Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

10.3 Maana Ya Ubatizo.

Moja ya sababu za ubatizo wa maji mengi ni kwamba kuzama ndani ya maji kunaashiria kuzikwa kwetu kaburini- tunajiunga na mauti ya Kristo, na kuonyesha ‘kufa’ kwetu kwenye maisha ya kwanza ya dhambi na ujinga. Kuinuka toka ndani ya maji kunatuunga na ufufuo wa Kristo, tunasimuliwa tumaini la ufufuo wa uzima wa milele akirudi, na sasa hivi kuishi maisha mapya, ushindi kiroho juu ya dhambi kwa sababu ya ushindi wa Kristo aliofaulu kwa kufa na kufufuliwa.

"Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake. Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende (yaani, tuishi kila siku) katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake (kwa Ubatizo), kadhalika mtaunganika kwa njia ya kufufuka kwake" (Rum 6:3-5)

Kwa kuwa wokovu umewezeshwa tu kwa kifo cha Kristo na ufufuo, ni muhimu kwamba tujiunge wenyewe na mambo haya ili tuokolewe. Mfano wa kufa na kufufuka na Kristo, ambao ubatizo unatupatia, ndio njia pekee ya kufanya hivi. Ieleweke ya kuwa kunyunyuzia maji hakutimizi ishara hii. Kwenye ubatizo, "utu wetu wa kale (mtindo wa maisha) umesulubiwa" pamoja na Kriso msalabani (Rum 6:6); Mungu "ametuhuisha pamoja na Kristo" wakati wa kubatizwa (Efe. 2:5). Ingawa hivyo bado tunao mwili wa kibinadamu baada ya ubatizo, na kwa sababu hiyo mtindo wa maisha ya mwilini utaendelea kujiinua. Basi ‘kusulubisha’ mwili wetu ni jambo linaloendelea ambalo lilianza pia kwenye ubatizo, ndivyo alimweleza aaminiye aubebe msalaba wake kila siku na amfuate, kama ilivyokuwa katika maandamano ya kuelekea Kalvari (Lk 9:23; 14:27). Wakati maisha ya kweli ya kusulubiwa na Kristo sio rahisi, kuna faraja na furaha isiyosemeka kwa kuungana pamoja na ufufuo wa Kristo.

Kristo ameleta "amani kwa damu ya msalaba wake" (Kolos 1:20); "amani ya Mungu ipitayo akili zote" (Flp 4:7). Kuhusu hii Yesu aliahidi, "Amani nawaachieni; amani yangu nawapa: niwapavyo mimi sio kama ulimwengu utoavyo (amani)" (Yn. 14:27). Hii amani na furaha kweli ni zaidi ya kusawazisha toka uchungu na shida zilizo wazi kwa kuungana wenyewe na Kristo msulubiwa: "Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu vivyo hivyo faraja inazidi kwa njia ya Kristo" (2 Kor 1:5). Tena upo uhuru unaokuja katika kujua ya kwamba nafsi yetu ya asili kwa kweli imekufa, kwa hiyo Yesu anaishi nasi kabisa kwa kila jaribu letu. Mtume mkuu Paulo alizungumzia mengi yote haya yaliyompata kwenye maisha yake: "Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilionao sasa katika mwili, ninao katika imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda (Gal. 2:20).

"….. ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi …… kwa kufufuka kwake Yesu Kristo" (1Petro 3:21) kwa sababu ya kuunganika kwetu na Kristo ufufuo wake kwa uzima wa milele unatupa njia ile ile akirudi. Ni kwa kushiriki ufufuo huu, wakati huo hatimaye tutaokolewa. Yesu alisema kuhusu jambo hili kwa maneno rahisi sana: "Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai" (Yohana 14:19). Vivyo hivyo Paulo: "Tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya mwana wake,….. tutaokolewa katika uzima wake" (Ufufuo; Rum. 5:10).

Mara kwa mara imesisitizwa ya kwamba kujiunga wenyewe na mauti ya Kristo na mateso kwa kubatizwa, na mtindo wetu wa maisha ya baadaye, hakika tutashiriki ufufuo wake wenye utukufu:-

  • "Kama tukifa pamoja naye (Kristo) tutaishi pamoja naye: kama tukistahimili, tutamiliki pamoja"(2Tim 2:11,12).

  • "Siku zote twachukua katika mwili kunawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu…. Tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu" (2Kor 4:10,11,14).

  • Paulo alishiriki "mateso yake (Kristo) ni kifananishwa (maisha magumu yaliyompata) na kufa kwake; ili nipate kwa njia yoyote kufikia kiama ya wafu kwa uzima wa milele kama Kristo alivyopata" (Flp 3:10,11 linganisha na Gal 6:14).


  Back
Home
Next