Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 22: Yesu wa Historia

Ikiwa, kama wengine wanavyodai, hakuna ushaidi wa kwamba Yesu wa Nazareti aliwahi kuishi, basi kuwepo kabisa Ukristo ni vigumu kueleza. Ni kuuliza jumla ya vitu vyote vikubwa kwa kutegemea mtu yeyote aamini kwamba mamilioni ya watu zaidi ya miaka 2,000 iliyopita wameweka imani zao kwa mtu fulani ambaye hakuwako, na kuwa na mkazo wa imani hii kwake hata wakakusudia kueneza imani yao kuhusu yeye ulimwenguni pote, aghalabu kwa hatari ya mateso na mauti. Wakristo na Wayahudi kwa ujumla hawana shida kukubali kuwa Mohamedi aliwahi kuwapo, ingawa wanakataa kazi yake na mafundisho. Kwa kweli tunakubali kuwa watu mashuhuri sana wa historia walikuwako bila kuhitaji kutazama tena kwa kuchunguza ushahidi. Mara nyingi uchambuzi umefanywa kwa upana wa matokeo yanayofahamika ya historia, k.m. ile vita ya Hastings ambayo ilifanyika mwaka 1066, ushahidi madhubuti umepatikana kwa kadiri ya ugumu kuupata kwa bahati.

Ni jambo la hakika kwamba kwa nguvu wanakana hivi kabisa kuwahi kuwako Yesu wa Nazareti hapana shaka ni kuuliza maswali ya jambo la uhakika kupita hali iliyotendwa, kutaka kutafuta udhuru wa kufaa kutokubali sababu zake kuwako na kufahamu kazi yake Masihi. Hili hasa linaonekana kweli inapofahamika kwamba wao wenyewe Wayahudi wa kwanza walikubali kuwa mtu aitwaye Yesu aliwahi kuishi katika karne ya kwanza. Ushahidi ufuatao wa historia ya kuwahi kuwako Yesu wa Nazareti unaonyesha kwamba hauwezi kuondoshwa kama theologia ya uvumbuzi wa watu. Taarifa nyingi za kusaidia katika sehemu hii ni habari zilizopatikana toka kwa Gary Hebermas,'Ushahidi wa Kale wa maisha ya Yesu’.

1). Ticitus alikuwa mwana -historia wa Roma ambaye vitabu vyake vikubwa viwili kuhusu karne ya kwanza ("Annals"- taarifa ya uvumbuzi ulioandikwa mwaka kwa mwaka, na"Histories"- masimulizi ya historia) vyote viwili vinamtaja Yesu na Ukristo. Aliandika katika"Annals"(karibu mwaka 115 B.K.).

"Kundi la watu waliochukiwa kwa machukizo yao, walioitwa Wakristo na watu wa vivi hivi. Kristo ni jina limetokana na Christus asili yake, alipata adhabu kubwa mno wakati wa kipindi cha utawala wa Tiberio kwenye mikono ya mmoja wa maliwali wetu, Pontio Pilato".

Mfalme Tiberio alitawala toka mwaka wa 14 - 37 B.K., wakati ambao ni kipindi Kristo aliuwawa, kulingana na taarifa. Ticitus vile vile anaeleza jinsi imani ya kundi hili"Ilivyotokea sio katika Uyahudi pekee, chanzo cha kwanza (mambo haya), bali hata katika Rumi", anaendelea kueleza jinsi Wakristo walivyochukiwa sana, nao wengi wao waliuwawa katika mji wa Roma. Taarifa yote hii ya Yesu inalingana na taarifa ya Agano Jipya, Wafuasi na mitume wa kwanza walieneza mafundisho yao kwanza Uyahudi, na kisha katika ulimwengu wote wa Roma, pamoja na mji wa Rumi, kwa upinzani mkubwa kwao.

2.) Suetonius, mwandishi wa historia mwingine wa Kirumi, alitoa maelezo juu ya utawala wa Klaudio (41- 54 B K): "Kwa kuwa Wayahudi katika mji wa Roma walisababisha ghasia zilizoendelea kwa kuanzishwa Ukristo, yeye (Klaudio) aliwafukuza toka kwenye mji". Kwa kutokea, Matendo ya mitume 18: 2 yametolewa maelezo jinsi Wayahudi wawili Akila na Prisila iliwabidi waondoke Roma kwa sababu ya mateso ya Wayahudi. Suetorius alitoa maelezo baadaye kuhusu adha iliyowapata Wakristo kwenye kipindi cha Nero: Baada ya moto mkubwa kwenye mji wa Roma …….. vile vile Wakristo waliadhibiwa kwa kupigwa, jamii ya watu wanaokiri dini yenye imani mpya yenye kugombanisha". Ushahidi huu wa kuwako kundi la watu walioitwa"Wakristo"kwenye karne ya kwanza unadokeza kwamba mtu aliyeitwa"Kristo"aliwahi kuishi mapema katika hiyo karne.

3.) F.F. Bruce ("Mwanzo wa Ukristo"uk. wa 29, 30) unavuta macho kuangalia ukweli kwamba kuna ushahidi wa historia ya Mashariki mwa Bahari ya Mediterania iliyoandikwa na mwandishi wa mambo ya kale aliyeitwa Thallus kuhusu mwaka 52 B K. Bruce anaonyesha kila mahali ("Hati za Agano Jipya", uk. 113) ya kuwa mwanafunzi aliyeitwa jina Julius Africanus alinukuu toka kwa Thallus, akifanya mzaha maelezo yake ya giza Yesu aliposulubiwa ilikuwa sababu ya kupatwa kwa jua. Haya yanadokeza kwamba Thallus aliandika maelezo ya kusulubiwa Yesu kulikotokea miaka mingine kabla hajaandika historia yake mnamo mwaka 52 B.K.

4.) Pliny, afisa wa serikali ya Kirumi, ametajwa kwa kirefu kuwahi kuwako kwa kundi tendaji la watu walioitwa Wakaristo kwa miaka iliyofuata ya karne ya Kwanza. Kushika kwao ibada ya kumbukumbu yeye ameitaja:"Walikuwa na desturi ya kukutana siku halisi iliyopangwa kabla, ilipokuwa nuru, wakaimba mistari miwili ya wimbo wa kumsifu Kristo"("Nyaraka za Pliny", zilitafsiriwa na W. Melmoth, Vol. 2, x: 96). Watawala wa Kirumi Trajani na Hadriani wote wawili wametaja matatizo ya kushughulika na Wakristo. Kwa Ushahidi wa hili, tazama"Nyaraka za Pliny", Vol.2,x:97 na Eusebio’ Historia ya Ukasisi, IV: IX - moja - moja. Kuwako kwa kundi hili tangu karne ya kwanza na mshikamano wao wa ajabu wakati wa mateso ulidokeza kuwa walikuwa wafuasi wa tabia ya mtu wa historia ya kweli aliyeishi katika karne ya kwanza.

5.) Talmud, kitabu kitakatifu cha Wayahudi, katika Sanhedrin 43a kifo cha Yesu kimetajwa. Kimekubalika ya kwamba sehemu hii ya Talmud tarehe zake toka kipindi cha kwanza cha kitabu hicho kutungwa (yaani, mwaka 70 - 200 B.K)

"Siku kabla ya sikukuu ya Pasaka Yeshu (Yesu) alitundikwa msalabani. Kwa muda w a siku arobaini kabla ya kuuawa, habari ilitolewa ya kusema,'Atapigwa kwa mawe kwa sababu amefanya uchawi na kuvuta Israeli kukengeuka. Yeyote anayeweza kusema lolote kwa kumsaidida, aje mbele kwa niaba yake’. Lakini tangu hakuna chochote kilicholetwa mbele kwa kumsaidida akatundikwa kabla ya siku kuu ya Pasaka"

"Kuangikwa"linaweza kuwa ni namna ya neno la kusema kusulubiwa limetumika kama hivyo katika Agano Jipya (Gal. 3: 13; Luk. 23: 39). Fungu hili la maneno linaeleza Wayahudi wakitaka Yesu apigwe mawe (kulingana na sheria ya Musa, labda ?), bali yametajwa kuwa alitundikwa katika Agano Jipya jinsi gani Wayahudi iliwabidi watumie sheria za Kirumi kutoa kifo cha Yesu - ambacho cha kutundikwa.

Sanhedrin 43a vile vile inaeleza jinsi wanafunzi watano wa Yesu walihukumiwa na kupewa adhabu ya kifo, tena inaonyesha kwamba kwa mafundisho yaliyotokea zamani Wayahudi waliamini kuwahi kuwako Yesu wa historia. Hata Sanhedrin 106b yasema ya kuwa Yesu alikuwa na umri wa miaka 33 alipokufa; kikamilifu kama Agano Jipya lilivyodai. Maier ("Siku kuu ya kwanza ya kufufuka", uk. 117, 118) ananukuu toka hati ya Wayahudi karne ya kwanza"Toledoth Jesu", yenye kadhia ya kwamba wanafunzi walijaribu kuuiba mwili wa Yesu baada ya kufa, lakini mtunza bustani aliyeitwa Yuda aliposikia mipango yao aliuhamisha mwili wa Yesu na kuupeleka mahala pengine, akaukabidhi baadae kwa Wayahudi. Justin Martyr akiandika mnamo mwaka 150 B.K ameandika kwamba Wayahudi walituma wajumbe maalumu ili waseme ya kuwa mwili wa Yesu uliibiwa ("Dialogue with Trypho", 108), na Tertullian ("On Spectacles", 30) ana maelezo mamoja wakati alipoandika katika mwaka 200 B. K.

Kati yao ushahidi huu unaoendelea wa historia unaonyesha kwamba Wayahudi wa karne ya kwanza B.K waliamini aliwahi kuwako Yesu wa historia na alipata kifo cha nguvu.

6.) Mtunga hadithi wa Kiyunani, Luciana, akiandika katika karne ya kwanza, anawafanyia mzaha Wakristo ambao"wanamwabudu mtu hata leo (ambaye) alisulubiwa"(Lucian, The Death of Peregrine - yaani kifo cha mwendo usio mkunjufu, uk. 11-13, in"The works of Lucian"- katika kazi ya Lucian, Vol 4, iliyofasiriwa na Fowler wa Foweler).

7.) Josephus ni mwandishi wa historia anayejulikana vizuri sana wa karne ya kwanza. Katika"Antiquities"- yaani mambao ya Kale, aliyoandika mwaka 90 -95 B K, anamtaja Yakobo,"ndugu yake Yesu, aliyeitwa Kristo". Vile vile anasema katika sehemu nyingine ya kitabu hicho hicho kwa maneno ambayo ni wazi yanathibitisha picha ya Yesu katika Agano Jipya:"Mara hiyo ulikuwa karibu muda huu Yesu mtu mwenye busara ….. Maana alikuwa ndiye aliyefanya matendo magumu ya kustaajabisha ….. Alikuwa Kristo ….. aliwatokea akiwa yu hai siku ya tatu, kama manabii wa Mungu walivyotabiri hivi mambo ya ajabu mengine kumi elfu yanayo muhusu yeye".

Maneno haya yameonyesha hivyo kama wengine walivyodai kwamba ni nyongeza katika kitabu. Kama bado ipo sababu ya kutumia maneno haya kusaidia shauri la kwamba alikuwepo mtu aliyeitwa Yesu wa Nazareti aliyeishi katika karne ya kwanza yametokelewa mambo ambayo lazima yakumbukwe ifuatavyo:

  • Eusebio (Historia ya Kanisa la Kikristo, 1: XI) anainukuu sehemu hii ya Josephus.

  • Wanafunzi walioheshimika wanasaidia somo hili la kwanza kuwa ni la asili, laweza kuonyesha kwamba sehemu hii imeandikwa kwa mtindo ule ule unaofungamana na kazi ya Josephus (tazama kanuni za Danieli,"Ukimya wa Yesu, wa wakati ule ule"Uk. 21; J.N.D. Anderson,"Ukristo: Ushahidi wa Historia"uk. 20; F.F. Bruce,"Hati za Agano Jipya"uk. 108, 109)

  • Kwa haya haupo ushahidi wa maneno ya kitabu kuwa nyongeza kwenye kitabu.

  • Profesa Schlomo Pines amedai kwamba toleo kwa lugha ya Kiarabu la kazi ya Josephus limevumbuliwa ambalo karibu lilikuwa lenyewe ni la mwanzo. Maneno yaliyotajwa juu yanatokea humo, Lakini bila taarifa ya mafundisho ya wazi kuhusu ufufuo na Yesu kuwa Masihi ambayo yalifanywa kwa kunakiliwa. Haya yanaonekana ni ya maana, kwa kuwa Josephus alikuwa Myahudi: Pines aliyoyapata ya kwanza aliyaweka katika majarida ya"The New York Times", Februari 12. 1972, ndani yake ananukuu mabishano wa maneno ya Josephus kuhusu Yesu toka toleo la Kiarabu"Kwenye kipindi hiki alipokuwepo mtu mwenye busara aliyeitwa Yesu > Mwenendo wake ulikuwa mzuri na alikuwa mwema. Watu wengi miongoni mwa Wayahudi na wa mataifa mengine wakawa wafuasi wake. Pilato alimuhukumu asulubiwe na kufa. Nao wale waliokuja kuwa wafuasi wake hawakuacha kumfuata. Walitoa taarifa ya kwamba aliwatokea siku tatu baada ya kusulubiwa na ya kuwa alikuwa yu hai; kwa kulingana, labda alikuwa ni Masihi ambaye Manabii wamesimulia maajabu"

Kwa ubora maelezo haya yanalaiki kwa yale ya Agano Jipya.


  Back
Home
Next