Misingi Ya BIBLIA
Somo La 8: Asili ya Yesu
Dibaji | Tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu | Asili Ya Yesu | Ubinadamu Wa Yesu | Uhusiano Wa Mungu Na Yesu | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Akiwa Yuna na namna ya Mungu") | Maswali

8.2 Tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu

Upo uwiano mzuri wa kuupokea kati ya maneno hayo yanayotia mkazo kiwango ambacho"Mungu alikuwa ndani ya Kristo", na hayo yatokezayo ubinadamu wake, fungu la maneno ya sasa yanamfanya Yesu asiweze kuwa Mungu mwenyewe kwa kuthibitisha kwa Biblia jambo hilo,"Mungu kabisa ambaye ni Mungu"kama mafundisho ya utatu kwa makosa yanavyosema.(Msemo huu:"Mungu kabisa ambaye ni Mungu"ulitumiwa kwenye baraza la Nicea katika mwaka wa 325 BK, ambako wazo la Mungu kuwa na ‘nafsi tatu’ lilitangazwa kwa mara ya kwanza, halikujulikana kwa wakristo wa kwanza) Neno ‘utatu’ halipatikani katika Biblia. Somo la 9 linachimba zaidi katika ushindi wa Kristo juu ya dhambi kabisa na sehemu ya Mungu ndani yake. Tunapoanza masomo haya, tukumbuke ya kuwa wokovu kuja kuupata unahitaji kumfahamu vyema Yesu Kristo wa kweli (Yohana 3:36; 6:53; 17:3). Mara moja tukifahamu ukweli wa yeye kushinda dhambi na mauti, tunaweza kubatizwa katika jina lake ili tushiriki wokovu huu.

Moja ya maelezo mafupi yaliyo wazi ya uhusiano kati ya Mungu na Yesu yanapatikana katika 1Tim 2:5;"Mungu ni mmoja na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu, Kristo Yesu ; Fikira juu ya maneno yaliyojitokeza sana yanatuongoza kwenye dhana inayojitokeza baada ya kufikiri sana ifuatavyo:-

Kuwepo Mungu mmoja tu, basi haiwezekani Yesu awe ni Mungu; ikiwa Baba ni Mungu na Yesu naye ni Mungu, basi wapo Miungu wawili."Lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba’(1Kor 8:6) ‘Mungu Baba’ kwa sabau hii ni Mungu pekee. Basi haiwezekani kwamba kunaweza kuwapo Mungu aliyejitenga aitwae ‘Mungu mwana’ kama mafundisho potufu ya utatu yasemavyo. Vivyo hivyo Agano la kale linatoa maelezo ya kumhusu YAHU, Mungu mmoja akiwa ni Baba (mfano Isaya 63:16; 63:8)

Nyongeza kwa Mungu huyu mmoja, kuna mpatanishi mwanadamu Kristo Yesu"-……… na mpatanishi mmoja……"Hili neno ‘na’ linaonyesha tofauti iliyopo kati ya Mungu na Kristo.

  • Kristo kuwa"mpatanishi"maana yake ni kwamba yeye husimama kati ya- hivyo yeye ni mjumbe. Mpatanishi kati ya binadamu mwenye dhambi na Mungu asiye na dhambi hawezi kuwa na dhambi Mungu mwenyewe; ilibidi awe mtu asiye na waa, aliye na mwili ulio na dhambi wa mwanadamu."Mwanadamu Kristo Yesu"tunaachwa bila shaka kwenye usahihi wa maelezo haya. Hata kama alikuwa akiandika baada ya kupaa kwa Yesu, Paulo hamsemi"Mungu Kristo Yesu".

Mara kadha tumekumbushwa kuwa"Mungu si mwanadamu"(Hes 23:19; Hosea 11:9); lakini ni wazi Kristo alikuwa ni"mwana wa Adamu", kama alivyoitwa mara nyingi katika Agano Jipya,"mwanadamu Kristo Yesu’’. Alikuwa ni"mwana wa aliye juu"(Luka 1:32). Mungu akiwa ‘Juu’ inaonyesha ana kipeo cha juu; Yesu kuwa"mwana aliye juu"inamaana hakuwa Mungu mwenyewe katika utu. Lugha kabisa ya Baba na Mwana ambayo imetumika kumhusu Mungu na Yesu, ni dhahirri haiwafanyi kuwa wapo sawa. Ingawa mwana anaweza kuwa na mifano halisi na baba yake, haiwezi kuwa ni mmoja yule yule, wala kuwa mzee kama baba yake.

Kwa kukubaliana na hii habari, kuna hesabu dhahiri iliyo tofauti kati ya Mungu na Yesu’ ambayo ni wazi inaonyesha ya kuwa Yesu hakuwa Mungu mwenyezi

MUNGU

YESU

"Mungu hawezi kujaribiwa (Yakobo 1:13)

Kristo"alijaribiwa sawasawa na sisi kaika mambo yote (Ebr 4:15)

Watu hawawezi kumwona Mungu 1 Tim 6:16 Kut. 33:23)

Watu walimwona Yesu na walimpapasa (Yohana 1:1 huu ni mkazo

Mungu hawezi kufa - Hapatikani na mauti (Zab 90:2; ! Tim 6:16)

Kristo alikufa kwa siku tatu (Math 12:40; 16:21).

Tujaribiwapo, tunasukumwa na tendo la kuchagua kati ya kutenda dhambi na kumtii Mungu. Aghalabu tunachagua kumwasi Mungu naye Kristo alikuwa na uamuzi ule ule, bali daima alichagua kuwa mtii. Kwa sababu hii alikuwa na uwezekano wa kutenda dhambi, ingawa hakutenda kwa kweli. Mungu hadhaniwi kwamba anauwezekano wowote wa kufanya dhambi. Tumeonyeshwa kuwa mzao wa Daudi aliyeahidiwa kwa 2 Sam 7: 12-16 ni dhahiri alikuwa Kristo. Mstari wa 14 unasema uwezekano wa Kristo kufanya dhambi ;"Akitenda dhambi nitamwadhibu".


  Back
Home
Next