Misingi Ya BIBLIA Somo La 5: Ufalme wa Mungu Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme | Kwa Sasa Ufalme Haujasimikwa | Ufalme wa Mungu uliopita | Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao | Miaka Elfu - Kikwi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Ufalme wenyewe, Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli) | Maswali |
5.2 Kwa Sasa Ufalme HaujasimikwaKwa upana kuna wazo limeshikwa ya kuwa ufalme wa Mungu sasa upo kwa ukamilifu, ukiwa unawaamini waliopo -'Kanisa’. Wakati katika matumaini waamini wa kweli 'Wameokolewa’ na kupewa nafasi za kuweza kuwa katika ufalme, Hapawezi kuwepo shaka kuwa sasa hatuwezi kikamilifu kuwamo katika ufalme, kwa kuwa Kristo bado hajarudi kuusimika. Hakuwa dhahiri kutokana na kile tulichojifunza mpaka hapo "yakuwa nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu"(1Kor. 15:50). Sisi"tu warithi wa ufalme ambao ameuahidi kwa hao wampendao" (Yakobo 2:5), kwa kuwa ubatizo unatufanya tuwe warithi wa Ahadi alizoahidiwa Abrahamu -ahadi zenye msingi wa Injili ya ufalme (Math. 4:23; Gal. 3:8,27 -29). kwa hiyo ni kawaida kuja katikati ya kurithi ufalme Kristo akirudi, wakati ahadi alizoahidiwa Abrahamu zitakapotimizwa (Math. 25:34; 1Kor. 6:9,10; 15,50; Gal. 5:21; Efe. 5:5).Matumizi kabisa ya Lugha ya urithi ujao yaonyeshwa ya kwamba ufalme sio miliki ya waamini waliopo sasa . Yesu akawaambia mfano wa kuwasahihisha wale waliodhani "kuwa Ufalme wa Mungu"utaonekana mara. Basi aliwaambia, mtu mmoja , kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi"Na wakati ule ule aliwaacha watumwa wake wakiwa na majukumu fulani ya kufanya. Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake , aliamuru waitwe wale watumwa"akafanya uamuzi nao (Luka. 19:11 -27). Kabaila ni Kristo aliyekwenda "nchi ya mbali" ya mbinguni kuupokea ufalme, ambao anarudi nao wakati wa hukumu, Yaani kuja mara ya pili. Kwa hiyo haiwezekani kuwa "Watumwa"wawe na ufalme hivi sasa, kipindi ambacho Bwana wao hayupo. Yafuatayo yanatoa ushahidi huu zaidi:-
UFALME WA MUNGU UMO NDANI YENU ? Mbali ya mkazo huu wote mkubwa kidogo, 'Wakristo’ wengi wa orthodox huchagua kuweka imani yao kuwa sasa ufalme umo mioyoni mwa waumini , juu ya fungu moja la maneno: "Ufalme wa Mungu umo (mioyoni) ndani yenu"(Lk. 17: 21). Hii kwa usahihi zaidi imetafsiriwa"Ufalme wa Mungu umo mioyoni mwenu (katika Biblia ya Kiingereza ya A. V). Biblia ya kiswahili cha kisasa - B.H.N - mstari umeandikwa"Ufalme wa Mungu umo kati yenu". Mstari unaonyesha ya kuwa Yesu alikuwa akizungumza na Mafarisayo (mst. 20); neno"Yenu"basi alikuwa akiwataja wao. Kwa hakika hawakuwa ni waamini wa Kristo - Ufalme wa Mungu haukuwekwa mioyoni mwao.Wayahudi walikuwa wakijionyesha kwa watu kuwa walikuwa na juhudi ya kumtazamia masihi. Kwa fungu hili la maneno,"Ufalme wa Mungu" laonyesha kuwa ni jina la masihi, wakiona atakuwa mfalme wa wafalme. Hivi Yesu alipoingia Yerusalemu , watu walishangilia,"Ndiye mbarikiwa (masihi) ajaye kwa jina la Bwana: umebarikiwa na ufalme ujao, wa Baba yetu Daudi"(Marko. 11:9,10). Hii inasawazisha masihi na 'Ufalme’ Naye Yohana mbatizaji alihubiri kuwa "Ufalme wa Mungu umekaribia. Maana huyu ndiye (Yesu) aliyenenwa na Nabii". (Math. 3: 2,3). Kwa fungu letu la maneno lililokatika Luka 17: 20 -24, Yesu alijibu swali lao lililohusu lini 'Ufalme wako utakapokuja’ kwa kusema kuhusu kuja kwa "Mwana wa Adamu". Maana ya Yesu ilikuwa kwamba Wayahudi walikuwa wanajionyesha sana kuwa walikuwa wakimtazamia masihi aje , wakitegemea atadhihirika katika nguvu, wakashindwa kutambua kwamba masihi -"Ufalme wa Mungu"- tayari ulikuwa kati yao katika mtu mpole Yesu. Hivyo akawaonya:"ufalme wa Mungu (masihi) hauji kwa kujionyesha …….. tazama, Ufalme wa Mungu uko kati yenu" (Luk. 17: 20,21). |