Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

10.4 Ubatizo Na Wokovu

Ubatizo unatuunganisha na mauti ya Kristo maana yake ni kwamba ni kwa kubatizwa tu ndipo tunaweza kupata msamaha. "Tumezikwa na Kristo kwa kubatizwa, na katika huo mkafufuliwa pamoja naye kwa….. na ninyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu…… aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote" (Kolos. 2:12,13). "tumeoshwa…… katika jina la Bwana Yesu Kristo" (1 Kor 6:11) -yaani kubatizwa katika jini la Yesu ndiyo njia ambayo dhambi zetu huoshwa.

Huu mfano ulionyeshwa nyuma katika Hesabu 19:13, mahali ambapo wale waliokuwa nje ya maji ya utakaso ilibidi wafe. Tumeonyesha kwa kuandika katika Somo la 10.2 jinsi ubatizo ni kuziosha dhambi (linganisha Mdo. 12:16). Maelezo ya waaminio ya kuwa wameoshwa dhambi zao katika katika damu ya Kristo basi yanashuhudia kutenda kwo kwa njia ya kubatizwa (Uf 1:5; 7:14; Tito 3:5) kusema hivi ni kama "kuoshwa kwa kuzaliwa tena", tunahitajiwa "kuzaliwa kwa maji" wakati wa kubatizwa(Yohana 3:5).

Kwa mwangaza wa yote haya, inafahamika ya kwamba jibu la Petro kwa swali, "Tutendaje?" (ili tuokoke) lilikuwa, "Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu" (Matendo 2:37,38). Kubatizwa katika jina la Kristo ni kwa ajili ya kusamehewa dhambi,; bila kufanya hiyo hapawezi kuwepo msamaha wa dhambi, na asiyebatizwa basi itambidi apate mshahara wa dhambi -mauti (Rum 6:23). Hakuna wokovu isipokuwa ni kwa jina la Yesu(Mdo 4:12), tunaweza kushiriki tu jina hilo kwa kubatizwa ndani yake. Huu ni uhakika ya kwamba dini zisizokuwa za Wakristo haziwezi kutuongoza kupata wokovu. Hakuna mwamini wa kweli wa Biblia anayeweza kukubali zinatoa njia ya wokovu; ni uhakika wa kwamba Ukatoliki na upana wa muungano wa Wakristo kwa mashauri ya watu matendo yao nao kufanya hivyo, ni wazo la kusikitisha juu ya msimamo wao kwenye Maandiko Matakatifu.

Ufufuo wa Kristo kwa uzima wa milele ulikuwa ni ishara ya ushindi wake juu ya dhambi. Sisi nasi kwa kubatizwa tunajiunga na huu, na kwa sababu hii tumesemwa kuwa tumefufuliwa pamoja na Kristo, dhambi haina nguvu tena juu yetu, kama ilivyokuwa haina nguvu juu yake. Kwa kubatizwa basi "tunawekwa huru mbali na dhambi….maana dhambi haitawatawala ninyi" baada ya ubatizo (Rum 6:18,14). Walakini, baada ya ubatizo bado tunakosa (1Yoh 1:8,9); dhambi bado ipo katika nafasi ya kututumikisha tena kama tukigeukia mbali na Kristo. Kwa hiyo tukishiriki katika mauti ya Kristo na mateso, ingawa ubatizo unatuonyesha jinsi gani nasi pia tumejiunga na ufufuo wa Kristo, tunalo tumaini kushiriki akirudi.

Tena kwa mtazamo tunakuwa mbali na dhambi. "Aaminiye na kubatizwa ataokoka" (Marko 16:16) Kristo ajapo mara ya pili. Wokovu wa mwisho hautokei mara baada ya kubatizwa, bali mbele ya kiti cha hukumu (1Kor 3:15). Kwa kweli hakuna haja ya mafundisho kuhusu hukumu ikiwa tunapata wokovu wakati wa kubatizwa wala itatupasa kufa. "Mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakaye okoka" (Math 10:22).

Hata baada ya ubatizo wake, Paulo (na Wakristo wote) iliwapasa kujitahidi kuelekea kwenye wokovu (Flp 3:10-13; 1Kor 9:27); alilitaja tumaini la uzima wa milele (Tito 1:2; 3:7; 1Thes 5:8; Rum 8:24) nasi kuwa "warithi wa wokovu" (Ebra 1:14). Mbele ya kiti cha hukumu, wenye haki wataingia katika uzima wa milele (Math 25:46). Wazo lililovuviwa ajabu na Paulo linang’aa katika Warumi 13:11 - alihoji ya kwamba baada ya ubatizo tunaweza kujua ya kuwa kila siku tunayoishi na kustahimili ni siku moja iliyokaribu kwa ujio wa mara ya pili Kristo, hivyo basi tunaweza kufurahi yakuwa "Sasa wokovu wetu umekaribia kuliko tulipoanza kuamini". Kwa hiyo sasa hatunao wokovu wetu. Wokovu ni kwa sharti: tutaokoka kama tukishika sana imani ya kweli (Ebra 3:12-14), kama tukikumbuka mafunzo ya msingi yanayofanya Injili (1 Tim4:16; 1Kor 15:1,2), na kama tukifanya mambo yale yaliyo ndani ya tumaini hili kuu (2 Petro 1:10)

Kiarifa cha Kiyunani kilichotafsiriwa "okolewa" basi wakati mwingine kimetumika kwa wakati unaoendelea, kuonyesha ya kwamba wokovu ni jambo linaloendelea linalotokea ndani yetu kwa sababu ya utii wetu ulioendelezwa kwenye Injili. Hivyo waaminio wamesemwa kuwa "wameokolewa" kwa kuitikia injili (Kor 1:18;.mifano mingine jambo hili tunaloandika lenye kuendelea inapatikana katika Matendo 2:47 na 2Kor 2:15). Neno hili la Kiyunani "Okolewa" limetumika tu kwa wakati uliopita kuhusu wokovu mkuu aliouwezesha msalabani, tunaoweza nasi kujiunga na kubatizwa (2 Tim 1:9; Tito 3:5).

Yote haya yameonyeshwa kwa mifano Mungu akishughulika na Israel wa mwili yanayofanya msingi wa uhusiano wake na Israel wa roho, yaani, waaminio. Israel waliondoka Misri, mfano wa ulimwengu na dini za uongo tulikokuwa awali kabla ya kubatizwa. Walipita bahari ya shamu na kisha walisafiri katika jangwa la Sinai kuelekea nchi ya ahadi, mahali ambapo walisimikwa kabisa kuwa Ufalme wa Mungu. Kuvuka kwao bahari ya shamu ni mfano wa kubatizwa kwetu (1Kor 10:1,2); Safari ya Jangwani ni maisha yetu yaliyopo, na Kanaani ni kuingia Ufalme wa Mungu. Yuda mstari wa 5 unaelezea ni wangapi kati yao waliangamia wakati wa kusafiri jangwani: "Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini" Basi Israel "aliokolewa" toka Misri, kama hao wote ambao wanaobatizwa leo"wameokolewa" katika dhambi. Ikiwa mmoja wa hao Israel aliulizwa, Je! Umeokolewa?’ jibu lao lingalikuwa ‘ndiyo’, lakini hii isingalikuwa na maana ya kwamba mwishowe wangeokolewa.

Kwa njia iyo hiyo kiasi kwamba Israel aligeuka nyuma kurudi Misri kwa mioyo yao (Matendo 7:39) na kurudia hali ya kwanza kwenye maisha ya kuufuata mwili na mafunzo potofu, hivyo hao walio "okolewa" toka dhambi kwa ubatizo wanaweza vivyo hivyo kugeuka toka kwenye nafasi yenye baraka ambayo wanasimama. Uwezekano wetu kufanya yale yale kama Israel wa mwili jangwani umetokeza katika 1 Kor 10:1-12; Ebra 4:1,2 na Rum 11:17-21. Ipo mifano mingi katika maandiko ya wale walio wahi "kuokolewa" kutoka dhambi kwa ubatizo, na baadaye kuangukia kwenye nafasi ambayo inamaana watahukumiwa Kristo akirudi (k.m Ebra 3:12-14; 6:4-6;10:20-29). "Walio wahi kuokolewa siku zote wameokoka" juhudi ya mafunzo ya wahubiri wa Injili imefunua ilivyo kwa maneno haya yaliyo kwenye mafungu- fikira za kudanganya kuufuata mwili kabisa.

Kama na mambo yote, akili sahihi ya matokeo ya mwisho yanatakiwa katika kutafuta kupata kujua upana gani "tumeokolewa" kwa ubatizo. Tendo lisionekane kama linatupatia nafasi ya wokovu- ni bora kadiri iwezekanavyo kuliko bila kubatizwa. Na kuwa "katika Kristo" kwa ubatizo, tunaokolewa kwa matarajio; kwa kweli tunalo tumaini la uhakika kuwamo kwenye Ufalme wa Mungu kama tukiendelea kuwa ndani ya Kristo kama tulivyo wakati tunatoka kwenye maji ya ubatizo wetu tuweze kuwa wanyenyekevu wa ujasiri wa kwamba bila shaka tutakubaliwa kuingia Ufalme wa Kristo akirudi. Hatuwezi kuwa na hakika hata mwisho, kwa sababu tunaweza kukengeuka siku inayofuata; hatujui wakati wetu wenyewe ujao kiroho katika maisha haya.

Yatupasa tufanye yote tuwezayo ili kudumisha dhamiri njema tuliyo nayo na Mungu kwenye ubatizo. Ubatizo ni "patano la dhamiri njema" (1 Pet 3:21 Kiyunani); Mtaka ubatizo anapatana(ahidi) kuitunza hiyo dhamiri iliyowazi mbele za Mungu.

Wakati ubatizo una umuhimu mkubwa kutupatia njia kuelekea wokovu mkuu unaopatikana kwa Kristo, yatupasa tuwe waangalifu tusiwaze ya kwamba kwa kazi moja au "tendo" la kubatizwa pekee tutaokolewa. Awali tumeonyesha jinsi gani ambavyo maisha yanayodumu kushiriki mateso ya Kristo ni muhimu. "Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia Ufalme wa Mungu" (Yn. 3:5). Uwiano huu na 1 Petro 1:23 unaonyesha ya kwamba kuzaliwa kwa Roho kunakotokea baada ya kubatizwa sharti tuongozwe pole pole kiroho na Roho/Neno. Wokovu sio tu kwa sababu ya kubatizwa; ni matokeo ya neema (Efe 2:8) imani (Rum 1:5) na tumaini (Rum 8:24), miongoni mwa mambo mengine. Shauri limesikika mara nyingi kuwa wokovu si kwa kuamini peke yake, na kwa hiyo "tendo" kama ubatizo halina umuhimu. Walakini, Yakobo 2:17-24 inaweka wazi kuwa kuwaza huku kunaweka tofauti potofu kati ya imani na matendo; imani ya kweli, k.m katika Injili imeonyeshwa kwa kuandika kuwa imani ya kweli kwa matendo ni yenye kuwa na matokeo, si kwa imani peke yake" (Yakobo 2:24). Kwa masuala kadhaa ya ubatizo, mwamini aliuliza imempasa ‘afanye’ nini aokoke; siku zote jibu limehusisha ubatizo (Mdo 2:37;9:6; 10:6; 16:30). "Kufanya" halafu "tendo" la kubatizwa kwa hiyo ni kionyesho cha lazima kwa jinsi tulivyoiamini Injili ya wokovu. Tendo la kutuokoa mwishoni limefanywa na Mungu na Kristo lakini tunahitajika kufanya "matendo yanayopatana na kutubu" na kuamini hili (Matendo ya Mitume 26:20 linganisha na Marko 16:15,16).

Awali tumeonyesha kwamba msemo wa kuoshwa dhambi unatajwa msamaha wa Mungu kwetu kwa sababu yetu kubatizwa katika Kristo. Kwa maneno mengine tumesemwa ya kuwa tumeoshwa dhambi zetu kwa imani yetu na kutubu (Mdo 22:16; Uf 7:14; Yer 4:14; Isaya 1:16); kwa mengine Mungu ameonekana kuwa yeye atuoshae dhambi zetu (Ezek 16:9; Zab 51: 2,7; 1Kor 6:11). Kwa uhalisi haya yanaonyesha jinsi gani kwamba kama tukifanya kwa upande wetu kubatizwa katika Kristo, wakati huo Mungu ataondoa dhambi zetu. Hivyo ‘kazi’ au tendo la ubatizo ni hatua muhimu katika kushika habari njema za neema ya Mungu (‘upendeleo usiostahili’), tuliokwisha pewa katika Neno lake.


  Back
Home
Next