Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 33: Mfano wa huduma ya Ubatizo

Ili kutoa wazo lingine la jinsi gani ubatizo unaweza kufanywa vema, ifuatayo ni habari ya huduma ya kubatiza iliyofanywa na Wakristadelfiani wa mjini Hartlepool, Uingereza siku ya Jumapili mchana Novemba 1990. Walakini, inabidi ieleweke ya kuwa kimsingi ubatizo ni wa kutumbukizwa katika maji kufuatia toba ya kweli na kuiamini Injili. ‘Huduma’ ni ya hiari sana kutoa maana inayostahili ya umuhimu wa jambo. Mpangilio wa mambo ulikuwa kama ifuatavyo:-

  1. Sala ya kufungua

  2. Somo toka Warumi mlango wa 6

  3. Hotuba fupi ya ubatizo (Yaliochapishwa chini; majina halisi yamebadilishwa)

  4. Sala

  5. Kuzamishwa kwa mtu katika bwawa la kuogelea

  6. sala

HOTUBA YA UBATIZO

Hapana shaka kuwa leo ni siku muhimu sana katika maisha ya Deve; kwa muda mchache ataingia ndani ya maji na kusimama mzima "katika Kristo", mzao wa Abrahamu na kuwa na hizo ahadi zenye utukufu ambazo zinafanya Injili aliyoahidiwa.

Mwisho wa jambo hili lililo rahisi kufanywa, laweza kuwa lakudanganya lakini Dave na sisi wote hapa tunaamini ya kwamba huku kutumbukia ndani ya maji kutamuunganisha na mauti na ufufuo wa Yesu, kama tulivyosoma katika warumi mlango wa 6 mst 3-5:

"Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliyobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, Kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika Upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake".

Kwa muda mfupi hebu tujaribu kufikiri tukio la ufufuo wa Yesu, kwa kuwa tumeona ya kwamba Dave alipopanda juu toka majini ataungana na kufufuka kwa Yesu toka kwa wafu.

Tunaweza kuwaza uzuri na utulivu wa hewa ya usiku, na hisia zenye utukufu wa maisha mapya ndani ya Yesu. Aliweza kuona taa za Yerusalemu zikimeta-meta kwa mbali;watu wa hapo hawakujua kabisa jambo la kushangaza lililokuwa linatokea karibu sana nao- la kwamba mtu alikuwa anafufuka kwa upya wa uzima. Kama Dave anavyotoka katika maji, ulimwengu unaotuzunguka haufahamu jambo lenye utukufu linalotokea; yote wanayoweza kuona, kama wakijali kutazama, ni kundi dogo la wanaume na wanawake wakitembea kuelekea katika bwawa la kuogelea na mtu mmoja akimzamisha mwingine. Lakini kama vile malaika walivyofurahi Yesu alipofufuliwa, basi sasa hatuwaoni, lakini Malaika wanafurahi kwa mtu mmoja anayetubu.

Tumesoma kwa Wrumi 6 ya kwamba tunatakiwa "tutembee katika maisha mapya" -Furaha ambayo Dave atakuwa nayo atakwenda nayo atembeapo kuelekea mbele katika maisha. Kama tulivyosoma hatakuwa mtumwa wa dhambi tena, bali wa Mungu, akifanya mapenzi yake kama yalivyodhihirika katika Biblia. Ni kujitia jaribuni kufikiri kwamba tutataka uhuru wetu wenyewe, lakini kwa kujitumikia wenyewe hatuwi huru, tunakuwa watumwa wa dhambi. Sasa Dave anabadili mambo, kumtumikia Mungu. Kwa wakati itaonekana kwamba vikwazo vinavyoonekana kuishi maisha mapya vinawekwa juu yetu ni vingi mno kuchukua, tunajaribu kuwa huru navyo. Lakini tukifanya hivyo, hatutakuwa huru, tutakuwa tunatumikia dhambi tena.

Paulo ameeleza katika 1 Kor 10:1,2 ya kwamba kupita kwetu katika maji ya ubatizo ni sawa na Israeli walipopita katika maji ya Bahari ya Shamu. Aina ya mfano unaweza kukuzwa toka huu, pamoja na masomo mengi kwa ajili yetu. Israeli walikuwa watumwa Misri, kuishi maisha yasiyo na maana, wakifanya kazi ngumu katika utumwa wao na kuzitumikia sanamu za Misri. Kwa maisha waliyoyapata wakamlilia Mungu aweze kuwaokoa, ingawa huenda hawakujua ni jinsi gani angewajibu.

Kwa kuwajibu Mungu alimtumia Musa kuwatoa Misri, kupitia Bahari ya shamu na kisha kupita Jangwani, na kuingia nchi ya ahadi. Israel nchini Misri walikuwa kama Dave na wote wanaokuja kwenye ubatizo; sasa Dave ameongozwa kama ilivyokuwa, ufukoni mwa Bahari ya Shamu. Mara akipita katika maji, hatakuwa mara moja katika nchi yenye Ahadi ya Ufalme, ataungana na sisi hapa katika kutembea Jangwani na Malaika, Ambaye daima alikuwa nao mchana na usiku. Basi na sisi, kila mmoja wetu ana Malaika anayetuzunguka, akituongoza katika maisha yetu kuuelekea wokovu (Zaburi 34:7;Ebra 1:14).

Israel walilishwa kila siku kwa mana, ambayo Yesu ameifafanua katika Yohana 6 kuwa ni Neno la Mungu. Kama wasingalikula wangekufa mapema katika Jangwa hilo - hapakuwepo chakula kingine cha kula. Kwa sababu hii kwa nguvu ya kutosha tutaweza kukukabidhi "Mwenza wa Biblia" jedwali la kusoma, ambapo unasoma Biblia kila siku, na kupata habari yote ya maneno unaposoma ndani. Ni muhimu kutenga muda wa taratibu ya kila siku, kwa hiari muda uo huo kila siku, ili kusoma hizo sura na kuzitafakari.

Kwa kupita, Israeli waliambiwa wsijaribu kukusanya mana nyingi kwa siku moja, bali wafanye bidii ya kwenda kuikota kwa kila siku. Kujilisha kwetu Neno inatakiwa kila siku. Na kiasi kama tusivyoweza kusahu kula chakula chetu cha mwili, hivyo kwa Moyo tufanye bidii kujilisha Neno la Mungu; kweli; Ayubu aliweza kusema ya kwamba alithamini maneno ya Mungu "kuliko chakula changu cha kawaida".

Vile vile Israel walikunywa maji ya kijito kilichotiririka toka mwamba uliopigwa:1Kor 10 tumeambiwa kuwa ulikuwa badala ya "Kristo"

Basi tujishibe na kunywa katika mfano wa Yesu, ambao tunaweza kufanya kwa ibada ya kumbukumbu kila juma. Kusema mikutano, iwe ni nia yetu ya kawaida kukutana na wengine wanaoshiriki tumaini letu. Msafiri kwenye jangwa halisi atachukua fursa yoyote ili akutane na msafiri mwingine kwa kujadili matatizo ambayo yapo mbele, na kushiriki yatupatayo. Hivyo sisi katika jangwa la maisha ya ulimwengu huu mbaya tufanye kila juhudi kukutana na kila mmoja wetu. Mara nyingi mikutano hii haiwezekani katika mwili kama tunavyopenda sana, lakini tuchukue kila nafasi ya kuwasiliana kwa kuandikiana waraka, kusoma magazeti ya Biblia n.k

Tumenena juu ya majukumu ya maisha mapya, lakini itakuwa ni kuwaza vibaya ya kwamba kama tukifanya mambo fulani, kama haya ya kusoma Biblia kila siku, ndipo Mungu itambidi atupe thawabu. Ni mapenzi ya Mungu, nia yake, kutupatia Ufalme kama kipawa, na si kama mshahara kwa matendo yetu (Rum 6:23). Itakuwa ni kosa kwetu kudhani ya kwamba ubatizo ni jambo jema kwa kuwa sasa tuna nafasi nzuri ya kuingia Ufalme. Ukweli na upendo wa Mungu, ushindi wa Kristo, haya yote mawili ndiyo yanayofanya hakika zaidi kuliko hivyo. Mungu kwa kweli anamtaka Dave na sisi sote hapa kuwamo katika Ufalme. Ukweli huu ni wenye utukufu mno ambao yatupasa tujikumbeshe wenyewe mara kwa mara ya kwamba hakika ni kweli katika mwangaza wake tuwe tunafanya aina nyingine ya kuitikia upendo wa Mungu.

Israeli walipovuka Bahari ya Shamu ilikuwepo furaha kubwa. Musa aliimba wimbo wake na watu wote wakafurahi Zaburi 105:35-41 yaeleza vizuri tukio hili, ikionyesha jinsi gani Mungu aligawa kila kitu kilichokuwa lazima kwa ajili ya Safari:-

"(BWANA) akaila miche ya nchi yao ya (Misri). Wakayala matunda ya ardhi yao. Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi, malimbuko ya nguvu zao.Akawatoa (Israeli) hali wana fedha na dhahabu, katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa. Misri walifurahi walipoondoka, maana kwa ajili ya hofu imewaangukia. Alitandaza wingu liwe kifuniko, na moto utoe nuru usiku. Walipotaka akaleta kware akawashibisha chakula cha mbinguni. Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, yakapita pakavu kama mto"

Furaha ile ni furaha yetu, ndugu na dada zako wa wakati ujao, ambao wapo hapa kushuhudia kubatizwa kwako. Ni furaha ya Mungu, ya Yesu na Malaika ambao kwa mkazo wanatutazama wakati huu. Sisi kila mmoja tuweze kushika Tumaini hili, na kushangilia huku "kwa uthabiti mpaka mwisho", hata tuweze kutembea pamoja katika ufalme.

Sasa tunaingia kwenye vyumba vyetu vya kubadilishia nguo, na kisha kuingia katika bwawa la kuogelea…


  Back
Home
Next