Misingi Ya BIBLIA
Somo La 8: Asili ya Yesu
Dibaji | Tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu | Asili Ya Yesu | Ubinadamu Wa Yesu | Uhusiano Wa Mungu Na Yesu | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Akiwa Yuna na namna ya Mungu") | Maswali

8.4 Ubinadamu Wa Yesu

Taarifa zilizo katika injili zinatoa mifano mingi jinsi Yesu alivyo kuwa na mwili wa mwanadamu kikamilifu. Habari imetolewa ya kwamba alichoka akaketi vivi hivyi kisimani (Yn 4:6)"Yesu alilia", Lazaro alipokufa (Yn 11:35). Kwa ukubwa sana, taarifa ya mateso yake ya mwisho yamekuwa ni ushahidi wa kutosha wa ubinadamu wake:"Sasa roho yangu imefadhaika", alikiri alipomwomba Mungu amuokoe toka kwenye kifo chake cha msalaba (Yn 12:27)."Aliomba akisema, Baba yangu ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke (cha mateso na mauti); walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe"(Math 26:39). Mstari huu unaonyesha kwamba kwa namna nyingine nia ya Kristo, au matakwa, yalikuwa tofauti na nia ya Mungu.

Wakati wa maisha yake yote Kristo alitoa mapenzi yake kwa kuyaelekeza kwa yale ya Mungu akijitayarisha kwa ajili ya majaribio ya mwisho msalabani. Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki; kwa sababu siyafuati mapenzi yangu mimi; bali mapenzi yake aliyenituma"(Yn 5:30). Tofauti hii kati ya mapenzi ya Kristo na ya Mungu ni ushahidi wa kutosha kwamba Yesu hakuwa Mungu.

Katika maisha yetu tunategemewa kukua katika maarifa ya kumjua Mungu, tukijifu- nza kutokana na majaribu tunayopata katika maisha. Kwa hili, Yesu alikuwa ni mfano wetu mkuu. Hakuwa na majaribu kamili ya Mungu yaliongizwa ndani yake zaidi kuliko tuliyonayo. Tangu utoto,"Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo (yaani, kukua kiroho mfano Efe 4:13), alimpendeza Mungu na wanadamu (Lk 2:52)."Yule mtoto, akakua akaongezeka nguvu (akakua) katika roho"(Luka 2:40). Mistari hii miwili inaonyesha ukuaji wa mwili wa Kristo ikiwa sambamba na kukuwa kwake kiroho; maendeleo ya ukuaji ulitoka ndani yake pande mbili kwa kawaida na kwa kiroho. Ikiwa"mwana ni Mungu", kama imani ya Athanasi isemavyo kuhusu ‘utatu’, hii isengewezekana. Hata mwisho wa maisha yake, Kristo alikiri kwamba hakujua hasa ni lini atarudi mara ya pili, ingawa Baba alijua (Marko 13:32).

Kutii mapenzi ya Mungu ni jambo lingine yanatupa sote kujifunza kwa kipindi chote cha wakati. Naye Kristo ilimpasa kupitia njia ya kujifunza kumtii Baba yake, kama ipasavyo mwana yeyote."Na ingawa ni mwana, alijifunza kutii (yaani kumtii Mungu) kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokukwisha kukamilishwa (yaani, akiisha kua ki- roho), akawa sababu ya wokovu wa milele."Kwa matokeo yake kamili ya kukua kiroho (Ebr 5:8,9), Wafilipi 2:7,8 (zaidi limefafanuliwa katika somo la kuacha kitambo kilichoandikwa sehemu ya 27) imetoa taarifa ya hii njia moja ya kukua Yesu kiroho, na kuishia kwenye mauti ya msalabani."Alijifanya hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa (yaani kwa mwenendo)……. alijinyenyekeza akawa mtii….. mauti ya msalaba."Msemo uliotumika hapa unaeleza jinsi gani kwa fahamu Yesu hakugeuka katika maendeleo ya kiroho, mwenyewe akijinyenyekeza zaidi na zaidi, kwa sababu hiyo"akawa mtii"kufanya mapenzi ya Mungu ili afe msalabani, Hivyo basi"akakamiliswa"kwa kuitikia kwa usahihi mateso yake.

Ni dhahiri kutokana na hii Yesu ilimpasa kuwa na fahamu, bidii yake mwenyewe kuwa mwenye haki; hakulazimishwa kuwa hivyo na Mungu, tendo ambalo lingemfanya yeye kuwa ni wa bandia tu. Kwa kweli Yesu alitupenda, aliutoa uhai wake msalabani toka kuendesha hivi. Mkazo ule ule juu ya upendo wa Kristo kwetu ingekuwa sio kweli ikiwa Mungu ndiye aliye mshurutisha kufa msalabani (Efe. 5:2,25; Uf 1:5; Gal2:20). Ikiwa Yesu alikuwa ni Mungu,basi asingekuwa na uchaguzi bali kuwa mkamilifu, ndipo afe juu msalabani. Kama Yesu alikuwa na chaguzi hizi, zatufanya tufahamu upendo wake, ili tutengeneze uhusiano wetu naye.

Ilikuwa sababu ya hiari ya Kristo kujitoa uhai wake hata Mungu akapendezwa naye: Ndiposa"Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili ni utwae tena. Hakuna mtu aniondoleye bali mimi nautoa uhai mwenyewe."(Yn. 10:17,18). Mungu akiwa amependezwa mno na utiifu wa hiari wa Kristo ni vigumu kuelewa ikiwa Yesu alikuwa Mungu, akiishi toka maisha ya kibinadamu kama kwa namna nyingine ya ushahidi wa kuwa pamoja na mwanadamu aliye wa dhambi (Math 3:17; 12:18;17:5). Taarifa hizi za Baba kufurahia utii wa mwanawe, ni ushahidi wa kutosha kuwa Kristo alikuwa na uwezekano wa kuasi, bali akiwa anasikia mwenyewe nafsini alichagua kutii.

KRISTO KUTAKA WOKOVU.

Kwa sababu ya asili yake ya mwanadamu, Yesu alipata ugonjwa mdogo uchovu n.k kama sisi tupatavyo. Kwa hiyo kinachotokea ni kwamba asingalikufa msalabani, angekufa kwa namna yeyote kama kwa uzee. Kwa mtazamo huu Yesu alihitaji kuokolewa na Mungu toka kwenye mauti. Kwa mkazo akitambua hili, Yesu"alimtolea yule awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti; maombi na dua pamoja na kulia sana machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu"(Ebra 5:7). Jambo la hakika ni kwamba Kristo alimwomba Mungu kusudi amwokoe kutoka katika mauti halielezwi lolote la yeye kuwa Mungu ndani ya mtu. Baada ya ufufuo wa Kristo, mauti"haimtawali tena"(Ram 6:9), ukidokeza ya kuwa hapo awali alikuwa na mwili uliotawaliwa na mauti.

Zaburi nyingi ni za kutabiriwa kwa Yesu; wakati aya zingine kutoka zaburi zikinukuliwa kumhusu Kristo katika Agano jipya, inafaa kusadiki ya kwamba mistari mingine katika Zaburi yamhusu yeye vile vile. Kuna idadi ya sababu ambazo zimekaziwa kwa kuonyesha ya kuwa Kristo anahitaji wokovu toka kwa Mungu.

  • Zab 91:11,12 imenukuliwa kumhusu Yesu katika Math 4:6. Zaburi 91:16 inatoa utabiri jinsi gani Mungu alimpa Yesu wokovu"Kwa siku nyingi (yaani uzima-wa milele) nitamshibisha, nami nitamuonyesha wokovu wangu". Zab.

  • : 69:21 kusulubiwa kwa Kristo (Math 27:34); Zaburi, nzima yatoa mawazo ya Kristo juu ya msalaba;"Ee Mungu uniokoe….Uikaribie nafsi yangu, uikomboe Mungu wokovu wako utaniinua"(Mst 1,18,29.).

  • Zab. 89 ni ufafanuzi juu ya ahadi ya Mungu kwa Daudi kumuhusu Kristo. Kuhusu Yesu, Zaburi 89:26 ilitabiri"Yeye ataniita (Mungu), wewe Baba yangu. Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu".

  • Maombi ya Kristo kwa Mungu ili kupata wokovu yalisikiwa; alisikiwa kwa ajili ya yeye kuwa kiroho, sio kwa sababu ya nafsi yake katika ‘utatu’(Ebra 5:7) Ya kwamba Mungu alimfufua Yesu na kumtukuza na mwili usiopatikana na mauti ni msemo mkuu kwenye Agano Jipya.

  • "Mungu …….alimfufua Yesu……. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kiume, awe Mkuu na Mwokozi"(Mdo 5:30,31).

  • "Mungu…..amemtukuza mtumishi wake Yesu,….. ambaye Mungu amemfufua katika wafu"(Mdo 3:13,15).

  • "Yesu huyo Mungu alimfufua"(Mdo 2:24,32,33).

  • "Yesu mwenyewe alitambua yote haya alipomuomba Mungu amtukuze (Yohana 17:5; 13:32; 8:54).

Ikiwa Yesu alikuwa ni Mungu mwenyewe, basi mkazo wote huu ungekuwa nje ya maana iliyoongelewa, kwa kuwa Mungu hawezi kufa. Yesu asingekuwa na haja ya kuokolewa ikiwa alikuwa ni Mungu. Kama alikuwa ni Mungu aliyemtukuza Yesu yanatolewa maelezo ya ubora wa Mungu zaidi yake, na utofauti wa Mungu na Yesu. Kristo hakuwa"Mungu wa milee kabisa (mwenye) miili miwili……mwili wa uungu na wa kibinadamu", kama nakala 39 za kwanza za Kanisa la Uingereza zisemavyo. Kwa maana kabisa ya neno, kiumbe anaweza kuwa na asili moja tu. Ushahidi tunauweka ni wa kuvunja kuwa Kristo alikuwa na asili yetu wanadamu.


  Back
Home
Next