Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

10.1 Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo

Mara kadhaa katika masomo yaliotangulia tumetaja maana muhimu sana ya ubatizo; ni hatua ya kwanza ya utii kwa ujumbe wa Injili. Ebra 6:2 unazungumzia ubatizo kuwa ni moja ya mafunzo ya msingi sana. Tumeacha tafakari yake hata hatua hii ya mwisho kwa sababu ubatizo wa kweli unaweza kutokea tu baada ya kufahamu kwa usahihi ukweli wa kina ambao ndani yake kuna Injili. Kwa haya sasa tumekamilisha somo letu; ikiwa unataka kweli kuungana na tumaini kubwa ambalo Biblia inatoa kwa Yesu Kristo, basi ubatizo ni wa muhimu kabisa.

"Wokovu watoka kwa Wayahudi" (Yohana 4:22) kwa maana ya kwamba ahadi zote kuhusu wokovu zilifanywa kwa Abrahamu pekee na uzao wake. Tunaweza kuwa na ahadi hizo tu zilizofanywa kwetu kama tukiwa ndani ya mzao, kwa kubatizwa katika Kristo (Gal. 3:22-29).

Basi ni wazi Yesu aliwaagiza wafuasi wake: "Enendeni ulimwenguni pote, mkahubiri Injili (ambayo ndani yake kuna ahadi za Abrahamu - Gal 3:8) wa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka" (Marko 16:16). Wazo juu ya neno hili "na" linadhihirisha kuamini Injili kwa weza kutuokoa; Ubatizo sio tu ni ziada ya hiari kwa maisha ya Mkristo, ni sharti la muhimu sana kwa wokovu. Hivi sio kusema kwamba tendo la ubatizo pekee litatuokoa; linabidi lifuatwe kwa maisha yote ya kuendelea kutii neno la Mungu. Yesu alikazia hili: "Amini amini, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho, hawezi kuingia Ufalme wa Mungu" (Yn. 3:5).

Huku kuzaliwa "kwa (Kiyunani ‘kutoka’) maji" anatajwa mtu anatoka ndani ya maji ya ubatizo kuja nje; baada ya kufanya hivi, yampasa azaliwe tena kwa roho. Hili ni jambo linaloendele katika maisha: "kuzaliwa mara ya pili….kwa Neno la Mungu" (1 Petr 1:23) Hivi ni kwa kuitikia kwetu kunako endelea mtu anaposikia na kutii Roho neno ndipo tunazaliwa kwa roho (ona somo la 22).

Tuna "batizwa katika Kristo" (Gal 3:27), katika jina lake (Mdo 19:5; 8:16; Math 28:19). Elewa ya kwamba unabatizwa katika Kristo- sio katika Wakristadelfiani au jumuia iwayo yote ya kibinadamu. Bila kubatizwa hatuwi "katika Kristo", na kwa sababu hii hatuwi tumefunikwa na kazi yake inayookoa (Mdo 4:12). Petro anatoa mfano wa nguvu kuzunguka ukweli huu, anailinganisha na Safina wakati wa Nuhu na Kristo, ikiwa Safina iliwaokoa Nuhu na jamaa yake toka hukumu iliyowajia watenda dhambi, basi kubatizwa katika Kristo kutawaokoa waaminio toka mauti ya milele (1 Petr 3:21). Jinsi Nuhu alivyoingia katika Safina tendo hilo limelinganishwa na namna nasi tunavyoingia katika Kristo kwa kubatizwa. Wale wote waliokuwa nje ya Safina waliangamizwa na gharika; kusimama karibu na Safina au kuwa rafiki wa karibu wa Nuhu hakukusaidia kabisa. Njia ya pekee ni kuwa ndani ya Kristo/ Safina. Ni bayana ya kuwa kuja mara ya pili, ambayo gharika ile ilikuwa ni mfanowe (Lk 17:26,27), kumekaribia sana (tazama Habari iliyo mwisho wa kitabu sehemu ya 3).Kuingia katika Kristo/Safina kwa njia ya kubatizwa basi ni muhimu zaidi. Maneno ya kibinadamu kweli yameshidwa kuleta maana ya umuhimu huu; huu mfano wa Biblia wa kuingia katika safina wakati wa Nuhu ni wenye nguvu zaidi.

Wakristo wa kwanza walitii agizo la Kristo kwenda ulimwenguni pote kuhubiri Injili na kubatiza; kitabu cha Matendo kinazo taarifa hizi. Ushahidi mkubwa wa muhimu kubatizwa unapatikana kwa namna ambayo taarifa inavyokazia jinsi gani watu mara wakabatizwa baada ya kupokea Injili (k.m. Mdo 8:12, 36-39; 9:18; 10:47; 16:15). Mkazo huu unafahamika mara moja ukikubalika kwamba bila ubatizo kujifunza kwetu Injili ni bure; Ubatizo ni hatua muhimu sana kutembea katika barabara ya kupata wokovu. Kwa masuala mengine taarifa iliyovuviwa inaonekana kujitokeza jinsi gani, mbali ya sababu nyingine wanadamu kuchelewesha ubatizo, na shida nyingi katika kulifanya tendo hili, ni muhimu sana watu wafanye kila jitihada kuyashinda yote haya, kwa msaada wa Mungu.

Mlinzi wa jela pale Filipi alitumbukia katika wakati muhimu sana wa maisha yake kwa tetemeko kubwa la ardhi lililobomoa gereza lake la ulinzi wa hali ya juu. Wafungwa walikuwa na nafasi kubwa ya kutoroka- jambo ambalo lingemgarimu maisha yake. Wakati ule imani yake kwa Injili ikawa kweli, kwa kadiri hiyo hata "Saa ile ile ya usiku….. akabatizwa….. wakati uo huo" (Mdo 16:33). Ikiwa awaye yote alikuwa na udhuru wa kuchelewesha ubatizo alikuwa ni yeye. Hivyo aliyashinda matatizo ya karibu sana ya tetemeko lilomzunguka kusongwa na ajira yake ya kila siku na mkazo wa maumivu ya mshituko alijikuta ndani mwenyewe -akabatizwa- . Wengi wenye wasi wasi atakaye ubatizo anaweza kuchukua uvuvia wa kweli toka kwa mtu huyo. Kama aliweza kufanya tendo hili la imani ni ushahidi wa kutosha kwamba tayari alikuwa na maarifa ya Injili iliyoelezwa, kwa kuwa imani hii ya kweli huja tu toka kusikia neno la Mungu (Rum 10:17; Matendo 17:11).

Matendo 8:26-40 inatoa taarifa ni jinsi gani Afisa wa Kushi alikuwa akisoma Biblia yake huku akisafiri na gari katika jangwa. Akakutana na Filipo ambaye kwa upana alimweleza Injili, pamoja na matakwa ya ubatizo. Kunena kibinadamu hapana budi ilionekana kutowezekana kutii agizo la kubatizwa katika jangwa hilo lisilo na maji. Lakini Mungu asingetoa agizo ambalo anajua watu wengine hawawezi kutii. "Walipokuwa wakiendelea mbele njiani, wakafika mahali penye maji", yaani chemi chem ya penye miti jangwani, mahali ambapo ubatizo uliwezekana (Mdo 8:36). Tukio hili linatoa jibu kwenye mapendekezo yasiyo na msingi ya kuwa ubatizo wa kuzamishwa kabisa ndani ya maji mengi ulifanyika tu katika maeneo yenye kufikiwa kwa urahisi mahali pa maji mengi. Siku zote Mungu atatoa njia iliyo ya kweli ya kutii maagizo yake.

Mtume Paulo alipata maono ya namna ya pekee toka kwa Kristo yalioichoma dhamiri yake hata mara hiyo ilipowezekana …"akasimama, akabatizwa" (Mdo 9:18). Lingekuwa ni jaribu tena kwake yeye kuchelewesha ubatizo wake, akifikiria umaarufu wake katika jamii na namna ya maisha ya kupata riziki yaliyotengezwa katika dini ya Kiyahudi. Lakini kuchomoza nyota ya ulimwengu wa Wayahudi alifanya uamuzi sahihi na wa mara moja kubatizwa na kutupilia mbali mtindo wa maisha yake ya awali. Baadae alitafakari uchaguzi wake kubatizwa; "Lakini mambo yote yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa ni hasara kwa ajili ya uzuri usio kuwa na kiasi wa kumjua Kristo….. nimepata hasara ya mambo yote (yaani, mambo yaliyokuwa mara ya kwanza ni ‘faida’ kwake), nikiyahesabu huwa kama mavi ili nimpate Kristo…. Nikiyasahau yaliyo nyuma (‘Mambo" ya maisha yake ya kwanza katika maisha ya Kiyahudi), nikiyachuchumilia yaliyo mbele, niifikilie mede ya thahabu ya mwito mkuu"(Flp 3:7,8,13,14).

Huu ni msemo wa mpiga mbio akijinyoosha kwa mbele kukata utepe. Huku kuongeza nguvu za akili na juhudi ya mwili iwe tabia yetu baada ya ubatizo. Inabidi ieleweke ya kwamba ubatizo ni mwanzo wa shindano la mbio kuelekea ufalme wa Mungu; sio kwa ishara tu ya kubadili makanisa na imani, wala kuwa ni kushindishwa kwa furaha katika maisha ya kustarehe ya ufuasi wa kwenda kirahisi kwenye yale machache yasiyoeleweka mambo yaliyosemwa na Ukristo. Ubatizo unatuunga pamoja katika maana inayoendelea kwa kusulubiwa na ufufuo wa Yesu (Rum 6:3-5) mambo yote ya mwisho yenye nguvu kwa kila njia.

Akiwa amechoka mzee mwenye furaha kiroho kwa sababu ya kushinda Paulo aliweza kukumbuka: "Sikuyaasi yale maono ya Mbinguni" (Mdo 26:19). Kama ilivyokuwa kweli kwa Paulo hivyo ndivyo kwa wote waliobatizwa kwa usahihi.Ubatizo ni uamuzi mtu hata jutia. Maisha yetu yote yatafahamu ya kwamba tulifanya uchaguzi ulio sahihi. Maamuzi machache ya mwanadamu tumewahi kuwa na hakika mno. Swali linapasa lijibiwe bila kucheka: ‘Ni kwa sababu gani nisibatizwe?’


  Back
Home
Next