Mwishoni Mwa Kitabu 1: Maelezo Mafupi Ya Msingi Wa Mafunzo Ya Biblia
- MUNGU
- Yupo mtu mmoja aitwaye Mungu
- aliye na mahali maalum katika mbingu
- aliye hai mwenye mwili halisi
- ambaye tumechukuwa sura yake
- Malaika ni wajumbe wake
- ambao hawatendi dhambi,
- wakishiriki tabia ya Mungu.
- Lipo umbo moja tu la kuwapo hai limefundishwa na Biblia - uwepo katika umbo la mwili. Mungu na Malaika wanaishi katika umbo la kimwili.
- Tumaini la Mkristo ni kupewa tabia ya Mungu katika umbo la kimwili Kristo akirudi.
- ROHO YA MUNGU
- Inapotajwa Roho ya Mungu ni uweza wake, pumzi na akili,
- ambayo kwayo anatimiliza mambo yote
- na kuwepo kila mahali.
- Roho Mtakatifu anatajwa uwezo huu uliotumika kutimiza miishi fulani.
- Kwenye nyakati mbalimbali zamani, watu wamekirimiwa kuwa na vipawa vyenye miujiza ya Roho.
- Hivi vimeondolewa,
- Uweza wa Mungu sasa umefunuliwa kwetu katika neno Lake.
- Roho Mtakatifu hawashurutishi watu kuwa wa kiroho kinyume na mapenzi yao wenyewe.
- Biblia ilivuviwa na Roho wa Mungu kabisa.
- Biblia tu ndio yenye mamlaka yetu katika uhusiano wetu na Mungu.
- AHADI ZA MUNGU
- Injili ilihubiriwa kwa namna ya ahadi zilizofanywa kwa mababa wa Kiyahudi.
- Uzao wa mwanamke katika Mwa 3:15 unataja Kristo na wenye haki, "waliochubuliwa" na wanachubuliwa kwa muda na dhambi, uzao wa nyoka.
- Kwa kutimilika ahadi za Mungu, sayari duniani haitaharibiwa.
- Uzao wa Abrahamu na Daudi alikuwa ni Kristo;
- twaweza kuwa ndani ya Kristo kwa kuamini na ubatizo,
- kwa hiyo basi ahadi hizi zinawahusu waamini wa kweli.
- MUNGU NA MAUTI
- Kwa tabia mwanadamu ni mfu, mwenye kuelekea kutenda dhambi, na
- amelaaniwa kwa matokeo ya kosa la Adamu.
- Kristo alikuwa na huu mwili wa kibinadamu.
- Nafsi hutajwa ‘sisi’, mwili wetu, mawazo au mtu.
- Roho ni kutaja nguvu za uhai wetu/pumzi na silika.
- Hakuna mtu awezaye kuishi akiwa na roho pasipo mwili.
- Mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu.
- Atakaporudi Kristo kutakuwa na ufufuo wa mwili kwa wale tu wenye kuijua Injili ya kweli.
- Maarifa na kufahamu Neno la Mungu vitakuwa msingi wa hukumu.
- Kupewa kabisa kutokufa kutatokea kwenye kiti cha hukumu.
- Adhabu ya waovu wahusika itakuwa mauti ya milele.
- ‘Kuzimu’ ni kaburi.
- ‘Jehanamu’ lilikuwa eneo nje ya Yerusalemu mahali pa takataka na walipochomwa wavunja sheria.
- UFALME WA MUNGU
- Watu wa Israeli walikuwa Ufalme wa Mungu zamani.
- Huu uliisha sasa, lakini utaanzishwa tena Kristo akirudi, kwa namna
- ya kuwa wa kuenea pote Ufalme wa Mungu duniani, ukitawaliwa na Kristo kwa niaba ya Mungu.
- Miaka 1000 ya kwanza (au ‘Kikwi’) ya huu Ufalme itaona waamini wa kweli wa zama zote watakuwa hai Kristo akirudi.
- Kwa hiyo sasa Ufalme kiutawala haujaanzishwa.
- Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani yetu, wala si kwa matendo yetu.
- MUNGU NA UBAYA
- ‘Ibilisi’ kwa maana ya neno ni ‘mshitaki’ au ‘msingiziaji’
- ‘Shetani’ kwa maana ya neno ni ‘adui’,
- laweza kutumika kutaja watu wa pande mbili wema na wabaya.
- Kwa mfano ibilisi na shetani yaweza kutajwa dhambi na mwili wa nyama.
- Nyoka wa Edeni alikuwa mnyama halisi;
- taarifa ya kitabu cha Mwanzo ya uumbaji wa mtu na kuanguka ieleweke ilivyo si kwa maneno ya kimfano.
- ‘Mashetani’ kama roho iliyojaa dhambi, roho waliotoka au nguvu ya dhambi hawapo.
- Kristo ‘kuwatoa pepo’ yaweza kufahamika kama sehemu ya lugha ambayo kwa namna yake inamaana ya kuwa aliponya magonjwa.
- Lusifa hatajwi Malaika aliyejaa dhambi.
- Mungu ni mwenye nguvu zote; hashirikiani uweza wake na kiumbe awaye yote mwenye dhambi apingaye njia zake.
- Majaribu katika maisha ya aaminiye mwisho huja toka kwa Mungu wala sio kwa matokeo ya ‘bahati mbaya’ au kwa kiumbe mwenye dhambi sana aitwaye Ibilisi.
- YESU KRISTO
- ‘Utatu’ kama kwa upana unavyofahamika katika Ufalme wa Kikristo ni elimu ambayo haijafundishwa katika Biblia.
- Kristo alizaliwa na bikira Mariamu
- aliyekuwa mwanamke wa kawaida mwenye mwili wa kibinadamu.
- Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu,
- ila alikuwa na tabia timilifu isiyo na dhambi,
- ingawa Mungu hakumshurutisha kutofanya dhambi; Yesu alikufa kwa hiari yake mwenyewe akiwa dhabihu timilifu kwa dhambi.
- Yesu alifufuliwa baada ya mauti yake msalabani.
- Kabla ya kuzaliwa Yesu hakuwahi kuishi,
- ingawa alikuwa katika nia/ kusudi la Mungu tangu mwanzo.
- Yesu alikufa akiwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu
- ili kupata wokovu kwa ajili yetu na yeye mwenyewe.
- Yesu alikufa akiwa mwakilishi wetu.
- Sio badala yetu kama kwa upana inavyoaminika na ufalme wa Kikristo.
- Kwa kifo cha Kristo Torati ya Musa ilikoma,
- Kwa sababu hiyo haitupasi kuitunza sasa, pamoja na Sabato.
- UBATIZO
- Bila ubatizo, hakuna tumaini la wokovu;
- kuamini na kubatizwa kunatuingiza kushiriki ahadi za Abrahamu,
- na kwa kupata msamaha wa dhambi
- Ubatizo ni kwa kuzamishwa ndani kabisa ya maji
- mtu mzima aliyeijua Injili.
- Hao waliozamishwa pasipo kuwa na elimu ya kutosha kwa Injili hawana budi kubatizwa tena. Kwa uzuri.
- Kufahamu Injili ya kweli unahitaji ubatizo kuwa thabiti.
- MAISHA KATIKA KRISTO
- Baada ya ubatizo, mwamini hanabudi kufanya bidii yenye akili kujitenga katika njia zilizojaa dhambi za ulimwengu,
- na kuendeleza tabia yenye sifa kama Kristo.
- Kujishirikisha katika shughuli za anasa zitakazopeleka kuvunja maagizo ya Mungu, k.m kutumia nguvu na unywaji pombe kupita kiasi, haiwezi kupatana kwa kweli na maisha ya Kristo.
- Waamini waliobatizwa wana wajibu kukutana na kushirikiana, popote wakati wowote kibinadamu ikiwezekana.
- Waamini waliobatizwa kila mara wamege mkate na kunywa divai kwa ukumbusho wa dhabihu ya Kristo.
- Sala ya kila mara na kusoma Biblia ni muhimu kwa mwamini aliyebatizwa.
- Mwamini aliyebatizwa tu ana ushirika na wale ambao wanashika mafundisho ya kweli na kujaribu kwa hali ilivyo kutenda kazi.
- Kwa hiyo ambaye anakoma kuamini au kuitendea kazi ile Kweli anakoma kuwa mshirika wa mwili wa waumini.
Angalia: Taarifa ya Imani moja ya utaratibu ambao umekuwa ukitumika zaidi ya miaka 100 unapatikana kwa wachapishaji.
|