Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 26: Melkizedeki.

Mwanafunzi wa Biblia amesema kwa ukunjufu mwingi'Ameni’ kwa maneno ya mtume Paulo alipoandika:"……. Ndugu yetu mpenzi Paulo …… katika nyaraka zake zote ….. katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na Elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapatavyo na maandiko mengine kwa uvunjifu wao wenyewe"(2 Pet. 3: 15, 16). Hakika huu unatumika juu ya ufafanuzi wa Paulo kwa Melkizedeki ulioandikwa kwa Waebrania; yeye mwenyewe alikiri aliingia ndani sana ya maandiko, akinena mambo ambayo yaweza kueleweka tu na waamini waliokomaa sana kwenye maandiko (Ebra. 5: 10, 11, 14). Basi sio kwa ajili ya kuweka elimu ya msingi juu ya mafunzo ya mistari hii; wala maneno ya Melkizedeki yasiyoonekane kwa upana kwenye fikira za hao ambao bado wanajifunza mafundisho ya msingi wa Maandiko.

"Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa selemu (Yerusalemu), kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki"; amesemwa kuwa"hana baba, hana mama, hana wazazi (kizazi), hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake; bali amefananishwa na mwana wa Mungu"(Ebra. 7: 1,3). Yesu alikuwako hasa kabla ya kuzaliwa, na kwa sababu hiyo hakuwa na wazazi wanadamu.

Yesu alikuwa na Baba (Mungu) na mama (Mariamu) na ukoo (tazama Math. 1, Luk. 3 na Yoh.7: 27). Kwa sababu hii'Melkizedeki’ hawezi kutajwa yeye mwenyewe. Isitoshe, Melkizedeki"alifananishwa na Mwana wa Mungu"(Ebra. 7: 3); hakuwa ni yeye mwenyewe Yesu, bali alikuwa na mfano mmoja halisi naye ambao umetumika na mwandishi kwa kusudi la kufundishia."Ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki", Yesu (Ebra. 7: 15) naye amefanywa kuhani mkuu'kwa mfano wa Melkizedeki"(Ebra. 5: 5,6).

Lugha ya Waebrania kumhusu Melkizedeki haiwezi kuchukuliwa tu kwa maneno jinsi yalivyo. Ikiwa Melkizedeki kwa maneno halisi hakuwa na Baba wala mama, basi mtu pekee anaweza kuwa ni Mungu mwenyewe; ni mtu wa pekee asiye na mwanzo (1 Tim. 6: 16; Zab.90: 2). Lakini taarifa hii haikubaliani na Ebra 7: 4:"Angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu"na vile vile kwa ukweli wa kwamba watu walimuona (ambapo Mungu hawezi kuonwa) na alimtolea dhabihu Mungu. Ikiwa ameitwa mtu huyo, basi huyo ilimpasa kuwa na wazazi halisi. Yeye kuwa,"hana Baba, wala Mama, na wazazi"kwa hiyo inabidi kutaja ukweli kwamba ukoo wa babu na wazazi wake taarifa zao hazikuandikwa. Taarifa za wazazi wa Malikia Esta hazikuandikwa, kwa hiyo maisha yake ya nyuma yameelezewa kwa namna hii. Mordekai"alimlea …..Esta, binti wa mjomba wake: kwa kuwa hana Baba wala Mama …… nao walipokufa Baba na Mama yake, yule Mordeklai alimtwaa kuwa binti yake yeye"(Esta 2: 7).

Kitabu cha Mwanzo mara kwa mara kinatutambulisha kwa kirefu maisha ya mwanzo wa jamii na sifa zetu ambazo kitabu kinatuonyesha. Bali Melkizedeki anatokea bila kutamkwa, bila taarifa za wazazi wake, na kupotea kwenye maelezo kulingana kusiko tazamiwa. Hata hivyo hapawezi kuwepo shaka kwani alistahili heshima kubwa kabisa; hata Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao Wafalme, akambariki, ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote, jambo hili linaonyesha wazi ubora wa Melkizedeki kumpita Ibrahimu (Ebra. 7:2, 7).

Paulo sio anafanya tu mazoezi ya akili na Maandiko. Lilikuwepo tatizo kweli kabisa katika karne ya kwanza ambalo mashindano ya maneno ya kuweza kutatuliwa kuhusu Melkizedeki. Wayahudi wanahoji:'Ninyi Wakristo tuambieni kama huyu Yesu sasa anaweza kuwa kuhani wetu mkuu, mwenye kutoa maombi yetu na matendo yetu kwa Mungu. Lakini kuhani inampasa ukoo wake ujulikane, akithibitishwa katoka kabila ya Lawi. Na kwa vyovyote, ninyi wenyewe mnakiri Yesu alitoka kabila ya Yuda (Ebra. 7: 14). Tunasikitika, kwetu sisi Ibrahimu ndiye Kiongozi wetu mkuu na mfano (wa kuufuata) (Yn. 8: 33, 39), hatutamheshimu huyu Yesu'.

Kwa hiyo Paulo anajibu:

‘Lakini mkumbukeni Melkizedeki. Taarifa ya kitabu cha Mwanzo imetengenezwa ili kuonyesha kwamba kuhani huyu mkuu hakuwa na ukoo wa babu yeyote; naye Masihi kwa pande zote mbili anakuwa mfalme na kuhani, ambaye ukuhani wake ni wa kufuata mfano mzuri wa Melkizedeki (Ebra. 5: 6; Zab. 110: 4). Ibrahimu alikuwa na cheo kidogo kuliko Melkizedeki,hivyo mpindue mkazo wenu utoke kwa Ibrahimu hadi kwa Yesu, na muache kuleta maswali ya nasaba - ukoo kuwa ni ya lazima (tazama 1 Tim. 1: 4). Ikiwa mnatafakari ni kiasi gani Melkizedeki yeye ni mfano wa Yesu (yaani, habari zake moja moja zililenga mbele kwake), ndipo mngekuwa na ufahamu mkubwa wa kazi za Kristo’.

Na sisi wenyewe hili liwe somo letu.


  Back
Home
Next