Misingi Ya BIBLIA Somo La 2: Roho ya Mungu Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali |
2.1 UfafanuziMungu akiwa ni mtu halisi (ieleweke kuwa tunaposoma mtu hatuna maana kuwa ni Mwanadamu) kwa sababu hiyo anayo mawazo na hisia, basi itegemewe kuwa atakuwa na namna nyingine ya kushirikiana mawazo na nia yake pamoja nasi, watoto wake na kwa kutenda kazi katika maisha yetu kwa mfano ambao una tabia ya sifa yake.Mungu anafanya mambo yote haya kwa 'Roho’ yake kama tunataka kumjua Mungu na kuwa na uhusiano wenye matendo pamoja naye, tunahitaji kufahamu jinsi hii " Roho ya Mungu" na namna inavyotenda kazi. Sio vyepesi kafafanua neno 'Roho’ hasa lina maana gani, ikiwa uliwahi kwenda kwenye sherehe fulani, tuseme harusi, unaweza kutoa maelezo ya jinsi mambo yalivyokwenda 'Watu waliohudhuria walikuwa na Roho nzuri’ Kwa msemo huu tunaelewa Kuwa una maana kwamba watu walikuwa wakarimu, wenye tabia nzuri n.k. mambo yote hayo yanafanywa na neno 'Roho’ iliyokuwepo pale. Hali kadharika Roho ya Mungu kwa njia nyingine inafanya muhutasari wa kila jambo linalo muhusu yeye. Neno la Kiebrania lililotafsiriwa "Roho" kwa lugha yetu katika Agano la Kale kwa uwazi kabisa limefafanuliwa Kuwa ni "Pumzi" au "nguvu"; kwa hivi roho ya Mungu ni 'Pumzi’ yake, Nafsi ya Mungu kabisa, ikieleza mawazo yake. Tutatoa mifano ya neno 'Roho’ lilivyotumika kuhusu mawazo ya mtu mwingine au mapenzi katika somo la 4.3. Ni dhahiri kwamba Roho sio tu inataja tupu nguvu ya Mungu ni kutoka Warumi 15:19 "Nguvu ya Roho ya Mungu" Ni mafundisho ya Biblia yaliyo ya kawaida ya kwamba jinsi mtu afikirivyo anajieleza katika matendo yake (Mithali. 23:7, Mathayo. 12:34); mawazo kidogo ya matendo yetu wenyewe, yanadhibitisha jambo hili. Tunafikiria kitu fulani na kisha tunakitenda. "Roho" yetu au nia inaweza kuonyesha juu ya ukweli kwamba tunaumwa njaa na tunahaja na chakula. Tunaona ndizi zimo jikoni, hivyo nia ya'Roho’ wakati huo inabadilika na kuwa tendo. Tunanyoosha mkono na kuchukua ndizi, tunamenya na kula. mfano huu rahisi unaonyesha kwa sababu gani neno'Roho’ lina maana mbili zote Pumzi au Nia, na vile vile Nguvu.Roho yetu ya nafsi yetu, yanatajwa mawazo yetu na hivyo pia matendo tunayofanya ya kuonyesha mawazo hayo au mapenzi yaliyo ndani yetu. Kwa kadri ya utukufu zaidi, Roho ya Mungu ipo hivyo hivyo, ni nguvu inayoonyesha nafsi ya utu wake, mapenzi na kusudi. Mungu anafikiri na hivyo anatenda mambo. "………Kama vile nilivyoazimia (Yaani nilivyofikiria), ndivyo itakavyokuwa, na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea". NGUVU ZA MUNGU Mafungu mengi ya maneno yanaonyesha Roho ya Mungu na nguvu zake. Kwa kuumba Ulimwengu,’ Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, iwe Nuru:'ikawa nuru’ (Mwa.1:2,3) Roho ya Mungu ilikuwa ni nguvu / uweza ambao vitu vyote, kama Nuru viliumbwa.'Hizo mbingu hupambwa kwa Roho yake, mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio’ (Ayubu. 26:13).'Kwa neno la bwana mbingu zilifanyika: na jeshi lake kwa pumzi ya kinywa chake’ (Zab. 33:6). Basi, Roho ya Mungu ni maelezo ya:- Pumzi yake Neno lake Mkono wake Kwa hiyo ni kwa nguvu zake anafanya vitu vyote. Waumini huzaliwa mara ya pili kwa mapenzi yake (Yoh. 1:13). Ambayo ni Roho yake (Yoh. 3:3-5). Mapenzi yake yanafanya kazi kwa Roho. Akiunena uumbaji wote wa asili, tunasoma "Waipeleka Roho yako, wanaumbwa: nawe (kwa Roho yako) waufanya upya uso wa nchi" (Zab.104:30). Hii Roho / Nguvu vile vile inavihifadhi hai vitu vyote, sawa sawa na kuumbwa kwao. Ni rahisi kudhani kwamba maisha haya yamepatikana kwa bahati bila kuingizwa Roho ya Mungu. Ayubu, mtu aliyechoshwa na maisha haya, alikumbushwa na Nabii mwingine: "(Mungu) akajikusanyia Roho yake na pumzi zake; wenye mwili wote wataangamia pamoja, nao wanadamu watarejea Kuwa mavumbi"(Ayubu. 34:14,15).Alipoondoka katika bonde la mfano mmoja wa huzuni, Daudi alimwomba Mungu aendelee kumtegemeza na Roho hii, yaani, kuhifadhi uhai wake (Zab. 51:12). Tutaona katika somo la 4.3 Roho ambayo tumepewa sisi sote na viumbe inayohifadhi uhai wetu. Ndani yetu tuna "Pumzi ya Roho ya uhai" (Mwa. 7:22) tuliyopewa na Mungu wakati wa kuzaliwa (Zab. 104:30; Mwanzo. 2:7). Hivi inamfanya awe ni Mungu wa Roho za wenye mwili wote. (Hes. 27:16; linganisha Ebra. 12:9). Kwa Kuwa Mungu ni mwenye nguvu ya uhai unaohifadhi viumbe vyote, Roho yake ipo kila mahali. Daudi alitambua kwamba kwa Roho yake Mungu daima alikuwa naye popote pale alipokwenda, na kwa Roho/ Nguvu aliweza kujua kila kona ya moyo wa Daudi unavyofikiri. Hivyo, Roho ya Mungu ndio inamfanya awe kila mahali, ingawa yeye mwenyewe makao yake ni mbinguni.
Jambo hili likifahamika vema linatudhihirishia Mungu kuwa Mungu ni mwenye nguvu sana, Nafsi itendayo kazi, watu wengi wamepevuka wakiwa hawajui vema'Kusadiki kwa Mungu’, katika mioyo yao Mungu amekuwa na wazo tu akilini akiwa ni sanduku jeusi kumjua Mungu wa kweli na uwepo wake kabisa akituzunguka pande zote kwa roho yake, kunaweza kubadili sana wazo letu la uhai. Tumezungukwa na Roho yake,kila siku tunashuhudia matendo yake, yanayotufunulia Mungu alivyo. Kwa yote haya, Daudi alipata faraja kikamilifu nia yake ilipobadilika:"Maarifa hayo ni ya Ajabu; yanishinda mimi" (Zab. 139:6) Lakini majukumu huja na maarifa haya; inatubidi tufahamu kwamba matendo na mawazo yetu yapo wazi kwenye mtazamo wa Mungu. kama tunapima hali yetu mbele zake, hasa tukifikiria juu ya Ubatizo, tunahitaji kukumbuka hii moyoni. Maneno makuu ya Mungu kwa Yeremia yanatumika kwetu pia. Je! mtu yeyote aweza kujificha mahala pa siri, nisimwone? asema Bwana. Je! mbingu na nchi hazikujawa (Kwa Roho) nami (Yer.23:24) ROHO MTAKATIFU Tumeona ya kwamba Roho mtakatifu ni wazo pana kufahamu; ni nia na mwelekeo wake, pia ni nguvu inayoweka mawazo yake yafanye kazi. "Maana (Mtu) aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo - yaani, jinsi mtu anavyowaza moyoni ndivyo alivyo, (Mithali 23:7); hivyo basi, ndivyo Mungu mawazo yake yalivyo, kwa maana hiyo ndivyo ilivyo Roho yake (Yohana 4:24). Ingawa hii haina maana ya kwamba Mungu si yake mwenyewe (Tazama tumeacha kitambo tulichoandika sehemu ya 1). Kutusaidia kuelewa upana huu wa roho ya Mungu, mara nyingine tunasoma'Roho wake Mtakatifu’. Neno "Roho Mtakatifu" linapatikana karibu kila sehemu katika Agano Jipya peke yake. Biblia ya kiswahili maneno Roho ya Bwana na'Roho Mtakatifu’ yametumika wazi. Hili ni sawa na mafungu ya maneno'Roho ya Mungu’ au Roho ya Bwana. Hili lipo dhahiri katika maneno kama ya Matendo 2, yanatoa taarifa ya kumwagiwa mitume Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Petro alisema kwamba Unabii wa Yoel ulikuwa unatimia, ambapo imesemwa nitawamwagia'Roho yangu’ (Mdo. 2:17). Tena, katika Luk. 4:1 tunasoma habari ya kwamba Yesu "akiwa amejaa Roho Mtakatifu alirudi toka Yordani; baadae kwenye sura hiyo hiyo Yesu akasema Unabii wa Isaya 61 unatimia. "Roho ya Bwana Mungu i juu yangu"katika masuala yote mawili (na katika mengi mengine) Roho Mtakatifu amelinganishwa na neno lililo katika Agano la Kale "Roho ya Mungu". Fahamu vile vile ni jinsi gani Roho Mtakatifu alivyo sambamba na nguvu za Mungu kwenye mafungu ya maneno yafuatayo:-
Yesu mwenyewe "alitiwa mafuta ya Roho Mtakatifu, na nguvu" (Mdo. 10:38).
|