Misingi Ya BIBLIA
Somo La 2: Roho ya Mungu
Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali

2.3 Vipawa Vya Roho Mtakatifu

Kwa nyakati mbalimbali Mungu alipo shughulika na watu, alituma watumie nguvu zake ('Roho Mtakatifu’) hao watu. Lakini, nguvu hii haikuwa katika namna ya " Hundi isiyo ya maandishi" kama ilivyokuwa, kuwawezesha kutenda walivyotaka siku zote kutumia Roho huyu Mtakatifu ilikuwa ni kwa kusudi maalumu. Kazi ilipotimizwa vizuri, kipawa cha Roho Mtakatifu kiliondolewa. Yatupasa tukumbuke kwamba Roho ya Mungu hutenda kazi kwa njia ambayo inapelekea mbele kusudi lake lililo moyoni mwake. Mara nyingi lengo lake linaacha muhula mfupi wa mateso katika maisha ya watu ili kuleta karibu kusudi lake la muda mrefu (tazama somo la 6.1) hivyo hatumainiwi huyo Roho Mtakatifu kutumika kutuliza uchungu wa maisha haya katika mwanadamu. Chochote kitulizo hiki kinamalizwa, kitakuwa kwa ajili ya kusudi la hali ya juu kinachoelezea hali ya Mungu kwetu.

Msimamo wa Ukristo wa walio wengi umeonekana kwa namna tofauti kabisa katika Roho Mtakatifu siku hizi; fikira zimetolewa kama kumwamini Kristo kuna thamani fulani kwa sababu ya faida ya mwili, k.m. kuponywa wagonjwa, ambayo Roho Mtakatifu amedhaniwa atatoa uponyaji. Huu utaeleza ni kwa sababu gani nchi zenye vurugu ya vita kama Uganda wamejitokeza watu wanaodai wana vipawa vya Roho ya kuponya na kihistoria mara nyingi kadhia ya jinsi hii ni matukio yanayojitokeza wakati ule ule wanadamu wanapokuwa na shida kubwa. Hii ndani yake yenyewe yanaonyesha madai ya kuwa na Roho katika hali ya mashaka mengine; Ikiwa mtu anatafuta jambo la kumpatia maarifa hayo yaliyo bora kuliko mambo ya mwanadamu yalivyo, ni rahisi kudai limepatikana jambo lingine linalojaza hesabu.

‘Wakristo’ wengi siku hizi wanadai wana vipawa vya Roho ya kutenda miujiza, lakini wanapo ulizwa kuhusu nini hasa madhumni yao, wanadokeza maana isiyotumainiwa. Mungu ametoa Roho yake bila kutengwa kwa kutimiza jambo moja hasa, malengo yaliyo ainishwa. Kwa sababu hii wale ambao walikuwa na vipwa vya Roho walijua hasa watavitumia kwa jambo gani. Basi hawakufaulu tu kwa sehemu katika kufanikiwa kwao walipovitumia. Hii hutofautiana na kushindwa kwingi na matibabu nusu yaliyo na wale wanaodai kuwa na vipawa vya kuponya leo.

Mifano yote ifuatayo inaonyesha sababu dhahiri na mambo yaliyokuwa nyuma ya kupewa vipawa vya Roho. Hapakuwepo hata kidogo masuala haya yoyote yanayozungumziwa kuwa pamoja na vipawa, wala hawakuwepo wenye vipawa walioweza kuvitumia kiasi kama walivyoona inafaa. Kwa sababu tunazungumzia Roho ya Mungu, haidhaniwi kwamba watu waliongoza matumizi yake, kwa kuwa walipewa ili kufahamu matakwa fulani ya Mungu kwa namna yake maalumu, kuliko hivyo vya watu walivyotumia hivyo kwa kitambo (Linganisha Isaya 40:13)

-Mwanzoni katika historia ya Israeli, waliagizwa watengeneze hema lenye madoido, (‘Maskani’) ambalo ndani yake kutakuwa na madhabahu na vitu vitakatifu vingine vitaweza kutunzwa; maelezo yalitolewa jinsi ya kufanya vitu vyote vilivyokuwa vya lazima kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Kutimiza hii kazi,Mungu aliwapa watu fulani Roho yake 'Walijazwa Roho ya Hekima ili waweze kushona mavazi ya Haruni …..’ (Kut. 28:3)

-Mmoja wa watu hawa, Bezaleli, "Alijazwa Roho ya Mungu, katika hekima na Maarifa, na ujuzi wa kazi ya kila aina ….. kuwa fundi wa dhahabu, na …. Kukata vito kwa kutiwa mahali …. Na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote" (Kut. 31: 3 -5).

Kitabu cha Hesabu 11:14 -17 kinatupatia habari ya jinsi baadhi ya Roho /nguvu aliyopewa Musa ilichukuliwa toka kwake wakapewa wazee wa Israeli, kwa kusudi la kuwawezesha kuamua kwa usahihi manung’uniko ya watu na kumpunguzia mzigo Musa. Kabla ya kifo chake, kipawa cha Roho kiliamishwa kutoka kwake akapewa Yoshua ili kwamba, naye vile vile, aweze kuwaongoza watu wa Mungu kwa Uzuri (Kut. 34:9)

Tangu wakati ule watu wa Israeli walipoingia nchi yao hadi kupata mfalme wao wa kwanza (Sauli) waliongozwa na watu walioitwa waamuzi. Wakati wa kipindi hiki watu walionewa na adui zao, lakini kitabu cha waamuzi kimetupatia taarifa jinsi Roho ya Mungu ilivyowajilia baadhi ya waamuzi, kwa muujiza wawaokoe Israeli toka kwa wavamizi wao Othiniel (Amu. 3:10), Gideoni (Amu. 6:34) na Yefta (Amu. 11:29) hawa wanaonyesha mifano hii:-

Mwamuzi mwingine, Samsoni, alipewa Roho ya kumuua Simba

(Amu. 14:5,6); kuua watu 30 (Amu. 14:19) na kukata kamba alizofungwa (Amu. 15:14). Huyu'Roho Mtakatifu’ Hakuwa na Samsoni siku zote alimjilia kutimiza mambo dhahiri na kisha aliondolewa.

Mungu alipokuwa na ujumbe maalum na watu wake, Roho ilimwongoza mtu mmoja miongoni mwao kunena neno la Mungu. Ujumbe ulipokwisha, kipawa cha Roho ya kutamka kwa niaba ya Mungu kiliondolewa mara moja, matamshi ya mtu yanakuwa ni yake mwenyewe tena sio ya Mungu. Moja ya mifano mingi:-

"Roho ya Mungu ikamjia Zekaria ……naye akawaambia (Watu), Mungu asema hivi, kwa nini ninyi kuzihalifu amri za Bwana….? (2 Nyak. 24:20)

Mifano mingine tazama 2 Nyak. 15: 1,2 na Luk. 4:18,19.

Kutokana na jambo hili, inakuwa bayana kwamba kupokea kipawa cha kutumia Roho ya Mungu kwa kusudi maalumu haikuwa

Ni uhakika wa wokovu
Ni jambo lililodumu katika maisha yote ya mtu
Ni nguvu ya Roho iliyojificha ndani yao
Ni jambo fulani linalopatikana kwa mtu kusikia furaha moyoni mwake

Inabidi kusema kwamba kumekuwa na sababu nyingi zisizodhahiri kuhusu vipawa vya Roho mtakatifu. Watu wanadai hupokea Roho Mtakatifu, na katika kumbi nyingi za Injili mhubiri hupunga mikono ya 'Kupokea vipawa vya Roho’ mbele ya wale wanaoona 'Wanampokea Yesu’ lakini swali inabidi liulizwe, Vipawa gani ? yaonekana kwamba watu hawajui hasa ni kipawa gani wanacho. Samsoni alipewa kipawa cha Roho kuua Simba (Amu. 14:5,6); alipomwona mnyama akiunguruma alijua hasa ni Roho gani aliyopewa na kwa sababu gani. Moyoni mwake hakuwa na shaka yoyote. Hii ni tofauti ngumu kwa wale ambao siku hizi wanadai wamempokea Roho Mtakatifu, huku hawawezi kufanya tendo lolote lililodhahiri, wala kujua ni vipawa gani walivyodhani wanavyo.

Bila shaka hakuna njia nyingine bali kumalizia kwamba watu wa jinsi hii waliwahi kuwa na mkazo wa mawazo mioyoni yaliyounganika na Ukristo, na mzunguko uliofuata katika mwenendo wa maisha yao wakiwa wameachwa na fikira ngeni za upya ndani yao wenyewe. Wakijua hivi, wameshika maneno ya Biblia juu ya vipawa vya Roho Mtakatifu, wakimalizia kwa kusema "Hivi inanibidi kuona mambo yakitendeka ! naye mchungaji wao walio na furaha huwapapasa kichwani na kusema,'Ni sawa hasa !

Bwana asifiwe ! akitumia mambo haya kuwa ni 'Ushahidi’ anapojaribu kuwadhibitishia wengine wampokee Roho Mtakatifu. Chanzo cha dhihaka hii hutokana na kukosa kuielewa Biblia tangu mwanzo wa elimu aliyokuwa nayo mtu kabla ya 'Kuongoka’ kwao wanakodhania.Tunaposhindana na udanganyifu wa mawazo yetu wenyewe (Yer. 17:9), yatupasa tutunze nyayo zetu juu ya mwamba ulio Imara ya mambo ya Biblia. Hakuna humu kinachohitajika wazi zaidi kuliko kujifunza ni jinsi gani Roho ya Mungu hufanya kazi. sote tunapenda kuwaza Kuwa nguvu za Mungu zatenda kazi nasi katika maisha yetu. Lakini ni jinsi gani na kwa sababu gani anafanya hivyo ? Je ! tuna vipawa kweli vya Roho kama watu walio katika taarifa za Biblia ? kama kweli tunataka kumjua Mungu na Kuwa na uhusuiano ulio hai naye, tutatambua umuhimu unaofaa kuelewa mambo haya.

SABABU ZA KUWA NA VIPAWA KATIKA

KARNE YA KWANZA

Tunapokumbuka mambo makuu tuliyojifunza tayari kuhusu vipawa vya Roho ya Mungu, sasa tunageukia taarifa iliyomo katika Agano Jipya juu ya vipawa vya Roho vilivyokuwa na kanisa la Kwanza (Yaani, vikundi vya waumini walioishi kwenye kizazi kilichokuwapo baada ya kipindi cha Yesu.)

Kristo agizo lake la mwisho, kwa mitume lilikuwa kwenda ulimwenguni pote kuhubiri Injili (Marko.16:15,16). Walilitekeleza agizo hili, na neno la kifo chake Kristo na ufufuo katika ujumbe wao ndio ulikuwa wa Kwanza. Lakini kumbuka kwamba wakati ule halikuwapo Agano Jipya kama tunavyolijua. Kama walivyosimama maeneo ya sokoni na katika masinagogi wakinena kuhusu mtu huyu Yesu wa Nazareti, masimulizi yao yangeonekana ya ovyo -Juu ya seremala toka Israeli aliyekuwa mkamilifu, aliyekufa kisha kufufuliwa kwa utimilifu barabara Agano la kale lilivyotabiri, ambaye sasa alikuwa anawataka wabatizwe na kufuata mfano wake. Katika siku hizo, watu wengine tena walikuwa wanajaribu kuwajenga wafuuasi wa dhehebu. Ikabidi iwepo njia nyingine ya kuwathibitishia ulimwengu kwamba ujumbe ulio hubiriwa na Wakristo ulitoka kwa Mungu mwenyewe, wala si kutoka kwenye elimu ya kikundi cha wavuvi waliotoka Kaskazini mwa Israeli.

Katika siku zetu tunavutwa na taarifa za Aganao Jipya juu ya kazi na mafunzo ya Yesu ili tuhakikishe kwamba ujumbe wetu unatoka kwa Mungu; Lakini katika siku hizo, kabla halijaandikwa na kupatikana, wahubiri walikubaliwa kutumia uweza wa Mungu - Roho wake Mtakatifu ili kutokeza ukweli wa kile walichokuwa wanasema. Hii ilikuwa ni sababu bayana ya kutumia vipawa mbele ya macho ya Ulimwengu; kukosekana Agano Jipya lililoandikwa pia kulifanya iwe shida kwa makundi mapya ya waumini kupevuka katika Imani. Matatizo yaliyojitokeza mengi ya utendaji kati yao yasingelikuwa na ufumbuzi ulio wazi, kwa wao mwongozo ungelikuwa mdogo katika kukua ndani ya imani iliyo kwa Kristo. Basi, kwa sababu hizi, Vipawa vya Roho Mtakatifu vikapatikana ili waumini wa kwanza waongozwe katika ujumbe ulioandikwa kwa uongozi wa Mungu, mpaka taarifa ya Agano Jipya juu ya ujumbe huu na mafundisho ya Yesu yalipoweza kuandikwa na kusambazwa.

Kama ilivyokuwa, sababu hizi za kugawiwa Roho Mtakatifu kwa wingi ilikuwa dhahiri:-

-"(Yesu) alipopaa kwenda (Mbinguni) ….. akawapa wanadamu vipawa (vya Roho) ….Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma (ya kuhubiri) itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe" yaani waumini (Efe. 4:8,12).

-Basi Paulo aliwaandikia waumini waliokuwa Rumi, 'Natamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya Rohoni’, (Kipawa cha Roho) ili mfanywe imara (Rum. 1:11).

Kuhusu kutumia vipawa kwa kudhibitisha mahubiri ya Injili, tunasoma:-

"Injili yetu haikuwafikia kwa maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu na uthibitifu mwingi" kwa miujiza iliyotendeka (2 Thes. 1:5 linganisha 1:5,6)

-Paulo aliweza kutaja "Neno alilolitenda Kristo kwa kazi yangu, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo (la miujiza) kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu" (Rum. 15: 18,19)

-Kuhusu wanaohubiri Injili, tunasoma, "Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi na kwa mgawanyo ya Roho Mtakatifu" (Waebrania 2:4)

-Kampeni ya kuhubiri Injili kule Kipro ilionyesha maajabu, hata ikawa "Liwali alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastajabia mafundisho ya Bwana (Mdo. 13:12).

Maajabu yalimwongoza aheshimu kwa kweli mafunzo aliyoelimishwa. Vile vile pande za Ikonio, "Bwana … alilishuhudia neno la neema yake, akawajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao" (Mdo. 14:3)

Yote haya yameelezwa kwa kifupi juu ya utii wa mitume kufuatia yale waliyoambiwa wahubiri: " Wakatoka na kuhubiri kila mahali, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulidhibitisha neno kwa ishara zilizoambatana nalo" (Marko. 16:20).

MAMBO DHAHIRI KATIKA NYAKATI

ZA NAMNA YAKE MAALUM.

Kwa hiyo, hivi vipawa vya Roho vilitolewa ili kufanya mambo dhahiri katika nyakati za namna maalumu .hivi laonyesha kosa la kudai kwamba Kuwa na kipawa cha Roho ni maisha yote ya mtu. Mitume, akiwemo Petro, "Walijazwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekosti, baada ya Yesu kupaa (Mdo. 2:4) kwa hiyo waliweza kunena kwa Lugha ngeni ili kuanzisha kuhubiri Injili ya Kikristo kwa kuitangaza kwa watu. Wenye mamlaka walipojaribu kuwatia nguvuni, "Petro akajaa Roho Mtakatifu" akaweza kuwajibu na kuwadhibitishia …. (Mdo. 4:8). walipoachiwa toka gerezani wakaweza kuendelea kuhubiri kwa usaidizi wa vipawa -"Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakasema neno la Mungu kwa Ujasili" (Mdo. 4:31)

Msomaji mwangalifu ataona kwamba taarifa haisemi kwamba'Tayari walikuwa wamejaa Roho’ Walijazwa na Roho Mtakatifu kufanya mambo halisi, lakini ilibidi wajazwe tena ili kutimiza jambo lingine katika mpango wa Mungu. Paulo vile vile "Alijazwa Roho Mtakatifu" alipobatizwa, lakini miaka mingine baadae "alijazwa tena Roho Mtakatifu" ili kumwadibu mtu mwovu kwa kumpiga upofu (Matendo. 9: 17; 13:9)

Katika kusema vipawa vya miujiza, Paulo aliandika kwamba waumini wa kwanza walipata " Kadri ya kipimo cha kipawa chake Kristo" (Efe.4:7). Neno la Kiyunani 'Kadri ya kipimo’ maana yake "Sehemu ndogo au Kiasi". Yesu peke yake ndiye aliyekuwa na vipawa bila kipimo, yaani alikuwa na uhuru wote wa kutumia kama alivyotaka (Yoh. 3:34). Sasa tutafafanua hivyo vipawa vya Roho vinavyoonekana kutajwa zaidi walikuwa navyo katika karne ya kwanza.

VIPAWA VYA ROHO KATIKA KARNE YA KWANZA

UNABII

Neno la Kiyunani'Nabii’ maana yake ni mtu anayetabiri neno la Mungu kwa mambo yaliyombele kabla jambo halijatokea - Basi ni kusema kwamba ni mtu aliyevuviwa kunena maneno ya Mungu, ambayo katika vipindi yalikuwa yanatabiri matukio ya wakati ujao (tazama 2 Pet. 1:19 -21). Hivyo,'Manabii’ - hao walio na kipawa cha kutoa unabii 'Walitoka Yelusalemu kwenda Antioki. Akasimama mmoja wao aliyeitwa Agobo, naye alionyesha ishara kwa Roho ya Kuwa itakuwepo njaa kubwa ulimwenguni pote: ilitokea katika siku za Klaudio Kaisari. Ndipo wanafunzi, kila mtu kwa kadri ya uwezo wake waliamua kutuma msaada kwa ndugu’ (Mdo. 11: 27 -29). Aina hii ya Unabii dhahiri, wa hali ya juu. Ambao ulikuwa wazi na ukamilifu ulikuwa kwa miaka michache, unakosekana kabisa miongoni mwao ambao sasa wanadai wana kipawa cha unabii; kweli, ni hakika mno kuwa katika kanisa la kwanza hiki kipawa kilikuwemo kati yao kwa kweli, hata walitoa muda wao na pesa ili kukabiliana na shida iliyokuwa imetabiriwa. Mifano michache ya jambo la aina hii yaweza kupatikana makanisa yaitwayo leo'Yaliyojazwa Roho’.

UPONYAJI

Kwa Kuwa mitume walikuwa wanahubiri habari njema (Injili) ya ufalme ujao wa Mungu wenye ukamilifu duniani, walifaa wauthibitishe ujumbe wao kwa kuonyesha miujiza ambayo ilionjesha kwa sehemu kipindi hicho kitakachokuwa, hapo "Macho ya vipofu yatakapofumbuliwa na masikio ya viziwi yatapozibuliwa. Ndipo kilema ataruka …." (Isaya 35: 5- 6). Zaidi kuhusu hali ya mambo kwenye ufalme wa Mungu tazama somo la 5. Ufalme wa Mungu utakaposimikwa duniani, ahadi za jinsi hii kama hizi hazitatimia kwa nusu kipimo, wala ufalme kutokuwa halisi hapa au sivyo. Kwa hivyo uthibitisho wa Mungu kwa huo ujumbe waufalme ulikuwa katika nguvu, wazi wazi usioweza kukanushwa; kwa hoja hii mingi ya miujiza ya uponyaji iliyofanywa na waumini wa kwanza ilikuwa machoni pa watu wote waweze kuona.

Mfano mashuhuri unapatikana pale Petro alipomponya mwombaji kilema aliyewekwa kila asubuhi penye mlango wa hekalu katika Matendo 3:2 tunasoma kuwa walimuweka kila siku - hivyo alizoeleka sana machoni pa watu. Akiisha ponywa kwa karama ya Roho iliyotumiwa na Petro, "Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda, akaingia ndani ya Hekalu pamoja nao akaenda kuruka ruka … watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu. Wakatambua ya Kuwa yeye ndiye alikuwa akiketi na kuomba sadaka kwenye mlango mzuri wa Hekalu; Basi, alipokuwa akiwashika Petro ….. watu wakamkusanyikia mbio katika tao … wakishangaa sana" (Matendo ya Mitume 3: 7 -11)

Ndipo Petro akaanza mara moja kusema kwa sauti kuhusu ufufuo wa Kristo. Wakiwa hawana la kuuliza, na wanapouona ushuhuda usiopingika mbele ya macho yao katika namna ya mwombaji aliyeponywa, tunaweza Kuwa na hakika ya kwamba waliyaelewa maneno ya Petro Kuwa yametoka kwa Mungu. Mlangoni mwa Hekalu "Saa ya Kusali" (Mdo. 3:1) Watu walikuwa wamesongamana, kama kwenye duka watu wanavyosongamana. Ilikuwa ni mahala kama hapo, Mungu alichagua kudhibitisha mahubiri ya neno lake kwa Muujiza huu uliodhahiri. Vivyo hivyo katika matendo 5:12 tunasoma ya kwamba "Kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu". Kadhia zifanywazo na wapentekosti wanaoponya na wengineo huzunguka mambo yaliyotokea pembeni mwa makanisa, kuliko njiani palipo wazi ili watu waone, na katika mkusanyiko wa'Waumini’ walio katika hali ya Roho ya kutazamia'Ishara’itokee, kuliko mbele ya watu wote wenye mioyo migumu.

Acha isemwe hii nafasi kwamba mwandishi wa sasa amekuwa na ujuzi mkubwa wa kujadili matukio haya na wanaodai siku hizi wamekuwa na Roho. Vile vile kwa kushuhudia kadhia nyingi za walio na Roho. Lakini 'Ushuhuda wangu mwenyewe’ wa kuona uponyaji mwingi ni ambao hauko dhahiri, na katika tiba nzuri sana kwa sehemu, haitakiwi kuwa katika mwendo wa kuzidi kutia maelezo; Mshirika yeyote wa makanisa haya mwaminifu atakubali kwamba mengi ya haya yanaendelea. Kwa nafasi nyingi nimezungumza na rafiki zangu wapentekoste wazuri, "Sio kwamba sipendi kuamini kuwa unaweza kuwa na uweza huu mkubwa. Lakini Mungu katika nyakati zote ni bayana ameonyesha ni nani aliye na nguvu zake na nani hana; hivyo si vibaya kwangu kukuuliza hali ya mafundisho yako, ambayo kwa sasa siwezi kwa kuwa hayawezi kupatana na maandiko" Kamwe hujawa bayana 'Kufafanua Roho na Nguvu’ kwa kunieleza mimi.

Kwa namna nyingine kabisa na kwa kufikiri kwangu, Wayahudi wenye msimamo mkali wa karne ya kwanza walifunga mioyo yao katika uwezekano wa kwamba wakristo walikuwa na vipawa vya kufanya miujiza ya Roho ya Mungu. Lakini hata hivyo iliwabidi wakubali, "Mtu huyu anafanya Ishara nyingi" (Yoh. 11: 47) na "Ishara mashuhuri imefanywa nao … ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu; wala hatuwezi kuikana" (Mdo. 4:16). Vivyo hivyo wale waliosikia mitume wakinena kwa lugha' Walishikwa na fadhaa" (Mdo. 2:6). Wapentekoste waongeao bila busara siku hizi hawafanyi hivyo. Ukweli ni kwamba watu wameweka katika hali inayofaa sana kwa 'Wapentekosti’ wa sasa na kuweza kukana kwamba kwa kweli wanatimiza miujiza, hapana shaka ni hatua ya maana kwa mjadala huu. kama ishara moja tu imekuwa ni habari kuu Yerusalemu pote, Je ! si haki kutoa shauri la kwamba ikiwa muujiza wa kweli ulifanywa Uingereza au bustani iliyo Nairobi, wakati huo kungekuwa na kutambua ya kwamba vipawa vyenye miujiza ya Roho ya Mungu vipo leo ? Badala yake, Wapentekosti wanangojea ulimwengu ushikilie aina zifuatazo za 'Ushahidi’ kuwa ndio sababu zao za kuamini :-

-(Hatimaye) kuponywa vidonda vya tumbo; njia ya kupona imedhaniwa ilianza baada ya mkutano wa maombi.

-Sehemu za mwili zilizolemaa kunyooka.

-Macho au Masikio yakipona, ingawa mara nyingi hali hurudi kama awali.

-Kuondolewa misiba mwilini.

Katika mifano hii inabidi kujumlisha kwa kusema kuwa magari ya kubebea wagonjwa yaliwachukua wagonjwa toka Hospitali hadi kituo cha Krusedi ya uponyaji cha T.O Osborn kilicho Nairobi, nchini Kenya; Madereva walikabiliwa na mashaka ikiwa wakae au warudi, walisalia - vile vile wagonjwa hawakupata ahueni yoyote.

Hata hivyo changamoto inataka watu waje kwenye mikutano hii kama matangazo yasemavyo:-" Njooni mtarajie Muujiza" kwa matakwa ya Roho ya binadamu namna zote hatua imepangwa inayotoa shauri yenyewe kama mfano huu. Hakuna mahala popote katika Agano Jipya panapodokeza kidogo mambo haya mengi ya matakwa ya Roho ya binadamu yenye lugha laini iliyohitajika kabla ya kutokea Muujiza au ishara. Ni dhahiri kwamba baadhi ya wale walioponywa katika karne ya kwanza hawakuwa na imani - k.m. mtu mmoja hakumjua Yesu alikuwa ni nani (Yoh. 5: 13; 9:36) .

Mfano mmoja wa Roho ya kuhoji -hoji unatimizwa na akili iliyopotoka na maombi yanayorudiwa mara ya pili, Sauti za ngoma na mziki wenye sauti. hapawezi kuwa na shaka kama ya busara yoyote kumjua Mungu - na jambo lolote lingine - kwa yote hayo yapo nje ya maana. mwandishi ameweza kukumbuka alivyohudhuria mikutano kadhaa katika sehemu mbali mbali, kila wakati alijisikia kuumwa kichwa kutokana na bidii ya kuendelea kuwa na busara iliyo sawa sawa, Ufahamu wa Biblia kwa kukabili jaribu la kutaka kupotezwa na mlio wa Ngoma na kupiga makofi. Kama yote hayo yanaonekana kuwa ya lazima kutangulia kabla ya kufanywa "Ishara" ya Wapentekosti basi ni ushahidi wa kutosha kwamba 'Uponyaji’ ni matokeo ya hangaiko la moyo na kutengenezwa Roho ya mwanadamu, kuliko shughuli moja kwa moja ya Roho ya Mungu. Kwa namna nyingine kabisa, Petro aliweza kutumia karama ya kweli ya ishara kwa kuponya watu walipolala katika njia kuu (Mdo. 5:15); Kutumia Paulo karama zenye miujiza mwenyewe alishuhudiwa na mtumishi wa Serikali asiyeamini (Mdo. 13: 12,13), vile vile na wapagani walioishi katika mji wa Listra (Mdo. 14: 8 - 13). Kama zilivyotakiwa kwa kusudi kabisa na hali ya karama za Roho, mambo ya uponyaji yalifanywa hadharani, na kwa njia yoyote hakukuwa na dalili ya kusita na maelezo mengine yoyote ila kukubali ya kwamba hapa kuna nguvu za Mungu zinazoonyeshwa dhahirii na watumishi wake.

Tokeo moja ambalo Kristo alionyesha uponyaji wa miujiza lilikuwa jinsi hii "Wakastaajabu wote (Yaani walioona), wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuona kamwe" (Marko. 2:12).

LUGHA

Mitume, baadhi yao walikuwa ni wavuvi wasiotengenezwa vizuri (k.m. Kielimu), walipata agizo kubwa la kwenda ulimwenguni pote, wakahubiri Injili (Marko. 16: 15, 16).Labda wazo lao la kwanza hasa lilikuwa,‘Lakini sijui kusema lugha nyingine !’ kwa wao halikuwa suala la 'Sikujifunza vizuri lugha nilipokuwa shuleni’ maana hawakuwa na shule. Juu yao wote imeandikwa ya Kuwa ni'Watu wasio na elimu, na wasio na maarifa’ (Mdo. 4:13) lilipokuja jambo la aina hiyo. hata kwa wahubiri walioelimika zaidi (k.m Paulo), Lugha ilikuwa bado ni kikwazo kikubwa kushindana. walipofanyika waongofu, tegemezi walilohitaji Kuwa nalo ni juu ya kila mmoja kwa kujengana (Agano Jipya lilipokuwa bado halijaandikwa) maana yake ilikuwa kwamba kutokuelewana lugha na kila mmoja lilikuwa ni tatizo kubwa.

Katika kushinda hili, wakapewa karama ya kunena katika lugha ngeni (‘Ndimi’) na kuweza kuzifahamu. Ni bayana kuna upinzani kabisa kati ya mtazamo huu wa 'Ndimi’ na huu wa Wakristo wengi waliozaliwa mara ya pili, wanaoeleza matamshi yao yenye furaha katika sauti zisizotambulika Kuwa ni ndimi. Mtafaruku huu unaweza kuondolewa kwa kuonyesha kwamba Biblia inaposema "Ndimi" ni'lugha ngeni’.

Siku ya Pentekosti, ambayo ni sikukuu ya Wayahudi, mapema baada ya kupaa juu mbinguni Kristo, mitume " Wote walijazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kunena lugha nyingine ….. Makutano wakakutanika (Mara nyingine karama ikaonyeshwa !). wakiwa wameshikwa na furaha, kwa Kuwa kila mmoja aliwasikia akinena kwa lugha yake. Wakashangaa wote, wakastaajabu na kuambiana, Tazama, hawa watu wasemao si wagalilaya hao ? Waparthi, Wamedi … tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu … wakashangaa wote"(Matendo ya mitume 2: 4-12) Haielekei ya kwamba huu mkazo maradufu wa mshangao wa watu na kustaajabu kwao ulikuwa wa lazima ikiwa walisikia mambo yasiyo na maana tu yakinenwa na hao wenye kadhia ya Kuwa na karama siku hizi.; yanayozuka katika maneno madogo ya uchokozi au kutopendelea, kuliko mshangao na uthibitisho unaotokana na kufahamu maneno yaliyonenwa, yaliyoshuhudiwa katika matendo 2.

Katika matendo ya mitume 2: 4-11 lugha zilizoandikwa zipo bayana na sehemu nyingine ya maandiko ya Agano Jipya; maneno "Watu wa kila Taifa na Lugha" yametumika mara tano katika Ufunuo kwa kusema watu wote walio kwenye sayari -dunia hii (Uf. 7: 9, 10:11, 11:9, 13:7, 17:15).Neno la Kiyunani‘ Ulimi’linatokea katika toleo la Kiyunani la Agano la Kale (Liitwalo'Septuagint’) na maana ya lugha (tazama mwa. 10:5, Kum. 28:49, Dan. 1:4) - katika Biblia yetu ya Kiswahili Kum. 28:49 ni sawa na Kiyunani.

1 Kor. 14 ni orodha ya maagizo yahusuyo kutumia kipawa cha Ulimi; mstari. 21 unanukuu Isaya 28:11 kuhusu ni jinsi gani kipawa hiki kitatumika kwa kushuhudia juu ya Wayahudi:'Katika sheria imeandikwa, kwa midomo (Ulimi) ya watu wageni na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa’ Kwa awali Isaya 28:11 inataja wavamizi wa Israeli wakisema na wayahudi kwa lugha ("Ndimi") ambazo hawakuzifahamu. Usawa uliopo kati ya 'Ulimi’ na 'Midomo’ unaonyesha ya kwamba 'Ndimi’ zilikuwa ni lugha ngeni. vipo vionyesho vingi vingine katika 1 Kor. 14 vya kwamba "ndimi ni lugha ngeni. Sura hii ni hukumu ya Paulo iliyovuviwa yenyewe kuhusu matumizi mabaya ya karama yaliyokuwa yanafanywa katika kanisa la kwanza, kama hivi, yanatoa namna nyingi juu ya ufahamu wa karama za Ulimi na Unabii. Sasa tutajaribu kutoa jumla ya fafanuzi chache juu yake. Aya ya 37 ni mstari wa kufungua:-

"Mtu akijiona Kuwa ni nabii , au mtu wa Rohoni, ayatambue hayo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya Bwana"

Ikiwa mtu awaye yote anadai Kuwa na karama ya Roho, yampasa akubali kwamba maagizo yanayotangulia juu ya kutumia karama ni kwa kuvuviwa na Mungu. Awaye yote ambaye anaasi hizo amri leo basi ni dhahiri wanakubali kwamba wanaona inafaa kudharau maneno yaliyoandikwa kwa Uongozi wa Mungu.

Aya ya 11 -17:-

"Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.

Vivyo hivyo nanyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za Rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.

Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kutafsiri

Maana nikiomba kwa lugha, Roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.

Imekuwaje basi, Nitaomba kwa Roho, tena nitaomba kwa akili pia, nitaimba kwa Roho, tena nitaimba kwa akili pia.

Kwa maana wewe ukibariki kwa Roho, yeye aketiye mahali pa mjinga ataitikiaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hajui usemalo.

Maana ni kweli, wewe washukuruu vema,bali yule mwingine hajengwi.

Basi kunena kwa lugha ambayo wale walio katika ibada hawaelewi haina maana. "Kusema bila maana nzuri" hakufai, maana ni jinsi gani yaweza kusemwa "Amina" ya ukweli mwishoni mwa 'Sala’ iliyoundwa kwa kupayuka -payuka kusikoweza kufahamika ? kumbuka kwamba "Amina" maana yake "Iwe hivyo’ yaani, nakubali kabisa na kilichosemwa katika sala hii. kunena lugha isiyoeleweka mbele za ndugu zako haiwajengi, asema Paulo.

Ninaukumbuka ugawaji vitabu vidogo nje ya ya mkutano wa kufukuza maovu uliofanywa na Billy Graham,wakiombwa watu warudi tena katika Ukristo ambao msingi wake ni katika Biblia. Mwanamke aliyeshikwa na msisimko akajaribu kunivuta kwa maneno yake ya kwamba mafundisho yangu ya Kristadelfiani 'Yaliongozwa na Ibilisi’ kwa kupayuka katika 'lugha’ kwa muda wa dakika 10. Kwa namna yoyote sikuweza 'kujengwa’ na hiyo, kwa kweli jambo hili ndilo hasa lile Paulo aliagiza lisifanywe kabisa.

Aya ya 18:-

"Namshukuru Mungu ya Kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote"

Kwa sababu ya kusafiri kwake katika maeneo mbali mbali kumhubiri, Kristo, Paulo alihitaji karama ya lugha ('Ulimi’) zaidi kuliko wote.

Mstari wa 19:-

"Lakini katika Kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kumi kwa lugha".

Hivi ni wazi kabisa. Mimi nitafanya vema kumhubiri Kristo kwa sentensi chache zilizo katika lugha ya Kiswahili kuliko mimi kuhubiri masaa mengi kwa lugha ngeni - au kuongea maneno yasiyofahamika vema.

Mstari wa 22:-

"Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio bali kwao wasioamini, lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini bali kwao waaminio".

Kwa hiyo matumizi ya lugha yalitakiwa yatumike zaidi katika kwenda nje kuhubiri Injili. Lakini wote wenye kadhia ya kunena kwa 'Lugha’ watoka miongoni mwa makundi ya 'Waaminio’ au (Kwa kuonekana) kwa mmoja wao anayepata wakati akiwa peke yake. Upo ukosefu sugu kwa mifano ya watu hawa ya kuweza kunena kimaajabu kwa lugha ngeni ili kueneza Injili. Mwanzoni mwa miaka ya 1990

ulifunguka mlango mpana katika kuhubiri Injili ya Kristo pande za Ulaya Mashariki, Lakini makanisa (yanayojiita) ya 'Kiinjili’ ilibidi yagawe vitabu vyao vilivyo na lugha ya Kiingereza kwa sababu ya vizuizi vya lugha ! kwa kweli karama ya kunena kwa lugha mpya ingetumika ikiwa walikuwa nayo ? naye Mwinjilisti wa mikutano mikubwa Reinhardt Seiber, huku akiwa na kadhia ya kuwa na Roho kwa ajabu bado ilimbidi aseme na makutano kwa kumtumia mkalimani pande za Kampala, Uganda.

Aya ya 23:-

"Haya ! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, Je ! hawatasema ya kwamba mna wazimu ?"

Hili ndilo jambo hasa limetokea. Waislamu na wapagani pamoja wamedhihaki mwenedo wao wa ovyo (Upuuzi) wa hao wanaodai wanacho kipawa cha ulimi Afrika Magharibi pote. Hata mkristo aliye sawa akilini akitega sikio kuzunguka kona ya mkutano wa Wapentekoste atadhania ya kuwa washirika walikuwa na wazimu.

Aya ya 27:-

"Ikiwa mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, naye mtu mmoja atafsiri".

Watu wawili watatu ndio waliohitajika kunena wakati wa Ibada. Haielekei kwamba walikuwepo wenye lugha zaidi ya tatu tofauti zilizosemwa na wasikilizaji wowote. Ibada itakosa mshikamano wote muda mfupi ikiwa kila sentensi ya msemaji ikibidi itafsiriwe zaidi ya mara dufu. Ikiwa karama ya lugha imekuwepo kwenye mkutano uliofanyika katikati ya jiji la Dar -es -Salaam, wamehudhuria watu wanaoongea Kiswahili, na wengine ni Waingereza na Wajerumani wakiwa ni watalii waliohudhuria,

Wanenaji wanaweza kuanza :-

Mtumishi: Habari za jioni.

Lugha ya msemaji wa kwanza: Bon Soir (Kifaransa)

Lugha ya msemaji wa pili: Guten abend (Kijerumani)

Lakini kwa kawaida wanapaswa kunena " Kwa zamu", anaanza mmoja baadaye afuate mwingine. Utatokea mtafaruku kwao wakinena kwa wakati huo huo; lakini kwa sababu ya msimamo uliopo unaochochewa na mawazo ya 'Kunena kwa Lugha’, tukio linakutwa katika vichwa vya watu wengi wakati huo huo. Tumegundua kwamba mara mtu mmoja akianza, wengine nao upesi wanavutwa kufanya hivyo hivyo.

Karama ya Lugha mara nyingi ingetumika pamoja na hiyo ya kutoa Unabii, ili kwamba ujumbe uliovuviwa kutoka kwa Mungu utabiriwe (kwa kutumia kipawa cha kutoa Unabii) mfano wa kutumia jinsi hii vipawa viwili unaweza kupatikana katika

Mdo. 19:6. Lakini, ikiwa kwenye mkutano mjini Dar -es-Salaam ukihudhuriwa na watu wa Tanzania na wafaransa wengi wageni, msemaji akinena kwa kifaransa, watu wanaoongea kiswahili waliopo'Hawajengwi’. Kwa hiyo kipawa cha kutafsiri ulimi

(au Lugha) kingekuwepo, ili kwamba kila mmoja aweze kufahamu, kama -katika mfano wetu siku hizi, katika kutafsiri toka kifaransa kwenda kiswahili au Kifaransa kwenda kiingereza. Vivyo hivyo ikiwa swali limeulizwa na mtu anayeongea kifaransa, mnenaji hawezi kumwelewa bila msaada, hata kama alikuwa na karama ya kunena kwa kifaransa pasipo mwenyewe kukielewa. Kwa sababu hiyo kipawa cha kutafsiri kitakuwepo kusaidia suala hili.Bila kuwepo mtu mwenye kipawa cha kutafsiri kinapohitajika, kipawa cha ulimi hakitatumika:" …….. mmoja na afasiri. lakini asipokuwepo mwenye kutafsiri na anyamaze katika Kanisa (1 Kor. 14:27,28). Jambo la hakika ni kwamba watu wengi siku hizi walio na kadhia ya kuwa na Karama ya'Ulimi’ wananena kwa 'lugha’ ambazo haziwezi kueleweka na yeyote, na bila mwenye kutafsiri, ni hakika suala la uasi kwa maagizo haya.

Mstari wa 32, 33 :-

"Na Roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, Vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya Watakatifu."

Kwa hiyo tendo la kuwa na karama za Roho Mtakatifu lisitiwe pamoja na ujuzi anaomchukua mtu nje ya mambo ya ufahamu wa kawaida; Roho huwa chini ya uongozi wa mtumiaji, kuliko lazimisho linalo wachukua upande mwingine ili kwamba watende bila kujua mara nyingi kwa makosa imedaiwa kwamba mashetani au 'Roho wachafu’ huwamiliki'Wasiookoka’ (tazama somo la 6.3), Bali ni kwamba Roho Mtakatifu wanajazwa waaminio. Lakini nguvu za Roho zilizotajwa katika 1 Kor. 14:32 zilikuwa chini yake mwenye kuiongoza kwenye kusudi la namna yake maalum; haikuwa shurutisho hai la wema ikipambana na nguvu ya uovu iliyo ndani ya mwili wa mwanadamu. Isitoshe awali tumeonyesha ya kwamba nguvu hizi za Roho Mtakatifu ziliwajia mitume wakati fulani ili kufanya mambo ya namna yake maalum, si kuwa nazo daima.

Ombi kwa wenye Kuwa na karama watumie kwa namna inayofaa upendo na amani ya Mungu na kuchukia machafuko (aya ya 33) Laonekana limeangukia kwenye masikio ya viziwi katika makanisa ya wa -Pentekosti wa siku hizi.

Aya ya 34: -

"Wanawake wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii kama vile inenavyo torati nayo."

Katika fungu hili la kutumia karama za Roho, hakujawekwa kukatazwa ya kwamba wanawake wasitumie karama wakati wa ibada ya kanisa. kutoangalia hili kwa upana linatarajiwa ikiwa jambo lililopo la kunena kwa 'Machafuko ya kupayuka’ laweza kuelezewa kwa maneno ya kuchochewa mawazo likipita toka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika mkusanyiko wao. Wanawake, Watoto - na yeyote anayekuwapo kwa hiyari - anaweza kuambukizwa na msimamo wa jinsi hii, kwa hiyo wanafanya matamshi ya kusikia furaha moyoni, yanayoishia kuwa kama ni 'lugha’.

Wanawake wajitokezao kwa kusemwa 'Wananena kwa lugha' na 'kutoa Unabii’ katika makanisa ya sasa hawapatani na agizo lililo wazi la aya hii. Maneno ya Upuuzi, ambayo ni mabaya yatokayo kwa watu ya kwamba Paulo alikuwa mchukia wanawake yamezimwa kwa aya chache baadaye: "Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa Rohoni, na ayatambue haya ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo yatokayo kwa Bwana" (1Kor. 14:37) siyo ya kutoka kwa Paulo mwenyewe.

Awaye yote aaminiye Biblia kuwa imevuviwa, basi, inambidi akubali kwa maagizo haya yaliyo katika 1 Kor. 14 si ya kufanyia mchezo bayana wa kuyabeza; kufanya hivyo kunaashiria kutokuwa na imani ya kutosha katika maandiko kwamba yameandikwa kwa uongozi wa Mungu pekee - au maneno yenyewe yajieleze kwamba huyu mtu hana karama ya Roho, kwa kuwa mtu mwingine asiye na karama atakana kwamba maagizo yaliyo katika 1 Kor. 14 ni maagizo ya Bwana yaliyo kwa ajili yetu.

Kuwanza kwa akili timamu maneno haya yatuambia, yanaharibu sana. katika mwangaza huu, ni vipi uweze kusalia Kuwa mshirika wa kanisa hili,au kupenda kufanya ibada nao.

Maneno yakiwa chini ya kitabu kwa sehemu hii, ni yenye maana sana ya kwamba hayo madhehebu yenye kadhia ya kunena kwa lugha yamedhibitishwa kisayansi Kuwa na huzuni upesi kulinganishwa na watu walio katika malezi mengine. Keith Meador, Profesa wa magonjwa ya moyo katika chuo kikuu cha Vanderbilt, Marekani, alianza uchunguzi mkubwa kujifunza kuchanganua uhusiano uliopo kati ya huzuni iliyo moyoni na malezi yaliyo katika dini. Aligundua kwamba " Idadi kubwa ya wenye huzuni ….. miongoni mwa Wakristo wa madhehebu ya Kipentekosti ilikuwa 5.4% kulinganishwa na 1.7 % kwa uchunguzi wa kundi zima" matokeo ya kazi hii yameandikwa katika kitabu cha mambo ya kila siku, 'Hospital and Community Psychiatry, Des, 1992.’

Maandishi ya kuvutia katika ukurasa, yaliyofikiwa kwenye dhana hiyo hiyo baada ya kuchunguza sana, yalitokea katika jarida lingine liitwalo International Herald Tribune, la Feb. 11, 1993; na kichwa cha habari yenyewe: "Wapentekosti wapo orodha ya juu wanapokuja na huzuni" Ni kwa sababu gani wapo kwenye hali hii ? kwa kweli inabidi wawiane na uhakika wa kwamba 'Ujuzi unaojipatia’ wa tendo la Kuwa na Roho, ambao wapentekosti (na wengineo) wenye kadhia hii, si lolote zaidi ya Kuwa wanauchungu sana wa m ioyo yao dhidi ya mazoea.


   Back
Home
Back