Misingi Ya BIBLIA Somo La 6: Mungu Na Ubaya Mungu Na Ubaya | Ibilisi Na Shetani | Mapepo - Mashetani | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Uchawi, Edeni palitokea nini?, Lusifa, Majaribu ya Yesu, Vita Mbinguni) | Maswali |
6.1 Mungu Na UbayaMadhehebu mengi ya mataifa ya Kikristo, sambamba na dini nyingine nyingi wanaamini kwamba kuna kiumbe au mtu asiye wa kawaida aitwaye Ibilisi au shetani ambaye ni Muasisi wa matatizo yaliyomo ulimwenguni na katika maisha yetu, na ni anayehusika na dhambi tunazotenda. Ni wazi Biblia inafundisha kuwa Mungu ni mwenye nguvu zote. Tumeona somo la 1.4 kuwa Malaika hawatendi dhambi. Ikiwa kweli tunaamini mambo haya, basi haiwezekani kuwa yupo kiumbe asiyewakawaida anayefanya kazi hapa ulimwenguni anayepingana na mwenyezi Mungu. Kama tunaamini kuwa huyu kiumbe yupo, basi tunahoji ukuu wa Mungu mwenyezi. Toleo hili ni la lazima sana ya kuwa kumfahamu vema Ibilisi na shetani inabidi fundisho la muhimu lipimwe; Tumeambiwa kuwa Yesu alimharibu Ibilisi katika Ebra. 2: 14 kwa kifo chake; kwa hiyo tusipomwelewa vema Ibilisi, hatuwezi kuelewa kazi ya Yesu, au Yesu ni nani. Katika ulimwengu kwa ujumla, hasa unaoitwa ulimwengu wa'Kikristo’, lipo wazo la kuwa mambo mema katika maisha yanatoka kwa Mungu na mambo mabaya yanatoka kwa Ibilisi au shetani. Hili sio wazo jipya; sio wazo pekee lililokomea kwenye ukristo uliokengeuka. Kwa mfano, Wakaldayo, waliamini kuwepo Mungu wawili, Mungu wa mema na nuru na Mungu wa uovu na giza, na kwamba walishikana katika kupingana sana. Koreshi, Mfalme mkuu wa Uajemi, naye aliamini hivi. Basi Mungu akamwambia, "Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu ….. mimi naumba nuru, na kuumba (kuhuluku) giza: Mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya (uovu) - B.H.N -"balaa": Mimi BWANA, niyatendaye haya yote" (Isa. 45: 5-7, 22). Mungu anafanya amani, na ubaya,au balaa. Mungu ni muumba"Ubaya"Kwa maana hii ipo tofauti kati ya ubaya na dhambi,hivi ni kosa la binadamu; Vimeingia ulimwenguni kama tokeo la binadamu, sio Mungu (Rum. 5:12). Mungu anawaambia Koreshi na watu wa Babeli kuwa "hayupo Mungu (mwingine) zaidi yangu"Neno la Kiebrania lililotafsiriwa'EL’ na kuwa Mungu kwa ukubwa maana yake'nguvu au chanzo cha uweza’. Mungu anasema kwamba hakuna chanzo cha uweza kilichopo mbali ya yeye. Hii ndiyo sababu kwa nini mwamini wa kweli kwa Mungu hawezi kukubali wazo la kuwepo Ibilisi asiyewa kawaida au mapepo. MUNGU: MLETA BALAA Biblia imejaa mifano jinsi Mungu aletavyo "Ubaya" kwa maisha ya watu na katika ulimwengu huu. Amosi 3:6 anasema kwamba ukiwapo ubaya mjini, ni Mungu amefanya. Kwa mfano, kama likiwepo tetemeko la ardhi katika mji, mara nyingi imedhaniwa kwamba Ibilisi amepanga juu ya mji huo, na kuleta msiba mkuu. Lakini mwamini wa kweli inampasa afahamu kwamba ni Mungu anayehusika na tukio hili. Basi Mika 1:2 anasema kwamba "msiba -ubaya umeshuka toka kwa Bwana umefika mpaka lango la Yerusalemu". Katika kitabu cha Ayubu tunasoma jinsi Ayubu, mtu mwenye haki, alivyopoteza vitu alivyokuwa navyo katika maisha yake. kitabu kinafundisha kwamba kupata 'Ubaya’ katika maisha ya mtu sio moja kwa moja ni kipimo kwa utii wao au uasi juu ya Mungu. Ayubu aligundua hilo "Bwana alitoa, na Bwana ametwaa" (Ayubu. 1:21). Hasemi Bwana alitoa na shetani ametwaa. Alifafanua kwa mke wake: Je ? tupate me,a mikononi mwa Mungu, nasi (pia) tusipate na mabaya"? (Ayubu. 2:10). Mwishoni mwa kitabu, rafiki zake Ayubu walimfariji kwa habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake"(Ayubu. 42: 11; 19: 21; 8: 4). hivyo Mungu ndiye chanzo cha 'Uovu’ kwa maana ya kuwa ni wa kwanza kuruhusu matatizo ambayo tunayo katika maisha yetu. "Maana yeye ambaye Bwana ampenda humrudi ….. kama mkistshimili kurudiwa …. Lakini baadaye huwaleta wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani" (Ebra. 12: 6 -11). Hii inaonyesha kwamba majaribu ambayo Mungu anatupatia yanatuongoza mwisho kukua kiroho. ni kupinga neno la Mungu juu yake kusema kwamba Ibilisi ni kiumbe anayetulazimisha kutenda dhambi na kutenda yasiyo haki, Wakati huo huo amedhaniwa kuleta matatizo katika maisha yetu ambayo yanatupeleka tupate maendeleo "matunda ya haki yenye amani". Hapa wazo la Orthodox juu ya Ibilisi lakimbilia kwenye matatizo makubwa. Makubwa hasa unapoona maneno kama nimempa shetani watu hao "ili wafundishwe wasimtukane Mungu au" kumtolea shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu" (1 Tim. 1:20; 1 Kor. 5: 5). Ikiwa shetani ni kiumbe anayefanya watu watende dhambi na kuwa na matokeo yasiyofaa juu ya watu, ni kwa sababu gani mafungu haya ya maneno yasema'Shetani’ kwa nuru ya hakika ? Jibu lipo kwa ukweli kwamba adui,'shetani’ au shida katika maisha, mara nyingi inaweza kuleta matokeo ya hakika kiroho katika maisha ya mwamini. Kama tukikubali kwamba ubaya watoka kwa Mungu, Basi tunaweza kumwomba Mungu afanye jambo lingine kuhusu matatizo ambayo tunayo k. m ayaondoe. Kama hafanyi hivyo, basi, tunajua yametoka kwake Mungu kwa ajili yetu kiroho. Sasa kama tunaamini ya kwamba kuna kiumbe fulani mbaya anayeitwa Ibilisi au shetani anayesababisha matatizo yetu, Basi hakuna namna ya kupatana na mema. Ulemavu, Ugonjwa, Kifo cha ghfla au msiba mkuu uchukuliwe kuwa ni bahati mbaya. Ikiwa Ibilisi ni Malaika mwenye dhambi aliye na nguvu, basi atakuwa ni mwenye nguvu nyingi zaidi yetu, hatutakuwa na kuchagua bali kuteseka mikononi mwake. kwa kuhitilafiana, tunafarijiwa kuwa chini ya uongozi wa Mungu, "mambo yote (katika maisha) hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema"kwa waamini (Rum. 8:28). Kwa hiyo hakuna kitu kama hiki 'bahati’ katika maisha ya mwamini. ASILI YA DHAMBI Inabidi kusisitiza kwamba dhambi hutoka ndani yetu. Ni kosa letu hata kutenda dhambi. Bila shaka, ingekuwa vema kuamini kuwa halikuwa kosa letu hata tukitenda dhambi. kwa hiyari tungetenda dhambi na halafu kutoa udhuru wenyewe kwa kuwaza kwamba kweli lilikuwa kosa la Ibilisi na ya kuwa lawama kwa dhambi yetu ingewekwa kabisa juu yake. Sio ajabu sana kwamba katika kesi ya mwenendo mbaya sana, mtu mwenye kosa anaomba msamaha kwa kuwa anasema ya kwamba alishikwa na shetani kwa muda na kwa sababu hii yeye mwenyewe hahusiki. Lakini ni sawa kabisa, udhuru huu dhaifu unahukumiwa kwa sababu hauna msingi kabisa, na mtu anapotishiwa hukumu juu yake. Tukumbuke kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti" (Rum. 6:23); dhambi huleta kifo. Kama sio kosa letu kutenda dhambi, bali ni Ibilisi, Bali Mungu mwenye haki yampasa amwadhibu Ibilisi kuliko sisi. Lakini ukweli ni kwamba tunahukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu wenyewe yaonyesha tunahusika kwa dhambi zetu. Wazo la kwamba Ibilisi ni mtu dhahiri aliye nje yetu kuliko kwamba ni jambo la dhambi ndani yetu ni kujaribu kuondoa kuhusika kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini huu ni mfano mwingine watu wanapokataa kupatana na Biblia inapofundisha kuhusu mwili wa binadamu: huo kwa asili ni wenye dhambi.
Wazo la kwamba kipo kitu fulani nje yetu kinachotuingia na kutusababisha kufanya dhambi halilingani na mafundisho yaliyo wazi ya Yesu hapa. Toka ndani, ya moyo wa mtu, hutoka yote haya mambo mabaya. Hii ndiyo sababu wakati wa gharika, Mungu aliona kwamba "mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake"(Mwa. 8:21. Yak. 1:14) anatuambia namna tunavyojaribiwa:"Kila mmoja (yaani mwanadamu) hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa" Tunajaribiwa kwa tamaa zetu wenyewe, mawazo yetu mabaya; sio kitu kingine chochote nje yetu. "Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyo kati yenu" ?. Yakobo anauliza; "Si humu katika tamaa zenu ?" (Yak. 4:1). Kila mmoja wetu ana majaribu yake binafsi. yanazalishwa na nia zetu mbaya, kwa sababu ni yetu wenyewe. ukweli umesemwa ya kwamba sisi wenyewe ndio adui zaidi mbaya. Kitabu cha Warumi kwa upana kinahusika na dhambi, asili yake, na jinsi ya kuishinda. Ni muhimu sana kwamba Ibilisi na shetani hawapatikani sehemu walipotajwa katika kitabu hiki; kwa maneno ya kusema kuhusu asili ya dhambi, Paulo hamtaji Ibilisi au shetani. Kwa njia hiyo hiyo'Ibilisi’ ni dhana ya Agano Jipya. Kama yupo kiumbe aliye nje anayefanya tutende dhambi, kwa kweli asingetajwa kwa upana katika Agano la Kale ?. Bali upo ukimya wa maana uliokwenda chini kuhusu hili. Taarifa ya kipindi cha waamuzi au Israeli jangwani, zinaonyesha ya kwamba nyakati hizo Israeli walitenda dhambi sana. Lakini Mungu hakuwaonya kuhusu kiumbe mwenye nguvu kuwa atawaingia na kuwafanya watende dhambi. Badala yake, aliwasisitiza kushika neno lake, ili wasivutwe kwenda nje ya mapenzi yake na kuufuata mwili wao (K/Torati 27:9,10; Yoshua 22:5) Paulo analia:"Ndani ya mwili wangu halikai neno jema …. Kutenda lililo jema sipati ….. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ile dhambi ikaayo ndani yangu"(Rum. 7:18 -21). Kutenda kwake dhambi hamlaumu kiumbe aliye nje aitwaye Ibilisi. Anaweka kwenye mwili wake mbaya kuwa ndiko asili ya dhambi:"Sio mimi nafsi yangu, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu". Basi, nimeona sheria hii (ndani yangu), ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililojema, lipo lililo baya (yaani - ndani) yangu. Hivyo anasema kwamba kipingamizi cha kuwa kiroho kinatoka kwingine anapoita"dhambi ikaayo ndani yangu". kila mtu mwenye mawazo ya kunia kiroho atafikia kwenye mawazo hayo hayo. Ijulikane ya kwamba hata mkristo mkubwa kama Paulo hakuona badiliko la mwili baada ya kuongoka, wala hakuwekwa kwenye nafasi ambayo hawezi kufanya dhambi. Makundi ya siku hizi ya "Kiinjili" yanadai kwamba wapo katika nafasi hii ya kutotenda dhambi, kwa hivyo wanamweka Paulo vema ndani ya 'wasiookoka’ kwa sababu ya taarifa yake hapa katika Rum. 7: 15 -21. Mistari hii imewaletea shida kubwa kwa madai yao. Daudi, mwingine pasiposhaka mtu mwenye haki, vivyo hivyo alifafanua juu ya mwili wake kabisa mwelekeo wa daima wa dhambi: "Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu alichukuwa mimba hatiani - dhambini"(Zab. 51:5). Biblia ipo wazi kabisa kuhusu ukubwa na ubaya wa mwili wa binadamu. Kama hili likikubalika, hakuna haja ya kutafuta mtu wa kufikiriwa aliye nje ya mwanadamu anayehusika na dhambi zetu. Yer. 17: 9 unasema kwamba moyo wa binadamu huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote ambapo hauwezi hasa kukubali upana mbaya sana wa dhambi zake. Naye Yesu alitia alama pia mwili wa mwanadamu kwa asili ni mbaya katika Math. 7:11; Mhubiri 9:3 (andiko la Kiebrania) halikuweza kuwa wazi;"Moyo wa wanadamu umejaa uovu", Efe. 4:18 inatoa sababu ya mtu asili ya kutengwa toka kwa Mungu kuwa ni "kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao". Ni kwa sababu ya upofu wa kiroho na ujinga wa mioyo, njia zetu za kufikiri zilizo ndani yetu, ndizo zimetuweka mbali na Mungu. Pamoja na mstari huu, Gal. 5:19 unasema dhambi zetu kuwa ni"Matendo ya mwili"; ni mwili wetu wenyewe, utu wetu kabisa na umbo, ndivyo hutufanya tutende dhambi. Hakuna hata fungu la maneno linaloeleza asili ya dhambi ndani yetu kuwa zimekuwemo kwa sababu ya Ibilisi aliyeziweka; maelekeo ya dhambi ni mambo mengine ambayo kwa kawaida tunayo tangu kuzaliwa; ni sehemu kubwa ya umbo la mwanadamu. |