Tumeacha Kitambo sehemu ya 18: Edeni palitokea nini?
Mwanzo 3 mstari 4 -5:"nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa: Kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayo kula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Miungu, mkijua mema na mabaya"
TAFSIRI YA WATU WALIO WENGI:
Imeaaminika kwa ubaya kwamba hapa nyoka ni Malaika aliye asi, ameitwa"Shetani". Akiisha kutupwa toka mbingu kwa sababu ya dhambi zake, akaja duniani na kumjaribu Eva kutenda dhambi.
FAFANUZI:
Maneno ya shetani yamesema "nyoka" maneno "Shetani"na"Ibilisi" hayamo katika kitabu kizima cha mwanzo. Ukweli ni kwamba nyoka wana mwili kama sisi, wanatambaa kwa matumbo yao, ni ushahidi wa kwmba nyoka katika Edeni alikuwa mnyama halisi. Wanaoamini vingine wanathubutu kufikiri kwamba popote wanapomwona nyoka halisi wanakuwa wamemwona 'shetani’ mwenyewe.
Kamwe nyoka hajasemwa ni Malaika
Kwa hiyo haishangazi kwamba hakuna mstari katika mwanzo kwa yeyote kutupwa toka mbinguni.
Dhambi huleta mauti (Ru. 6: 23). Malaika hawezi kufa (Luk. 20: 35 -36), kwa hiyo Malaika hawatendi dhambi. Thawabu ya wenye haki ni kufanywa kuwa sawa na Malaika bila kufa tena (Luka 20:35 -36). Ikiwa Malaika waweza kutenda dhambi, ndipo na wenye haki nao wataweza kufanya dhambi na kwa hiyo watakuwa na uwezekano wa kufa, ina maana kwa kweli hawatakuwa na uzima wa milele.
Sifa zinazowatofautisha za wahusika kwa taarifa ya kitabu cha Mwanzo kuhusu kuanguka kwa mtu ni: Mungu, Adamu, Eva na nyoka. Hayupo mwingine aliyetajwa. Hakuna ushahidi kuwa kitu chochote kilimwingia nyoka kumfanya alichotenda.Paulo anasema nyoka"alimdanganya Hawa kwa hila yake"(2 Kor. 11: 3). Mungu alimwambia nyoka:"Kwa sababu umefanya hayo ….."(Mwa. 3:14). ikiwa "Shetani’ alikuwa anamtumia nyoka, ni kwa sababu gani hajatajwa na kwa nini naye hakuadhibiwa ?
Adamu alimlaumu Eva dhambi yake:"Huyo mwanamke ndiye aliyenipa matunda ya mti" (Mwa. 3: 12). Eva alimlaumu nyoka:"Nyoka alinidanganya, nikala" (Mwa. 3: 13). Nyoka hakumlaumu ibilisi - hakutoa udhuru.
Kama ikisisitizwa ya kwamba nyoka wa leo hawana uwezo wa kusema au fikira kama nyoka wa Edeni aliokuwa nao, kumbuka kwamba: -
Punda aliwahi kufanywa anene na kuhojiana na mtu (Balaamu): "Punda (wa kawaida) asiyeweza kusema, akanena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule (2 Pet. 2, 16) na
Nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote (Mwa. 3,1). Laana juu yake iliondoa uwezo wake wa kunena na Adamu na Hawa.
8.Mungu alimwambia nyoka (Mwa. 3, 1) mwingine aitwaye "Shetani"na kugeuka kuwa nyoka, kama tunasadiki hivi basi tuna maana ya kusema mtu fulani anaweza kuingia katika maisha ya mwingine na kumwongoza. Hili ni wazo la kipagani, sio la Biblia tu kama ukitiwa mkazo wa kwamba Mungu asingemuumba nyoka kwa sababu ya dhambi kubwa aliyomshawishi Adamu na Hawa kuitenda, kumbuka dhambi iliingia ulimwenguni kutoka kwa mtu (Rum. 5: 12); kwa hiyo nyoka kuwekwa kujua baya na jema alinena kutokana na kuangalia mwili wake, na kwa hivi hakuwa na la kujibu kwa Mungu na kwa sababu hii hakutenda dhambi.
Wengine wanadokeza kwamba nyoka wa Mwa. 3 amewiana na Maserafi. Walakini, neno la kawaida la Kiebrania"nyoka"ambalo limetumika katika Mwanzo 3, haliwiani kabisa na"Maserafi"Neno la Kiebrania lililotafsiriwa "Maserefi"kimsingi maana yake "Mkali"au wa moto na limetafsiriwa"nyoka za moto"katika Hesabu 21: 6, lakini sio neno lililotafsiriwa"nyoka" kwenye kitabu cha Mwanzo 3. Neno la Kiebrania shaba linakuja toka asili moja kama neno'nyoka’ katika mwanzo 3. Shaba inaelezwa au ni mfano wa dhambi (Amu. 16: 21; 2 Sam. 3: 34; 2 Fal. 25: 7; 2 Nyak. 33: 11; 36: 6), mistari hii yote ieleweke kwamba vifungo walivyokuwa wanafungwa navyo ni vya shaba, ukiwa na Biblia Habari njema sehemu zingine utakuta pameandikwa pingu za shaba lakini hii Biblia yetu tuliyoizoea ya Afrika Mashariki sentensi haimaliziwi na neno shaba. Hivyo nyoka aweza kuunganishwa na jambo la dhambi, lakini sio Malaika mwenye dhambi.
MAELEZO YALIYODOKEZWA kama maana ya mafungu haya ya maneno:
Hakuna sababu ya kuwa na shaka ya kile tulichoambiwa kuhusu uumbaji na kuanguka katika sura za kwanza kitabu cha mwanzo hizo habari zake zieleweke vivyo hivyo."Nyoka"alikuwa ni nyoka halisi. Ukweli tunaona nyoka wa leo kutambaa kwa tumbo ni utimilifu wa laana iliyowekwa juu ya nyoka wa kwanza (Mwa. 3,14), unathibitisha jambo hili. Vivyo hivyo twaona mwaume na mwanamke wakisumbuka kutokana na laana iliyowekwa juu yao wakati ule ule.Tunaweza kufahamu kuwa Adamu na Hawa walikuwa ni mwanaume na mwanamke kama tunavyojua mwanaume na mwanamke wa siku hizi, wakifurahia hali njema ya mwili wanao ishi nao, kwa hiyo nyoka wa kwanza alikuwa ni mnyama halisi, ingawa alikuwa mwerevu sana kuliko nyoka wa leo.
Vifuatavyo ni vielelezo vinavyoendelea kuwa sura ya kwanza kwa kitabu cha Mwanzo kisomwe kilivyo: -
Yesu alitaja taarifa ya uumbaji wa Adamu na Hawa ikiwa ni msingi wa Mafundisho yake juu ya ndoa na talaka (Math. 19: 5- 6); hakuna dokezo kuwa aliisoma kwa mfano.
"Maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Hawa. Adamu hakudanganywa (na nyoka), bali mwanamke alidanganywa na akaingia hali ya kukosa" (1 Tim. 2: 13 -14) - hivyo Paulo, naye, alisoma kitabu cha Mwanzo bila kukigeuza. Na ya muhimu zaidi aliandika mapema kuhusu namna "nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake" (2 Kor. 11: 3) - fahamu kwamba Paulo hamtaji ibilisi akimdanganya Hawa.
Je ! upo ushahidi wowote kabisa wa kwamba kuna kitu kingine pembeni kwenye taarifa ya uumbaji na kuanguka ambao usomwe kimfano ?. Ulimwenguni uliumbwa kwa siku sita kulingana na Mwanzo 1. Kama hizi zilikuwa ni siku halisi za masaaa 24 zimethibitishwa kwa ukweli wa kwamba vitu mbali mbali viliumbwa kwa siku tofauti zisingefaa kuwepo bila kila moja kwa namna yake zilivyopo kwa zaidi ya siku chache. Tena ni siku, havikuwa ni vipindi vyovyote vya miaka 1000, bali alikufa baada ya siku saba akiwa na umri wa miaka 930 (Mwa.5: 5). Ikiwa siku ya saba ilikuwa ni kipindi cha miaka 1000 basi Adamu angekuwa zaidi ya miaka 1000 alipokufa.
Ushahidi unaendelea wa siku halisi za uumbaji unaweza kukutwa katika sheria ya Sabato ya Kut 20: 10, 11. Sabato ilikuwa na saa 24 za kupumzika, kwa sababu Mungu alipumzika siku ya saba, akiisha fanya kazi kwa siku sita (kama Israeli walivyofanya kabla ya kutunza sabato yao). Kama mimea ingechipuka siku ya miaka ingetegemea nyuki n.k walioumbwa siku ya sita.. Kupishana kwa nafasi ndefu kati ya kuumbwa kwao kwa sababu hii haifai kutumika.
-
Kwa sababu nyoka alilaaniwa kwa kufanya atambae kwa tumbo lake (Mwa. 3: 14). Hii inaweza kudokeza kwamba awali alikuwa na miguu, pamoja na uwezo wake bayana na kuhojiana, labda umbo la maisha ya mnyama lilikaribiana na mtu ingawa bado alikuwa ni mnyama - jinsi moja na "Wanyama wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu" (Mwa. 3: 1 -14).
-
Labda nyoka alikula matunda ya mti wa ujuzi, ambao ulimweleza hila yake. Hawa "alipoona ule mti … ni mti wa kutamanika kwa maarifa" (Mwa. 3: 6). Ni jinsi gani aliweza kuuona huu, isipokuwa aliona matokeo ya kula matunda katika maisha ya mwingine aliyejifanya hivyo tayari ?. Yawezekana vema kwamba Hawa alifanya mazungumzo na nyoka kabla ya taarifa moja iliyo katika Mwa. 3.Taarifa ya maneno ya kwanza yaliyoandikwa ya nyoka kwa Eva ni,"Ati ! hivi ndivyo alivyosema Mungu ….." (Mwa. 3: 1) - neno 'Ati’ inawezekana kwamba linadokeza hili lilikuwa ni endelezo la mazungumzo yaliyotangulia ambayo hayajaandikwa.
|