Misingi Ya BIBLIA
Somo La 3: Ahadi za Mungu
Dibaji | Ahadi Katika Edeni | Ahadi Kwa Nuhu | Ahadi Kwa Abrahamu | Ahadi Kwa Daudi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12)., Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza") | Maswali

3.1 Dibaji

Kwenye hatua hii ya masomo yetu tumefikia kufahamu upana wa Mungu ulivyo na jinsi anavyofanya kazi kwa kufanya hivyo tumepanga idadi ya makosa yahusuyo mambo haya. Sasa tunataka kuangalia kwa uhakika zaidi mambo ambayo Mungu "amewaahidi wampendao" (Yakobo 1:12; 2:5) kwa kushika amri zake (Yah. 14:15)

Ahadi za Mungu katika Agano la kale zinatumaini la Kikristo ndani yake. Akijitetea hukumuni, Paulo alizungumzia thawabu ijayo iliyomfanya awe tayari kupoteza vitu vyote: "Na sasa nasimama hapa nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi ya baba zetu …….. nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo" (mdo. 26:6,7). alitumia muda mwingi wa maisha yake kuhubiri "Habari njema (Injili), jinsi Mungu alivyofanya ahadi kwa mababa, Mungu amewatimizia …… kwa kumfufua Yesu" (mdo. 13:32,33). Paulo alieleza kuwa kuamini hizo ahadi kulitoa tumaini la ufufuo toka wafu (mdo. 26:6 -8 na 23:8). Kufahamu kuja kwa pili yesu kwa hukumu na ufalme wa Mungu ujao (Mdo. 24:25; 28:20, 31).

Ahadi zote hizi zinadhamisha hadithi ya kuwa Agano la kale ni historia tu iliyotembea ya Israel isiyousema uzima wa milele. Mungu hakuamua ghafla miaka 2000 iliyopita kuwa atatupatia uzima wa milele kwa njia ya Yesu. Ni kwamaba kusudi lilikuwa naye tangu mwanzo.

"Katika tumaini la uzima wa milele, ambako Mungu asiyeweza kusema uongo, aliuahidi kabla ya ulimwengu kuanza;akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe kwa kuhubiri" (Tito 1:2,3). "Ule uzima wa milele, uliokuwa na Baba, ukadhihirika kwetu"(1 Yoh. 1:2)

Kwa kuwa kusudi la Mungu la kuwapa watu wake uzima wa milele lilikuwa naye tangu mwanzo , haikuwa na maana kuwa angebakia kimya kuhusu huo wakati wa miaka 4000 ya kujishughulisha na watu taarifa iliyo katika Agano la Kale. Kwa kweli, Agano la kale limejaa ahadi na unabii ambazo kila moja inatoa maelekezo ya tumaini hili ambalo Mungu amewatayarishia watu wake.

Ni kwa sababu hii ya kuwa kutambua ahadi za Mungu kwa mababa wa Wayahudi ni za muhimu kwa wokovu wetu: zaidi hapa Paulo aliwakumbusha waaminio katika Efeso ya kwamba kabla ya kujua mambo haya, "hawa kuwa na Kristo wakiwa wamefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa ahadi ile, mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani" (Efe. 2:12) - ingawa pasipo shaka walidhani ya kuwa imani yao ya awali ya kipagani iliwapa tumaini lingine na maarifa ya kumjua Mungu. lakini hili ni jambo la kufikiria sana kutokujua ahadi za Mungu katika Agano la kale -kwa ukweli "ni kutokuwa na tumaini,na pasipo na Mungu duniani’. Kumbuka jinsi Paulo alivyofafanua tumainai la Kikristo kuwa ni "tumaini la ahadi zilizofanywa na Mungu kwa baba wa Wayahudi" (Mdo. 26:6).

Ni ukweli wa kusikitisha kuwa makanisa machache yanaweka mkazo juu ya sehemu hizi Agano la kale ambazo wanatakiwa. "Ukristo" Ukristo umeharibika tabia na kuwa dini ambayo msingi wake ni Agano Jipya - ingawa hata wakati huo wanaelekea kutumia mistari michache ya kutoka hilo.Yesu ameweka kwa uwazi mkazo unaozunguka njia sahihi:

"Wasipowasikia Musa (yaani, Vitabu vya kwanza vitano vya Biblia alivyoandika) na mnabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu" (Luka. 16:31).

Nia ya mwili inaweza kufikiri kuwa kuamini kwamba Yesu alifufuliwa yatosha (Luka. 16:30), Lakini Yesu alisema ya kuwa pasipo kuelewa vema Agano la Kale, hii haitawezekana kabisa.

Kukata tamaa kwa Wanafunzi baada ya kusulubishwa kulifuatishwa na Yesu kwa kutoangalia kwao kwa makini kwenye Agano la Kale.

"Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote (kwa usahihi) waliyoyasema manabii: Je? Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake ? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe" (Luka. 24:25 -27).

Ona mkazo wake juu ya namna Agano lote la kale lilivyomsema yeye. sio kwamba Wanafunzi hawakuwahi kulisoma au kusikia maneno ya Agano la Kale, bali hayo maneno hawakuyaelewa Vizuri, na kwa sababu hii hawakuweza kuyaamini kwa kweli. hivyo kuelewa kwa usahihi neno la Mungu, kuliko kusoma tu, ni muhimu kukuza imani ya kweli. Wayahudi walikuwa washupavu kwa kusoma agano lao la kale (mdo. 15:21), Lakini hawakuelewa mistari yake iliyataja mambo ya Yesu na Injili yake, kwa kweli hawakuamini, na hivyo Yesu akawaambia:-

"Kama mungalimwamini Musa, mungeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu? (Yoh. 5:46,47).

Mbali ya kusoma Biblia yao, hawakuwa wanaona ujumbe wa kweli kumhusu Yesu, ingawa walipenda kudhani walikuwa wamehakikishiwa wokovu. Yesu ilimbidi kuwaambia.

"Mwayachunguza maandiko.(Yaani, kwa uzuri -mdo. 17:11); kwa sababu mnadhani kwa ujasiri kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yaliyonishuhudia" (Yoh. 5:39)

Na ndivyo inaweza kuwa na watu wengi walio na elimu ya habari ndogo ya maneno ya maana ya matukio baadhi na mafundisho ya Agano la Kale: ni marifa tu ambayo yamechukua kwa kubahatisha. ujumbe wa ajabu wa Kikristo na Injili ya ufalme wa Mungu bado unawaepuka. ni lengo la somo hili kukutwaa toka nafasi hiyo kwa kukueleza maana ya kweli ya ahadi kubwa za Agano la Kale:-

  • Katika bustani ya Edeni
  • Kwa Nuhu
  • Kwa Abrahamu
  • Kwa Daudi

Habari zake zinapatikana katika vitabu vya kwanza vitano vya Biblia (Mwanzo - Kumbukumbu la Torati) vilivyoandika na Musa na katika manabii walio kwenye Agano la Kale. Yote yalishikamana na Injili ya Kikristo inapatikana humu. Paulo alieleza kuwa mahubiri yake ya Injili hii - akasema "Sisemi neno ila yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa; ya kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatanganza habari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa" (Mdo. 26:22,23), na katika siku zake za mwisho wimbo ulibakia ule ule: "Yeye (Paulo) akawaeleza kwa taratibu na kumshuhudia ufalme wa Mungu ….. kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu Asubuhi hata Jioni" (mdo. 28:23)

Tumaini la Paulo, hilo kuu la Kikristo, liwe tumaini linalotuchochea nasi pia; kama ilivyokuwa nuru yenye utukufu mwishoni mwa tundu la maisha yake, vivyo liwe ni tumaini kubwa kwa kila Mkristo. likiwasha kwa kichocheo hiki, sasa tunaweza "Kuyachunguza Maandiko".


  Back
Home
Next