Misingi Ya BIBLIA
Somo La 2: Roho ya Mungu
Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 6: Mambo ya kelvini

Miaka mia chache iliyopita, Kelvini alifundisha wazo la kwamba uteuzi ulikuwepo katika maisha yetu hapo kabla, hivyo basi uchaguzi wa kufanya tupendavyo kwa hiyari hauna juhudi juu ya wokovu wetu; aidha tulikwishachaguliwa kabla ili tupate wokovu au kukataliwa. wazo hili tena limeweka sura mpya katika mashauri mengine siku hizi:

kama hakuna maana kufanya bidii kubwa ya kujifunza Biblia au dini, kwa sababu kama tunaokolewa basi tutakuwa namna yoyote.

Ya kama yupo kiumbe aitwaye Ibilisi atulazimishaye kutenda dhambi na kuleta matata katika maisha yetu bila kujali mapenzi yetu. Wazo hili lisilo la kweli limejadiliwa katika somo la 6.

Ya kama hakuna haja kuomba matunzo ya Mungu katika hali ya maisha yetu, kama kulindwa wakati wa safari, kwa kuwa namna yoyote kila jambo lilikwisha pangwa. Walimwengu wana msemo, mara nyingi limesikika kwa bahati katika vyumba vya kuondokea wasafiri uwanja wa ndege,'Kama namba yako itatokea, itatokea tu’.

Makanisa ya kiinjili yanafundisha ya kwamba kwa muumini haiwezekani au kufahamu Biblia bila Roho Mtakatifu kutusaidia tuelewe.

Zipo sababu nyingi kamili za Biblia za kukataa hii aina ya elimu : -

Wazo lote la kumtii Mungu linafanywa kuwa ni upuuzi. tunaendelea kuambiwa siku zote katika Biblia kwamba yatupasa kutunza amri za Mungu, na kwa kufanya hivyo tunaweza kumpendeza au kutompendeza. Jambo hili lenye maagizo halina maana ikiwa Mungu anatulazimisha tumtii. Kristo anatoa wokovu kwa "Watu wote wanaomtii" (Ebra. 5:9).

Waebrania 11 yaonyesha kwamba Mungu anapoingilia katikati ya maisha yetu na hatimaye kutupatia wokovu kumehusisha na imani yetu. Mifano mingi ya Biblia kuomba wokovu wa Mungu shida haiwi na maana kama kila jambo lilikwisha pangwa kabisa. Vivyo hivyo wazo la wokovu likiwa ni toleo la imani yetu kwa Kristo haliwi na maana tena.

Ubatizo ni sharti la wokovu (Marko. 16:16; Yoh. 3:3 -5). Hili wenye imani ya Kelvini wamekana. lakini, wokovu umewezekana kwa sababu ya kazi ya Kristo (2Tim.1:10), si kupitia wazo la kuwazika la kuchaguliwa kabla ya wakati . yatupasa sisi wenyewe kwa ufahamu tuchague kujiunga naye, mpango tunaofanya kwa kubatizwa. Mafungu ya maneno katika warumi 6:15 -17 yanatunena tunavyobadili mabwana katika Ubatizo, toka maisha ya dhambi hadi kuwa mtu wa kutii. "Kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yeye mnayemtii". Lugha hii ya kujitoa mtu mwenyewe ni dhahiri inadokeza mapenzi ya hiari kama yalipopingana na kwisha chaguliwa kusiko na sharti. Kujitoa ni kwa kutii katika moyo mafunzo ya Injili (Rum. 6:17).

Hakuna maana kwa Mungu kutoa neno lake, kama namna yoyote tulikwisha chaguliwa. tena hakuna maana ya kuhubiri; lakini Biblia, pande zote mbili katika amri na kuandika mifano ya hii, inaonyesha kwamba ni kwa kuhubiri neno hata wanaume na wanawake kufika katika wokovu. "…..Neno la wokovu huu" (Mdo. 13:26) inabidi lipelekwe kwa watu.

Tutahukumiwa sawa sawa na matendo yetu (Uf. 22:12). Kwa nini, kama kutenda kwetu matendo tupendayo si muhimu katika kulingana na wokovu ? Paulo alisema ya kwamba Wayahudi wamejihukumu wao wenyewe kuwa hawastahili uzima wa milele kwa kulikataa neno la Mungu (Mdo. 13:46). Walikuwa wanajihukumu wenyewe - Mungu hakuwazuia. kama tukisema ya kwamba Mungu amewachagua watu wengine tangu mwanzo kupata wokovu na wengine wahukumiwe, basi kwa matokeo Mungu anawashurutisha watu kuwa watenda dhambi, kwa jinsi hiyo hiyo kama alivyotaka kuwalazimisha watu kuwa wenye haki. Kwa sababu ya dhambi ya Adamu "Mauti imewafikia watu wote, maana wote wametenda dhambi" (Rum. 5:12). ndiyo maana watu hufa, ikiwa ni adhabu kwa ajili ya dhambi kwa maana nyingine katika kipindi kabla ya dhambi ya Adamu.

1 Kor. 10 na mafungu mengi mengine ya maneno yameshika mfano wa waliokuwa zamani waliwahi kuwa na uhusiano na Mungu, lakini wakati ule wakaanguka, yakiwa maonyo kwa waumini. Uhakika ni kwamba upo uwezekano wa kuanguka toka hali ya neema (Gal. 5:4) maana yake ni kwamba hapawezi kuwepo 'aliyewahi kuokolewa siku zote akiwa ameokolewa’ utaratibu wa wokovu kama unavyotakiwa na wenye imani ya Kelvini. Tukiendelea tu kushika mafundisho ya kweli tutaweza kuokolewa (1 Tim. 4:16).

Ni dhahiri Yesu alifundisha ya kwamba kuelewa neno la Mungu kunategemea hatua fulani iliyo juu ya bidii yetu kufanya tupendavyo. "Asomaye, na afahamu" (Mathayo. 24:15). Hivi tunajiruhusu wenyewe kufahamu neno - hatulazimishwi. kati ya hivi upo usawa wa maneno yaliyorudiwa mara nyingi na Yesu ya kuwa "Aliye na masikio yenye kusikia ……. Na asikie" au afahamu. Kwa sababu hii kuwa na masikio yanayosikia, kumelinganishwa na kusoma neno la Mungu. Kwa kuwa Roho ya Mungu kwa ukuu sana imedhihirika katika neno lake kwa upana ambao Yesu aliweza kusema kwamba maneno yake yenye kuvuviwa na Mungu ni "Roho" (Yoh. 6:63) haiwezekani kwamba roho ya Mungu itatenda kazi juu ya mwanadamu, bila neno lake, ili kumshurutisha mwanadamu kuwa mtii katika neno.

"Yeyote atakaye" na "ayatwae maji ya uzima bure" (Uf.22:17), kwa kuitikia neno la uzima lipatikanalo katika Injili. Kwa kweli, hapa, ni kupenda kutenda atakavyo mtu kuliko kuchaguliwa tangu mwanzo bila kufikiri haja yetu binafsi kupata wokovu. vivyo hivyo matendo 2:21 "Na itakuwa kila (awaye yote) atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa" kwa kubatizwa katika jina hilo.


   Back
Home
Back