Tumeacha Kitambo sehemu ya 25: "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58)
Maneno haya mara nyingi yametumiwa vibaya ya kwamba Yesu alikuwako kabla ya Abrahamu kuwepo. Ingawa hivyo, uchunguzi wa karibu unadhihirisha ukweli upo kinyume.
Yesu hasemi"Yeye Abrahamu asijakuwako, mimi nilikuwepo"Alikuwa ni mtoto aliyeahidiwa Abrahamu; ikiwa tunasema ya kwamba kimaumbile Yesu alikuwepo kabla ya wakati wa Abrahamu, ahadi alizoahidiwa Abrahamu tunazifanya zisiwe na maana.
Maneno yenyewe kwa Yohana 8: 58 ni mazungumzo ya Kristo na hao Wayahudi kuhusu Abrahamu. Kwa kadiri walivyohusika, Abrahamu alikuwa mtu mkuu ambaye ataishi. Yesu anasema"Mimi hivi sasa, kama ninavyosimama hapa, ni wa muhimu zaidi kuliko Abrahamu". Kama walivyosimama pale, Yesu alikuwa ni mtu wa kuheshimiwa kuliko Abrahamu. Anasema'Mimi ni wa muhimu sasa zaidi kuliko alivyo Abrahamu’ Inawezekana kuelewa neno"kabla"lililo katika Yohana 8:58 pamoja na kutaja wakati mwingine, katika maana ya kwamba kabla ya kuwapo Abrahamu, Kristo alikuwemo ndani ya mpango wa Mungu tangu mwanzo kabisa wa ulimwengu. Ilikuwa ni sababu ya Yesu kuwapo"kabla"ya Abrahamu katika maana hii ya kwamba alikuwepo"kabla"yake kwa umuhimu wake.
Neno la kuthibitisha linapatikana katika Yohana 8: 56;"Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile alivyoiona siku yangu, naye akaiona, akafurahi". Muda pekee ambao Ibrahimu amesemwa alicheka na kufurahi moyoni ni pale alipopewa ahadi ya kuwa kwake atazaliwa mtoto; alifahamu kwamba mwishowe hiyo ahadi ilikuwa inamtaja Yesu (Mwa. 17: 17). Ibrahimu"aliona"mbele kwa Kristo alivyoahidiwa ahadi kumhusu Yesu. Katika maana isiyoeleweka kirahisi alitoa ufafanuzi kuhusu dhabihu ya Yesu kwa wakati uliokuwa unakuja:"Katika mlima wa Bwana itapatikana"(Mwa. 22: 14). Ilikuwa ni katika maana hii ambayo Yesu anamsema Ibrahimu kama alimwona. Ni kwa maneno haya ya kuzungumzia kuhusu ahadi ambayo Yesu aliweza kusema "Kabla ya Ibrahimu kuwako, mimi niko". Alielewa kama tulivyokwisha eleza katika sehemu ya 3. 1 ya kuwa ahadi ambazo Mungu alimwahidi Ibrahimu zilikuwa zinafunua mpango kumhusu Yesu ambao Mungu alijua tangu mwanzo wa ulimwengu. Shabaha hiyo, iliyokuwepo"Kabla ya kuwako Ibrahimu", ilifunuliwa kwa Ibrahimu kwa ahadi alizoahidiwa, na sasa zilitimilika machoni pa Wayahudi wa karne ya Kwanza, waliposimama makutano kumzunguka Yesu,"neno (la ahadi) lililofanywa mwili".
Mara nyingi imedaiwa Yesu anataja katika kusema Jina la Mungu anaposema"Mimi niko". Tulieleza katika Tumeacha tulichokuwa tunaandika sehemu ya 3 ya kuwa Yesu na watu wa kawaida kweli wanaweza kuchukua Jina la Mungu, pasipo maana hii ya kwamba wao ni Mungu mwenyewe katika mtu. Walakini, inaweza kuwa kwamba Yesu anatumia kiarifa cha wakati uliopo'kuwa'. Muundo wa maneno mamoja kwa Kiyunani unatokea katika Yn. 9: 9 mistari michache inayofuata. Majirani wa yule mtu kipofu aliyeponywa waliulizana ikiwa kweli alikuwa mtu yule aliyekuwa akikaa na kuomba:"Wengine walisema, huyu ndiye: wengine walisema, Amefanana naye: Lakini yeye mwenyewe alisema, Mimi (ndiye). Hivyo mtu kipofu anasema"Mimi", kiasi kama Yesu aliposema"mimi niko"anathibitisha kwamba yeye ni Mungu kabisa, Basi inatubidi tuseme kwamba naye kipofu pia alikuwa"Mungu kabisa". Lakini, inafaa kujua kwamba Yahweh - au Kiswahili YAHU Jina la Mungu, kwa kweli maana yake ni"Mimi nitakuwa ambaye mimi nitakuwa"(Kut. 3:14 - kwenye pambizo la Biblia ya Kiingereza ya R.S.V. na R.V) kuliko kuwa "Mimi niko".
|