Misingi Ya BIBLIA Somo La 1: Mungu Uwepo wa Mungu | Nafsi yake Mungu | Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake | Malaika | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Mungu ni roho" (Yohana 4:24), "Matumizi ya jina la Mungu", "Ufunuo wa Mungu") | Maswali |
1.1 Uwepo wa Mungu"Mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kuwa yeye yupo na kwamba huwapa dhawabu wale wamtafutao" (Ebr 11:6). Lengo la masomo haya ni kuwasaidia wale wanomwendea Mungu, wakiisha mwamini "Kwamba yupo"; kwa sababu hii hatutajitia kwenye ushahidi usiothibitisha imani ya kuwa Mungu hayuko.katika kupima muundo wa miili yetu (Zab 139:14) Ushahidi wa kielelezo katika ua, Kukazia macho juu kwenye anga pana wakati wa usiku kukiwa wazi bila mawingu, haya na mengine yasiyohesabika, Mawazo ya kangaliifu juu ya maisha, hakika yanafanya imani ya kutosadiki kuwa Mungu hayupo iwe ni ya kushangaza. Kusadiki kuwa Mungu hayuko hakika inahitajika imani zaidi kuliko kuamini yupo,pasipokuwepo Mungu mpangilio haupo, Kusudi au kutoa maelezo ya asili ya Ulimwenguni basi hii itafikiriwa katika maisha ya mtu asiyeamini kuwa Mungu yupo. Tukikumbuka hili, siyo ajabu kuwa watu wengi wanakiri kwa kiwango fulani cha kumwamini kuwa Mungu yupo hata katika jamii ambayo vitu vya mwili ni Mungu anayeshinda maisha ya watu. Lakini ipo tofauti pana kati ya kuwa na fikra isiyodhahiri ya kwamba ipo nguvu ya juu, na hasa kweli kuwa na uhakika kwa kile ambacho Mungu anampa mtu anayemtumikia kwa Uaminifu. Waebrania 11:6 jambo hili tunasoma; "Yatupasa tuamini kuwa (Mungu) yupo na Kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii" Maelezo mengi ya biblia ni historia ya watu wa Mungu Israeli; mara kwa mara neno limetolewa kwamba kukubali kwao kuwa Mungu yupo hakukulingana na imani zao kwa ahadi zake.Waliambiwa na mkubwa kiongozi wao Musa'Kwa hiyo ujue…….Ukaweke moyoni mwako, ya kuwa BWANA ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini, hapana mwingine. Basi, zishike sheria zake, na amri zake (Kum. 4:39:40). Neno hili hili limetolewa - ufahamu wetu katikati yetu ya kuwa Mungu yupo hakumaanishi kwamba tunakubalika mbele za Mungu bila kufikiri.Ikiwa bila mchezo tunakubali kwamba kwa kweli tunaye Muumba,'Kwa sababu hiyo tuzishike sheria na amri zake’ Ni shabaha ya mfululizo huu wa masomo kuelezea amri hizi jinsi zilivyo na namna ya kuzishika. Tunapochungunza maandiko kwa kufanya hivi, tutakuta kwamba imani yetu kuwa Mungu yupo inatiwa nguvu. ‘Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Mungu’ (Rum 10:17). Vile vile, (Isaya 43:9-12) yaonyesha namna ya kufahamu unabii wa Mungu kuhusu wakati ujao - Unabii unatufanya tujue'kuwa mimi ndiye’ (Isa. 43:13)- yaani hilo jina la Mungu, 'Mimi niko ambaye NIKO’ kwa ukamilifu ni kweli (Kut. 3:14.) Mtume Paulo alifika kwenye mji unaoitwa Beroya, eneo hili kwa sasa liko kaskazini mwa Uyunani (Ugiriki) kama kawaida, akahubiri injili (Habari njema) ya Mungu; lakini badala ya watu kusikia neno la Paulo alilokuwa anasema, tunasoma kwamba, " Walilipokea kwa kusikia neno (la Mungu, sio la Paulo) kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini (mdo 17:11,12) Imani yao ilikuja kwa kuwa mioyo yao ilikuwa wazi, sawa sawa (‘ Kila siku’) na kwa utaratibu wa (‘mambo hayo’) waliyachunguza katika Biblia, Basi kupata imani ya kweli haikuwa Mungu aliwafanya wawe nayo ghafla kwa aina fulani ya upasuaji wa moyo wa kiroho, pasipo kujihusisha na neno la Mungu. Ni jinsi gani basi watu wa Ulimwengu wanaweza kufuata kwa moyo pigano juu ya maovu la Bill Graham au uamsho wa mikutano ya wapentekoste kisha wanahama tena kama'Waamini’ ? Ni muda gani wameendelea katika masuala haya wakiwa wanachunguza maandiko kila siku ? Kwa kweli kukosekana huku kwa imani ambayo msingi wake upo kwenye Biblia bila shaka kunaonyesha utupu wa'Waongofu’ hawa na kujikuta baadae kwa wanayopata Wakristo, na ni kwa sababu gani wengi wanaondoka kutoka kwenye Ushirika wa Madhehebu ya wa-Injilisti. Masomo haya lengo lake ni kukupa mjengo wa utaratibu wako mwenyewe kuchunguza maandiko, ili kwamba nawe pia uweze basi kuamini muunganiko kati ya kusikia Injili ya kweli na kuwa na imani ya kweli mara nyingi kumejitokeza wazi katika taarifa ya kuhubiri injili.
|