Misingi Ya BIBLIA
Somo La 3: Ahadi za Mungu
Dibaji | Ahadi Katika Edeni | Ahadi Kwa Nuhu | Ahadi Kwa Abrahamu | Ahadi Kwa Daudi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12)., Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 10: Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza"

Wazo limetangulizwa mbele na mtu kama H.W. Armstrong katika 'Ukweli dhahiri’ wa muungano wa ahadi alizoahidiwa Abrahamu zimetimilika kwa Waingereza na watu wa Amerika, ambao, imedaiwa ni wa kabila la Efraimu na Manase. Washirika wa Uisraeli wa Uingereza wanaamini kwamba Wafalme na malkia wa Uingereza wametokea kwa Wayahudi walianza na mfalme Daudi ili kuhakikisha nadharia zao wameweza kusema kwamba Wayahudi wamekataliwa kuwa watu wa Mugnu na watu wa Uingereza wamechaguliwa badala yao.

Ikiwa tafakari ya somo la 3 limefuatwa, itakuwa dhahiri uwa kwa Biblia madai haya hayana ukweli wowote, yafuatayo ni machache kati ya alama nyingi zanyongeza zinazoweza kufanywa: -

  • Watu wote sawa sawa wapo chini ya laana ya dhambi (Rum.3: 23), na kwa hiyo kristo alikufa ili kuwezesha watu watokao mataifa yote wawe na nafsi ya wokovu. malezi ya taifa lolote tutokako siyo ya muhimu kama tumebatizwa katika Kristo na kuwa sehemu ya Israeli kiroho (Gal. 3:27 -29). tumeamriwa kuhubiri Injili kwa mataifa yote. na kubatiza aaminiye (Marko. 16:15,16); hivyo Israeli mpya inakuwa na watu watokao mataifa yote, siyo Uingereza tu.

  • Ni shida kuthibitisha asili ya watu wa Uingereza na Amerika; wao ni watu mchanganyiko toka sehemu nyingi za ulimwengu. kwa sababu tu mtu kazaliwa kwenye nchi hizo hakuna maana ya kuwa wao ni watu walio teuliwa na Mungu.

  • Uisraeli wa Uingereza unadaiwa kwamba baraka alizoahidiwa uzao wa Abrahamu zimetimizwa kwa watu wa Uingereza, bila kujali utii wao kwa Mungu. Hili ni jambo linalopingana na baraka za Mungu ni katika hali ya utii. sura zote za Law. 26 na Kum. 28 zaeleza baraka zitakazokuja juu ya Israeli kama wangetii neno lake, na laana itakayokuja kama hawatii. kudai kuwa Mungu ameipa Uingereza baraka hizi bila kujali utii wao kwa neno lake , na mara nyingi mbele yao huwa wepesi kuliasi, kwa kweli ni kufanya jeuri kwenye maneno ambayo Mungu anatoa baraka hizi.

  • Kidokezo cha kuwa Mungu amewatupilia mbali watu wake wa Israeli na badala yao amewaweka Waingereza kinaruka kwenye uso wa fungu la maneno kama Rum. 11: 1, 2: "Je ! Mungu amewasukumia mbali watu wake ? hasha !. Kwa kuwa mimi (Paulo) ni Mwisraeli, mmoja wa wazo wa Abrahamu, ….. Mungu hakuwa sukumia mbali watu wake aliowajua".

  • Ufalme wa Mungu ulikuwa ni ufalme wa Israeli zamani (2 Nyak.9:8). ulipinduliwa kwa kutotii, Lakini ufalme utarudishwa tena (Ezek. 21: 25 -27).Ufalme utarudi Yerusalemu (Mika. 4:8) Yesu atakapo tawala juu ya kiti cha Enzi cha Daudi (Luka. 1:32). Watu wa Israeli wa sasa ambao wametawanyika watakusanywa tena toka sehemu mbali mbali za dunia walikotawanyika: "Nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda na kuwaleta kwenye nchi yao wenyewe. nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi yao, juu ya milima ya Israeli" (Ezek. 37: 21,22). Unabii huu umetimia kwa namna Wayahudi asili walivyorudi nchini kwao; utimilifu kamili utakuwa katika ufalme, kurudi kwa Israeli waliopo kwenye nchi yao kunaonyesha itabidi kuja mapema huu ufalme.

Maelezo chini ya ktabu: Wale ambao hasa wamependezwa katika habari hii wanaweza kupata kitabu cha bure, 'Uisraeli wa Uingereza Umepimwa’, kinapatikana kwa wachapishaji.


  Back
Home
Next