Misingi Ya
BIBLIA
DibajiWatu wote ambao wamekubali kuwa Mungu yupo, na kwamba Biblia ni ufunuo wake kwa mwanadamu, Kwa kusema kweli wanahitaji wao wenyewe watafute ujumbe wamsingi uliomo katika Biblia. Wengi wanao jiita ni ‘Wakristo’ wanazembea kwenye kazi hii, kwani, husoma mistari michache toka Agano Jipya siku za Jumapili wengine huwa na Biblia mahali fulani majumbani mwao ambamo kamwe haifunguliwi, Kwa uwazi hawaoni na kukumbuka habari nyingi zilizo kwa wingi katika Biblia. Ajabu ndogo ni kwamba kwa tabia hii dhidi ya Mungu kwa neno lake la kwanza , Kumekuwepo na mtafaruku mno usiotegemewa katika maisha na mioyo ya wengi Kwa upande mwingine , wapo wale ambao wana malezi kidogo ya kikristo ambao huamua kujaribu kuufikiria ujumbe wa Biblia, lakini wanakuta kwamba kila mtu wanae mkaribia hujaribu kuwapa furushi lilojaa tele mafunzo ya elimu ya mwanadamu inayodumisha mapokeo ya imani kwenye dini ya Kikristo isiyoleta sifa ya maneno ya Biblia. Ni lengo la kitabu ‘Misingi ya Biblia’ kuchambua ujumbe wa Biblia kwa makini kwa njia ya taratibu. Kimepangwa kusomwa moja kwa moja kama kitabu , au kwa shauri la pili kinaweza kutumika kama kuandikiana masomo ya kumfunza mtu mwingine . Majibu ya maswali yaliyomo mwishoni mwa kila somo yaweza kutumwa kwa kufuata anuani utakayo pewa chini , Kisha majibu yako yatapelekwa kwa mfunzi wako ambae wakati huo ataweza kuwasiliana nawe kwa kadri unavyosonga mbele na masomo hayo. Inafahamika ya kwamba wasomaji wengine watakuwa wenye soni kutokana na wazo la kujibu maswali , lakini badala yake watauliza maswali yahusuyo maeneo ambayo hawajayaelewa au hawakubaliani na tafsiri iliyotolewa hapa . Basi, ikiwa kutumiana barua huku kunaelekezwa kufuata anuani hiyo hapo chini, Majibu yako unaweza kupewa. Ni nia ya mbuni kitabu ya kwamba ujumbe wa msingi wa Biblia hudhihirika wazi . Ingawa hivyo, daima yatakuwepo mafungu mengine ya maneno au habari ambayo inaweza kuonekana kijuu juu kutofautiana na jambo zima la maandiko. Baadhi ya haya, pamoja na maelekezo mengine ya Injili yanaweza kuwavutia wasomaji wengine pekee , yamejadiliwa katika sehemu iitwayo ‘Acha kwa kitambo habari inayoandikwa’ itawezekana kuelewa ujumbe wa msingi wa Biblia pasipo kusoma sehemu ya tumeacha kwa kitambo yaliyoandikwa, lakini inatazamiwa kuwa wanafunzi wengi watasoma yote. Kwa ujumbe tafsiri iliyotumika katika masomo haya ni kutoka Union Version - Biblia ya kiswahili. Lakini kukiwepo kutokueleweka vizuri katika tafsiri, basi tuna nukuu kuto tolea lingine la Biblia . Lipo toleo lingine la Biblia iitwayo ya kisasa hii ni kwa ajiri ya kuelewesha vema somo - hii ni ‘Biblia Habari Njema .’ kwa Kiswahili. Wapo watu wengi ambao inabidi kuwashukuru kwa msaada wao katika kukitengeneza kitabu hiki, hasa nawiwa na Clive Rivers kwa uhodari mfululizo wa kutoa picha na wale waliofafanua juu ya maandiko lakini, kuwiwa kwangu kikubwa kupo kwa mamia ya watu walio Africa, West Indies, Ufilipino na Ulaya Mashariki na wenye maswali ya upekuzi na kiu ya kujua ukweli wamenishurutisha kuona hata mwisho kwenye misingi hii ya Biblia mara kwa mara. Ubora wake na nguvu pekee vinaongezeka na kwa kutazama kutoka kona nyingi tofati tofauti. Kwenye mkusanyiko wa taxi, kwenye magari makubwa yaliyo wazi, kwenye vyumba vya mkutano tulivu hadi kwenye hoteli zenye roshani zisizo na raha shauri ya joto na vijijini. Masuala haya yamejadiliwa, kubishaniwa na wanafunzi wengine wameonyesha shauku katika Biblia kutoka kwenye nyendo zote za maisha. Ndugu zangu wakristadelfiani ambao nilibahatika kufanya nao katika kazi hii wamekuwa ndio chanzo cha msaada na kunitia moyo. Sehemu muhimu nyingi zinazoitwa Kuacha kwa kitambo kile kinachozungumuziwa katika kitabu hiki mara nyingi karatasi zilichanwa katikati yetu kwenye vyumba vya hoteli, baada ya balaza lenye majadiliano makali na kundi la wanafunzi wanaopokea masomo. Ushirika na urafiki unaokuja kwa kufungamana pamoja katika mafunzo haya ya msingi iliyo ya Biblia ya kweli ni hakika hauna kifani katika maarifa ya mwanadamu. Basi kwa yote hayo "Wafanyakazi wenzangu katika ufalme wa Mungu" nataja sifa nikitumaini kwamba watakuta kitabu hiki ni msaada katika kazi kubwa ya kuchapisha Injili ya kweli "kwa mataifa yote." Kushika ukweli halisi wa injili kama ulivyofundishwa katika kurasa za Biblia kutabadilisha kila sehemu za maisha yetu, kuwaongoza wanaume na wanawake na ulimwengu zaidi, hasa kutoa utukufu wa Mungu kama alivyokusudia , pande zote mbili sasa na hata milele. Kila mtu anayepata ukweli anakuwa amepata ‘Lulu ya thamani kubwa’ atajua mawazo ya Yeremia kwa ajili yake mwenyewe. "Maneno yako yalionekana, nami nikayala ; na maneno yako yalikuwa furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu" (Yer. 15:16). Ili kufaulu katika suala hili, hakikisha unaomba msaada wa Mungu uelewe neno kabla ya kushughulika na masomo haya . "Basi sasa nawaweka katika mikono ya Mungu , na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa" (Matendo 20:32). D.H. VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA KATIKA MASOMO HAYA KWA VITABU VYA BIBLIA
Maswali yaliyo mwisho mwa kila somo ni ya aina mbili: Uchaguzi wenye sehemu nyingi (ambapo inakupasa uchague jibu moja kati ya majibu yaliyoorodheshwa ikiwa ni jibu sahihi kwa swali lililoulizwa.) Na maswali ya kawaida yanayohitaji sentensi chache kwa majibu. Andika majibu yako kwenye kipande cha karatasi tofauti , Usisahau kuandika jina lako na Anuani inayosomeka kwa uwazi. Tuma majibu yako kwa anuani hii hapa chini Misingi Ya Biblia , au www.carelinks.net au Bible Basics, |