Misingi Ya BIBLIA Somo La 8: Asili ya Yesu Dibaji | Tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu | Asili Ya Yesu | Ubinadamu Wa Yesu | Uhusiano Wa Mungu Na Yesu | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Akiwa Yuna na namna ya Mungu") | Maswali |
8.1 DibajiInabidi iwe ni moja ya fikira kubwa zaidi za kuhuzunisha katika ukristo ya kuwa Yesu Kristo hajapata heshima na kuinuliwa vinavyomstahili kwa sababu ya kushinda dhambi, kwa kuendeleza tabia kamilifu. Fundisho lililoenea la watu linamfanya Yesu ni Mungu mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hajaribiwi (Yakobo 1:13) na wala hawezi kufanya dhambi. Kwa hiyo maisha yake hapa duniani yatakuwa ya kujisingizia, akiishi nje ya yale yanayowakabili wanadamu, lakini bila ya hisia za kiroho na kwa mwili kuchagua kati ya mambo mawili yanayowakabili watu, kwa kuwa yeye mwenyewe hakudhurika nayo. Mawazo yao kwa mbali, makundi kama wamormoni na mashahidi wa Yehova kwa uzuri wanashidwa kufahamu ajabu ya Kristo ya kuwa ni Mwana pekee wa Mungu. Kwa hivi asingekuwa Malaika au mwana wa kawaida wa Yusufu? Watu wengine wamedokeza kwamba wakati wa maisha yake mwili wa Kristo ulikuwa kama ule wa Adamu kabla ya kuanguka. Mbali ya kukosa ushahidi kutoka kwenye Biblia kwa mtazamo huu, kufahamu ya kwamba Adamu aliumbwa na Mungu toka katika mavumbi kunakosekana, wakati Yesu ‘aliumbwa’ kwa kuzaliwa na Mungu ndani ya tumbo la Mariamu. Basi, ingawa Yesu hakuwa na baba binadamu, mimba yake ilitungwa na kuzaliwa kama sisi kwa jinsi zote. Watu wengi hawakubali ya kuwa mtu mwenye mwili wa dhambi ulio wetu aliweza kuwa na tabia timilfu. Ni ukweli ambao ni kizuizi cha kumwamini Kristo katika imani ya kweli. Kuamini ya kuwa Yesu alikuwa na mwili kama wetu, bali hakuwa na dhambi kwa tabia yake, sio rahisi daima kushinda majaribu haya. Taarifa za maisha yake kikamilifu zimeandikwa kwa kirefu, zimeungana pamoja na maneno mengi ya Biblia yanayokana kuwa Yesu alikuwa Mungu, kwa kuthibitisha ufahamu na imani katika Kristo wa kweli. Ni vyepesi mno kudhani kwamba alikuwa Mungu mwenyewe, na kwa sababu hii alikuwa mkamilifu mwenyewe bila sharti. Hata hivyo mtazamo huu unahitaji ushindi mkuu ambao Yesu alishinda dhambi na mwili wa kibinadamu. Alikuwa na mwili wa kibinadmu; alishiriki kila moja ya mienendo yetu ya kutaka kufanya dhambi (Ebra 4:15), hata hivyo alishinda kwa kujiweka kwenye njia ya Mungu na kutafuta msaada toka kwake ili kushinda dhambi. Kwa hiari Mungu alimtoa, kwa upana na kwamba"Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake"kwa njia ya mwanae mwenyewe kabisa (2 Kor 5:19) |