Misingi Ya BIBLIA Somo La 2: Roho ya Mungu Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali |
Tumeacha Kitambo sehemu ya 5: Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni MtuWengine itakuwa vigumu kufahamu maelezo ya kawaida yanayomtaja Ibilisi kuwa ni kiumbe au mtu, kwa sababu Ibilisi ametajwa mara nyingi katika Biblia kana kwamba ni mtu, labda maelezo haya yanawachanganya watu wengine. Haya kwa urahisi yameelezwa kwa kuonya kuwa ni sura za Biblia zilizotambulika za kwamba kitu kisicho na uhai kama Hekima, Mali, Dhambi, na Kanisa vyote hivi vinatajwa kana kwamba ni mtu, lakini katika suala la Ibilisi pekee baadhi ya nadharia za kuwazika tu zimetungwa kuzunguka pande zote. Mifano ifuatayo itaeleza kiini:- HEKIMA IMEITWA KAMA MTU "Heri mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye anathamani kuliko marijani, wala vyote uvitamanivyo havilingani naye" (Mithali 3:13 -15). "Hekima ameijenga nyumba yake, amezichonga nguzo zake saba" (Mith. 9:1) Mafungu haya ya maneno, kwa kweli sura zilizobaki ambamo yanaonekana, yanaonyesha ya kwamba hekima imeitwa kana kwamba ni mtu kama mwanamke katika Biblia ya kiingereza, bali kwa sababu hii, hakuna mtu anayewaza ya kuwa hekima ni mwanamke halisi mzuri anayetembea akizunguka pande zote za dunia; wote wanajua kwamba ni tabia ya kutamanika sana ambayo watu wote walijaribu kujipatia. MALI IMEITWA KANA KWAMBA NI MTU. "Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili: kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mali" (Mith. 6:24). Hapa tunasoma Mali imefananishwa na Bwana. Watu wengi wanajitahidi mno kupa ta mali na kwa njia hii anakuwa ni Bwana wao. Yesu anatuambia hapa ya kwamba hatuwezi kufanya hivyo na halafu kumtumikia Mungu inavyostahili wakati huo huo. Fundisho ni jepesi lenye maana, lakini hakuna mtu awaye yote anayekubali toka hili ya kwamba mali ni mtu aliye na jina. DHAMBI IMETAJWA KAMA NI MTU "…… kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi" (Yoh. 8:34). " Dhambi imetawala katika mauti" (Rum. 5:21). "Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki" (Rum. 6:16) Kama ilivyo katika suala la Mali, dhambi imelinganishwa hapa na Bwana, nao wale watendao dhambi ni watumwa wake. Si usomaji mzuri kwa fungu la maneno linalothibitisha kwa kukubali ya kwamba Paulo anafundisha ya kuwa dhambi ni mtu. ROHO IMEITWA KANA KWAMBA NI MTU FULANI "Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote: kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe …" (Yoh. 16:13). Hapa, Yesu aliwaambia mwanafunzi wake ya kwamba watapokea nguvu za Roho Mtakatifu, nalo jambo hili lilitimia kwenye siku ya Pentekoste, kama lilivyoandikwa katika matendo 2:3 -4, mahali ambapo pamesemwa ya kuwa "Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto, uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa "Roho Mtakatifu" kwamba mamlaka yao itakuwa kwa Mungu. Roho Mtakatifu hakuwa mtu fulani bali ilikuwa ni nguvu, na Yesu alipokuwa anainena alitumia tamshi lake'Yeye’. MAUTI IMEITWA KAMA MTU "Tazama, farasi ya rangi ya kijivu jivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti" (Ufunuo. 6:8) TAIFA LA ISRAELI LIMEITWA KANA KWAMBA MTU "Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako ……" (Yer. 31:4).'Hakika nimesikia Efraimu, akijililia hivi; umeniadhibu nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizolea nira; unigeuze, nami nitageuzwa; kwa maana wewe u Bwana, Mungu wangu’ (Yer. 31:18). Fungu lenyewe la maneno haya linafunua dhahiri ya kwamba nabii hamtaji bikira halisi au Efraimu akiwa ni mtu, bali ni taifa la Israeli, ambalo katika mfano huu limetajwa kana kwamba ni mtu. WAAMINIO KATIKA KRISTO WAMEITWA KANA KWAMBA NI MTU MMOJA "Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata kuwa'Mtu’ mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo" (Ef. 4:13)."Upo mwili mmoja" (Ef. 4:4) "Ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake" (1Kor. 12:27). "……Kristo ni kichwa cha Kanisa: naye ni mwokozi wa mwili" (Ef. 5:23). "Naye (Kristo ndiye kichwa cha mwili; ….. sasa anayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake,yaani, Kanisa lake" (Ko.. 1:18,24). "Nimewaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi" (2 Kor. 11:2) " …..harusi ya mwana kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari" (Uf. 19:7) Ni bayana haya hizi zote zataja jamii ya watu waliokuwa waumini wa kweli wa Kristo, mara nyingine wametajwa ya kuwa ni'Kanisa’ Ingawa hili halipaswi kujumuishwa na makanisa yoyote ya kiorthodox yaliyopo siku hizi, ambayo ni muda mrefu yamekoma kuwa ni ya waumini wa kweli kwa Kristo. Waumini wa kweli, yaani, wanaoshika na kuamini mafundisho ya kweli yaliyofundishwa katika Biblia, mara nyingine wametajwa kuwa ni "Bikira safi" wakionyesha usafi wa maisha wanayoendea'Kama mwili’ mfano unaofaa kwa kuwa kiasi kama mwili wa asili ulivyo na viungo vingi, vivyo kanisa la kweli lina majukumu mengi na kufanya kazi mbali mbali. Kanisa linaposhuhudiwa kuwa ni "Mwili", hakuna mtu anayekosea maana ya mtu mmoja mmoja, wala watafanya kosa juu ya Ibilisi au shetani maana ya upuuzi kuwa ni mtu asiye na desturi ya kawaida au malaika aliyetupwa, wanawake hawakupata mawazo mabaya toka katika makanisa yaliyopotoka kwa siku zilizopita. Yametengenezwa katika "Ufalme wa wakristo Umepotoka" (Christeridom Astray) na Robert Roberts. |