu ya 18 kuhusu maneno yalivyo katika kitabu cha Mwanzo). "BWANA Mungu akafanya mtu kwa mavumbi ya ardhi …. Katika hiyo (ardhi) ulitwaliwa (Wewe Adamu) kwa maana u mavumbi wewe nawe mavunbini utarudi" (Mwa. 2:7; 3:19). Hapa hakuna kidokezo kabisa kuwa mtu yeyote amerithi kitu kisicho kufa; hakuna sehemu iliyo ndani yake inayoendelea kuwa hai baada ya kufa.

Upo mkazo wa Biblia ulioonyeshwa juu ya ukweli kwamba mtu kwa ukubwa ametokana na mavumbi tu: "Sisi tu Udongo" (Isa. 64:8); "Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo" (1Kor. 15:47); Mtu msingi wake ni katika mavumbi" (Ayu. 4:19); "mtu hurejea tena kuwa mavumbi" (Ayu. 34:14,15). Abrahamu alikiri kwamba alikuwa "ni mavumbi na majivu tu" (Mwa. 18:27).Mara baada ya kuvunja amri ya Mungu pale Edeni, Mungu akamfukuza huyo mtu ….. asije akanyoosha mkono wake, akatwaa matunda ya mti wa uzima , akala, akaishi milele" (Mwa. 3:24,22). ikiwa mtu alikuwa na kitu kisichokufa kwa kawaida ndani yake, hii amri isingekuwa ya lazima kumzuia.

SHARTI LA KUTOKUFA.

Ujumbe wa Injili uliorudiwa usiobadilika ni kuwa mtu anaweza kuiona njia na kupata uzima wa milele na kutokufa kwa kupitia kazi ya Kristo. Huu ukiwa ni mfano pekee wa kutokufa ambao Biblia yausema, jambo linalofuatia kama kuteseka huku mtu akiwa na fahamu kwa kutenda mabaya Biblia haisemi lolote kuhusu hili. njia peke ya kupata kutokufa ni kwa kutii amri za Mungu, na wale ambao wanatii hizo watatumia maisha ya kutokufa wakiwa na hali ya ukamilifu - thawabu ya kuwa mwenye haki. Mafungu yafuatayo ya maneno ni ushuhuda wa kutosha wa kuwa huku kutokufa ni sharti, na si jambo fulani analo mtu wa kawaida: -

  • "Kristo amefunua uzima na kutokufa (Kutoharibika)kwa ile Injili" (2 tim. 1:10; 1Yoh. 1:12).

  • "Msipokula mwili wake mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu (Yaani mliourithi ndani yenu). Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milel; nami nitamfufa siku ya mwisho" na kumpa huu "Uzima wa milele" (Yoh. 6:53,54). Fikira za Kristo katika sura ya 6 ya Yohana yote ni kwamba yeye ni chakula -"Mkate wa Uzima", ni kwa usahihi pekee wa kumkubali tumaini lolote laweza kuwepo la kutokufa (Yoh. 6:47,50, 51,57, 58).

  • "Mungu ametupa sisi (Waaminio) uzima wa milele, na uzima huu umo katika mwanawe" (1 Yoh. 5:11). haliwezi kuwepo tumaini la kutoharibika kwa wale wasio'Katika Kristo’. Ni kwa Kristo pekee kutoharibika kumewezekana.

  • Yeye ni "Mkuu wa uzima (wa milele)" (Mdo. 3:15) - "(Mkuu) sababu ya wokovu wa milele kwa wote wanaomtii" (Ebra. 5:9). Basi kutokufa kwa watu kulianzishwa na kazi ya Kristo.

  • Mwamini wa kweli anatafuta kutoharibika, atapewa thawabu ya kipawa cha uzima wa milele - jambo lingine kwa kawaida asilonalo (Rum. 2:7; 6:23; Yoh. 10:28). Mwili wetu wa kufa, inabidi uvae kutoharibika Kristo atakaporudi (1Kor. 15:53); hivyo kutokufa ni jambo lingine lililoahidiwa, kwa sasa halipo (1 Yoh. 2: 25).

  • Mungu pekee ana asili ya kutoharibika (1 Tim. 6:16).


  Back
Home
Next