Misingi Ya BIBLIA
Somo La 6: Mungu Na Ubaya
Mungu Na Ubaya | Ibilisi Na Shetani | Mapepo - Mashetani | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Uchawi, Edeni palitokea nini?, Lusifa, Majaribu ya Yesu, Vita Mbinguni) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 21: Vita Mbinguni

Ufunuo 12: 7 -9 "Kulikuwa na vita mbinguni, Mikaeli na Malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na Malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapa kuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na Malaika zake wa katupwa pamoja naye".

TAFSIRI YA WALIO WENGI: -

Hii ni sura mojawapo ambayo watu wengi wameitumia kutoa shauri kuwa ulikuwepo uasi mbinguni miongoni mwa Malaika, uasi ukasababisha ibilisi na Malaika zake kutupwa duniani toka mbinguni, ambapo akiwa na namna ya nyoka, wakaanza kufanya matatizo na kuleta vurugu duniani.

FAFANUZI: -

  1. Yote tuliyojifunza mpaka hapa katika somo hili inabidi yaletwe na kuchukuliwa juu ya fungu hili la maneno. Tumekwisha ona ya kuwa Malaika hawawezi kutenda dhambi na ya kuwa uasi hauwezi kuwepo mbinguni. Hivyo hili fungu la maneno ambalo ni la aina yake pekee - inabidi litafsiriwe kwa njia ambayo haiwahusishi Malaika kutenda dhambi au kuwepo Malaika wenye dhambi wanaowafanya watu kufanya dhambi duniani, kwa kuwa dhambi inakuja toka ndani yetu sio nje yetu sisi (Marko. 7: 20 -23)

  2. Kutupwa nyoka - joka toka mbinguni, inadokezwa asili alikuwa huko - Lakini nyoka halisi wa Edeni aliumbwa na Mungu toka mavumbi ya ardhi (Mwa. 1: 24 -25). Hakuna kidokezo kwamba ibilisi alishushwa toka mbinguni na kumwingia nyoka ndani yake.

  3. Fahamu kwa makini kwamba hakuna ushahidi wowote hapa wa Malaika akifanya dhambi au akifanya uasi juu ya Mungu, ni vita iliyokuwa mbinguni. Uwezekano hakuna wa mtu yeyote akipigana na Mungu mbinguni: "Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu"(Kum. 32: 39).

  4. Baada ya mfululizo wa mambo yaliyo katika mstari wa 7 -9, mst. 10 unasema kwamba "kukawa na sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu wa nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na Mamlaka ya Kristo wake: kwa maana mshitaki wa ndugu zetu ametupwa chini, Yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku". Ikiwa mst. 7 -9 mambo yake yalitokea mwanzo wa ulimwengu, kabla wakati wa Adamu na Hawa, ni jinsi gani imesemwa kuwa baada ya kutupwa shetani ukaja wokovu na ufalme wa Mungu ? Baada ya dhambi ya Adamu, walimwengu wameanza historia yao mbaya ya utumwa wa dhambi na hali ya kushindwa kufanya kitu - hali ya shida kuieleza kuwa"Wokovu"na ufalme wa Mungu. Kuna furaha ya kuwa ibilisi - mshitaki - ametupwa chini hadi duniani. kwa sababu gani kuwe na furaha ikiwa kuja kwake duniani kulikuwa ni mwanzo wa dhambi na msiba kwa binadamu ?. Basi, kuanguka toka mbinguni kuja duniani kukieleweka kwa maneno ya mfano sio kwa maneno yenyewe hasa, kuwa maana ya kuanguka toka kwenye mamalaka (kama ushahidi wa Isa. 14: 12; Yer. 51: 53; Omb. 2:1;Math 11: 23), unavyosema, zaidi mno maana inaweza kufanywa ka yote haya. Kama yote haya yalitokea kabla ya kipindi cha Adamu, au kabla ya kuanguka kwa mtu, ni jinsi gani ibilisi alikuwa anawashitaki "ndugu zetu"kuona hawa kuwepo wakati ule ?.

  5. Hakuna ishara inayoonyesha yote haya yaliyotokea kwenye Bustani ya Edeni. Kipengele cha muhimu kipo kwa Uf. 1: 1 na 4: 1 - kwamba ufunuo ni unabii wa"Mambo ambayo hayanabudi kuwako upesi". Sio maelezo basi ya kile kilichotokea katika Edeni, bali ni unabii wa mambo yaliyokuwa yanatokea wakati mwingine baada ya karne ya kwanza, hapo ufunuo ulipotelewa na Yesu. Yeyeto ambaye kweli ni mnyenyekevu wa Neno ataona kwamba haya mabishano ya maneno pekee yanazuia kabisa hata kutowezekana majaribio yote ya kutaja ufunuo 12. kwenye bustani ya Edeni. Swali linabidi lijibiwe kama ni kwa sababu gani ibilisi yule yule na habari kuhusu kile kilichotokea Edeni itunzwe mpaka mwisho wa Biblia kabla ya kubainishwa.

  6. "Joka kuu yule …… nyoka wa zamani" (Uf. 12: 9). Joka alikuwa na "Vichwa saba na pembe kumi" (mst. 3), kwa hiyo hakuwa nyoka halisi. Kuitwa "nyoka wa zamani"yaonyesha kwamba alikuwa na tabia ya yule nyoka wa zamani aliyekuwa Edeni, kwa maana ya kuwa mdanganyifu kama nyoka aliyekuwa. Hali moja, "Uchungu wa mauti ni dhambi" (1 Kor. 15: 56), Lakini hiyo haina maana ya kuwa mauti ni nyoka yule. Anatabia ya nyoka, kwa kuunganika na dhambi.

  7. Ibilisi alitupwa duniani na kwa ukali alianzisha ugomvi "akijua ana wakati mchache tu"(mst. 12). Ibilisi kama alitupwa katika Edeni, alikuwa na nafasi ya kumtesa binadamu wakati wake wote wa historia ndefu - ambayo ni vigumu kwa kuwa na" Wakati mchache"tu wa kufanya maangamizi makuu.

  8. Ni jinsi gani Ibilisi amemdanganya "ulimwengu wote"(mst. 9) kabla ya kutupwa mbinguni, kwa kuwa hapa kuwepo mtu yeyote ulimwenguni kabla ya Adamu ?.

  9. Mst. 4 unasema kwamba joka akakokota theluthi ya nyota za mbinguni kuja chini kwa mkia wake. Ikiwa huu unasomwa kwa jinsi ya maneno yalivyo - Ufunuo 12. unabidi usomwe kwa maneno yalivyo ili kusaidia tafsiri ya watu walio wengi - ukubwa kamili wa joka ni mkubwa sana - theluthi ya ulimwengu wote (au karibu mfumo wa sayari) aliweza kuwemo kwa mkia wake. Hakuna jinsi ya sayari dunia kuwa kubwa kiasi cha kutosha kuenea kiumbe huyu mkubwa akitambaa juu yake. Nyota nyingi ni kubwa kuliko dunia yetu - inakuwaje theluthi yake kuanguka juu ya dunia ?. Imekadiriwa kwamba theluthi ya nyota zitaenea kwa karibu maili trilioni tano. Hivi ndivyo urefu wa mkia wa joka inabidi uwe !. Kumbuka kwamba haya yote yametokea, au yatatokea, baada ya karne ya kwanza B.K. wakati unabii huu ulipotolewa

  10. Kwa mtazamo huu na mwingi wa mambo mengine katika Uf. 12 (na unabii wote) ambao hauwezekani kwa kutumia kwake kokote, sio ajabu tumeambiwa kabla ya yote (Uf. 1: 1) ni kwamba ujumbe huu umeandikwa kwa "ishara"yaani, kwa msemo wa kuashiria, au kwa mfano. Kana kwamba kutia mkazo huu kwa maneno yenyewe ya Uf. 12, Ufunuo 12: 1 unaeleza tendo lililofuata kuwa "Ishara kuu".

  11. Kwa kusoma anachofanya Ibilisi anapokuwa duniani, hakuna maelezo yake yeye akiwafanya watu watende dhambi; kweli mstari wa 12 - 16 inaonyesha ya kwamba ibilisi hakufaulu kwa majaribio yake kusababisha matatizo duniani mara alipofika hapa. Taarifa hii inapingana na tafsiri ya watu wengi.

  12. Maana moja ya maswali ni kuelewa endapo fungu hili la maneno lasaidia wazo la kuwepo vita mbinguni kwenyewe, iwapo "Mbingu" zilizosemwa hapa ni za maneno halisi au za maneno ya mfano. Tulieleza awali kwamba "mbingu"zaweza kwa maneno ya msemo wa mfano kutaja eneo la mamlaka. Ufunuo kikiwa ni kitabu cha mifano, tulitegemea jambo hili hapa.

Mwanamke wa mstari wa 1 "amevikwa jua, na mwezi upo chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji za nyota kumi na mbili" Mkusanyiko huu wa mbinguni, vile vile na mwanamke, ni dhahiri walining’inia mbinguni, maneno hayawezi kuwa na maana hiyo. Mwanamke hawezi kuvikwa jua, au nyota kubwa kama dunia kuwa juu ya kichwa chake.

Ishara nyingine inaonekana mbinguni mst. 3 - joka jekundu. Mstari huu umechukuliwa ulivyo kwa kawaida, Lakini kwa nini iwe hivyo, Kwa kuwa mbingu ni zile zile zilizotajwa katika mst. 1, ni wazi huu ni maneno ya mfano? mstari wa 4 unamwonyesha joka akiziangusha nyota katika nchi toka mbinguni. Tumeona kwamba kwa sababu ya ukubwa wa nyota na dunia, Basi hauwezi kutaja nyota tulizonazo angani au mbinguni. Ufalme wa Mungu utawekwa duniani (Dan. 2: 44; Math. 5: 5), ambao hautaweza kusimikwa kama dunia itaangamizwa kwa kuangukiwa na nyota juu yake.

Mwanamke "akazaa mtoto wake mbinguni", yyeye atakaye wachunga ….. mtoto akanyakuliwa kwa Mungu na kwa kiti cha enzi"(mst. 5). Kiti cha enzi cha Mungu kiko mbinguni. Kama tayari mwanamke alikuwa mbinguni, ni kwa sababu gani mtoto wake "akanyakuliwa"kwenda mbinguni. Mwanamke alikuwa mfano wa kitu kingine duniani, ingawa kwa maneno ya kimfano"mbinguni"alikuwa. Kisha akakimbilia"jangwani"(mst. 6). Kama alikuwa katika mbingu halisi, hii ina maana ya kwamba jangwa lipo mbinguni. Inafaa zaidi mwanamke alikuwa eneo la kimbingu, na kisha kukimbilia kwenye jangwa la mfano duniani.

Ndipo tukafika mst. 7 -"kulikuwa na vita mbinguni" ushahidi mwingine toka kwa "mbingu"za Uf. 12 ukiisha kuwa ni maneno ya mfano, inaonekana tu hii vita ilikuwa katika mbingu za mfano. Suala hili linabidi liwe hivyo, kwa sababu uasi haupo au dhambi katika mbingu halisi tunazo ziona (Math. 6: 10; Zab. 5: 4, 5; Hab. 1: 13). Mtazamo wa wengi, madai ni kwamba Malaika wamefungwa kuzimu; Lakini hapa wako mbinguni. Basi sivyo Malaika halisi.

Mwandishi aliyepo mara nyingine anawauliza waaminio wazo la orthodox la Ibilisi kwa swali lifuatalo: Je ! unaweza kunipa historia fupi ya Ibilisi wa Biblia, kulingana na tafsiri yenu kwa maneno ya Biblia ?

Jawabu linapingana mno. Kulingana na hoja ya orthodox, kujibu kunakuwa kama hivi: -

  1. Ibilisi alikuwa Malaika mbinguni aliyetupwa kwenye bustani ya Edeni. Alitupwa duniani katika Mwa. 1.

  2. Amedhaniwa alikuja duniani na akaoa katika Mwa. 6.

  3. Kwenye kipindi cha Ayubu amesemwa alikuwa anapita sehemu zote mbili mbinguni na duniani.

  4. Wakati wa Isaya 14 alitupwa toka mbinguni hadi duniani.

  5. Katika Zekaria 3 yuko mbinguni tena.

  6. Yupo duniani kwa Math. 4"Alitupwa nje"kwenye kipindi cha Yesu kulingana na wazo la wengi "mkuu wa ulimwengu huu" akiisha "tupwa nje"kipindi kile.

  7. Upo unabii wa Ibilisi "wa kutupwa"katika Uf. 12.

  8. Ibilisi amefungwa "mnyororo" katika Uf. 20, bali Malaika zake walifungwa minyororo katika Mwanzo, kufutana na kawaida ya kutazama Yuda mst. 6. Kama alifungwa na "minyororo ya milele" basi, ni jinsi gani ameitwa kwa kufungwa minyororo tena katika Uf. 20.

Kutokana na hili itakuwadhahiri kwamba mtazamo wa watu wengi wa kuwa ibilisi alitupwa toka mbinguni kwa kutenda dhambi sio kweli, kwa kuwa amesemwa bado yuko mbinguni baada ya kila kutokea na'Kutupwa’. Ni muhimu kuelewa pande zote mbili 'mbingu’ na ibilisi kwa maana ya maneno ya mifano.

MAELEZO YALIYODOKEZWA: -

  1. Kujaribu na kutoa maelezo ya sura hii wazi kabisa ni nje ya upeo wetu s sasa. Maelezo yote ya mistari hii inatakiwa ufahamu wote wa kitabu kizima cha ufunuo ili kupata maneno yake.

  2. Matata katika mbingu za mfano - yaani, sehemu ya madaraka ilikuwa basi kati ya makundi ya Mamlaka mbili, kila moja likiwa na wafuasi wake, au malaika.Kumbuka kwamba tumeonyesha ya kwamba ibilisi na shetani mara nyingi wameshirikishwa na mfumo wa Waroma ama Wayahudi.

  3. Kama ibilisi - joka maana yake aina nyingine ya Mamlaka ya kisiasa ilivyoonyeshwa na kuwa na 'taji juu ya vichwa vyake’ (mst. 3); Ufu. 17: 9,10 pia hufafanua juu ya joka huyu:"Hapa ndipo penye akili zenye hekima"- yaani - usijaribu kuelewa mnyama huyu kuwa ni kiumbe halisi - Vichwa saba ni milima saba …. Ambao ni wafalme saba" na mwingine hajaja bado "naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache"labda anaunganika na Ibilisi - joka mwenye "wakati mchache"wa Ufunuo 12: 12.


  Back
Home
Next