Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 32: Mnyang'anyi Msalabani

Mnyang’anyi "alimwambia Yesu, Bwana nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amini, nakuambia, Leo hii utakuwa pamoja nami peponi" (Lk. 23:42,43). Aya hizi zimechukuliwa kuwa na maana moja ya kuwa ubatizo si wa muhimu kwa wokovu, na ya kwamba mara baada ya kufa tunakwenda mbinguni. Mbali toka ushahidi wote mwingine kutofautiana, kusoma fungu la maneno kwa karibu linadhihirisha yafuatayo:

  1. Agizo la kubatizwa katika mauti ya Kristo na ufufuo lilitolewa baada ya kufufuka kwa Kristo (Marko 16:15,16). Yule mnyang.anyi alikuwa bado anaishi chini ya Torati ya Musa Kristo aliponena naye.

  2. Ubatizo wa kweli ni katika mauti na ufufuo wa Yesu. Kwa kuwa Yesu alipozungumza na mnyang’anyi wala matukio hayo hayakutokea, kubatizwa katika Kristo haukuwezekana.

  3. Ubatizo unaashiria kufa kwetu na Kristo (Rum 6:3-5). Mnyang’anyi ndiye pekee aliyefanya hivi.

  4. Inawezekana kabisa ya kwamba yule mnyang’anyi alikuwa ni mmoja wa wale waliowahi kubatizwa na Yohana mbatizaji. Wengi waongofu wake zamani walikuwa na tabia isiyonyoofu (Math 21:32).Kusema mnyanganyi hakubatizwa ni kuleta sababu za kupinga kutokana na ukimya; ambalo ni jambo kamili tu juu ya kutoa udhuru sisi wenyewe kutoka agizo la kubatizwa. Vivyo hivyo fungu lipo kimya kuhusu maneno ‘nafsi’ na ‘mbinguni’

  5. Mnyang’anyi alimwomba Yesu amkumbuke kwa mema hapo Yesu akirudi "katika" Ufalme wake (R.S.V). Kwa hiyo mnyang’anyi hakuwa mjinga wa kutojua Injili ya Ufalme wa Munngu aliyokuwa Yesu anahubiri(Math 4:23). Alijua ya kwamba itakuwepo siku ya hukumu wakati wa kuanzishwa kwa Ufalme huo, na kwa sababu hii alimwomba Yesu, aliyemjua atafufuka katika wafu na hatimaye kufanya hukumu siku hiyo, amkumbuke kwa wema. Bila shaka yule mnyang’anyi hakuwa mtu asiyejua; alitambua ya kwamba wokovu katika siku ya ufufuo na hukumu utatamkwa toka midomo ya Kristo.`

  6. Yesu alijibu ya kwamba mnyang’anyi atakuwa naye "peponi"(Kiyunani ni Paradiso)- neno hili siku zote linataja hali timilifu duniani. Limetumika kuhusu kurudia Bustani ya Edeni itakoyoonekana katika Ufalme ujao wa Mungu duniani (Uf. 2:7). Wakati wa Ufalme wa Mungu, ulimwengu utarudi kwenye hali ya Paradiso ya Bustani ya Adeni (Isa 51:3; Ezek 36:35), laana itakapo kuwa imeondolewa (Uf. 22:3). Kwa kiswahili tuna neno ‘peponi’ kuwa na maana sehemu yenye raha, hivyo imedhaniwa ni mbinguni kutokana na uongo kama wa ‘Kupotea Paradiso ya Milton’. Ahadi ya Yesu kwa mnyang’anyi kuwa na sehemu katika paradiso ilikuwa ni haja yake kuwa katika Ufalme wa Kristo. Tumeonyesha katika somo la 5 kuwa Ufalme utakuwa duniani; ‘peponi’ kwa hiyo patakuwepo vile vile.

  7. Njia ambayo mstari wa 43 kwa kawaida umetafsiriwa unafanya uonekane kana kwamba Kristo na mnyang’anyi walikwenda siku ile ile ‘peponi’ Lakini ni dhahiri Ufalme haukuwa umeanzishwa duniani. Hawakwenda katika Ufalme siku ile. Yesu alikwenda kaburini (Mdo 2:32); kama alivyotabiri, alikuwa "siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi".(Math 12:40 linganisha 16:21) baada ya kufa kwake msalabalani . Hata baada ya kufufuka alisema "Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba"(Yn. 20:17). Basi Yesu hakwenda mbiguni siku alipokufa.

Lakini Yesu anaonekana akimwahidi mnyang,anyi "Leo utakuwa nami peponi". Jibu kwa utofauti hii inayoonekana inapatikana kwa ukweli wa kwamba katika Kiebrania na Kiyunani asilia aya za Biblia, hakuna kutenga maneno au aya kwa vituo vifaavyo herufi kubwa. Inawezekana kutenga tena maneno kwa vituo na kuweza kusoma "Amini nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponi" (Luka 23:43).Mnyang’anyi alikuwa anamwomba Yesu amkumbuke kwa wema kwenye siku ya hukumu; alijua ya kwamba alihusika kuhukumiwa, naye atatakiwa pale. Lakini Yesu alimpa uhakika wa kushangaza - ‘Naweza kukuambia saa hivi! Usisubiri mpaka wakati huo wa hukumu yangu juu yako- utakuwa pamoja nami katika Ufalme!.

8.Kutokana na vipengele kujulikana hapo juu, yawezekana kutoa orodha ya mafunzo ambayo mnyang’anyi ni dhahiri aliyafahamu:

  • Ufalme wa Mungu
  • Kuja mara ya pili
  • Ufufuo na hukumu
  • Wajibu
  • Wokovu kwa njia ya Imani iliyo kwa Kristo.
  • Ufufuo wa Kristo
  • Ukamilifu wa Kristo ("mtu huyu hajafanya lolote baya")
  • Haja ya kumfuata Kristo (alimwita "Bwana ")
  • Hali ya dhambi ya mwanadamu ("kweli inayo tustahili")

Basi hakuna maana kumtumia mtu huyu kuwa ni udhuru wa kudhania ya kuwa mtu yeyote anaweza kuokoka kama akionyesha kidogo mapenzi kwenye Ukristo; inabidi pawepo msingi wa aina ya mafundisho aliyokuwa nayo. Bila hivi, asingekuwa na uwezo wa kuinuka kufikia imani aliyokuwa nayo. Kristo hakumpa tumaini lolote la wokovu yule mnyang’anyi mwingine, ambaye msimamo wake ulikuwa "Ukiwa ndiwe Kristo jiokoe mwenyewe na sisi". Huyu alikuwa ni mtu aliyesema, "Kama kuna shughuli yoyote kwa huyu Yesu, sioni kwa nini nisipate jambo lingine". Ni kwa sababu alikosa ufahamu wa mafundisho ambayo mnyang’anyi wa pili alikuwa nayo ambapo hakuweza kupata wokovu wa kweli mwishoni mwa siku zake, ijapokuwa mapenzi yake yalikuwa yakipita kwa Kristo.


  Back
Home
Next