Misingi Ya BIBLIA Somo La 2: Roho ya Mungu Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali |
Tumeacha Kitambo sehemu ya 7: "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu"Petro alihutubia mkutano mkubwa siku ya Pentekoste, akamalizia kwa ombi lililo katika aya ya 38 kutubu, kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Huku kutajwa kipawa cha Roho ya Mungu kupo katika maneno yenyewe ya mitume wakiisha tumia karama hizo za kunena katika lugha katika mkutano, kunaelezea ya kwamba kufanya hivyo walikuwa wanatimiza unabii wa Yoeli unaohusu kupewa karama za kufanya miujiza (Mdo. 2:16 -20).kwa sababu hiyo inafaa kukubali kuwa ni kweli kwamba Petro alikuwa anaahidi karama za Roho kwa ule mkusanyiko wa Wayahudi waliokuwa wanamsikiliza. Mkutano ulikuwa ni wa Wayahudi, si watu wa Mataifa (Mdo. 2:5).Unabii wa Yoeli kupewa karama ulihusika hapo kwanza na Wayahudi pekee. Basi, Petro ana maana hii kwao: "Ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu" (Mdo. 2:39), labda ilikuwa yataja unabii wa Yoeli ya kwamba Wayahudi watapewa Roho na watoto wao (Mdo. 2:17 linganisha Yoeli 2: 28 -32). Panaweza kuwa na kidokezo hapa cha kwamba ahadi ya karama hizi zenye miujiza ilikuwa kwa vizazi vile viwili pekee - waliokuwa wanamsikiliza Petro, na watoto wao. Tumeonyesha ya kwamba mwishoni mwa karne ya Kwanza (Yaani, karibu miaka 70 baada ya hotuba ya Petro) vipawa vilifikia mwisho. Jambo hili tena limethibitishwa na taarifa za kihistoria. Pia kipindi cha vizazi hivyo vipawa vya Roho vilipatikana kwa watu wa Mataifa: "Na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie" (Mdo. 2:39). Fahamu jinsi watu wa mataifa wanavyoelezewa ya kuwa "walio mbali" katika Waefeso 2: 14 -17. Walakini, kuna sababu nzuri ya kuamini kwamba lililotokea katika Mdo. 2 ulikuwa ni utimizo mdogo tu wa hayo maneno ya Yoeli 2. Utimilizo mkubwa utakuwa hapo Israeli akiisha vamiwa na Jeshi kisha nalo likiisha haribiwa (Yoeli. 2:27), "Hata itakuwa, baada ya hayo ya kwamba nitamimina Roho yangu juu yao wote wenye mwili ….." (2:28). Si hata hayo masharti yakionekana tutaweza kutafuta utimizo wowote mwingine wa maneno ya Yoeli, mbali toka utimilizo huo mdogo ulionekana siku ya Pentekoste kama ulivyoelezewa katika matendo ya mitume 2. Ahadi ya kupokea kipawa cha Roho baada ya ubatizo, bado kinaweza kusomwa na ushahidi mwingine kwetu leo. Kuna roho moja, lakini yaweza kuthihirika kwa njia mbali mbali (1 Kor. 12:4-7; Efe. 4:4).Katika karne ya kwanza hii ilikuwa katika vipawa vya miujiza; sasa kama vimeondolewa ni halali kabisa katika kuona utimilizo wa hiki "Kipawa cha Roho" kwa namna nyingine kilivyoahidiwa. "Kipawa cha Roho Mtakatifu"chaweza kutajwa 'Kipawa ambacho ni Roho Mtakatifu’, au katika kipawa ambacho Roho Mtakatifu anakisema yaani - kipawa cha msamaha wa wokovu ambao Roho -Neno lenye kuvuviwa la Mungu liliahidiwa. Ipo mifano mingi mingine ya matumizi haya ya neno " ya, cha, na wa" (yenye kufahamika kuwili, katika ustadi) "Maarifa ya Mungu" (kol. 1:10) yaweza kuwa na maana maarifa ambayo Mungu anayo. Au maarifa juu ya Mungu. "Upendo wa Mungu" na "Upendo wa Kristo" (1 Yoh. 4:9; 3:17; 2Kor. 5:14) ina maana upendo ambao Mungu na Yesu wamekuwa nao kwetu, au upendo ambao tunao kwao. "Neno la Mungu" laweza kuwa na maana neno kumhusu Mungu. Au neno ambalo limetokea kwa Mungu. Kipawa "cha" Roho Mtakatifu basi chaweza kutajwa kipawa ambacho Roho Mtakatifu anawezesha mambo na kuzungumzia sawa na kipawa ambacho kina nguvu za Roho Mtakatifu. KIPAWA CHA ROHO : MSAMAHA Rum. 5:16 na 6:23 inaeleza wokovu kuwa "Kipawa" - ikivuta mlinganisho na "Kipawa" cha Roho katika mdo. 2:38.Yaonekana kabisa kuwa matendo 2:39 unanukuu toka Yoeli 2:32 kuhusu wokovu kana kwamba hivi ndivyo kipawa cha Roho kilivyonukuliwa. Petro alitaja kipawa kilichokuwa kimeahidiwa kwa wale "Walio mbali" anataja katika kusema kwa Isaya 57:19: "Amani (ya Mungu kwa kusamehewa) kwake yeye aliye mbali". Waefeso 2:8 aya hii inaeleza kipawa hiki kuwa ni wokovu, na kusema kwamba "katika Roho mmoja (Kipawa hiki) sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba" (2:18). hiki kimefanywa thabiti kwa uhakika kwamba Efe. 2:13 -17 tena kinatajwa kwa kusema katika Isaya 57:19: "Ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu …..akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali" Isaya 30:1 unawalaumu Wayahudi kwa kuutafuta msamaha kwa njia yao wenyewe kuliko toka kipawa cha Roho ya Mungu:'Wajifunikao kwa kifuniko (upatananisho) lakini si cha Roho yangu, wapate kuongeza (Badala ya kutoa) dhambi juu ya dhambi" Isaya 44:3 unaeleza msamaha wa siku hizi kwa Israeli kwa maneno haya: "Kwa maana nitamimina maji …… na vijito vya maji juu ya mahali pakavu (ukavu kiroho - Isa. 53:2): nitamwaga Roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa" Baraka ya uzao wa Ibrahimu ni kwa kusamehewa kwao kwa njia ya Kristo (Mdo. 3: 25, 26) msamaha uliopo hapa ni sawa na kumwagiwa Roho juu ya Wayahudi.Huu msemo wazi wa Yoeli 2, na matendo 2. Gal. 3:4 unaweka yote haya katika maneno mengi sana; ili kwamba baraka ya Ibrahimu (Msamaha) uwafikie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho" Basi 1 Kor. 6:11 unanena kuoshwa dhambi zetu "Kwa Roho ya Mungu wetu" Upo usawa kwa warumi kati ya sisi kupokea "neema …..upatanisho …. Roho" (1:5; 5:11; 8:15), na kuonyesha muungano kati ya kipawa ("Neema") ya Roho na msamaha unaotuongoza hata kupata upatanisho. Ni vigumu kuelezea zaidi ni kiasi gani Agano Jipya linategemea msemo na mtungo wa maneno ya Agano la Kale, hasa kwa mtazamo wa kwanza wa Wayahudi na ushawishi uliokuwa na nyaraka. Mara kwa mara katika vitabu vitano vya kwanza katika Biblia (Pentateuch) na Yoshua Mungu anaahidi kuwapa nchi watu wake - "nchi akupayo Bwana Mungu wako uimiliki" ni maneno ya kawaida. Kifani cha nchi iliyochini ya Agano Jipya ni Wokovu; basi ni kipawa cha Mungu ambacho sasa ni mtazamo, na kuwa pamoja na msamaha wa dhambi. Gal. 3: 2,5 linganisha na 3:8 -12, inasawazisha kupokea roho na. Kupokea baraka za Ibrahimu za wokovu na msamaha. "Ahadi ya Roho"(Gal. 3:14) imesemwa katika maneno yenyewe ya ahadi kwa Ibrahimu. Petro aliwataka wayahudi watubu kabla ya kuweza kupokea kipawa; hiki kilihusisha sala ya mtu binafsi. hapo yaonekana kusadiki ya kwamba kipawa cha Roho ni namna ya kuelezea sala iliyojibiwa. Kupewa "Vitu vyema wale waombao" katika sala ni mamoja kama kupewa (kipawa) cha Roho Mtakatifu (Math. 7:11; linganisha Luk. 11:13).Wafilipi 1:19 unasawazisha "Kuomba kwenu ni kuruzukiwa Roho wa Yesu Kristo". Vile vile, 1 Yoh. 3:34 tunasoma ya kwamba tunapewa Roho kama toleo la kutii kwetu amri; aya ya 22 inasema kwamba kutii amri hizo kunapelekea kujibiwa maombi yetu. Basi, ujasiri wetu ni kwa sababu maombi yetu yamesikiwa (1Yoh. 5:14) na tena kuwa na Roho (1 Yoh. 3: 21, 24; 4: 13), elewa maelezo haya yanalingana Neno'Kujifunza’ kwa neno la kiyunani ni'Charis’, mara nyingi limetafsiriwa "Neema" litaonyesha kwamba mara nyingi limetumika kwa muunganiko na kipawa cha Roho. "Kwa (kipawa) cha neema ya Bwana Yesu Kristo tutaokoka" (Mdo.15:11). Lakini wazo la'neema’ mara nyingi limegawanyika na ombi lililojibiwa (kama kutoka 3: 12; 34:9; Hesabu 32: 5; Zab. 84:11; 2Kor. 12:9; Ebr. 4:16; Yakobo. 4:6 na mstari wa 3). Zakaria 12:10 unasema siku ya mwisho kumwagiwa "Roho ya neema na kuomba" wayahudi. Huu unaelezea kwa ufupi tunachodokeza - kuwa sala ("Maombi") yanaleta kipawa cha Roho katika maana ya msamaha, na huku kupewa Roho kwa kujibu maombi kumeonyeshwa katika namna ya toba ya kiyahudi ya karne ya kwanza na siku za mwisho. kwa maneno hayo hayo yenyewe ayasemayo Paulo, "Karama na mwito wa Mungu" kufikia toba na msamaha (Rum. 11 29). MSAIDIZI Kukaribia huko huko kunaweza kutumika katika ahadi ya msaidizi katika milango ya Yohana 14: na 16. Kimsingi huyu alitajwa ni nguvu zenye miujiza walizopewa wafuasi, ambao waliahidiwa hapo kwanza, pia ahadi inaweza kutuhusu nasi katika maana isiyo na miujiza. Karama zilikuwa kwa "Kuwakumbusha mambo yote, niliyowaambia" (Yoh. 14:26), kwa kuthubutu kuwezesha kuandika taarifa za Injili. Neno "kuwakumbusha" lenyewe lawekea mipaka jambo lenye miujiza ya ahadi ya msaidizi kwa wafuasi, walioishi na Yesu wakati wa utumishi wake. Waliweza kuwa na maneno ya Yesu tu yaliyorudi katika kumbukumbu zao na msaidizi. Lugha ya ahadi ya'Msaidizi’ inatumika pia katika uwezo wa Biblia iliyokamilika. Kwa sababu hiyo tunaweza kumalizia ya kuwa hizi na ahadi nyingine za Roho zilitumika katika mfano wa miujiza kwenye karne ya kwanza, lakini sasa yatuhusu sisi katika ufunuo wa Roho kwa njia ya neno la Mungu lililoandikwa katika Biblia. Bila shaka, ni kweli kwamba Roho ya Mungu ilidhihirika katika neno lililoandikwa zamani, lakini hili ulikuwa ni ufunuo wa sehemu ukilinganishwa na utimilizo ("Ukamilifu") ambao sasa tunao katika neno la Mungu lililokamilika (1 Kor.13:9 -13). kwa sababu hii ni kwamba haujakuwepo ufunuo wowote mwingine ulioandikwa toka kwa Mungu baada ya kuondolewa karama mara Agano Jipya lilipokamilika. Kadhia za kitabu cha Wamormoni na vingine kama hivi vilivyochapishwa, vinadokeza kwamba Biblia si ufunuo uliotimilika - kutokuwepo karama za roho leo kunathibitisha ni hivyo. Kama tunataka kuutumia utimizo wote wa Mungu katika ufunuo wake ulio katika Biblia, yatupasa tutumie kila sehemu yake, sehemu zote mbili Agano la Kale na Agano Jipya, wakati huo tu mtu wa Mungu anaweza kuanza kuwa kamili kama ukamilifu wa Mungu, uliodhihirika katika neno. |