Misingi Ya BIBLIA Somo La 2: Roho ya Mungu Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali |
2.2 Maongozi ya MunguRoho ya Mungu tumeifafanua ya kwamba ni Uweza wake, Mawazo, Maelekeo au tabia ambayo anaifunua kwa matendo yanayofanywa na Roho yake. Tulitaja katika sehemu iliyotangulia jinsi gani Roho ya Mungu ilionekana kazini katika uumbaji: " Hizi mbingu hupambwa kwa Roho yake" (Ayubu. 26:13) -Roho ya Mungu ikatua juu ya uso wa maji kuleta viumbe vilivyopo (Mwa. 1:2). Hata hivyo tunasoma kwamba'Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, na jeshi lake lote . (Zab. 33:6). Kama ilivyoonyeshwa mfano wa taarifa iliyo katika mwanzo ya Kuwa 'Mungu alisema’ vitu viliumbwa, vikatokea. Kwa hiyo, Roho ya Mungu imeonyeshwa sana kabisa neno lake - kadri maneno yetu yanavyoonyesha mawazo yetu ya ndani na matakwa - yetu halisi kwa usahihi kabisa. Kwa busara Yesu alisema'Kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake’ (Mathayo. 12:34) Basi, kama tunataka kutawala maneno yetu, kabla ya yote yatupasa tugeuze mawazo yetu. Hivyo neno la Mungu, ni wazo la Roho yake au mawazo. Hii ni baraka ya kwamba katika Biblia tuna maneno ya Mungu yameandikwa ili tuweze kuifahamu Roho ya Mungu au nia yake. Mungu alifanya muujiza huu kwa kueleza Roho yake katika maneno yaliyoandikwa kwa njia ya KUVUVIWA. Neno hili msingi wake umezunguka neno'Roho’ KUVUVIWA -KUONGOZWA NA ROHO "Roho" inamaanisha "Pumzi" au kupumua, "Kuvuviwa" maana yake ni " Kupuliziwa Pumzi". Hapa pana maana ya kwamba maneno ambayo watu waliandika "Wakivuviwa" toka Mungu yalikuwa ni maneno ya Roho ya Mungu. Paulo alimtia moyo Timotheo kwamba asijione kuwa mzoefu wa Biblia hata asahau ukweli kwamba ni maneno ya Roho wa Mungu, na kwa sababu hiyo tumepewa yote ambayo twahitaji ili kwamba tuwe na elimu ya kweli katika kumjua Mungu:-
Ikiwa kuvuviwa na maandiko kunaweza kutoa elimu ya jumla, basi haipo haja ya kuwa na 'Nuru ya ndani’ nyingine ya kutuonyesha ukweli juu ya Mungu. Lakini ni mara ngapi watu husema mawazo yao wenyewe na ujuzi kuwa ndio chanzo cha wao kumjua Mungu ! ikiwa linakubalika neno lenye kuvuviwa na Mungu kikamilifu linatosha kumwandaa mtu katika maisha ya Ukristo, hakuna haja ya nguvu nyingine ya haki katika maisha yetu. Kama ipo hii haja, basi neno la Mungu halijatuandaa kikamilifu, kama Paulo alivyotuahidi Kuwa litafanya hivyo. Kushika Bibilia mikononi mwetu na kuamini kwamba Biblia ni neno la Roho ya Mungu huchukua imani nyingine kabisa. Israeli walivutwa kusikiliza kile ambacho Mungu katika neno lake, kama ilivyo kwa "Wakristo" wengi siku hizi. Sisi sote tunahitaji kwa uangalifu kuwaza katika Waebrania 4:2:-
Badala ya kusimama katika imani timilifu iliyo kwenye nguvu za Roho / neno la Mungu lililosikiwa, Kiroho ni rahisi kuvutwa na kuchukua njia ya mkato. Kwa kudhani kwamba nguvu ya haki hutujia ghafla juu yetu itakayo tufanya tubadilike mbele za Mungu, kuliko kujua inabidi kupata uchungu wa kuyaleta maisha yetu kutii neno laMungu, kwa hiyo kuruhusu roho ya Mungu ivute mioyo yetu kwa kweli. Kutopenda kufahamu mno nguvu kubwa za kiroho zilizo ndani ya neno la Mungu matokeo yake'Wakristo’wamediliki kuhoji ikiwa maandiko yote tele yameandikwa kwa uongozi wa roho ya Mungu. Wamedokeza kwamba mengi sana tuyasomayo ndani ya Biblia yameandikwa na watu wenye busara zamani kwa mawazo yao tu. Lakini kwa matokeo, Petro anakomesha mawazo ya maneno ya jinsi hii:-
"Zaidi ya yote" yatupasa tuamini kwamba Biblia imeandikwa kwa uongozi wa Mungu.kwa sababu hii tumeifanya kuwa mlango wa msingi mmoja katika mapatano ya maneno yanayoelezea mashauri ya Imani ya Kristadelfiani (Christadelphlan statement of faith) WAANDISHI WA BIBLIA Kwa hiyo, ni muhimu kabisa kuwa na imani thabiti ya kuwa maandiko yamekuja kwa kuvuviwa na Mungu;bila kuzuiwa na mtu, Waandishi wa Biblia walivuviwa na Roho, kwa sababu hii waliyoandika hayakuwa yao wenyewe. Kwa kuwa neno ndio kweli (Yoh.17:17) linakaripia na kuadibisha (2 Tim.3:16 -17), kwa watu wengi, sio ajabu kuona kwamba neno haliwaelimishi - maana ukweli unauma.Nabii Yeremia alisumbuka sana kutokana na upinzani alioupata kwa sababu ya kusema maneno yaliyovuviwa na Mungu, basi aliamua asiyaandike wala kutangaza maneno aliyopewa. Lakini basi kuandika neno la Mungu ni zao la mapenzi ya Mungu kuliko matakwa ya mwanadamu,'Akaongozwa na Roho ya Mungu’ kwa hiyo akawa hana uchaguzi wa jambo hili.'Umenihadaa, Nami nimehadaika……Nami nikasema sitamtaja wala sitasema tena kwa jina lake, basi ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, Nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia’. (Yer. 20:7,9). Vivyo hivyo, Balaamu alipotaka kuwalaani Israeli, Roho ya Mungu ikamfanya awabariki badala yake (Hes. 24:1 -13; Kum.23:5) idadi ya kushangaza ya watu ambao Mungu aliwaongoza kutamka neno lake, walipita kwenye vipindi vya kutopenda kufanya hivyo. Orodha ni ya kuvutia:- Musa (Kut. 4:10) Ezekieli (Ezek. 3:14) Yona (Yon. 1:2,3) Paulo (Mdo. 18:9) Timotheo (1 Tim. 4:6 -14) Balaamu (Hes. 22:24) Yote hayo yanatudhibitishia tulichojifunza katika 2 Pet. 1:19 -21 ya kwamba neno la Mungu si wazo la watu binafsi, bali ni sababu ya watu kuvuviwa kuandika yaliyofunuliwa kwao. Nabii Amosi alinena "Bwana Mungu amesema, ni nani awezaye neno ila kutabiri ?" (Amosi 3:8) kwa kitambo, Musa alipoteza akili yake mwenyewe, Kule kuvuviwa kwake na Mungu kulikuwa na nguvu sana: "Maagizo hayo yote Bwana alimwambia Musa……." (Hes. 15:22, 23); maneno haya yalisemwa na Musa hasa (mstari wa 17) Ushahidi mwingine wa maendeleo haya ni kwamba waandishi wa Biblia hawakutambua kikamilifu mambo waliyokuwa wanaandika. walitafuta maana ya tafsiri sahihi -'Wakafunuliwa kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo’ waliyoandika (1Petro. 1: 9-12) maneno waliyoandika hasa, hayakuwa ni tafsiri yao wenyewe, bali hayo waliyochunguza. Yafuatayo yanatoa mifano iliyodhahiri:- Daniel (Dan. 12:8 -10) Zakaria (Zak. 4:4 -13) Petro (Matendo 10:17) Kama watu hawa walivuviwa kwa sehemu tu, basi hatuna njia ya kulifikia neno la kweli au Roho ya Mungu.Ikiwa hakika lile waliloandika lilikuwa neno la Mungu, basi, kwa hiyo iliwabidi waingiliwe kikamilifu na Roho ya Mungu wakati wa kipindi cha kuvuviwa pengine neno la Mungu lisingekuwa limehakikishwa. Kufahamu kwamba neno la Mungu ni la kale kabisa, linatupatia zaidi kusudi la kusoma na kutii.'neno lako limesafika sana, kwa hiyo mtumishi wako amelipenda’ (Zab. 119:140) Kwa hiyo, vitabu vya Biblia ni kazi yake Mungu kwa njia ya Roho yake, kuliko Kuwa na vitabu vya watu.Ukweli wa jambo hili umeonyeshwa kwa kupima jinsi Agano jipya linavyoshuhudia maandishi ya Agano la Kale:- -Math. 2:5 panasemwa ni jinsi gani 'yaliandikwa na manabii’ Mungu alikuwa anaandika kwa kupitia kwao. ‘Roho Mtakatifu alivyonena kwa kinywa cha Daudi….’ (Mdo. 1:16) -Hivi ndivyo petro alivyonukuu toka Zaburi: linganisha na (Ebra. 3:7) -‘Roho Mtakatifu alinena vema kwa kinywa cha Nabii Isaya’ (mdo. 28:25 - ndivyo alinukuu Paulo katika Isaya (Luk 3:4) anasema kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya kuliko kusema, Kitabu cha Isaya tu. Kwa hiyo wanadamu waliobuni vitabu vya Biblia hawakuwa muhimu kulingana na Wakristo wa kwanza, Ukweli ni kwamba maneno yao yalivuviwa na Roho ya Mungu na ndiyo iliyokuwa ya maana. Tutamalizia sehemu hii kwa orodha ya mistari inayoonyesha Kuwa Roho ya Mungu imefunuliwa kwetu ndani ya neno lake lililoandikwa:- -Yesu alisema wazi wazi,'Maneno hayo niliyowaambia……. Ni Roho’ (Yoh. 6:63);Alisema ni ya kuvuviwa toka kwa Mungu. (Yoh. 17:8, 14:10). -Tumesemwa ya Kuwa tumezaliwa mara ya Pili pande mbili kwa Roho (Yoh. 3:3-5) na kwa neno la Mungu (1Pet. 1:23) -‘Tazama nitawamwagia Roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu’ (Mith. 1:23) yanatia pamoja kufahamu neno la Mungu kweli na tendo la Roho yake juu yetu kusoma kitabu bila kuelewa yaliyoandikwa hakuna faida, kwa kuwa Roho / nia ya Mungu huwa hatujafunuliwa. Kuna usawa kati ya Roho ya Mungu na neno lake katika mafungu ya maneno: " Roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako …." (Isaya 59:21)‘Kwa ajili ya neno lako, na kwa moyo wako mwenyewe (Roho)’ (2 Sam. 7:21); 'Nami nitatia Roho yangu ndani yenu (katika mioyo yenu, tazama maneno yenyewe)…; Nitatia sheria yangu ndani yao …… na katika mioyo yao nitaiandika’ (Ezek. 36:27, Yer.31:33). UWEZA WA NENO LA MUNGU Roho ya mungu haishuhudii nia yake / madaraka peke, bali pia ni nguvu ambayo yaelezea mawazo hayo, ya kuwa neno /Roho yake sio tu ni taarifa yake; vile vile kuna nguvu inayofanya kazi katika neno hilo Kuufahamu ukweli uweza huo kutatufanya tuwe na shauku kuutumia; mawazo yoyote ya kutuzuia kusonga mbele yaliyo pamoja na kufanya hivyo yatashindwa kwa elimu yetu na kutii neno la Mungu kutatupatia nguvu tunazohitaji kusonga mbele kutoka mambo madogo ya maisha haya, kuelekea kwenye wokovu. Kutokana na mengi yaliyompata, Paulo aliandika:- " Siionei haya Injili (Neno) ya kristo: maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu" (Rum.1:16) Luka 1:37 ameandika jambo lile lile " Hakuna neno (Roho) lisilowezekana kwa Mungu". Kwa hiyo, kujifunza Biblia na kuyaelewa kuyatumia katika maisha yetu ni mwendo unaoendelea. Hauhusiani kabisa na bila kuwa mwema , kujaribu kufundisha elimu ya kibinadamu na vile vile Ukristo wa makanisa mengi wa kujisikia vema, ambako maneno machache yananukuliwa kifupi, lakini hakuna juhudi imefanywa ili kufahamu au kuyatumia. "Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu" 'Kwa amri (Neno) la Uweza (wa Mungu)’ (Ebr. 4:12; 1:3).'Neno la ujumbe wa Mungu ….. litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini’ (1Thes. 2:13). Kwa neno, Mungu anafanya kazi katika mioyo ya waumini wa kweli, kila saa ya siku. Ujumbe -Msingi wa Injili unaojifunza basi ni uweza kweli wa Mungu; kama ukiuruhusu kweli kufanya hivyo, Injili inaweza kufanya kazi katika maisha yako na kukubadili; uwe mtoto wa Mungu, ukionyesha Roho / nia ya Mungu kwa kiwango fulani katika maisha haya, ukiandaliwa katika badiliko la kupata mwili wa kiroho wa Mungu Kristo atakaporudi (2Pet. 1:4). Mahubiri ya Paulo yalikuwa katika "Kuonyesha dalili ya Roho na nguvu" (1Kor. 2:4). Tumezungukwa na hao wenye imani nusu katika Biblia kuwa ni Neno la Mungu, mbali na madai ya kumtumikia Kristo. Kwa mfano mmoja wanadai wanamwamini Mungu, Lakini wanashindwa kufahamu kwamba yeye anaishi kweli. Kwa kukana kabisa kuwa maandiko yamevuviwa, na ukuu wake juu ya mwazo na nia zetu, wanakana nguvu za Mungu. Maneno ya 2 Tim 3:5 yanatujia akilini:'Wenye mfano wa utauwa, lakini wanakana nguvu zake’ yaani, nguvu za neno la Injili Msimamo wa imani yetu unadhihakiwa na ulimwengu ('Je ! unaamini kama hivyo, Unaamini ?’), ndivyo Paulo na kundi lake la wahubiri: "Kuhubiri neno la msalaba kwao wanapotea ni upuuzi, bali sisi kwetu tunaookolewa ni nguvu ya Mungu" (1Kor.1:18) Tukikumbuka haya yote, hatuwezi kila mmoja kushika Biblia mikononi mwetu na kipimo kikumbwa cha kuiheshimu, kuisoma na shauku zaidi ya kufahamu na kutii. ?. MWENENDO WA WATU WA MUNGU KATIKA NENO LAKE Kusoma haraka taarifa za Biblia zaonyesha kwamba waandishi wa Biblia sio tu walitambua kwamba walivuviwa, bali waliwaona waandishi wengine wa Biblia kuwa wanaongozwa na Mungu. Bwana Yesu alikuwa ni bora zaidi katika jambo hili. Yesu aliponukuu toka Zaburi na Daudi, alianza maneno "Daudi katika Roho ……" (Math. 22:43), akionyesha kutambua kwake ukweli wa kwamba maneno ya Daudi yalivuviwa. Vile vile aliyasema," Maandishi" ya Musa (Yoh. 5:45-47), kwa kuonyesha kwamba alimwamini Musa kuwa aliandika vitabu vitano. (Pentateuch). Wakristo waitwao watafuta makosawakuu katika Biblia wamekuwa na shaka ikiwa Musa aliweza kuandika, lakini ni dhahiri mwenendo wa Kristo unapingana na njia zao. Aliyaita maandishi ya Musa kuwa ni 'amri ya Mungu’ (Marko. 7:8,9)Kundi hilo hilo la wenye mashaka wasioamini wanadai kwamba mengi yaliyo kwenye Agano la Kale ni hadithi, Yesu alisema Malikia wa sheba ukiwa ni ukweli unaofahamika kihistoria (Math. 12:42); hakusema, 'kuwa ni hadithi inayoendelea juu ya Malikia wa sheba ….’ Mwenendo wa Mitume ulikuwa wa hali moja na wa Bwana wao. Umeandikwa kifupi na Petro aliyesema ya kwamba uzoefu wake mwenyewe kusikia maneno ya Kristo kwa masikio yake mwenyewe alipatwa na'Lile neno la Unabii lililo imara zaidi’ (2Pet. 1:19-21). Petro aliamini kwamba nyaraka za Paulo yalikuwa ni'Maandiko’ zaidi kama'Maandiko mengine’ msemo ambao kwa kawaida umetumika juu ya Agano la kale maandishi yake. Hivyo, Petro aliona nyaraka za Paulo kuwa ni zenye mamlaka kama Agano la Kale. Yapo mengi ambayo yametajwa katika matendo, Nyaraka na ufunuo katika Injili (kwa mfano, linganisha (Mdo 13:51, Math. 10:14) yakionyesha sio tu kwamba yote yalivuviwa na Roho yeye yule, bali kwamba taarifa za Injili ziliandikwa kwa uongozi wa Mungu na waandishi wa Agano Jipya. Paulo katika (1 Tim. 5:18) ananukuu sehemu mbili Kum.25:4 (katika Agano la Kale) na Luka 10:7 kuwa ni'Andiko’. Paulo alifanya kazi nzito ya maana kwamba ujumbe wake ulitoka kwa Kristo, sio kwake mwenyewe (Gal. 1:11 -12; 1 Kor. 2:13; 11:23; 15:3) kazi yake ilitambuliwa na mitume wengine, hivyo Yakobo 4:5 ananukuu maneno ya Paulo kwa Gal. 5:17 kuwa ni "Andiko" Mungu 'amesema’ nasi kwa Kristo; kwa hiyo hatuna haja na Ufunuo mwingine zaidi (Ebr. 1:2). Yaweza kuonekana kuwa Biblia inataja maandishi mengine yaliyovuviwa yasiyopatikana sasa. (k.m. kitabu cha Yasheri, maandishi ya Nathani, Paulo kwa Wakorintho na waraka wa tatu wa Yohana unadokeza kwamba Yohana aliandika barua ambayo haikutunzwa katika kanisa ambalo Diotrefe alikataa kutii). Ni kwa sababu gani maandishi haya hayakutunzwa kwa ajili yetu ? Ni dhahiri, kwa kuwa mambo yenyewe hayakuwa yanatuhusu sisi. Mara nyingine imedaiwa kwamba pole pole vitabu vya Agano Jipya vikakubalika kuwa vilivuviwa, Lakini ni hakika kwamba Mitume waliona maandishi ya kila mwingine kuwa yalivuviwa haikosi huku ni kudhibitisha uongo. Ilikuwepo miujiza ya kipawa cha Roho ili kupima ikiwa nyaraka na maneno yaliyodaiwa kuvuviwa kuwa kweli yalikuwa hivyo (1Kor. 14:37, 1Yoh. 4:1, Uf. 2:2). Hii ina maana kwamba nyaraka zilizovuviwa mara moja zilifahamika kuwa zimeandikwa kwa uongozi wa Mungu. Kama ulikuwepo uchaguzi wowote wa Mwanadamu asiyeongozwa kwa yale yaliyoingia katika Biblia yetu, ndipo kitabu kisingekuwa na Mamlaka. |