Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

10.2 Tubatizwe Jinsi Gani?

Kuna mtazamo umeshikiliwa wa kwamba ubatizo unaweza kufanywa, hata kwa watoto wadogo, kwa kuwanyunyuzia maji kwenye vipaji vya nyuso zao (yaani, kuwabatiza). Huu ni tofauti kabisa na ubatizo unaotakiwa na Biblia.

Neno la Kiyunani ‘baptizo, ambalo limetafsiriwa ‘batiza’ katika Biblia za kiswahili halina maana ya kunyunyuzia; lina maana kamili kuosha na kutumbukiza ndani ya maji (tazama kwenye mfuatano wa maneno -concordances- ulioandikwa na Robert young na James Strong). Neno hili limetumika katika daraja bora la waandishi wa Kiyunani kuhusu meli ikizama ni kuwa ‘imebatizwa’ (Yaani, imetota) katika maji. Vile vile limetumika katika kutaja kipande cha nguo kutiwa rangi kwa kuchovya katika maji yenye rangi na kuwa rangi nyingine. Kubadili rangi ya nguo, ni bayana ya kwamba imetumbukizwa kabisa ndani ya maji, kuliko kuwa kugeuka rangi iliyo nyunyuziwa juu yake. Ikiwa kuzamisha kweli ni namna sahihi ya ubatizo inakubalika kwa aya zifuatazo.

  • "Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea wakabatizwa" (Yohana 3:23). Hapa inaonyesha ya kwamba "maji tele" yalikuwa kwa ajili ya ubatizo; kama ulifanyika kwa kunyunyuziwa matone kadhaa ya maji, wakati ule, ndoo moja tu ya maji ingalitosha katika mamia ya watu. Watu walikuja mahali penyewe kwenye kingo za mto Yordani kwa ajili ya kubatizwa, sio Yohana aliwazungukia akiwa na chupa ya maji.

  • Yesu naye, alibatizwa na Yohana katika mto Yordani: "Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini" (Math 3:13-16). Ubatizo wa Yesu ni dhahiri ulikuwa wa kuzamishwa ndani ya maji mengi- "aliinuka… toka majini" baada ya kubatizwa. Moja kati ya sababu za Yesu kubatizwa ilikuwa ni kuweka mfano, hivyo kwamba hakuna mtu ataweza kudai bila mzaha ya kwamba anamfuata Yesu pasipo kuiga mfano wake wa kubatizwa katika maji mengi.

  • - Kwa desturi ya mfano mmoja, Filipo na afisa wa Ethiopia "waliteremka wote wawili majini…… naye akambatiza. Kisha walipopanda kutoka majini…" (Mdo 8:38,39). Kumbuka kwamba, afisa aliomba ubatizo alipoona maji: "Tazama maji haya, ni nini kinachonizuia nisibatizwe?" (Mdo 8:36). Ni hakika ya kwamba huyo mtu asingefanya safari jangwani bila kuwa na kiasi cha maji ya kunywa kama katika chupa. Ikiwa ubatizo ilikuwa ni kwa kunyunyuziwa, basi ungeweza kufanyika pasipokuwa na haja ya maji ya chemi chem ya jangwani.

  • Ubatizo ni kuzikwa (Kolos 2:12), ambao unadokeza kufunikwa kabisa.

  • Ubatizo umeitwa ni ‘kuosha’ dhambi (Mdo 22:16). Maana ya kweli ya kuongoka imelinganishwa na ‘kuoshwa’ katika Uf 1:5; Tito 3:5; 2Petro 2:22; Ebra 10:22n.k. Huu msemo wa kuoshwa ni wa maana mno kwa ubatizo wa kuzamishwa kuliko kunyunyuziwa.

Kama vielekezo kadhaa kwenye Agano la kale ambavyo vinakubali kumkaribia Mungu ilikuwa kwa namna nyingine ya kuoshwa au kuoga.

Makuhani iliwapasa kuoga kabisa ndani ya bafu liloitwa ‘birika’ kabla ya kumkaribia Mungu kumtumikia (Law 8:6; Kut 40:32). Israel iliwabidi kuoga wenyewe ili wawe safi kutokana na unajisi fulani (K.m Kumb 23:11), ambao ulikuwa ni mfano wa dhambi.

Mtu alieitwa Naamani alikuwa mtu wa mataifa mwenye ukoma aliyetafuta kuponywa na Mungu wa Israel. Kama hivi alikuwa anaonyesha mwanadamu aliyetaabika na dhambi, kwa maana anatembea katika mauti hai kwa sababu ya dhambi. Tiba yake ilikuwa kujichovya ndani ya mto Yordani. Kwa kuanza tendo hili jepesi ilikuwa vigumu kwake kukubali, akidhani ya kwamba Mungu angemtaka afanye jambo fulani kwa ghafla, au kujichovya katika mto mkubwa unaojulikana, k.m Abana. Kwa namna mmoja, tunaweza kuona wokovu wetu. Yanapendeza sana kudhania kwamba matendo yetu wenyewe kwa kujiunga na kanisa kubwa, linalojulikana vyema na watu wengi (kama mto Abana) kuweza kutuokoa, kuliko tendo hili rahisi la kujiunga na tumaini la kweli la Israel. Baada ya kujichovya katika mto Yordani mwili wa Naamani "ukarudi ukawa kama wa mtoto mchanga, akawa safi" (2Fal. 5:9-14)

Sasa hakuna shaka ya kwamba ‘ubatizo’ unahusisha kabisa kujichovya ndani ya maji baada ya kuelewa kwanza ujumbe wa msingi wa Injili. Ufafanuzi huu wa Biblia kuhusu ubatizo hautoi ushahidi wowote wa cheo cha mtu ambaye hasa anafanya ubatizo. Ubatizo ukiwa wa kuzamishwa ndani ya maji baada ya kuamini Injili; kwa nadharia mtu anaweza kujibatiza mwenyewe. Lakini, kwa kuwa kubatizwa ni ubatizo tu kwa sababu ya mafunzo sahihi ambayo mtu ameshika wakati wa kuzamishwa, kwa kuweka wazi inafaa kubatizwa na mtu mwingine aaminiye mafundisho ya kweli, ambaye awali ya yote anampima kiwango cha elimu ya mtu aliyonayo kabla ya kuzamishwa ndani ya maji hasa.

Basi pamekuwepo mafundisho tokea zamani miongoni mwa wa -Kristadelfiani ya kufanya mjadala wa kina na mtaka ubatizo yeyote kabla ya kuzamishwa majini. Orodha ya maswali kama hayo yanayopatika mwishoni mwa kila somo katika kitabu hiki yaweza kuwa msingi wa mjadala huu. Wa- kristadelfiani wamesafiri maili maelfu ili kumsaidia mtu mmoja tu kuja kwenye tumaini la kweli la uzima wa milele, ni kwamba kwa kuanza hatuhusiki na uwingi wa wanaoongoka. Ni ubora, wala sio idadi ndiyo lengo letu la kumwendea.


  Back
Home
Next