Misingi Ya BIBLIA Somo La 6: Mungu Na Ubaya Mungu Na Ubaya | Ibilisi Na Shetani | Mapepo - Mashetani | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Uchawi, Edeni palitokea nini?, Lusifa, Majaribu ya Yesu, Vita Mbinguni) | Maswali |
6.3 Mapepo - MashetaniSehemu mbili zilizotangulia zaeleza sababu zilizotufanya tusiamini kuwa Ibilisi au shetani ni kiumbe binafsi au mtu mkubwa aliye mbaya sana. Kama tunakubali ya kwamba hayupo kiumbe huyu, basi ni kweli kuwa mapepo, ambao wamedhaniwa kuwa ni watumishi wa Ibilisi, vile vile hawapo. Watu wengi wanafikiri ya kuwa Mungu anatupatia mambo mema ya maisha, naye ibilisi na mapepo yake watupatia mambo mabaya, na wanatunyang’anya mambo mema atupayo Mungu. Ni wazi Biblia yafundisha kwamba Mungu ndiye chanzo cha nguvu zote (tazama somo la 6.1), na kuwa Yeye ndiye mhusika wa yote mawili mambo mema na mambo mabaya katika maisha yetu: -
Basi tunapopata majaribu, tufahamu ya kwamba yametoka kwa Mungu, lawama zisipelekwe kwa Ibilisi au mapepo. Ayubu alikuwa ni mtu aliyepoteza vitu vingi vizuri alivyobarikiwa na Mungu, Lakini hakusema, "Mapepo haya yamechukuwa yote aliyonipa Mungu". Hapana; sikiliza alichosema: -
Mara tukifahamu kuwa mambo yote yatoka kwa Mungu, wakati tuna matatizo katika maisha tunaweza kumwomba Mungu ayaondoe, na kama hafanyi hivyo, twaweza kuwa na hakika ya kuwa anatupatia hayo ili tabia zetu zikue kwa ajili ya faida yetu katika safari ndefu. "Mwanangu usiyadharau marudia ya Bwana, wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, (sio mapepo). Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye ? Basi kama hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali"(Ebra. 12: 5-8). MUNGU: CHANZO CHA NGUVU ZOTE Mungu ndiye chanzo cha nguvu zote: -
Mistari hii inatokea mara nyingi katika Biblia yote. Kwa kuwa Mungu ndiye chanzo cha nguvu zote na Mungu pekee, basi ni Mungu mwenye wivu, kama anavyotukumbusha mara nyingi (k.m Kutoka 20:5; K/torati. 4:24). Mungu anaingiwa na wivu hapo watu wake wanapoanza kuiamini miungu mingine, kama wakimwambia, ' Wewe ndiye Mungu mkuu, Mungu mwenye nguvu, lakini pia bado naamini wapo miungu wengine mbali na wewe, hata kama si wenye nguvu kama wewe’.Hii ndiyo sababu hatuamini yapo mapepo au Ibilisi yupo sawa na Mungu wa kweli. Hili ni kosa ambalo Israeli walifanya. Mengi yaliyo katika Agano la Kale yametumika kuonyesha jinsi Israeli walivyomchukiza Mungu kwa kuamini Miungu wengine kama yeye. Tutaona toka biblia kuwa "Mapepo"ambayo watu wanayaamini siku hizi ni kiasi kama wale Miungu wa uongo ambao Israeli waliamini kuwa wapo. MASHETANI NI SANAMU Katika 1 Wakorintho, Paulo ameeleza sababu za Wakristo kutotakiwa kujihusisha na ibada za sanamu au kuyaamini mambo haya. Katika nyakati za Biblia watu waliyaamini mapepo kuwa ni miungu wadogo ambao nao waabuduwe ili wazuie matatizo yasije katika maisha yao. Kwa hiyo walitengeneza aina ya mashetani, ambao walikuwa sawa na sanamu, wakawatumikia. Hii ni kwa nini Paulo anaeleza kwa kutumia maneno "pepo"na "sanamu" kwa kubadilishana katika waraka wake: "Lakini vitu vile wavitoavyo sadaka watu wa mataifa, wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani ….. lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka ya sanamu, msile, kwa ajili yake …….." (1Kor. 10:20,28). Hivyo sanamu na mashetani ni maana moja. Tazama jinsi Paulo anavyosema walitoa sadaka "kwa mashetani (sanamu) si kwa Mungu" - Mashetani hawakuwa Mungu, kwa kuwa yupo Mungu mmoja, kinachofuata ni kwamba mashetani hawana uwezo wowote wa kweli kabisa, Si Miungu. Sababu hasa inatoka katika 1Kor. 8:4:- "Basi …… vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua kuwa sanamu si kitu katika huu ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja" Sanamu, au mashetani hayaishi kabisa. Yupo Mungu mmoja wa kweli tu, au uweza, ulimwenguni. Paulo anaendelea katika (mst. 5,6): - "Ijapokuwa wako waitwao miungu …….. (kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi), (kiasi kama watu wanavyoamini kuwepo aina nyingi za mashetani siku hizi - shetani mmoja asababisha upoteze kazi yako, na mwingine asababishe mkeo au mumeo akuache,n.k) Lakini kwetu (waaminio wa kweli) Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake (Vitu vibaya na vizuri, kama tulivyokwisha ona maana zilizotolewa awali)" Ushahidi zaidi ambao watu wa nyakati za Agano Jipya waliamini mashetani kuwa ni sanamu au ' miungu’ unapatikana katika matendo 17: 16 -18: huu unaeleza jinsi Paulo alivyohubiri katika mji wa Anthene, ambo ulikuwa umezungukwa na sanamu, kwa hiyo wakizitumikia sanamu za aina mbalimbali Baada ya kumsikia Paulo akihubiri Injili, watu wakasema,"Aonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni (mashetani): Kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo. Watu walidhani kwamba "Yesu"na"ufufuo"walikuwa mashetani wapya au sanamu ambazo walielezewa. Kama ukisoma sura yote, utaona Paulo jinsi alivyoendelea kufunza ukweli wetu hawa, na katika mstari 22 anasema, "ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini"(yaani, mnajitoa sana kuwatumikia mashetani), akawaeleza jinsi Mungu asivyokuwamo katika mashetani yao, au sanamu. Kumbuka kwamba Mungu ndiye muasisi wa nguvu zote. Kama hayumo katika mashetani, basi mashetani hawana uwezo wowote kwa sababu hakuna chanzo kingine cha uweza katika ulimwengu huu - yaani, hawaishi. ‘MASHETANI’ WALIO KATIKA AGANO LA KALE ZILIKUWA NI SANAMU Tukirudi kwenye Agano la Kale, upo ushahidi zaidi kuwa "mashetani"ni mamoja kama sanamu. Katika K/torati 28:22 -28, 59 -61 yalitabiriwa magonjwa ya akili kuwa moja ya adhabu kwa ajili ya kutumikia sanamu /mashetani. Huu unabii waeleza muungano wa mapepo na magonjwa ya akili katika Agano Jipya. Lakini ijulikane ya kwamba msemo wa mashetani au mapepo umeungana na maradhi, sio dhambi. Hatusomi kuwa Kristo alitoa mashetani au mapepo ya husuda, uuaji n.k. Inabidi pia ieleweke kwamba Biblia inapowasema watu wenye pepo / maradhi si kusema mashetani yaliyosababisha maradhi. Ni muhimu kujua kuwa tafsiri ya kiyunani ya Agano la Kale (Septuagint) neno lililotumika ni 'daimonion’ kwa maana ya'Sanamu’ katika K/torat. 32: 17 na Zab. 106: 37 hili ndilo neno lililotafsiriwa'pepo’ katika Agano Jipya. Zaburi 106: 36 -39 yaelezea makosa ya Israeli na kulinganisha sanamu za Kanaani na mashetani: -
Kumbukumbu la Torati 32: 15 -24 laeleza ni kiasi gani Mungu anakasirika watu wake wanapoamini mashetani:"Israeli akamdharau mwamba wa Wokovu wake. Wakamtia wivu kwa miungu migeni, wakamkasirisha kwa machukizo. Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, kwa miungu wasiowajua, kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, ambayo baba zenu hawakuiogopa …... (Mungu) akasema, Nitawaficha uso wangu …… maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi, watoto wasio imani ndani yao. Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; wamenikasirisha kwa ubatili wao …… nitaweka madhara juu yao chungu chungu". Hivyo Mungu anasema mashetani ni sanamu, machukizo, na ubatili - mambo ambayo haifai kuyaamini, hayana uhai. Kuamini kwamba mashetani yapo ni kukosa imani ya kusadiki kwa Mungu. Sio rahisi kuamini kuwa Mungu anatoa kila jambo, pande zote mbili, baya na jema, katika maisha. Ni vyepesi kudhani kuwa mambo mabaya yanatoka kwa mwingine, Kwa sababu mara tukisema yanatoka kwa Mungu, basi tutakuwa tumwamini Mungu kwamba mambo mabaya atayaondoa au ni kwamba yatakuwa ni yenye faida kwa hatima yetu. MASHETANI / PEPO WALIO KATIKA AGANO JIPYA Lakini, waweza kusema,"Ni vipi mafungu yote ya maneno yaliyomo katika Agano Jipya ambayo ni dhahiri yasema habari za pepo ?". Kwa jambo moja yatupasa tuwe wazi: Biblia haiwezi kupingana yenyewe, ni neno la Mungu mwenyezi. Ikiwa ni wazi tumeambiwa kuwa Mungu ndiye aletaye matatizo yetu na kwamba yeye ndiye muasisi wa nguvu za aina zote, basi Biblia vile vile haiwezi kutuambia kuwa pepo - Miungu wadogo washindanao na Mungu - hutuletea mambo haya sisi. Ni jambo la maana kujua kwamba Neno'pepo’ linaonekana kutokeza mara nne katika Agano la Kale na daima laelezea kutumikia sanamu, bali limetokea mara nyingi katika taarifa za Injili. Tunadokeza hii ni kwa sababu, wakati Injili zilipokuwa zikiandikwa, ulikuwa ni msemo wa siku zile kuusema ugonjwa wowote ambao haukufahamika ulikuwa ni sababu ya mapepo. Kama kweli pepo wanaishi nao wahusika na kuugua na matatizo yetu, basi tungesoma habari zake zaidi katika Agano la Kale. Bali hatusomi taarifa zake kabisa fungu hili la maneno katika sentensi humo. PEPO KATIKA AGANO JIPYA. Kusema kuwa pepo walikemewa na mtu ni kusema ya kwamba maradhi ya akili yaliponywa, au ugonjwa ulipokuwa haueleweki muda huo. Watu walioishi karne ya kwanza kwa kila kitu ambacho hawakukifahamu walielekeza lawama juu ya viumbe wa kuwazika waitwao'pepo’. Maradhi ya akili yakiwa ni shida kuyaelewa kwa usawa wao wa elimu ya Kitabibu, watu waliwasema wale wenye shida kuwa'Walipagawa na pepo’. Kwa nyakati za Agano la Kale, Roho mbaya au mchafu ilikuwa inatajwa hali ya akili iliyotaabika (Amu. 9: 23; 1 Sam. 16:14; 18: 10). Kwa nyakati za Agano Jipya, msemo wa roho chafu / kupagawa na pepo ulifikia kuwasema waliokuwa wanasumbuliwa na maradhi ya akili. Muunganiko kati ya pepo na ugonjwa umeonyeshwa kama ifuatavyo:"Wakamletea (Yesu) wengi wenye pepo: akawatoa pepo kwa neno lake …… ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya (Katika Agano la Kale) akisema, mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, na kuchukua magonjwa yetu"(Math. 8: 16, 17). Hivyo udhaifu na magonjwa ya mwanadamu ni mamoja na kupagawa na "pepo"na "Roho wachafu". Watu walimdhania Yesu alikuwa na wazimu na walisema hii inabidi iwe ni kwa sababu alikuwa na pepo -"Ana pepo huyu, tena ana wsazimu"(Yoh. 10: 20; 7:19, 20; 8: 52). Kwa hiyo waliamini kwamba pepo walileta wazimu. KUPONYA UGONJWA Walipoponywa, watu "waliokuwa na pepo"wanasemwa walirudi kuwa na "Akili zao timamu" - Marko. 5:15; Luka 8: 35. Hii inadokeza ya kuwa "kupagawa na pepo"ni njia nyingine ya kusema mtu fulani si mzima kiakili - yaani, hana akili timamu. Wale "waliokuwa na pepo"wamesemwa "waliponywa"au "alikemea"- Mathayo. 4:24; 12: 22; 17: 18 - husema kwamba kuwa na pepo ni njia ya kueleza ugonjwa. Katika Luka 10:9 Yesu aliwaambia mitume wake 70 kwenda "kuponya wagonjwa", walifanya hivyo walirudi na kusema, mst wa 17,"hata pepo wanatii kwa jina lako"- tena, pepo na magonjwa yamelinganishwa. wakati mwingine mitume walikemea watu kwa jina la Yesu na hapa tuna mfano huu (tazama pia Matendo 3: 6; 9: 34). MSEMO WA SIKU ZILE Basi tunaona kwamba katika Agano Jipya ulikuwa ni msemo wa siku zile wa kusema mtu mwingine kuwa ana pepo ikiwa walikuwa wagonjwa wa akili au walikuwa na ugonjwa ambao hakuna aliyeufahamu. Warumi wa wakati ule na Wayunani malezi ya imani yao ilikuwa kwamba watu waliokuwa na pepo, kwa sababu hii walipata ugonjwa wa akili. Hao "Wakristo" Waaminio kuwepo kwa pepo wana maana ya kusema kwamba imani za kipagani za wakati ule kwa eneo hili zilikuwa sahihi kabisa. Biblia imeandikwa kwa Lugha ambayo watu wanaweza kuielewa. Kwa sababu inatumia msemo wa siku hizo haina maana kwamba yenyewe au Yesu aliamini kuwepo mapepo. Kwa njia hiyo hiyo kwa Kiswahili tuna neno 'kupigwa na mwezi’ huwa ni kueleza mtu mwenyewe wazimu wakati mwezi ukiwa mchanga. Miaka ya zamani watu waliamini kwamba mtu akitoka nje wakati wa usiku nuru ya mbalamwezi ikiwa inang’aa, wanaweza kupigwa na mwezi na kupata ugonjwa wa akili.Tunatumia neno hilo 'kupigwa na mwezi’ siku hizi ni kusema mtu aliye na wazimu, lakini haina maana kwamba tunaamini wazimu unasababishwa na mwezi. Ikiwa maneno haya yaliandikwa na kusomwa tena kwa kipindi cha miaka 2000 - Yesu kama hajarudi - watu watafikiri tuamini kwamba mwezi huleta wazimu, Lakini watakosea kwa sababu tunatumia msemo wa siku zetu tu, kama Yesu alivyofanya miaka 2000 iliyopita. Ni dhahiri kwamba Yesu hakuzaliwa tarehe 25 Desemba; lakini mwandishi wa sasa bado anatumia neno'Siku ya Krismasi’ inaposemwa siku hiyo, ingawa siamini kwamba tusherehekee siku ya kuzaliwa Kristo. Majina ya siku za juma yamewekwa juu ya kuabudu sanamu ya kipagani - k.m.'Jumapili’ maana yake'siku iliyotolewa kuabudu jua’; 'Jumamosi’ ilikuwa ni siku ambayo sayari ya Saturn ya sita toka kwenye jua ilikuwa iabudiwe, Jumatatu kwa ajili ya mwezi n.k. Kutumia majina haya haina maana kwamba tunashiriki katika imani za kipagani za hao wa kwanza kuvumbua misemo yetu ya sasa. Vile vile 'Influenza au flu’ - Makamasi - mafua ni majina yatumiwayo kwa pamoja siku hizi; maana yake 'aliyevutwa na pepo’.Danieli alipoitwa jina lingine'Belteshaza’ jina lenye maana ya Mungu wa kipagani, taarifa iliyovuviwa katika Dan. 4: 19 yamwita'Belteshaza’ bila kuonyesha kuwa hili jina linaonyesha fikira potofu. Nasema kuhusu'Papa’ kama njia ya kumtambulisha mtu, ingawa nadhani ni kosa hasa kuamini kwamba ni 'papa’ au baba (Math. 23: 9). Ilikuwepo hadithi ya uongo katika kipindi cha Ezekieli ya kwamba nchi ya Israeli ilihusika na balaa kwa walio ndani yake. Hii haikuwa kweli, hata hivyo Mungu alihojiana na Israeli, akitumia wazo lililokuwa wakati ule na watu wengi, "Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa watu hukuwaambia, wewe nchi u mwenye kula watu, nawe umekuwa mwenye kufisha watu wa taifa lako; basi (wewe nchi) hutakula watu tena, asema Bwana Mungu"(Ezek. 36: 13, 14). Lilikuwepo wazo la mazoea ya kipagani la kuwa bahari ilikuwa ni mtu mkubwa na mbaya sana atakaye kuimeza dunia. Wakati hii ni dhahiri siyo kweli, mara nyingi Biblia inatumia mfano huu ili kusaidia usomaji wake wa kuanza kupata kuelewa jambo lililoonyeshwa: Ona Ayubu.7: 12; Amosi. 9: 3; Yer. 5: 22; Zab.89: 9; Habakuki 3:10; Math. 14:24; Marko. 4:30 (neno la Kiyunani); Hadithi za Waashuri waliita mnyama huyu mkaidi wa baharini 'Rahabu’ na hili ndilo jina hasa alilopewa mnyama wa bahari ya Misri katika Isa. 52: 10. Kwa kuwa Biblia imevuviwa na Mungu, haiwezekani kwamba Biblia yaeleza tu ushawishi wa kipagani uliokuwa ukitumika kwenye kipindi ilipoandikwa. Inabidi iwe kwamba Mungu alikuwa anafahamu kutaja imani za wakati ule ule, ili kuonyesha kwamba Yeye ni muasisi wa nguvu; ndiye pekee anayemtawala'mnyama mkubwa’ wa bahari, kwa matokeo anafanya mapenzi yake. Kwa sababu hii Mungu alisahihisha kosa kubwa la imani za watu hawa, ambazo zilikuwa kwamba zilikuwepo nguvu zingine zikifanya kazi ulimwenguni ambazo haziko chini ya mamlaka ya Mungu, na kwa hiyo kwa kuzisema zilikuwa mbaya. Ingawa hivyo, kwa mfano huu, Biblia haiachi njia yake kujaribu kuondoa upumbavu wa kuamini kwamba kuna mnyama mkubwa anayejificha baharini, au kuwa bahari ni mnyama . Mfano mwingine ni maelezo ya radi na dhoruba ya mawingu kuwa ni "nyoka aendaye mbio" (Ayu. 26: 13 Isa. 17: 1). Kwa uwazi huu alikuwa anataja imani za wapagani wa siku zile kuwa radi na muundo wa wingu litishalo yalikuwa hasa ni maono ya nyoka mkubwa. Maneno haya hayabainishi ujinga wa wazo hili, au jarabio la kuelezea kisayansi. Mwenendo wa Kristo kwa imani iliyoenea ya pepo kwa sababu hii ulikuwa ule ule; miujiza yake ilibainisha kwamba uweza wa Mungu ulitimilika kabisa, haukufungwa na imani za uongo wa watu kuhusu yaitwayo 'pepo’. Hao wanaoamini kwamba Agano Jipya limeandika habari za ' pepo' ili kuthibitisha viumbe hawa wanaishi kwa kweli ni kazi inayoelekea kukubali kuwa bahari kweli ni mnyama, na ya kuwa radi ni joka mkubwa hasa. Hii kweli ni maana yenye nguvu; inabidi ijulikane kwamba Biblia inatumia lugha ya siku zile ambayo ilitumika kuandikwa, bila ulazima wa kusaidia imani zinazofanya msingi wa msemo huo. Tumeonyesha matumizi yetu ya lugha kuwa ni mamoja. Biblia yafanya hivi ili kuthibitisha aina ya ukweli wenye msingi tuliouona katika masomo ya 6.1 na 6.2 - ya kwamba Mungu ni mwenye nguvu zote; Anahusika na majaribu yetu; dhambi hutoka ndani yetu - mambo yote haya yanaweza kuleta maana ya kukubali ukuu wa uweza wa Mungu kuokoa. Waitwao 'Watafiti wakuu’ daima wanachimbua vitu ardhini vinavyounga kati ya msemo wa maandiko na imani na mawazo ya tamaduni zinazozunguka ambazo Biblia ilivuviwa na kuandikwa taarifa. Hizi zinaeleweka, mara ikieleweka kwa matumizi ya lugha ya Biblia inayoweza kutaja kwa kuandikwa imani ya mahali, lakini yafanya hivyo ili kumaanisha kwamba Yahweh, Mungu wa kweli wa pekee, ni mkuu sana kuliko imani hafifu za watu ambazo zilijulikana kwa wale waliosoma kwanza maneno yaliyovuviwa, mapya toka Kiywani mwa nabii. Jambo hili likiwa moyoni inastajaabisha kuweza kupata mifano mingi kiasi gani katika Agano Jipya la msemo wa siku zile ulivyotumika bila msemo huo kusahihishwa. Hapa kuna mifano mingine: -
Mwenendo wa Kristo kwa pepo wa Agano jipya ulikuwa hivyo hiyvo; miujiza yake aliyopewa na Mungu ilibainisha sana kuwa maradhi yalisababishwa na Mungu. Sio nguvu yoyote ingine kwa kuwa ni Mungu aliyekuwa ni mwenye uweza kuwaponya.
Hata wakati Wayahudi walipoleta maneno mabaya (kwa makusudi) ya kuwa Yesu alikuwa "anajifanya kuwa sawa na Mungu" (Yoh. 5:18), Yesu hakukana wazi wazi; badala yake kwa nguvu alisisitiza kuwa miujiza yake ilimwonyesha kuwa ni mtu atendaye kwa niaba ya Mungu, na kwamba hakuwa sawa na Mungu. Miujiza ya Yesu vivyo hivyo ilionesha kosa la kusadiki kuwa kuna pepo. Muujiza wa Kristo wa kumponya mlemavu kwenye bwawa ulikuwa ni wa kuonesha ujinga wa hadithi ya Wayahudi ya kuwa wakati wa Pasaka Malaika aliyagusa maji ya bwawa la Bethesaida, na kutoa nguvu humo. Hadithi hii imeandikwa bila kukana moja kwa moja ukweli wake; taarifa ya miujiza ya Kristo ni kuweka wazi ujinga wao (Yoh. 5: 4). 2 Petro 2: 4 kusemwa watu wabaya kutupwa shimoni, ni sawa na kusema kuzimu, inaonekana kama ni nchi nyingine; Petro hasahihishi wazo hilo bali ana litumia kama ishara ya maangamizo kamili na adhabu kwa ajili ya dhambi. Matumizi ya Yesu kwa neno Jehanamu ni mamoja (ona somo la 4.9). JE ! NI KWELI PEPO ANALETA UGONJWA ? Kila mmoja anayeamini kuwa pepo anaishi inabidi ajiulize wenyewe swali: "Ninapo ugua, je ! ugonjwa umeletwa na pepo ?"Kama unadhani Agano Jipya linapotaja pepo linahusu Miungu wadogo wanaozunguka kutenda mabaya, basi inakubidi useme"ndiyo"kwa suala hilo, utaelezaje ukweli wa kwamba magonjwa yanayolaumiwa kuwa ni pepo sasa yaweza kutibiwa au kudhibitiwa na madawa ?. Malaria ni mfano bora unaojulikana sana. Watu wengi wa Afrika waliamini mpaka hivi karibu ya kuwa malaria ililetwa na pepo. lakini tunajua kwamba malaria inaweza kutibiwa na kwinini au vidonge vingine. Basi unasema kwamba pepo aonapo vidonge vidogo vya njano vikishuka kooni wanatishika na kuruka na wakakimbia ?. Magonjwa mengine ambayo Yesu aliponya, yanayosemwa ni matokeo ya pepo, yametambulika kama tetenasi au kifafa - yote yanaweza kutulizwa kwa dawa. Rafiki yangu anatoka kijiji kilicho nje ya Kampala Uganda. Alituambia kwamba watu waliamini Malaria yanaletwa na pepo, lakini mara walipoona dawa jinsi inavyodhibiti kwa urahisi sana, wakaacha kutupia lawama kwa pepo. Ingawa hivyo, wakati mtu mmoja aliposhikwa na malaria ya kichwani (ikisababisha ugonjwa wa akili) bado wakalaumu pepo. Tabibu akaja toka mji ulio jirani na kuwapa dawa yenye nguvu kubwa kuzuia malaria iwe tiba, walikataa kwa sababu walisema walihitaji kitu kingine cha kupingana na pepo, sio malaria. Daktari alirejea baadaye na kusema, "Nina dawa ya kufukuza pepo"; mgonjwa kwa furaha alichukuwa dawa, naye akapona. Vidonge vya pili vilikuwa vile vile kama vya kwanza. Daktari hakuamini pepo, bali alitumia msemo wa siku hiyo ili kumponya huyo mtu - kiasi kama "Tabibu Mkuu"Bwana Yesu, kwa miaka 2000 iliyopita. |