9.3 Kutoa Dhabihu Kwa Ajili Yetu Na Kwa Ajili YaNafsi Yake Mwenyewe
Kuhani mkuu wa wayahudi ilimpasa kutoa dhabihu ya kwanza kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, na halafu kwa ajili ya hao watu (Ebra 5:1-3). Dhabihu ya Kristo ilikuwa na muundo u huu mara dufu. Ingawa yeye mwenyewe hakuwa na dhambi yeyote, bado Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu, alihitaji wokovu toka mauti. Wokovu huu ulitolewa na Mungu, kwa sababu ya dhabihu yake mwenyewe Kristo; hivyo kwa pande mbili Yesu alikufa ili apate wokovu wake mwenyewe, na kuuwezesha wa kwetu vile vile. Maneno mengi yanataja hii.
Sehemu hii ni orodha ya aya zinazothibitisha kuwa dhabihu ya Kristo ilikuwa kwa faida yake mwenyewe sambamba na sisi. Ni mbali kuliko kuthibitisha maana hii; lakini ina maana kuwa jambo hili tunalolizungumzia ni la muhimu kufahamu ikiwa ubinadamu wa Bwana wetu uweze kueleweka vizuri. Kwa kumalizia kitabu hiki unaweza wakati mwingine utakaofuata ukataka kufikiri kuhusu mambo haya kwa undani, kwa hiyo mambo haya yamejumuishwa.
Kuhani Mkuu "imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe; kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi….. vivyo hivyo Kristo" alitimiza mfano wa kuhani mkuu wa kipindi cha Musa kwa kuangalia hili (Ebra. 5:3,5). Neno la kiyunani "imempasa" kwa namna yake maalum maana yake kuwa na deni la fedha- likiwa linataja Bwana wetu ananunua ukombozi wake mwenyewe vile vile na wa kwetu. Ulikuwa ni "kwa sababu ya" ubinadamu wake (Ebra 5:3) ambao inambidi kufanya hivi. Hapa haina maana kwamba alikuwa na dhambi yake yoyote ambayo alihitaji kuilipia. Jambo hili haliwezi kukaziwa mno. Tulikombolewa kwa damu yake ya dhabihu -basi na yeye pia.
Kristo "hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yake alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake" (Ebra 7:27). Hakuna shaka ya kwamba Paulo anakazia hali ya kufanana ya matokeo ya kuhani kwa vitu viwili kati yake na Kristo. Anafanya hivyo tena katika Ebra 9:7 (mst 12,25). Tofauti ilikuwa kwa Kristo kufanya hivyo mara moja, bali kuhani mkuu kila mwaka. Ikiwa tofauti ilikuwa kwamba Kristo alitoa tu dhabihu kwa ajili ya watu, basi hii ingejitokeza. Fahamu kwamba dhabihu ya Kristo ilikuwa kwa ajili ya "dhambi" zake mwenyewe ambazo zilitofautiana na za watu - ‘dhambi’ zake hazikuwa zetu alizichukua. Kwa sababu kwa mfano alitoa dhabihu iliyojitenga kwa ajili yetu. Kwa kuwa Yesu alikuwa mkamilifu, tabia isiyo na dhambi, hapa ‘dhambi’ ni namna nyingine ya kuueleza mwili wa dhambi ya mwanadamu. Sababu (mwili ulio na dhambi) umesemwa kama ni tokeo. Lakini bado inahitajika kukazia ya kwamba Bwana wetu alikuwa mkamilifu, hawezi kuthibitishwa kuwa ana dhambi.
Mungu "akamleta tena kutoka kwa wafu mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya Agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu" (Ebra 13:20), yaani damu yake mwenyewe. Basi, kwa pande mbili Bwana wetu alikuwa mchungaji, kwa kuwa alikwenda mwenyewe kwa mchinjaji, na kwa damu yake Mungu akamfufua; na kwa jinsi iyo hiyo kwa pande zote mbili alikuwa anatoa dhabihu na ni kuhani.
Katika Biblia ya Kingereza A.V kwa Zekaria 9:9 unasema vizuri kwenye pambizo: "Mfalume wako (Yesu) anakuja kwako; ni mwenye haki, anajiokoa mwenyewe, (UV ‘naye ana wokovu’)" . Hizi tafsri mbili za kufaa zimedokeza kwamba kwa kujiokoa mwenyewe Bwana wetu ametuletea wakovu. Kwa dhabihu yake msalabani, yaani alilipia mwili wake mwenyewe ili kwamba afanikishe ukombozi wetu. Sio busara kufikiri mauti yake nje ya maneno yenyewe kwa kusudi lake la kutaka kutuokoa
Inabidi ifahamike kuwa ushahidi wote wa kumwaga damu ya mnyama kuwa dhabihu chini ya torati kwa namna nyingine yahusu dhabihu yenyewe ya Kristo. Madhabahu, alama ya Kristo,ilifanyiwa upatanisho mara moja kila mwaka kwa damu (Kut 30:10), ikionyesha ni jinsi gani Kristo alijitakasa mwenyewe kwa kutoa dhabihu yake. Hakika ile hema nzima ya kukutania jangwani ilimwakilisha Kristo, ilibidi isafishwe kwa damu (Ebra 9:23). Vyombo vya mle ndani ya maskani havikutenda dhambi yeyote, ingawa vilitakiwa vitakaswe kwa sababu ya kushirikishwa na dhambi. Ndivyo na Bwana wetu.
Kuhani Mkuu mwenyewe ilimpasa kuanza utumishi wake kwa kunyunyuziwa damu, naye Kristo alihitaji dhabihu yake mwenyewe ili aanze utumishi wake kwa ajili yetu Mbinguni (Law 8:23).
Ya kwamba Yesu alijipatanisha mwenyewe haina maana kuwa alikuwa na dhambi zake mwenyewe. Kutoa dhabihu yake kwa dhambi siku zote haina maana kuwa mtoaji dhabihu amekosa (Yaani; Law 12 mwanamke ilimbidi afanye hivi baada ya kuzaa).
|