Misingi Ya BIBLIA
Somo La 3: Ahadi za Mungu
Dibaji | Ahadi Katika Edeni | Ahadi Kwa Nuhu | Ahadi Kwa Abrahamu | Ahadi Kwa Daudi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12)., Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza") | Maswali

3.5 Ahadi Kwa Daudi

Daudi, kama Abrahamu na wengine wengi wapokeaji wa ahadi za Mungu, hawakuwa na maisha rahisi. Alikuwa ni kijana mdogo wa mwisho katika jamaa kubwa ambaye, katika Israeli 1000 K.K., ilimaanisha kuchunga kondoo na kukimbia safari fupi za kupeleka ujumbe au kitu kwa ndugu zake wakubwa wapendao kidogo kuwa na mamlaka (1 Samweli sura ya 15 hadi 17). Katika kipindi hiki alijifunza kufika kumwamini Mungu ambaye watu wachache tangu wakati ule walimkaribia.

Siku ikafika hapo Israeli walipokabiliwa na shindano la mwisho toka kwa majirani zao wenye kuanzisha ugonvi , Wafilisti; walitakiwa wapeleke mmoja k ati yao apigane na jitu kubwa - Goliati ; Mfilisti aliyekuwa wa kwanza kujitokeza akifahamu kuwa yeyote atakayeshinda atamiliki juu ya upande unopoteza pigano. Kwa msaada wa Mungu Daudi akamshinda Goliati kwa kutumia kombeo, lililompatia umaarufu mkubwa kuliko mfalme wao (Sauli). "Wivu ni mkali kama ahera (Kaburi)" (Wimbo ulio bora 8:6). maneno yaliyothibitisha kuwa kweli kwa mateso aliyopata Daudi toka kwa Sauli kwa miaka 20 iliyofuata akimwinda kama panya huko na huko jangwani kusini mwa Israeli.

Hatimae Daudi akawa mfalme, na kuonyesha shukrani zake kwa upendo wa Mungu wake katika maisha yake nyikani, akaazimia kujenga hekalu la Mungu. Jibu toka kwa Mungu likawa mwanae Daudi, Suleimani akawa ndiye atakayejenga hekalu na ya kuwa Mungu alitaka kumjengea nyumba Daudi (2 Sam. 7:4 -13). Ndipo yakafuata maelezo ya ahadi yanayorudia na mambo mengi aliyoambiwa Abrahamu, ambapo pia yalijaa katika maelezo mengine:-

"Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, naye atakuwa mwanangu. Akitenda maovu, nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya mwanadamu, lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwaondolea Sauli, niliyemwandoa mbele yako. Na nyumba yako, na ufalme wako,vitadhibitishwa milele mbele yako: nacho kiti chako kitafanywa imara milele" (mstari wa 12 -16).

Toka masomo yetu yaliyotangulia tulitazama "Mzao" kuwa ni Yesu. Maelezo yake kuwa ni mwana wa Mungu (2 Samweli 7:4) yanathibitisha hivi, kama yafanyavyo mengine yanayomtaja katika sehemu zingine za Biblia :-

"Mimi ….. shina la mzao wa Daudi", Yesu alisema (Uf. 22:16).

"(Yesu), aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili" (Rum. 1:3)

"Katika uzao wake mtu huyo (Daudi) Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaana Yesu, kama alivyoahidi" (Mdo. 13:23).

"Malaika alimwambia Bikra Mariamu kuhusu mwanae Yesu: "Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi Baba yake (babu) yake …… ufalme wake hautakuwa na mwisho"(Luka. 1:32,33) Hii ni ahadi inayotumika kwa mzao wa Daudi, katika 2 Sam.7:13, kwa Yesu.

Pamoja na uthabiti wa mzao amejulikana kuwa ni Yesu, idadi ya maelezo sasa yamekuwa ni yenye maana : -

1) MZAO.

"Mzao wako …… atakayetoka viunoni mwako …… nitakuwa Baba yake, naye atakuwa mwanangu" " ……Wazao wa mwili wako nitawaweka katika kiti chako cha enzi" (2 Sam 7:12,14 ; Zab. 132: 10,11). Yesu, mzao, hasa alitoka kwa jinsi ya mwili kwa watoto wa Daudi, bali Mungu akiwa ni Baba yake. Jambo hili linawezekana tu kwa kuzaliwa na Bikira kama alivyoelezwa katika Agano Jipya; Mama yake Yesu alikuwa Mariamu, aliyetoka katika ukoo wa Daudi (Luka.1:32), lakini hakuwa na Baba mwanadamu. Mungu alifanya muujiza katika tumbo la Mariamu kwa njia ya Roho Mtakatifu ili kumzaa Yesu, basi Malaika alitoa ufafanuzi "Kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu’ (Luk. 1:35). "Kuzaliwa na Bikira" ilikuwa ndiyo njia pekee ya Ahadi hii aliyoahidiwa Daudi kuweza kutimia vema.

2) NYUMBA.

"Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu" (2 Sam. 7:13) inaonyesha kuwa Yesu atajenga Hekalu la Mungu - mwili halisi na la Kiroho. Ezekieli 40 -48 ni sura zinazoeleza jinsi Milenia (Miaka 1000 ya kwanza ya ufalme wa Mungu baada ya Yesu kurudi Duniani) hekalu litajengwa Yerusalemu. 'Nyumba’ ya Mungu ni mahali anapopenda kuishi, na Isaya 66: 1,2 tunaambiwa kuwa alikuja kuishi katika mioyo ya watu walio wanyenyekevu wa neno lake. Basi Yesu anajenga Hekalu la kiroho ili Mungu akae ndani, linaloundwa na waamini wa kweli. Maelezo yanamsema Yesu kuwa jiwe la msingi wa hekalu la Mungu (1 Pet. 2:4 -8) na wakristo ni mawe ya hekalu (1 Pet. 2:5) yanayopangwa sasa katika nafasi.

3) KITI CHA ENZI

"Nacho kiti cha enzi cha ufalme wake (Kristo) nitakifanya imara milele ….. nyumba yako (Daudi) na ufalme wako ….. kiti chako kitafanywa imara milele (2 Sam.7: 13,16 ; Isaya 9: 6,7)". Basi ufalme wa Kristo utakuwa juu ya ufalme wa Daudi wa Israeli; ina maana kwamba ufalme wa Mungu unaokuja utaanzisha tena ufalme wa Israeli - ona somo la 5.3 zaidi kuhusu huu. kwa kutimiza ahadi hii, Kristo itambidi atawale "kiti cha enzi" cha Paulo, au mahali pa utawala. huu utawala wenyewe ulikuwa Yerusalemu. Huu ni ushahidi mwingine wa kuwa ufalme itabidi uanzishwe hapa duniani ili kutimiza ahadi hizi.

4) UFALME

"Nyumba yako na ufalme wako vitathibitishwa imara milele mbele yako" (2 Sam.7:16 mstari unadokeza ya kuwa Daudi atashuhudia kuanzishwa kwa ufalme wa milele wa Kristo. kwa hiyo ahadi hii haikuwa ya moja kwa moja, hata atakapofufuliwa Kristo atakaporudi ndipo ataweza kuona kwa macho yake mwenyewe ufalme ukisimamishwa ulimwenguni pote, na Yesu akiwa anatawala tokea Yerusalemu.

Mambo haya aliyoahidiwa Daudi ni ya muhimu kabisa kufahamu. kwa furaha Daudi aliyasema mambo haya kuwa ni "Agano la milele …..maana ni wokovu wangu wote, na shauku yangu yote" (2 Sam. 23:5). mambo haya yanataja wokovu wetu pia; Kuyafurahia kuwa shauku yetu yote. Hivyo tena maana imeyafanya haya mafunzo kuwa muhimu. Ni jambo liletalo huzuni kama Wakristo kufunza mafundisho yanayopingana kabisa na ukweli huu wa ajabu :-

  • Ikiwa Yesu mwenyewe "aliwahi kuwepo kabla" yaani alikuwepo kabla ya kuzaliwa, basi hizi ahadi hazina maana hata Yesu awe "Mzao" wa Daudi, au kuwa mtoto.

  • Ikiwa Ufalme utakuwa mbinguni , basi Yesu hawezi tena kuanzisha ufalme wa Daudi wa Israeli, wala kuweza kutawala toka kwenye 'Kiti cha enzi’ cha daudi au mahali pa utawala. Mambo haya hasa yenyewe yalikuwa Duniani, na hivyo tena kuyaanzisha tena inabidi iwe ni mahali pale pale.

YALITIMIA KWA SULEMANI ?

Mwana halisi wa Daudi, Suleimani, alitimiza sehemu ya ahadi alizoahidiwa Daudi. Akajenga hekalu halisi la Mungu (1 Fal. 5 -8), akawa na ufalme uliostawi sana. Mataifa toka pande zote yalituma wawakilishi wa kutoa heshima kwa Sulemani

(1 Fal. 10), na kukawa na baraka kubwa za kiroho kutokana na kutumia hekalu. kwa hiyo utawala wa Sulemani ulilenga kwa kuonyesha mbele kwenye utimilifu mkubwa zaidi wa ahadi alizoahidiwa Daudi utakaoonekana katika ufalme wa Kristo.

Wengine wamedai kwamba ahadi kwa Daudi zilitimia kabisa kwa Sulemani, lakini hii inakanushwa na yafuatayo: -

  • Ushahidi mwingi wa Agano Jipya unaonyesha kuwa 'Mzao’ ni Kristo, siyo Sulemani.

  • Daudi anaonekana akiunga ahadi alizo ahidiwa na zile zilizofanywa kwa Abrahamu. (1 Nyakati.17:27 Mwa. 22:17,18:).

  • Ufalme wa'Mzao’ hautakuwa na mwisho - wa Sulemani ulikuwa na mwisho.

  • Daudi alitambua kuwa ahadi zilikuwa zinahusu uzima wa milele, ambapo zinapinga kabisa kutaja yeyote wa jamaa yake ya karibu: "sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA; lakini amefanya nami Agano la milele" (2 Sam. 23:5).

  • Mzao wa Daudi ni masihi, Mwokozi wa watu toka dhambi (Isaya 9:6,7; 22:22; Yer. 33:5,6,15; Yoh. 7:42). bali Sulemani alimwacha Mungu baadaye (1 Fal. 11: 1 -3' Neh. 13:26) kwa sababu ya kuoana na walio nje ya tumaini la Israeli.


  Back
Home
Next