Misingi Ya BIBLIA Somo La 1: Mungu Uwepo wa Mungu | Nafsi yake Mungu | Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake | Malaika | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Mungu ni roho" (Yohana 4:24), "Matumizi ya jina la Mungu", "Ufunuo wa Mungu") | Maswali |
1.3 Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa YakeIkiwa Mungu yupo, inafaa kufikiri kuwa atakuwa amevumbua njia nyingine ya kutuambia habari zinazo mhusu yeye mwenyewe. Tunaamini ya kwamba Biblia ni ufunuo wa Mungu kumjulisha Mwanadamu, na humo ndani ya kitabu tunaona kudhihirika tabia ya sifa ya Mungu. Hii ndio sababu Neno la Mungu linasemwa kuwa ni'Mbegu’ yake (1 Petro 1:23) Kwa kuwa kama likigeuza hali ya mioyo yetu, kiumbe mpya anaumbwa ndani yetu ambaye ana sifa za Mungu (Yakobo. 1:18, 2Kor. 5:17). Kwa hiyo sisi wenyewe tunapotumia zaidi neno la Mungu na kuchukua masomo sisi wenyewe, ndivyo zaidi tutafanana mfano wa mwana wake (Rum, 8:29) ambaye kwa tabia ya sifa alikuwa mfano kamili wa Mungu (Kol. 1:15).Kwa hii imelala thamani ya kusoma sehemu za historia ya Biblia, Zimejaa kadhia ya masomo jinsi Mungu alivyojishughulisha na watu pamoja na matifa, Daima akionyesha msingi ule ule wa sifa. Katika Kiebrania jina la mtu mara nyingi lilileta tabia ya sifa zao au taarifa zinazowahusu. Mifano mingine iliyowazi:
Katika Yeremia 48:17, kuwajua watu wa Moabu ni sawa sawa na kufahamu jina la moabu.Mara nyingi zaburi zinamlinganisha Mungu mwenyewe na jina lake, neno lake na matendo (Zab. 103:1, 105:1, 106:1,2,12,13.) Kwa sababu hii itegemewe kwamba majina ya Mungu na heshima vitatupatia habari nyingi kuhusu yeye mwenyewe, kwa kuwa yapo maelekeo mengi ya tabia ya sifa na kusudi kwa kweli ana jina zaidi ya moja.Somo lenye kueleza jambo moja moja la jina Mungu linafaa baada ya Ubatizo; kufahamu zaidi sifa na tabia ya Mungu kumeelezwa katika jina lake, ni jambo lingine ambalo liendelee wakati wa maisha yetu yote katika Bwana. Linalofuata sana kwa hilo, mengi ni Utangulizi. Musa alipotaka aelimishwe kwa undani kuhusu Mungu ili imani yake iimalike wakati wa kipindi kisicho sahaulika sana cha maisha yake. Malaika,'Alitangaza jina la BWANA: BWANA,BWANA Mungu, Mwingi wa huruma, Mwenye fadhili, Si mwepesi wa hasira, Mwingi wa rehema na kweli, Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, Mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; Wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia,’ (Kut. 34:5-7) Huu ni ushahidi ulio wazi wa kwamba majina ya Mungu yanaweka sifa zake.Tendo la kuwa nazo ni uhakika kuwa ni mtu mmoja, si busara kufikiri ya kwamba fungu la roho laweza kuwa na dalili na sifa ya tabia hizi ambazo vile vile zaweza kuendelezwa ndani yetu wanadamu. Mungu amechagua hasa jina moja ambalo amependa ajulikane na kukumbukwa na watu wake, ni kwa ufupi, maelezo mafupi, ya kusudi lake kwa watu. Israeli walikuwa watumwa Misri, Walihitajika kukumbushwa lengo la Mungu kwao. Musa aliambiwa awaambie Jina la Mungu, ili kwamba hili liwasaidie kuwaletea kusudi la kuondoka Misri na kuanza safari kuelekea nchi ya Ahadi (1Kor. 10:1) Nasi pia tunahitajika kuelewa mambo ya msingi yahusuyo jina la Mungu kabla ya kubatizwa na kuanza safari yetu ya kuelekea Ufalme wa Mungu. Mungu aliwaambia Israeli kuwa Jina lake alikuwa YAHWEH-YAHU (Zab 89:8 uv); Maana yake"Mimi niko ambaye NIKO" au limetafsiriwa kwa usahihi zaidi,'Nitakuwa ambaye Nitakuwa’(Kut 3:13-15) Jina hili, kidogo likapanuka wakati ule:" Tena Mungu akamwambia (Ikiwa ni nyongeza) Musa, Hivi ndivyo utawaambia wana wa Israel, BWANA (Yahweh) Mungu wa Babu zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, ….Hili ni Jina langu Milele, la kumbukumbu yangu kwa vizazi vyote. (Kut. 3:15). Kwa sababu hiyo jina kamili la Mungu ni "BWANA Mungu" Zaidi Agano la kale liliandikwa kwa Kiebrania na tafsiri ya Kiswahili ni lazima kutukia visivyo sawa sawa wakati ujapo wa kutafsiri maneno ya Kiebrania hasa neno "Mungu" mengi ya maelezo moja moja yakosekana - Tafsiri yetu ya Kiswahili imetoka kwenye Kiingereza. Moja ya maneno yanayotumiwa na Kiebrania limetafsiriwa'Mungu’ ni Elohim (ELOI) maana yake'Wenye Nguvu’ Kumbukumbu ya jina la Mungu, jina ambalo anatutaka tumkumbuke, kwa sababu hiyo. YAHWEH ELOHIM - YAHU ELOI Kwa hiyo ni kusudi la Mungu kuidhihirisha tabia ya sifa yake, Umuhimu wake katika kundi kubwa la watu. Kwa kulitii neno lake tunaweza kukuza sifa zingine za Mungu ndani yetu wenyewe sasa, hivyo basi kadri ya busara sana. Mungu alijifunua mwenyewe kwa waamini wa kweli katika maisha haya.lakini jina lake Mungu ni la Unabii wa wakati ujao hapo dunia itakapo jaa watu watakao kuwa sawa naye, pande mbili kwa tabia na mwili (2Petr 1:4). Ikiwa tunataka kuungana na lengo la shabaha ya Mungu na kuwa kama Mungu bila hata kufa tena, kuishi milele katika uadilifu wote uliokamilika, basi yatupasa sisi wenyewe tujiunge na jina lake. Namna ya kufanya hivi ni kubatizwa katika jina, yaani la Yahweh Elohim (Math. 28:19). Hili linatufanya tuwe watoto (‘Uzao’) wa Abrahamu (Gal,. 3:27-29) uliohaidiwa kurithi milele nchi (Mwa. 17:8; Rum. 4:13) Kundi la wenye nguvu (Elohim -Eloi) ambao unabii wa jina la Mungu utatimilika. Limeelezwa zaidi kwa habari katika somo la 3.4. |