Misingi Ya BIBLIA
Somo La 1: Mungu
Uwepo wa Mungu | Nafsi yake Mungu | Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake | Malaika | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Mungu ni roho" (Yohana 4:24), "Matumizi ya jina la Mungu", "Ufunuo wa Mungu") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 2: "Matumizi ya jina la Mungu"

Tumefahamu kwamba Jina la Mungu na hilo la mwanae Yesu yana maana ya kina sana. Tunaposema 'Mungu’ tunagusa juu ya kila mwelekeo wa kusudi lake la Ajabu la upendo na kweli. Ya kwamba Jina la Mungu litumike bure kama upole usio na maana au kwa maelezo ya kukasirisha, ni moja ya mambo ambayo mtu hufanya na kumnena vibaya zaidi Muumba wake. Kwa sababu hii kila mtu anayetaka kumpendeza Mungu na kumheshimu atafanya kila jitihada kutotumia vibaya Jina la Mungu kirahisi- rahisi. Katika jamii ulimwenguni pote kufuru hii imekuwa sehemu ya kawaida kwa Lugha za siku hizi; Kukatisha ile iliyokuwa ni tabia ya mazoea haita kuwa kazi rahisi. Sala ya kweli ya kuomba msaada wa Mungu hakika itasikika. Wale ambao wapo ndani ya shughuli yetu ya kuwaongoza na kuwavuta, Mf. Watoto, pia watakumbushwa hatari ya kukufuru:"Maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia alitajaye jina lake bure (Kum. 5:11)

Kwa upande mwingine wapo wale wanaosisitiza kwamba tusipotumia maneno ya Kiebrania Yahweh au Yehova (Njia tofauti ya kutamka neno lile lile) Tunapozungumuza kuhusu Mungu, wakati huo tunakuwa tumepotea sana. Miongoni mwao zaidi ya hawa ni Chama cha mlinzi, wanasisitiza kuwa Mkristo asipojiita mwenyewe ni'Shahidi wa Yehova’ Basi hana uhusiano na Mungu.

Kwa kufanya hivi, watu hawa wanatumia jina takatifu la Mungu na la ajabu kuchochea aina fulani ya mfumo wa Imani wa kuelimisha kiroho, ambapo wanawadharau watu wengine tu kwa matamshi au matumizi ya neno moja. Hii sio kusema kuwa ni vibaya kutumia Jina la Mungu; Hasa kweli linafaa kutumika kwenye Sala zetu wenyewe mara tukibatizwa kwa usahihi katika Jina lake. Ingawa hivyo, Agano Jipya halitupatii ishara yoyote kuwa hili ni lazima au inatakiwa na Mungu. Aliongoza kuandika Agano Jipya hivyo basi liliandikwa kwa Kiyunani (Kigriki) likitumika neno moja la'Mungu’ -‘theos’ likiwa na maana "Mtu mkubwa".

Hakuna tofauti iliyofanywa ndani yake kati ya'Mungu’ na 'Yahweh’ wala haipo amri yoyote dhahiri inayohusiana kwa waamini wakiwa ni jumuiya wajiiteje.Petro anamsema mwamini kuwa ni " Mkristo" kuliko kumwita ni'Mtu wa Yehova’ au jambo lingine kama hili (1 Petro 4:16) kutilia mkazo zaidi katika matumizi ya Jina la 'Yehova’ kunapelekea kupunguza thamani ya kazi na Nafsi ya BWANA'Yesu’ kwa njia hii ambayo wakristo wengi wa kiinjili wanatia msukumo zaidi kwenye jina na kazi ya Yesu huku wakiacha kuangalia nafsi ya nguvu zaidi iliyo ya Mungu.

Majina mengine ambayo jumuia ya waaminiao ya wakristo wa kwanza waliyojiita wenyewe, hayatii ndani jina la Yehova:-

‘Jamii ya Israeli’ (Ef. 2:12)

‘Mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza’ (Ebr. 12:23)

‘Kanisa lake Mungu’ (Matendo 20:28)

‘Kanisa la Mungu aliye hai, Nguzo na Msingi wa kweli’ (1 Timotheo 3:15)

‘Nyumba ya Mungu’ (1 Timotheo 3:15)

Tunapopita, ujue kuwa waamini hawakujiita wenyewe'Wakristo’. Neno hili maana yake lilikuwa la kuvunja heshima, hawa watu wa Kristo walibezwa na maadui zao.


  Back
Home
Next