Misingi Ya BIBLIA
Somo La 6: Mungu Na Ubaya
Mungu Na Ubaya | Ibilisi Na Shetani | Mapepo - Mashetani | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Uchawi, Edeni palitokea nini?, Lusifa, Majaribu ya Yesu, Vita Mbinguni) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 19: Lusifa

Kabla ya yote hili ni jina la mtu, lakini msomaji hutokuta linapatikana ndani ya Biblia zenu za kiswahili isipokuwa Biblia zingine za Kiingereza. ukifungua Biblia yako utaona nyota ya alfajiri sio Lusifa. Maneno yenyewe yameandikwa hivi: -

Isaya 14 mstari 12 -14: "Jinsi alivyoanguka kutoka mbinguni Ewe lusifa, mwana wa asubuhi. jinsi alivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa: Nawe ulisema moyoni mwako nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za Kasikazini: Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye aliye juu".

TAFSIRI YA WATU WALIO WENGI

Amesadikika kwamba Lusifa aliwahi kuwa Malaika mwenye nguvu aliyekosa wakati wa Adamu, kwa hiyo alitupwa chini duniani, ambako anawasumbua watu wa Mungu.

FAFANUZI: -

  1. Maneno hayo"Ibilisi", "Shetani"na "Malaika"hayamo katika sura hii. Hii ni sehemu pekee katika maandiko ambayo neno "Lusifa" limeonekana - lakini sio katika Biblia yetu ya Kiswahili.

  2. Haupo ushahidi wowote katika Isaya 14 unaoelezea jambo lolote lililotokea kwenye Bustani ya Edeni; kama upo, basi ni kwa sababu gani tumeachwa miaka 3000 toka wakati wa Mwanzo kabla ya kuambiwa sababu ya kweli iliyotokea pale ?

  3. Lusifa amesemwa amefunikwa na funza (mst. 11) na kudhihakiwa na watu (mst. 16) kwa sababu hana uwezo tena baada ya kutupwa toka mbinguni (mst. 5 -8); basi hakuna haki ya kudhani kwamba Lusifa sasa yupo duniani kuwapotosha waaminio.

  4. Ni kwa sababu gani Lusifa ameadhibiwa kwa ajili ya kusema kwamba "Nitapanda mpaka mbinguni" (mst. 13) ikiwa tayari aliwahi kuwapo kule ?

  5. Lusifa anaoza kaburini:"Fahari yako imeshushwa hata kuzimu ….., funza wametandazwa chini yako na vidudu vinakufunika"(mst. 11). Malaika hawawezi kufa (Luk. 20: 35 -36), kwa hiyo Lusifa hawezi kuwa Malaika; msemo umefaa sana kwa binadamu.

  6. Mstari wa 13 na 14 ina muungano na 2 Thes. 2: 3-4, ambayo inamuhusu "mtu wa kuasi"- huyu Lusifa anaonyesha mbele kwa mtu mwingine, sio Malaika.

MAELEZO YALIYOTOLEWA: -

  1. Tafsiri yetu ya Biblia imeanza andiko la Isaya sura za 13 -23 kuwa ni mfululizo wa "Ufunuo"juu ya mataifa mbalimbali, k.m. Babeli, Tiro na Misri. Isa. 14:4 inaanza kueleza fungu dogo la maneno ya mistari tunayoipima: "Utatunga mithali hii (mfano) juu ya mfalme wa Babeli …… ? Basi, unabii unamhusu mfalme mwanadamu wa Babeli, ambaye amesemwa ni "Lusifa". Kwa kuanguka kwake:"wao wakuonao …… watakuangalia sana, wakisema, Je ! huyu ndiye aliyeitetemesha dunia …. ?"(mst. 16). Kwa hivi Lusifa amebainishwa kuwa ni mtu.

  2. Kwa sababu Lusifa alikuwa mwanadamu mfalme,"Walio wakuu wote wa dunia …. Hao wote watakujibu na kukuambia, Je ! wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi ? wewe nawe umekuwa kama sisi ?" (Mst. 9 -10). Kwa hiyo Lusifa alikuwa mfalme kama mfalme yeyote mwingine.

  3. Mstari wa 20 unasema kwamba uzao wa Lusifa utaangamizwa. Mstari wa 22 unasema ya kuwa uzao wa Babeli utaharibiwa, hivi wao wanasawazishwa.

  4. Ukumbuke kwamba hii ni "Mithali juu ya mfalme wa Babeli"(mst. 4)"Lusifa" maana yake "nyota ya Asubuhi"ambayo inang’aa zaidi ya nyota zingine. Katika mfano, nyota hii kwa kiburi inaamua kupanda (kupaa) kwenda mbinguni …. Nitakiinua kiti changu juuu ya nyota zingine za Mungu" (mst. 13)Kwa sababu hii nyota inatupwa chini duniani. Nyota ni mfalme wa Babeli. Danieli mlango wa 4 unaeleza jinsi gani Nebukadreza mfalme wa Babeli kwa kiburi aliuchunguza ufalme mkuu alioujenga, akafikiri kwamba aliyashinda mataifa mengine kwa uwezo wake, Kuliko kutambua ya kwamba Mungu ndiye aliyempa mafanikio. "Ukuu wako umekuwa na kufika mpaka mbinguni"(mst. 22). Kwa sababu hii"alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege"(mst. 33). Kutwezwa huku ghafla kwa mmoja wa watu wa ulimwengu wenye nguvu sana na kutiwa wazimu lilikuwa ni tukio lisilotazamiwa ikahitajika mithali ya kuhusu kuanguka kwa nyota ya Asubuhi toka mbinguni kuja chini. Nyota ni mfano wa watu wenye nguvu, k.m. Mwa. 37:9; Isa. 13:10 (kuhusu viongozi wa Babeli); Ezek. 32: 7 (kuhusu kiongozi wa Misri); Dan. 8: 10, 24. Kupaa mbinguni na kuanguka toka mbinguni ni maneno yasiyotumika isivyokawaida mara nyingi yametumika kwa kuongezeka katika kiburi na kwa maana ya kushushwa - tazama Ayubu 20: 6; Yer. 51: 53 (kuhusu Babeli); Omb. 2: 1; Math. 11:23 (kuhusu Kapernaumu):"Nawe Kapernaumu, Je ! utakuzwa mbinguni ? utashushwa mpaka kuzimu"(kaburi).

  5. Mstari wa 17 analaumiwa Lusifa kwa kuufanya "Ulimwengu ukiwa, (kuuharibu) miji yake; asiyewafungua wafungwa wake waende kwao …..". Haya yote ni maelezo ya utaratibu wa jeshi la Babeli - likiteketeza eneo lote (kama walivyofanya kwenye mji wa Yerusalemu), wakiwahamisha mateka kwenda maeneo mengine bila kuwaruhusu warejee nchi zao (kama walivyowafanyia Wayahudi), Wakijenga miji mipya na kutwaa kodi ya dhahabu toka mataifa yaliyokandamizwa. Kwa hivi upo mkazo juu ya ukweli kwamba Lusifa hakupata maziko kama wafalme wengine walivyokuwa nayo (Mst. 18 -19), Ukidokeza kuwa alikuwa ni mfalme mwanadamu tu kama wao, kuona mwili wake ulihitajika kuzikwa.

  6. Mstari wa 12 unasema kwamba Lusifa alikuwa "akatwe kabisa"unadokezwa kuwa alikuwa mti. Huu unatoa muunganiko unaoendelea na Danieli 4: 8 -16, ambapo Nebukadreza na Babeli wamelinganishwa na mti ukikatwa kabisa.

  7. Babeli na Ashuri mara nyingi wanabadilishana maneno katika manabii; hivi akiisha kusema kifo cha mfalme wa Babeli, Msta. 25 unasema "Nitamvunja huyo mwashuri ……" Unabii kuhusu Babeli katika Isa. 47 umerudiwa kuhusu Waashuri kwa Nahumu 3: 5, 4, 18 na Sefania 2: 13,15; na Nyaka. 33: 11 kusema kwamba mfalme wa Ashuri (alimchukua) alimtwaa manase utumwani Babeli - ni kuonyesha kubadilishana kwa kuita maneno. Amosi. 5: 27 unasema kwamba Israeli walikuwa wanakwenda utumwani "mbali kupita Dameski"yaani Ashuru, lakini Stefano ananukuu mstari huu kuwa"mbali kupita Babeli" (Matendo. 7: 43). Ezra 6:1 ni maelezo ya Dario mfalme wa Babeli akitoa amri ya kujenga tena hekalu. Wayahudi walimtukuza Mungu kuugeuza"Moyo wa mfalme wa Ashuru" (Ezera. 6: 22), tena inaonyesha kwamba ni maneno yanayobadilishana. Unabii wa Isaya 14, pamoja na mwingi mwingine kwa Isaya, unapatana vema kwa maneno ya uvamizi wa Sennakeribu kipindi cha Hezekia, huo mst. 25 unaeleza kuvunjwa kwa mwashuri. Msta. wa 13 ni mwepesi kuufahamu ikiwa unazungumzia kuhusu maneno ya kufuru ya kuuhusuru Yerusalemu Waashuri, walitaka kuingia Yerusalemu na kuteka hekalu kwa ajili ya miungu yao. Awali mfalme wa Ashuru, Tiglath -pileseri, pengine alitaka kufanya yale yale (2 Nyak. 28: 20, 21); Isa. 14: 13 "Maana umesema moyoni mwako, nitapanda mpaka mbinguni ….. (ya mfano wa hekalu na sanduku la agano - 1 Fal. 8: 30; 2 Nyak. 30: 27; Zab. 20: 2, 6; 11: 4 Ebra. 7: 26). Nami nitaketi juu ya mlima wa makutano (mlima sayuni lilipokuwa hekalu) katika pande za mwisho za Kaskazini"(Yerusalemu - Zab. 48: 1, 2).


  Back
Home
Next