Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

7.4 "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno"

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo"(Yn. 1: 1-3).

Mistari hii, inapoeleweka vema, huthibitisha na kufunua mawazo ambayo yamefikiwa katika sehemu ya mwisho. Ingawa hivyo, fungu hili la maneno ni mojawapo lisiloeleweka zaidi sana kuwa linafundisha ya kwamba Yesu alikuwako mbinguni kabla ya kuzaliwa. Kuelewa kwa usahihi mistari hii kunahusiana na kukubali nini maana ya"Neno"lenyewe. Halimtaji mtu moja kwa moja, kwa sababu mtu hawezi kuwa"na Mungu"halafu awe ni Mungu wakati huo huo. Neno la Kiyunani'Logos’ ambalo limetafsiriwa hapa"neno"ndani yake lenyewe halina maana'Yesu’ Aghalabu limetafsiriwa kuwa"neno", lakini vile vile kuwa ni: -

Maelezo      Kusudi

Kupasha habari      Elimu au Mafundisho

Nia      Kuhutubu

Hoja      Methali

Habari

"Neno"halina maana kumtaja Yesu, ingawa'Logos’ ni la kiume katika Lugha ya Kiyunani. Kwa Kiingereza ni'he’. Tafsiri ya Kijerumani (Luther) husemwa"das Wort"(si kiume wala kike); tafsiri ya Kifaransa (segond) inasema"la parole"ya upande wa kike, inaonyesha kwamba"Neno"halina lazima ya kujulisha mtu mume.

"HAPO MWANZO"

‘Logos’ kwa nguvu laweza kutaja wazo la moyoni ambalo limeelezwa kwa upande wa nje kwa maneno na kupashana habari kwingine. Hapa mwanzo'Logos’ alikuwa nayo Mungu. Nia hii isiyokuwa ya kawaida kiini kilikuwa kwa Kristo. Tumeonyesha jinsi Roho ya Mungu inavyoweka mawazo yake yatende kazi, hapa ni muungano kati ya Roho yake na Neno lake (tazama sehemu ya 2.2). Roho ya Mungu ilipotimiza mpango wake kwa watu na kuvuviwa neno lake liandikwe tangu mwanzo, kwa hiyo lilipasha wazo la habari ya Kristo katika kutenda kazi yake na maneno. Kristo alikuwa'Logos’ wa Mungu, basi Roho ya Mungu ilieleza mpango wa Mungu wa Kristo kwa shughuli zote. Hizi zinaeleza sababu za matukio mengi yaliyo katika Agano la Kale ni ya mfano hasa wa Kristo. Walakini, haliwezi kukaziwa zaidi kwamba Kristo kwa utu hakuwa"neno"; lilikuwa ni mpango wa Mungu wa wokovu kwa njia ya Kristo ambaye alikuwa"neno".'Logos’ ("Neno") mara nyingi sana limetumika kuhusu Injili inayomhusu Kristo. k.m"neno la Kristo"(Kol.3: 16; Math. 13:19; Yn.. 5:24; Mdo. 19: 10; 1 Thes 1: 8 n.k). Fahamu kuwa'Logos’ linamhusu Kristo, kuliko yeye mwenyewe binafsi. Kristo alipozaliwa, hili"neno"liligeuka na kuwa umbo lenye mwili na damu -"neno alifanywa mwili"(Yn.. 1: 14). Yesu binafsi alikuwa ni neno lililofanywa mwili kuliko kuwa"neno"; yeye binafsi alikuwa"neno"kwa kuzaliwa na Mariamu, sio alikuwa vingine wakati wowote wa kwanza.

Mpango, au ujumbe, unamhusu Kristo ulikuwa na Mungu tangu mwanzo, lakini uliwekwa wazi katika utu wa Kristo, na kuhubiri Injili inayomuhusu yeye kwenye karne ya kwanza. Hivyo Mungu alitangaza neno lake kwetu kwa njia ya Kristo (Ebra. 1: 1, 2). Wakati mwingine tena umetiwa mkazo wa kwamba Kristo alitangaza neno la Mungu na alitenda miujiza kwa amri ya neno la Mungu ili kumfunua Mungu kwetu (Yn.. 2: 22; 3: 34; 7: 16; 10: 32, 38; 14 10,24).

Paulo alitii agizo la Kristo kuhutubu Injili inayomhusu yeye"kwa mataifa yote"."Kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawa sawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele, ikadhihirika wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu"(Rum. 16: 25,26; 1 Kor. 2: 7).

Uzima wa milele umewezeshwa tu kwa mtu, kwa njia ya kazi ya Kristo (Yn.. 3: 16; 6: 53); lakini hapo mwanzo Mungu alikuwa na mpango huu wa kumpa mwanadamu uzima wa milele, akijua kama alivyofanya dhabihu ambayo Yesu aliifanya. Ufunuo timilifu wa toleo lile ulikuja tu baada ya kuzaliwa na kifo cha Yesu:"Uzima wa milele ambao Mungu …… alifunua neno lake (la uzima) katika ujumbe"(Tito.1: 2, 3) Tumeona jinsi manabii wa Mungu wanavyosemwa kuwa wanaishi siku zote (Luk. 1: 70) katika maana ya kwamba"neno"walilolitangaza lilikuwako na Mungu tangu mwanzo.

Mahubiri ya mifano mingi yalifunua mambo haya; kwa hiyo alitimiza unabii unaomhusu yeye mwenyewe,"Nitafumbua kinywa changu kwa mifano; Nitayatamka yaliyosotirika tangu awali - yaani tangu mwanzo wa ulimwengu"(Math. 13: 35). Ilikuwa ni kwa maana hii ya kuwa"neno alikuwa na Mungu ……. Hapo mwanzo"ili"lifanyike mwili"Kristo akazaliwa.

"NENO ALIKUWA MUNGU"

Sasa tupo katika nafasi ya kupima ni kwa namna gani "neno alikuwa Mungu". Mipango yetu na mawazo kwa sehemu ya muhimu ni yetu.'Ninakwenda Uingereza ni'neno’ au kupasha habari inayoeleza kusudi langu, kwa sababu ni nia yangu. Vivyo hivyo mpango wa Mungu kwa Kristo unaweza kueleweka hivi."Maana (mtu) aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo"(Mithali 23: 7), naye Mungu aonavyo, ndivyo alivyo. Basi neno la Mungu au fikira ni Mungu:"neno lilikuwa na Mungu". Kwa sababu hii upo muungano ulio karibu sanan kati ya Mungu na neno lake: kama usambamba wa Zaburi 29: 8 ni mmoja:"Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwani; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi".Taarifa kama"ninyi hamkunisikiliza, asema Bwana"(Yer. 25: 7) ni ya kawaida katika manabii. Kwa matokeo ya Mungu ana maana"ninyi hamjasikiliza neno langu lililonenwa na manabii"Daudi alichukuwa neno la Mungu kuwa taa yake na mwanga (Zab. 119: 105), lakini pia alisema:"Wewe u taa yangu, Ee Bwana: Na Bwana ataniangazia giza langu"(2 Sam. 22: 29), usambamba kati ya Mungu na neno lake unaonekana. Kwa sababu hii, linaeleweka kuwa neno la Mungu limeitwa kama vile ni mtu yeye mwenyewe, yaani, limesemwa kana kwamba ni mtu ingawa sivyo (tazama sehemu inayoitwa kuacha kitambo kilichokuwa kinaandikwa sehemu ya 5'Jambo la kuita kitu kama vile ni mtu’).

Mungu ni kweli yenyewe (Yn. 3: 33; 8: 26; 1Yoh. 5: 10), na kwa sababu hii neno la Mungu ni kweli pia (Yn. 17: 17). Kwa jinsi hii Yesu mwenyewe anajitambulisha kwa maneno yake yanayokaribiana sana hata neno lake analitamka kama vile ni mtu:"Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililonena ndilo litakalo mhukumu siku ya mwisho"(Yn. 12: 48). Yesu anatamka neno lake kama ni mtu hasa, yaani, mwenyewe. Maneno yake yameitwa kama kwamba ni mtu, kwa sababu yalijumuika kwa karibu na Yesu.

Vile vile neno la Mungu limetamkwa kana kwamba ni mtu, yaani, Mungu mwenyewe, kwa Yohana 1: 1-3. Tumeambiwa kuhusu Neno hivi,"Vyote vilifanyika kuwa huyo"(Yn. 1: 3). Ingawa hivyo"Mungu aliumba"vyote kwa neno lake alililoamuru (Mwa. 1: 1). Kwa sababu hii, Neno la Mungu limesemwa kama vile ni Mungu mwenyewe. Kutokana na jambo hili la maana ya Ibada, inatakiwa kujua kwamba kwa njia ya neno lake kuwamo mioyoni mwetu, Mungu anaweza kutukaribia sana.

Ni bayana toka Mwanzo 1 ya kuwa Mungu aliumba, kwa kutumia neno lake, sio Kristo binafsi. Lilikuwa neno ambalo limesemwa limefanya vyote, kuliko Kristo mwenyewe (Yn. 1: 1 -3)."Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika; na jeshi lake lote (yaani, nyota) kwa pumzi ya kinywa chake …….. maana yeye alisema, ikawa"(Zab. 33: 6,9). Hata sasa ni kwa neno lake hata viumbe vya asili vinatenda kazi:"Huipeleka amri yake juu ya nchi: Neno lake lapiga mbio sana. Ndiye atoaye theluji kama sufu ……. Hulituma neno lake ….. maji yakatiririka"(Zab. 147:15 -18).

Neno la Mungu likiwa nguvu yake kuumba, alilitumia kumzaa Yesu toka tumbo la Mariamu. Neno, mpango wa Mungu limewekwa katika shughuli maalumu kwa Roho yake Mtakatifu (Luk. 1: 35), likafanya itunge mimba ya Kristo. Mariamu alitambua hili kwa kuitikia kwake habari kuhusu kutungwa mimba ya Kristo iliyokuwa inakuja:"Na iwe kwangu kama ulivyosema neno lako"(Luk. 1: 38).

Tumeona kwamba Neno /Roho ya Mungu imeleta kusudi lake, ambalo lilitangazwa kwenye Agano la Kale lote. Kiwango ambacho hii ni kweli kimeonyeshwa katika Matendo 13: 27, mahali ambapo Yesu amesemwa anasawazishwa na maneno ya manabii wa Agano la Kale:"(Wayahudi) hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii"Kristo alipozaliwa, Neno /Roho yote ya Mungu ilielezwa na mtu Yesu Kristo. Kwa kuvuviwa, mtume Yohana alifurahi mno jinsi gani mpango wa Mungu wa uzima wa milele ulivyoelezwa na Kristo, ambaye wanafunzi waliweza wao wenyewe kupapasa na kuona. Basi, alitambua ya kuwa walikuwa wanalipapasa Neno la Mungu, mpango mzima wa wokovu unaopatikana kwa Kristo (1 Yoh. 1: 1-3) Wakati sisi wenyewe hatuwezi kumwona Kristo, nasi vile vile, tunaweza kufurahi kwamba kwa kumfahamu hakika yeye, tunaweza kufahamu kusudi lake Mungu kwetu na kwa sababu hiyo kuwa na uhakika wa uzima wa milele (1 Pet. 1: 8,9). Imetupasa tujiulize swali sisi wenyewe:'Je ! ni kweli namjua Kristo ?. Kukubali tu kwamba mtu mzuri aitwaye Yesu aliwahi kuishi hakutoshi. Kwa kudumu, kuomba dua na kujifunza Biblia, inawezekana kwa haraka kumfahamu kuwa ni mwokozi wako na kujihusisha wewe mwenyewe naye kwa kubatizwa.

Maelezo mafupi chini ya ukurasa:"Hapo mwanzo kulikuwako Neno"huenda linafafanushwa wazo la Wayahudi kuwa Torati (Vitabu vitano vya Musa) vilikuwako kabla ya uumbaji. Yohana 1: 1-3 inasema ya kwamba jambo la muhimu kuelewa ni kuwa maneno hayo ya Mungu yalitabiri kumhusu Yesu; mpango wa Mungu kumhusu yeye ulikuwako kabla ya uumbaji (Luk. 1: 70).


  Back
Home
Next