Misingi Ya BIBLIA Study 9: Ushindi Wa Yesu Ushindi Wa Yesu | Damu Ya Yesu | Kutoa Dhabihu Kwa Ajili Yetu Na Kwa Ajili YaNafsi Yake Mwenyewe | Yesu Ni Mwakilishi Wetu. | Yesu Na Torati Ya Musa | Sabato | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Sanamu ndogo ya Yesu Msalabani, Je? Yesu alizaliwa December 25?) | Maswali |
9.1 Ushindi Wa YesuSomo lilotangulia limeonyesha kwa maneno jinsi gani Yesu alikuwa na asili yetu wanadamu, alijaribiwa kutenda dhambi kama sisi tu. Tofauti iliyopo kati yetu na yeye ni kwamba alishinda dhambi kabisa; wakati ana mwili ulio na dhambi, alionyesha tabia iliyo kamilifu ya kumpendeza Mungu. Ajabu ya hii isikome kutufunua tunapoongeza kuielewa. Upo mkazo ulio rudiwa rudiwa katia Agano Jipya kuhusu tabia kamilifu ya Kristo:
Taarifa za Injili zinaonyesha kwa maneno jinsi gani watu, ndugu zake walivyotambua ukamilifu uliotirika kutoka kwenye tabia yake, ulijionyesha katika maneno yake na matendo . Mke wa Pilato alitambua ya kwamba alikuwa ni " mtu mwenye haki" (Math 27:19) asiyesitahili kuadhibiwa: askari wa Kirumu aliyetazama mwenendo wa Kristo wakati ametundikwa juu ya msalaba ilibidi atoe maelezo, "Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki" (Luka 23:37). Awali katika maisha yake, Yesu aliwauliza Wayahudi swali: "Ni nani miongoni mwenu anishuhudiae ya kuwa nina dhambi?" (Yohana 8:46). Kwa hili hawakuwa na jibu. Kwa ajili ya tabia yake kamilifu Yesu alikuwa udhihirisho wa Mungu katika mwili(1 Tim 3:16); Alitenda na kunena kama Mungu alivyotaka afanye binadamu. Kwa sababu hii alikuwa anarudisha nuru kamili ya Mungu."mfano wa Mungu asiyeonekana" (Kol.1:15). Kwa sababu hii hakuna haja kwa watu wanaopatikana na mauti kumwona Mungu kwa mwili wake.Kama vile Yesu alivyoeleza "aliyeniona mimi amemuona Baba"; basi unasemaje! wewe,Tuonyeshe Baba (kimwili)?" (Yohana 14:9). Akiishi katika ulimwengu wa dhambi, na kusumbuliwa na dhambi katika mwili wetu kabisa, ni vigumu kwetu kufahamu ujumla na ukubwa wa Kristo kiroho na ukuu wake; ya kwamba mtu aliye na mwili wetu afunue kabisa haki ya Mungu katika tabia yake. Kuamini jambo hili inatakiwa imani ya kweli zaidi kuliko kukubali tu nadharia ya wazo la kwamba Kristo alikuwa Mungu mwenyewe; inaeleweka ya kuwa mafundisho potofu ya utatu wa Mungu na "Uungu wa Kristo yana watu wengi mno kwa kuwa ni rahisi kuyakubali." Kwa kuwa alikuwa ni wa asili yetu, Kristo inambidi afe. Alikuwa mtoto wa Adamu kwa kuzaliwa na Mariamu, na watoto wote wa Adamu inabidi wafe (1Kor 15:22). Inawapasa wazao wote watokanao na Adamu kufa kwa sababu ya dhambi yake, bila kutazama haki zao: "Walakini mauti inatawala…. Ikiwa kwa kukuosa kwake yule mmoja (Adamu) wengi walikufa….. Uamuzi- hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja (Adamu) ikaleta adhabu (kifo) …. Kwa maana ikiwa kwa kukuosa mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi; na kwa sababu hii inawapasa kufa (Rum 5:14-19; 6:23). Akiwa mzao wa Adamu Kristo ,‘alifanywa’ kuwa ‘mwenye dhambi’ na kwa hiyo ilimbidi afe, kama watoto wote wa Adamu walivyoainishwa kuwa watenda dhambi nao wamestahili mauti kwa sababu ya dhambi. Mungu hakubadili jambo hili, Aliliacha likamdhuru Kristo naye pia. Mungu "alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, yeye asiyejua dhambi" (2Kor 5:21) Mbali ya Yesu, wazao wote wa Adamu wamestahili kupata adhabu hii, kwa maana sisi sote tumekosa. Yesu ilimpasa kufa kwa sababu alikuwa na maumbile yetu, akishiriki laana iliyokuja juu ya watoto wa Adamu. Lakini kwa kuwa yeye hakufanya chochote kinachostahili afe "Mungu akamfufua kutoka katika wafu, akaufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao"(Matendo 2:24 U.V).Kristo alidhihirishwa kwa uweza kuwa mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu" (Rum 1:4). Hiyo ilikuwa sababu ya tabia kamilifu ya Kristo, "roho yake ya utakatifu", hata akafufuliwa kwa utukufu. Kristo sio tu alikufa msalabani kwa sababu alikuwa na mwili wa kibinadamu. Kwa hiari yake aliutoa uhai wake kamili kuwa kipawa kwetu; alionyesha upendo wake kwetu na kufa "kwa ajili ya dhambi zetu" (1 Kor 15:3) akijua ya kwamba kwa njia ya mauti atatupatia wokovu toka dhambi na mauti (Efe. 5:2, 25; Ufunuo 1:5; Gal 2:20). Kwa kuwa Yesu alikuwa mkamilifu kitabia aliweza kushinda matokeo ya dhambi kwa sababu ya kuwa wa kwanza kufufuka toka wafu na kupewa uzima wa milele. Wale wote ambao wana jishirikisha na njia ya Kristo kwa njia ya ubatizo na kuishi kama Kristo wanatumaini la ufufuo huu na kupewa thawabu. Ndani ya jambo hili imelala maana yenye utukufu wa ufufuo wa Kristo. Ni "Uhakikisho" wa kwamba tutafufuliwa na kufanyiwa uamuzi kwa yale tuliyotenda katika mwili (Mdo 17:31), na kama kweli tumeishi kama yeye tutashiriki thawabu yake ya uzima wa milele, "tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana wetu Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu" (2Kor 4:14; 6:14; Rum 6:3-5). Jinsi tulivyo wakosaji tumestahili mauti ya milele (Rum. 6:23). Lakini, kwa sababu ya maisha kamilifu ya Kristo, utiifu hata katika mauti yake na kufufuliwa kwake, Mungu anaweza kutupatia kipawa cha uzima wa milele, kulingana kabisa na mambo yake yote makuu. Kwa kuhamisha matokeo ya dhambi zetu, Mungu "atatuhesabia kuwa na haki" (Rum. 4:6) kwa njia ya imani katika ahadi zake za wokovu. Tunajua ya kwamba dhambi huleta mauti, kwa hiyo kama kweli tunaamini ya kwamba Mungu atatuokoa nayo, yatupasa tuamini ya kwamba atatuhesabu kana kwamba sisi ni wenye haki, ingawa sivyo. Kristo alikuwa mkamilifu; kwa tendo kweli la kuwa ndani ya Kristo, Mungu anaweza kutuhesabu kana kwamba sisi tuwakamilifu, ingawa sisi wenyewe hatupo hivyo. Mungu alimfanya Kristo "kuwa dhambi kwa ajili yetu, yeye asiyejua dhambi; ili tuweze kufanywa wenye haki na Mungu kwa yeye (Yesu)" (2Kor. 5:21) yaani, kwa tendo la kuwa ndani ya Kristo kwa njia ya kubatizwa na kuishi kama Kristo. Hivyo kwa wale walio "katika Kristo",….. alifanywa kwetu… haki, na utukufu na ukombozi" (1Kor. 1:30,31); aya zifuatazo basi zinatutia moyo kumtukuza Kristo kwa mambo makuu aliyotenda; "Kwa maana Habari Njema inaonyesha wazi jinsi Mungu anavyowakubali watu kuwa waadilifu, jambo hili hufanyika kwa imani"(Rom 1:17 B.H.N). Basi kuelewa mambo haya ni sehemu muhimu ya kujua Injili ya kweli Yote haya yamewezeshwa kwa kufufuka kwake Kristo. Yeye alikuwa "limbuko" la mavuno yote ya wanadamu watakao pewa uzima wa milele kwa kufaulu kwake(1Kor. 15:20), "mzaliwa wa kwanza"wa jamaa mpya wa kiroho watakaopewa mwili wa Uungu (1Kor :18; Efe 3:15). Basi, ufufuo wa Kristo umemwezesha Mungu awahesabu wamino katika Kristo kana kwamba ni wenye haki, kwa kuwa wamefunikwa na kuzungukwa na haki yake. Kristo "alitolewa kwa njia ya makosa yetu na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki" (Rum 4:25). Inachukua fikira zetu, kuamua kuamini mambo haya ili kwa kweli kusadikishwa ya kwamba tunaweza kweli kuhesabiwa na Mungu kana kwamba sisi ni wakamilifu. Kristo anaweza kutulinda kwenye kiti cha hukumu "bila mawaa mbele ya utukufu wake" "watakatifu wasio na mawaa wala lawama" (Yuda mst: 24, Kolos 1:22; Efes 5:27). Kuwa na mwili ulio na dhambi na kushindwa daima kiroho, kwa kweli kuamini jambo hili kunahitaji imani thabiti. Kuweka mkono wetu juu tu kwenye mafundisho yaliopangwa hayahusiani na aina hii ya imani. Kwa kufahamu vema ufufuo wa Kristo kunako leta kusudi la imani yetu: "… Mungu, aliyemfufua katika wafu…. hata imani yenu na tumaini lenu (kama hili la ufufuo) liwe kwa Mungu" (Petro 1:21). Ni kwa kubatizwa vyema katika Kristo ndipo tunaweza kuwa "ndani ya Kristo" na kwa sababu hii kuzungukwa na haki yake. Kwa ubatizo sisi wenyewe tunashiriki mauti yake na ufufuo (Rum 6:3-5), ambao ni njia yetu kukombolewa toka dhambi, ‘kwa kuhesabiwa haki"(Rum 4:25) Mambo ya kustaajabisha ambayo tumeona sehemu hii yapo nje kabisa na fahamu zetu ila tukibatizwa. Kwenye ubatizo wenyewe tunashiriki damu ya Kristo iliyomwagika msalabani; waaminio hufua "mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya mwana kondoo" (Ufu. 7:14). Katika mfano, basi wanakuwa wamevikwa mavazi meupe maana yake ni haki ya Kristo ambayo wamehesabiwa haki (Ufu 19:8). Inawezekana kuzitia uchafu hizi nguo kutokana na dhambi zetu (Yuda mst 23); tukifanya hivi baada ya kubatizwa, yatupasa tena kutumia damu ya Kristo kuziosha ziwe safi kwa kumuomba Mungu atusamehe kwa njia ya Kristo. Kinachofuata baada ya kubatizwa ni bado tunatakiwa kujitahidi kubaki ndani ya nafasi ambayo wakati huo tumeingia. Ipo haja ya kawaida, siku zote kujihoji kujipima nafsi kwa dakika chache kila siku, kwa kusali daima na kumuomba msamaha. Kwa kufanya hivi siku zote kwa unyenyekevu tutakuwa na ujasiri wa kwamba, kwa ajili ya kufanikiwa na haki ya Kristo, kwa kweli tutakuwepo kwenye ufalme wa Mungu. Yatupasa tutake kukutwa tukiwa ndani ya Kristo siku ya kufa kwetu na Kristo ajapo, "tusiwe na haki (yetu) wenyewe….bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani.(Filip 3:9). Mkazo ulirudiwa-rudiwa ni kuwa na imani kunakosababisha kuhesabiwa haki, kunaonyesha kwamba kwa vyovyote hatuwezi kupata wokovu kwa matendo yetu; kupata wokovu ni kwa neema: "mmeokolewa kwa neema kwa kuwa na imani ;sio kwa nafsi zenu ni kipawa cha Mungu sio kwa matendo" (Efes 2:8:9). Ikiwa kuhesabiwa haki ni ‘kipawa’ (Rum 5:17), nao wokovu vilevile. Makusudi yetu katika kufanya matendo yoyote ya utumishi wa Kikristo basi uwe ule wa kushukuru kwa kile alichotendea Mungu kutuhesabia haki kwa njia ya Kristo, na kwa sababu hii kutupatia njia ya wokovu. Ni jambo la kutisha kufikiri tukitenda matendo ndio tutaokoka. Hatutafanikiwa kuwa katika kupata wokovu kama tu tukifikiria hivi: ni kipawa ambacho hatutapata kwa upendo tu wa kuitika kwa kushukuru kwa undani, ambako hautaonekana katika matendo yetu. Imani ya kweli huzaa matendo kama haizai imekufa (Yakobo 2:17). |